Chipukizi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 3,949
- 5,980
Kama nilivyotumiwa
Ukhty leo nina mkasa nimeukuta hospitali ya mkoa wa Dodoma nilienda kusalimia wagonjwa,nikakuta binti wa kazi amelazwa kapigwa na boss wake mpaka kamjeruhi kisa alichelewa kuamka kumchemshia maji ya kuoga huyo mama ambae ni mwalimu wa shule ya msingi Mlimwa C iliyopo hapa mjini Dodoma.
Binti anaonekana kidogo ana matatizo ya akili japo anajielewa vizuri,alipata ujauzito boss wake akamwambia asiseme kwa yeyote kama ana mimba,mpaka kajifungua kamwambia asiwaambie hata majirani kama ana mtoto kwani hapo hakuja kuzaa bali alikuja kumlelea watoto wake.
Kwa hiyo huyo mtoto akawa anamfungia kwenye kabati lake la nguo huyo boss ili majirani wasisikie sauti ya mtoto kwa muda wa miezi mitano hadi Jana alipompiga hadi akazimia ndio siri ikagundulika.
Binti yupo Hospitali na mwanae,hali ya hako katoto ni ngumu mno,ukiambiwa ana miezi mitano huwezi kuamini.
Kwa kweli nimeumia hadi nimelia, sijaamini sisi wanawake kama ni wakatili kwa kiwango hiki.