MKASA WA KUSISIMUA: HAKUNA LAANA MBAYA KAMA KUMKANA MAMA YAKO MZAZI

ng'ombo

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
418
619
*Binti mmoja ambaye alitokea katika familia masikini alifanikiwa kusoma kwa shida mpaka kufanikiwa kuwa mwanasheria. Alipata kazi nzuri, akiishi katika nyumba nzuri ya kifahari.*

*Pamoja na maisha mazuri lakini binti aliwasahau kijijini kwao, alikua akituma pesa kidogo lakini hakutaka kwenda. Alitaka kuyasahau maisha yake yote ya mateso ya kijijini.*

*Hata kwa marafiki zake alijitambulisha kama kazaliwa Dar huku akidanganya kuwa wazazi wake wamefariki nayeye alikua ndiyo mtoto pekee, hii ni kwasababu marafiki zake wote walikua wakitoka katika familia za kitajiri.*

*Baada ya kukaa muda mrefu bila kufika kijijini kwao wazazi wake walipata wasiwasi, huku wakiwa na wasiwasi kuwa kuna kitu kimempata, walichangisha nauli na Mama yake ambaye alikua mzee sana alipanda gari na kwenda kumuona mjini.*

*Alipelekwa na jirani yao mmoja ambaye alikua akifahamu alipokua akiishi yule binti. Mama alifika na kukuta binti akiwa na afya nzuri, hana tatizo lolote. Binti alikasirika sana kumuona Mama yake kwani alikuja bila taarifa.*

*Hakumsalimia vizuri na kila saa alikua akimlaumu kwanini hakupiga simu kwanza na kama ni hela si angesema amtumie. Mama huku akitokwa na machozi ya furaha alisema shida yake haikuwa hela bali kumuona mtoto wake baada ya muda mrefu.*

*Binti alimdanganya Mama yake kua ile nyumba ni nyumba ya kampuni hivyo haruhusiwi kuishi na mtu yoyote kutokana na kazi aliokuwa anaifanya hivyo yeye asingeweza kuishi pale.*

*Mama hakuwa na maneno, alimuambia hamna shida yeye kwakua ashamuona mwanae roho yake imetulia kwani hakuenda kukaa pale alienda tu kumuona.*

*Binti alimuacha Mama yake apumzike siku ile na kesho yake ili siku inayofuata apande gari kurudi kijijini. Siku iliyofuata baada ya kutoka kazini rafiki zake walikuja, kulikua na sehemu ambayo walishapanga kwenda.*

*Walimkuta Mama yake akiwa nnje akipunga upepo. Walimsalimia vizuri na binti alipowaona aliwakimbilia kuwawahi ili Mama asijitambulishe kwao, alifika na kuwaharakisha rafiki zake ili waondoke.*

*Walipotaka kujua ni nani, alijikuta anadanganya “ Huyo Mama amepotea njia, alipita hapa alikua anamtafuta mtoto wake akakosea nyumba, sasa ndiyo namsaidia, aligonga kwangu kuomba simu, kwani alikua na namba ya mwanae kwenye kikaratasi.*

*Nimeshampigia mwane atakuja kumchukua. Binti alionge akiamini kuwa kesho yake anamuondoa Mama yake mule ndani hivyo rafiki zake hawatamuona tena.*

*Wakati akiongea yale maneno hakujua kuwa Mama yake anasikiliza, alistuka baadaye alipogeuka wakati anafungua mlango wa gari ili aingie. Mama yke alikua anatokwa na machozi, binti alijikaza kama vile hakumuona akaingia kwenye gari na kuondoka.*

_____________________
*Baada ya mizinguko yake binti alirudi nyumbani, hakumkuta Mama yake, alimuuliza mfanyakazi wa ndani akasema hajui, alijua wameondoka wote kwani alimuacha nnje wakati yeye anatoka na gari.*

*Binti alianza kupaniki, alisubiria mpaka usiku wa mamnane lakini Mama yake hakurejea. Hapo alianza kuchanganyikiwa, kichwa kikikumbuka maisha ya shida waliyopitia, namna ambavyo Mama yake alivyoteseka kwaajili yake.*

*Machozi yalinza kumtoka akijutia mambo aliyomfanyia Mama yake. Alimtafuta yule Kaka ambaye alimleta Mama yake pale lakini hakuwa akijua chochote. Usiku ulipita akiwa macho, asubuhi alilazimika kwenda kazini kwani alikua na kikao.*

*Lakini mchana alishindwa kuvumilia, ilibidi kwenda Polisi na kuanza kumtafuta Mama yake lakini hakupatikana. Siku moja ilipita na hatimaye yapili ilipita bila kumuona Mama yake, alianza kuwa na wasiwasi.*

*Akiwa ofisini hajui hili wala lile rafiki yake mmoja alikuja, walianza kuongea akiwa hana raha kabisa. Rafiki yake alimuuliza tatizo lilikua nini akaamua kumuambia, lakini kabla hajaanza kuonge arafiki yake alisema.*

*“Halafu shogaa nilitaka kusahau, unamkumbuka yule Bibi ambaye tulimkuta kwako jana?”*
*``Ndiyo namkumbuka! Amefanya nini? Umemuona wapi?” Alijikuta anadakia kwa haraka kutaka kujua.*
*Basi jana wakati natoka kazini nikapita sehemu, nimekuta watu wamezunguka, kumbe kagongwa na bodaboda kaumia kichwani, watu wakawa wanakimbia kukwepa ushahidi.*

*Namimi nikapita, sasa baadaye narudi kumbe watu walimuacha pale Bibi wawatu mpaka Polisi wanakuja lisaa lizima baadaye basi Bibi wawatu kashafariki. Kusema kweli roho iliniuma sana kwa kumpita bila kumsaidia…”*

*Rafiki yake aliongea kwa masikitiko, lakini kabla hajamalizia yule binti alidondoka na kupoteza fahamu. Alizinduka yuko hospitali kazungukwa na marafiki zake na mchumba wake.*

*Walimuuliza sababu ndipo alipoamua kuwaelezea, kila mtu alimshangaa kwa kumficha Mama yake, walihangaika kumtafuta wakakuta maiti yake, wakamsaidia kusafirisha maiti mpaka Kijijini.*

*Walizika salama lakini baada ya kurudi mchumba wake alimuacha, marafiki zake wote aliokuwa akiwaona wa maana walimtenga kutokana na tabia zake. Binti alishikwa na msongo wa mawazo.*

*Kila siku ilikua mtu wa kulia tu, alishindwa kufanya kazi vizuri, jambo lililopelekea *afukuzwe kazi*.

*Kafukuzwa nyumba ya kifahari aliyokua akiishi na sasa yuko mtaani akitafuta ajira huku akiona hata aibu kurudi nyumbani kuwaona ndugu zake.*

Nakutakia Jumapili Njema, Mungu Akubariki na kukulinda

Screenshot_2017-06-17-20-10-01-1.png
 
So sad kwa kweli..Tuwapende, tuwaheshimu na tuwathamini Mama zetu.. Ukifanikiwa isiwe ni sababu ya dharau..

[HASHTAG]#KarmaWorks[/HASHTAG]
 
Dah hii stori inafundisha sana tena sana. Hili jambo unaweza ona ni masihara au kama ni hadithi lakini yanatokea katika jamii zetu kwa namna tofauti tofauti kila siku.

Mfano: unakuta mwanamke amebahatika kuolewa na mwanaume mwenye uwezo basi hapo ni shidaa humuambii kitu, na ndugu zake anawaona takataka kabisa na ukichukulia yupo mjini basi hataki kumuona hata mama yake au baba yake anayepigwa na maisha huko kijijini aje mjini kumtembelea tu hata kwa mara moja. Anaona amemaliza maisha yote! kimbembe kinakuja siku akiachika kwa huyo mume hapo sasa ndio anapo-aibika, mbaya zaidi wengine huonyesha nyodo wazi wazi.

Kwa upande wa wanaume hili huwakuta sana tena sana na mara nyingi huwa laana ya mama zao LAKINI chanzo kikubwa huwa ni mwanamke/mke wake. Unakuta mwanaume amesomeshwa kwa shida hadi kafanikiwa kimaisha na yupo juu. Sasa anakuja kumpata mwanamke wa mjini mjini wa ki-digitali ambao wapo busy mitandaoni wakifundishana kuwa ndugu wa mume ni sumu hasa mawifi na mama mkwe ndio wanaovuruga ndoa zao.

Katika hali kama hiyo sasa ikatokea mama mkwe amepanda basi toka mkoani/kijijini huko NAMUPA au Nanjilinji au Mingoyo amekwenda DARISALAAM kumtembelea kijana wake aliyemzaa na kumsomesha kwa shida....ndio unakuta anakutana na dada zetu hawa na kupokelewa kwa maneno na dharau + kejeli na maneno ya mafumbo muda wote. Mwisho wa siku Mama mkwe anaona isiwe taabu anamuaga kijana wake anaondoka anarudi kijijini na anaapiza sirudi tena na sikanyagi tena Darisalaam kwa mwanangu...acha waishi kwa raha zao!

Laana hiyo haimuachi kijana salama hata siku moja; mwisho wa siku mabalaa kazini yanaanza, uchumi unayumba, na kaunza kuhangaika kama sio kufukuzwa kazi kabisa. Hali ikiwa mbaya ...unakuta yule yule dada aliyemfanya mama wa kijana ni wakuja.....anasepa kwa kumuacha jamaaa kwa sababu tayari amefulia hana kitu..hajui bila huyo mzazi kukomaa yeye asingeyafurahia hayo maisha kutoka kwa huyo kijana.

USHAURI: Akina dada badilikeni, kumbuka bila mzazi wa mume/mpenzi wako kumfikisha hapo alipo wewe usingempenda hata kidogo au pengine hata msingefahamiana kabisa kwa sababu angekuwa huko kijijini Nanjilinji au Mingoyo anauza ming'oko au kuwinda sungura na ndege porini.
 
Hii itakuwa Bongo muvi inayotarajia kuingia sokon. Au unajifundisha uandishi wa muvi(script) nisikukatishe tamaa endelea hivyo hivyo unaweza kuwa mwandish hapo baadae
 
Back
Top Bottom