Mkasa wa kusisimua: Nilimsababisha Mateso Mke wangu

MWANAMASOKO

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
211
92
NILIMSABABISHIA MATESO MKE WANGU
Mkurugenzi mkuu wa "Merumba Group"alikuwa ofisini kwake akimsimulia binamu yake Richard mkasa uliomkuta miaka miwili iliyopita.
"Kuna mdada mrembo sana alikuja ofisini kwangu hapa na kuniambia."
"Samahani bosi."
"Bila samahani nikusaidie nini?"
"Naomba unisaidie kupata ajira."
"Ajira gani?"
"Nikupikie ,nikufulie,nikunyooshee nguo,nikufagilie nyumba,nikuoshee vyombo,nikutandikie kitanda,nikuogeshe na kadhalika."
"Ehee makubwa!Si useme unataka kuwa mke wangu ,naona kazi zote ulizozitaja zinafanyika nyumbani na hapa ni ofisini kulikoni?"
Yule mrembo kilio kikamtoka kikiambatana na machozi na kutamka :–

"Siyo mimi ndo nataka kuwa hivyo ila ni maisha ndiyo yanataka hivyo.Nilimaliza chuo kikuu Mzumbe mwaka 2005 na kutunukiwa shahada ya kwanza ya utawala/uongozi wa biashara nikiwa mwanachuo bora niliyepata alama za juu kuliko wanachuo wote katika "faculty of commerce" kwa mwaka huo.

Kutokana na matokeo yangu kuwa juu mno kwa kupata "gpa" ya 4.8, chuo kilinitafutia kazi katika benki ya biashara ya kimataifa inayofanya shughuli zake hapa nchini.Baada ya kukamilisha taratibu zote za usaili na kuajiriwa rasmi,siku ya kwanza ambayo natakiwa kuanza kazi niligongwa na gari nikiwa navuka barabara kuelekea ndani ya jingo la hiyo benki.

Aliyenigonga akakimbia,wasamalia wema wakaniokota na kunipeleka hospitali.Nilipooza nusu mwili kutokana na mshituko nilioupata kwa kulala kitandani kwa muda wa miaka mitano.

Baba aliuza kila kitu ili aweze kunitibu ,mwishowe akaingia kwenye madeni na kuukumiwa kwenda jera kwa kushindwa kulipa deni la shilingi milioni hamsini kwa ajili ya matibabu yangu nchini India.

Mama alipandwa na shinikizo la damu siku ambayo baba aliukumiwa kwenda jera miaka kumi na mitano na kufariki pale pale mahakamani.

Baba akiwa gerezani baada ya miaka miwili alifariki kutokana na kuugua ugonjwa wa moyo uliosababishwa na msongo mwingi wa mawazo juu yangu na hatima yake gerezani,kazi ngumu alizokuwa akifanyishwa,mlo duni waliokuwa wanapewa wafungwa pamoja na mazingira machafu ya gereza.

Benki ile ambayo nilitakiwa nianze kufanya kazi hawakutoa msaada wowote kwa kigezo kuwa bado nilikuwa sijaanza kiufanyia kazi.

Baada ya kurudishwa hospitalini Muhimbili kwa msaada wa ubalozi wa Tanzania nchini India kutokana na fedha za matibabu kuisha ambazo baba alikopa na ugonjwa wangu kushindikana kutibika na baba na mama wameshafiriki,hospitalini hapo nilibaki mimi peke yangu kwa maana hata ndugu nao walinikimbia.

Ikabidi watafutwe watawa wanichukue kwa ajili ya kuniuguza.
Siku moja usiku wa saa tisa baada ya miak mitano tokea siku ile niliyopata ajali, mvua kubwa ilikuwa inanyesha ikiambatana na radi na ngurumo za kutisha ,muda huo nilikuwa macho wazi, niliona kama mwanga wa tochi umepenya katika bati na kunimulika usoni.

Ghafla mwili wangu ukaanza kutetemeka kama mtu mwenye kifafa na kupoteza fahamu. Nilikuja kushituka saa kumi na moja alfajili na kujiona mwili ni mwepesi na nilipojaribu kuinuka nikajikuta nainuka,ahah nikajishangaa nikajikuta napiga kelele mama aha ,watawa waliokuwa katika misa ya alfajili wakaja na waliponiona na wao wakashangaa.

Baada ya miaka miwili mwili kuwa sawa nikaamua nirejee uraiani kutafuta maisha.Sikuwa na pa kwenda kwa maana vitu vyote baba aliuza ila nilimwomba mungu aniongoze niende mahali salama.

Nikiwa natembea tembea barabarani usiku nilikutana na dada mmoja na kumweleza shida yangu akakubali kunisaidia na akaniambia yeye anauza baa na sharti nikitaka kukaa kwake nami niuze baa.

Sikuwa na na jinsi ikanibidi nikubaliane nae.Nikawa nauza baa, meneja anataka nivae nguo fupi mapaja yawe wazi na nguo ya juu iwe inaacha sehemu kubwa ya matiti nje.

Usiku wanaume walevi wananitongoza nikafanye nao ngono kwani tayari wameshamlipa meneja ,nikakataa.Wanaume wale walienda kumfokea meneja ."We meneja mbona Malaya wako hataki kwenda kutuburudisha?Hajui kama tumeshakupa fedha kwa ajili yake ?Turudishie fedha zetu ."

Meneja alinitaka niende kufanya ngono na wale wanaume ,nikamkatalia na kumwambia "Mimi sijiuzi bali ninafanya kazi ya kuwaudumia wateja vinywaji ."Meneja alikasirika sana na kuniambia kama sitaki basi na mimi kazi sina.Akanifukuza kama mbwa mdowezi huku akinikashifu ."Mwanamke gani wewe hutaki kuwastaheresha wanaume?

Hujui kuwa kazi ya mwanamke hapa duniani ni kuwaliwaza wanaume kingono?Pumbavu kabisa toka hapa ."
Nilitoka pale huku nalia nikarejea kwa yule dada muuza baa siku hiyo alikuwa mapumzikoni,hata kabla sijakaa akaniambia."Eheee bibi,meneja kanipigia simu na kunieleza yote uliyoyafanya na mimi sikutaki tena uishi humu ndani,unazani mimi ninaishije hapa mjini ?Mimi ninafanya kazi kama hiyo meneja aliyokuambia wewe hutaki,unazani nani atakulisha na kukulaza bure?

Embu toka ndani mwangu mpumbavu wewe ,hapa ni mjini ukitaka kula vya watu na wewe lazima uliwe hata Raisi wako anasemaga, kwenda huko ukafie mbali alah umeniuzi kama nimekufumania na buzi langu kenge wewe.

Nililia sana siku ile, dunia niliiona chungu sikutamani hata kuendelea kuishi lakini kama kuna mtu alikuwa ananiambia moyoni "Kama sikuweza kufa katika ile ajali na kulala kitandani miaka mitano basi sitaweza kufa mpaka muda wangu wa kuishi hapa duniani utakapo kwisha."

Siku hiyo nililala sokoni ambalo lipo maeneo hayo.Maisha yangi yakawa hapo sokoni nikiwa na akina dada wengine ambao nao hawana sehemu ya kulala tukiwa tunafanya kazi ya kubeba matenga yaliyoletwa na malori kutoka mikoani.

Baada ya mwaka mmoja nikiwa pale sokoni kuna mdada mmoja alikuwa ananunua tenga la nyanya na muuzaji aliniita ili nilibebe na kulipeleka kwenye gari la huyo mdada.Ahaah, yule mdada alishituka na kunifanya na mimi nimuangalie kwa umakini na kumtambua ni rafiki yangu tulisoma wote shule ya sekondari Jangwani.

Tulikumbatiana na kuanza kulia,alishangaa mno kuniona niko vile ndipo nikamueleza kila kitu kilichonitokea,alilia sana na kunichukua mpaka kwake anapoishi na mumewe na muda huo alikuwa safarini kibiashara nchini Ufaransa na angerudi baada ya miezi sita.

Mimi na rafiki yangu huyo tulianza kufuatilia vyeti vyangu vipya kuanzia sekondari mpaka chuo na kufanikiwa kuvipata na kuanza kuomba kazi sehemu mbalimbali na nilipoitwa kwa ajili ya "interview" niliishia kuombwa rushwa ya ngono nikakataa na kazi nikanyimwa ingawaje nilikuwa napata alama za juu kuliko waombaji wote katika kila interview niliyokuwa nakwenda kuifanya.

Rafiki yangu alipata safari ya kwenda nchini Malaysia kibiashara na baada ya hapo aliunganisha safari kwenda Ufaransa kwa mumewe ila ndege aliyopanda ilidondoka baharini na kupotelea huko.

Pale kwake nilibaki mimi na kodi ya nyumba ilipoisha,mwenye nyumba akanifukuza kwani walikuwa wamepanga nikarudi tena mitaani kupambana na maisha.

Baada ya miaka miwili ya mateso na misukosuko mingi nilibahatika kupata kibarua cha kubeba zege hapa Posta Katika ghorofa jipya linalojengwa na kuweza kupanga chumba kimoja maeneo ya Mbagala.

Na jana wakati narudi nyumbani kutoka kibaruani ndo nikaliona bango la ofisi yako kule chini limeandikwa "MERUMBA GROUP".Kuna kitu moyoni kikaniambia nichukue vyeti vyangu na kuja kujaribu kuomba kazi hapa.

Lakini nikajiambia kila ninapokwenda kuomba kazi naishia kuombwa rushwa ya ngono na nikikataa nanyimwa kazi basi nikajisemea nikifika hapa niombe kazi zinazofanyika nyumbani."Alimaliza kusimulia yule mrembo huku akilia na machozi yakimtoka.

"Daah aise Richie nililia sana alivyonisimulia vile kwa maana yule mdada mimi ndiye niliyemgonga ,alafu yule rafiki yake aliyeanguka na ndege alikuwa ni mke wangu kama unakumbuka vizuri mke wangu alikufa katika ajali ya ndege miaka mingi imepita.Na nilipopata taarifa ya ajali ile nilizimia kwa muda wa mwaka mmoja na namshukuru mungu wazazi wangu walinitibu mpaka nikapona.

Alinishangaa kwa nini nami nalia vile nikamweleza kila kitu kilichotokea ,tulikumbatiana na kubaki tunalia wote. Nikamwomba msamaha kwa kumgonga na gari na kukimbia na kumsababishia matatizo makubwa ila mungu aliacha jambo hilo litokee kwa makusudi maalum na yeye akanisamehe.

Nilimchukua kutoka pale ofisini na kumpeleka moja kwa moja kwa wazazi wangu na kuwaeleza kila kitu nao wakawa wanalia.Mwezi mmoja nikafunga nae ndoa maana kusema ukweli ni mrembo sana ingawa matatizo yaliuficha urembo wake na alikuwa hajaguswa kabisa waswahili wanaita kigori yaani bikra.

Nakumbuka hata wewe ulipokuwa nchini Japani ulishangaa kwa nini naoa ghafla bila ya kutoa taarifa mapema na wewe kushindwa kuuzulia harusi yangu ni kutokana na kutaka kuondoa machungu aliyokuwa nayo na mimi pia.

Sasa hivi nimpatia kazi kama mkurugenzi mkuu msaidizi akisimamia makampuni na biashara zangu zote ninazomiliki na yupo nyumbani ana mimba ya miezi tisa kasoro siku chache ajifungue niitwe na mimi baba teh teh teh.

Dah nilimsababishia mateso mke wangu na kweli maisha hayatabiriki lakini mungu ni mwema sana kwetu sisi binadamu.

MWISHO.

The Marketer.
 
Ka story katamu kweli.

Still mkasa huo haumfanyi ke kutuliza akili zao baada ya ndoa, hawa ke hawa, basi tu Mungu kawapa ile kitu tunapenda.

Btw: kama kastori ni ka kweli, Mungu awajalie waishi kwa amani.
 
Unataka kutufundisha nin!?

Maisha jinsi yanavyobadilika kutoka ktk matarajio na mtu kuingia ktk matatzo mazito, migogoro lakn mwisho wa siku anayashinda.lete hoja mdau kubadilishane mawazo.The marketer.
 
Pole na hongera pia mungu ni mkuu

Kwa Mungu kila kitu kinawezekana na hakuna marefu yasiyo na mwisho. maisha hayatabiliki kabsa yaan ni mungu pekee ndye anaejua.lete hoja mdau tuchangie. The marketer.
 
Ka story katamu kweli.

Still mkasa huo haumfanyi ke kutuliza akili zao baada ya ndoa, hawa ke hawa, basi tu Mungu kawapa ile kitu tunapenda.

Btw: kama kastori ni ka kweli, Mungu awajalie waishi kwa amani.

Ni kwel mdau,mwanamke kama ni mapepe ni mapepe tu hata akutane na matukio gan na kuolewa bado anaweza kufanya umapepe wake ndyo maana mtu anapokuwa na mpenz anakuwa anajitoa kafara kwa lolote lile.lete hoja mdau tuchangie.The marketer.
 
Kastory kazuri sana,maisha ni safari ndefu sana,whats goes around comes around.

Hapo kwenye Mungu tunayemzungumzia ambaye ni mkuu tafadhali anza na herufi kubwa yaani Mungu na si mungu.
 
Kastory kazuri sana,maisha ni safari ndefu sana,whats goes around comes around.

Hapo kwenye Mungu tunayemzungumzia ambaye ni mkuu tafadhali anza na herufi kubwa yaani Mungu na si mungu.

umeona ehe? tunajaribu kufundisha kwa mifano ili watu waelewe.ni kama mwalmu awapo darasan bla kutoa mifano wanafunzi hawataelewa na ndyo dhumuni la kuandika mkasa huu.ha ha ha ha natumia simu ndyo maana nashndwa kuandka vzur ila ujumbe umeeleweka.hahaha lete hoja mdau tuchangie.The marketer.
 
NILIWALIZA NAMI NIKALIZWA
"Wewe uliwaliza nawe ukalizwa ,unamaanisha nini?"Robin alikuwa anamuuliza rafiki yake amfafanulie maana ya maneno aliyoambiwa na rafiki yake huyo anayeitwa Frank.
"Dah Robin ni "story" ndefu mno yaani niliwaliza kweli kweli nami nika\lizwa haswa."Alisema Frank.
"Oya acha kunichanmganya,nieleze nini maana ya hayo maneno?"Alifoka Robin.
"Aha tulia kaka,naona una hamu sana ya kujua kilichojili mpaka unafoka?Haya ni hivi,,,,,,."
"Mwaka 2000 nilimaliza kidato cha sita shule ya sekondari Azania na kupata alama za juu sana katika mitiani ya taifa na kuwa "Tanzania One" almaarufu kama T.O nikimaanisha mwanafunzi aliyepata alama za juu mno kuliko wanafunzi wote kwa mwaka huo.Nilifurai sana \nilipotangazwa kuwa T.O .Wale wengine walioingia tatu bora tulikwenda kuonana na Mheshimiwa Raisi pale Ikulu na kutupongeza sana na kutupa zawadi mbalimbali na kututaka kila mmoja achague nchi anayotaka kwenda kusoma masomo yake ya elimu ya juu nikimaanisha masomo ya chuo kikuu.Wenzangu wakataja nchi wanazotaka kwenda ila mimi nikamwambia kuwa nataka kubaki hapa hapa bongo.Alinishangaa sana na kuniuliza kwa nini nataka kubaki bongo na sitaki kwenda kusoma nje ya nchi kama wenzangu.Nikamwmbia mimi ni mzalendo siwezi kuiacha nchi yangu na kwenda kusoma nje,nikifanya hivyo ni kama nimeizarau elimu inayofundishwa hapa nchini.Nikamweleza mbona elimu ya sekondari sijasoma nje ya nchi lakini nimesoma hapa hapa bongo na kuweza kuongoza kitaifa hivyo elimu ya hapa bongo ni nzuri na waokimbilia nje ya nchi ni malimbukeni na wanakwenda kuwa watumwa wa elimu za nchi nyingine.Mheshmiwa Raisi aligwaya kwa jibu nililompa,akulitegemea kabisa.Akainuka kwenye kiti na kunifuata na kunikumbatia na kusema "WEWE NI MZALENDO WA KWELI NA KUANZIA SASA UTAKUWA MSAIDIZI WANGU NDANI YA IKULU HII HUKU UKIENDELEA KUSOMA.UTAPOKEA MSHAHARA MNONO KILA MWEZI NA UTAPEWA NYUMBA NA GARI LA KUTEMBELEA LA KIFAHARI HUKU UKIFANYA KAZI HAPA IKULU." Nilifurahi sana kuambiwa vile hata wenzangu walinionea wivu.
Nikaanza masomo chuo kikuu cha Dar es salaam nikisomea sheria.Nilikuwa mwanachuo pekee niliyekuwa naingia na gari ya kifahari chuoni mle.Jina langu likapaa na kuwa maarufu sana ukizingatia mimi ndiye nilikuwa T.O hivyo nikawa nazungumziwa kila mara,kila nilipokuwa napita nikawa naitwa Tanzania One wengine wananiitaT.O mpaka nikayazoea hayo majina.Kama kawaida yangu nikawa naliongoza darasa langu kila mitihani tuliyokuwa tunafanya kwani nilikuwa na usongo sana nisome kwa bidii ili nimfuraishe mheshimiwa Raisi kwani ameshanipatia kazi na mara kwa mara nilikuwa nipo Ikulu nikiwajiba kwa kazi nilizokuwa naagizwa nizifanye huku nikiwa kijana mdogo kuliko wote kwa watumishi wa mle ikulu.Sifa zangu zikaenea kila mahali chuoni na wakajua kuwa nafanya kazi Ikulu.Hapo sasa fujo zilipoanza,mhadhili wa kike anayenifundisha akanipenda sana,akanishawishi kwa kila hali nimkubalie kwani na mimi sikuwa najiusisha na mapenzi toka utotoni yaani wenzangu walikuwa wananitania mimi ni bikra wa kiume.Ukizingatia mhadhili yule ni mzuri na mrembo sana ingawa alinizidi miaka nane mwishowe nilishindwa kukwepa vishawishi vyake tukawa wapenzi.Aha nilipoonjeshwa utamu wa mapenzi nilipagawa mtoto wa kiume.Muda wote nikawa nawaza mapenzi tu.Nikawa mimi na mapenzi,mapenzi na mimi.Huku nikiendelea kimapenzi na mhadhili wangu wanachuo wa kike nao wakawa wanajileta wenyewe kutoka kila kozi iliyofundishwa chuni mle.Mwanaume sikujivunga nikawa nawala kama sina akili nzuri.Mhadili wangu alipogungua kuwa mimi ni kicheche alilia sana na kila aliponiambia nitulie nae nikawa namjibu kuwa yeye kashazeeka wacha mimi nile damu changa zenye umoto umoto.Alinivumilia lakini mwishowe aliniacha baada ya kugundua kuwa natembea na mlezi wa wanafunzi."
"Wanachuo wa kike waliokuwa wakjileta wenyewe nikawa nawabadilisha kama nguo na kila mara fumanizi lazima litokee.Walikuwa wanapigana wenyewe kwa wenyewe mpaka wanapasuana na kupelekana polisi wakinigombania.Wasichana wengi walikuwa wakinililia sasa sikujua walikuwa wananipenda kweli au walitamanishwa na mali na umaarufu wangu.Nilitembea na wanafunzi mpaka nikawachoka na kuanza kutoka na majimama au mashangingi kama yanavyoitwa .Aise huko napo nilidatishwa,majimama matamu bwana tena yanajua mapenzi balaa na ukiwa dogo dogo utalelewa kama mtoto mchanga.We niliwabadili na walikuwa wananililia kama mimi Mungu vile ili nisiwaache lakiniwapi kila mara nilikuwa natafuta jimama lipya.Nikiwa chuoni mwaka wa mwisho nilikutana na msichana mmoja chotara wa kisomali na mwarabu akiwa mwaka wa kwanza weeeeeeeeeeee kaka mtoto alikuwa mzuri sijapata ona maishani mwangu.Wala yeye hakunipapatikia kama wenzake bali mimi ndo nikampapatikia.Kwa mara ya kwanza nikampapatikia msichana toka niyaanze mapenzi.Mtoto wa kike akajifanya mgumu lakini mwishoew nikamweka himayani mwangu.Wacha nijilie mautamu kaka yaani sitomsahau yule binti mhm aha mapenzi matamu bana.Yule binti baada ya miezi sita akaumwa ghafla na kufariki.Nililia sana kwa kufariki kwake ,Baada ya mwezi nikaanza kuumwa sehemu zangu za siri.Zilikuwa kama zinaoza na kuuma sana,nililia mpaka nikawa napoteza fahamu,niliangaika kila hospitali hapa bongo lakini sikupona.Sehemu zangu za siri zikawa zinazidi kuaribika ni kama embe lililoiza na kuanza kuoza na kutoa funza.Mheshimiwa Raisi ndiye aliyenipeleka Uingereza nikatibiwe baada ya kupewa taarifa zangu.Uingereza nikatibiwa kwa miezi miwili ndo nikapona na kurejea bongo.Nilipofanya uchunguzi nikagundua ugonjwa ule niliambukizwa na yule chotara wa kisomali na ndo uliomuua huo ugonjwa kwani wa kwake ulikuwa umekomaa sana kiasi kwamba ukashindikana kutibika.Nilizani nimeambukizwa na ukimwi lakini nilipopimwa Uingereza nikaonekana sina ukimwi.Daah kaka sikuwa na hamu tena na wanawake toka nilipopona.Ikanibidi nirudie mwaka wa mwisho lakini chuo kingine kwani nilikuwa naona aibu kutokana na habari zangu kuonea sana pale chuoni UD.Niliamia Mzumbe ndipo nilipohitimu shahada yangu ya kwanza ya sheria.Baada ya kuhitimu siku moja nikiwa na Mheshimiwa Raisi nyumbani kwake aliniomba nimsimulie kisa cha kusababisha mimi kuumwa vile ndipo nilipomsimulia.Nilipomaliza akaniambia WEWE ULIWALIZA NA WEWE UKALIZWA. Hiyo ilitokana na machozi yaliyokuwa yanawatoka wale wasichana kwa ajili yako wewe ukiwatenda ndivyo sivyo.Hivyo ni kama laana ya wasichanaa juu yangu ndiyo iliyosababisha mimi kuumwa vile na ningetakiwa kufa kabisa sema Mungu tu ndo ameninusuru."Alisimulia Frank.
"Aise pole sana Frank lakini nadhani umepata fundisho hivyo ukome kuwatenda vibaya wanawake kisa mali na umaarufu wako."Alisema Robin.
"Nilishakoma, nimekoma na nitaendelea kukoma ama kweli ukitenda ubaya utalipwa ubaya na malipo ya ubaya ni hapa hapa duniani,duu niliwaliza nami nikalizwa sina hamu mie mweee."
MWISHO.
The Marketer.
 
story nzuri aiseee asa huyo nae alozimia mwaka mmoja niko natafakari hapa

Ha ha umeona ehe? ndugu yangu haya matukio watu ukutana nayo bla ya kutegemea.we ombea usome tu kama hv lakin yasikukute.embu pata pcha wewe ndye ungekuwa kama huyu muhucka mkuu ingekuaje kwako? ha ha ha ucogope mdau.lete hoja tuchangie.The marketer.
 
Mhhhhhhh!! Ze marketer mbona story mpya ndani ya story,kastory hako kapya na kenyewe kazuri zuri. Ushauri jitahidi kuweka Aya vizuri maana kwa wavivu wa kusoma ni shida ndo maana unaona kasi ya watu kuchangia ni ndogo.
 
Mhhhhhhh!! Ze marketer mbona story mpya ndani ya story,kastory hako kapya na kenyewe kazuri zuri. Ushauri jitahidi kuweka Aya vizuri maana kwa wavivu wa kusoma ni shida ndo maana unaona kasi ya watu kuchangia ni ndogo.

Nimekuelewa mdau kwani nataka kuwa na thread moja ambayo ninapost mikasa tofautitofauti ihusiyo mapenzi,mahusiano na urafiki.ila muache uvivu wa kusoma.ha ha ucnichoke mdau.lete hoja,maoni na masahihisho tuchangie.The marketer.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom