Mkasa wa kusikitisha Dodoma: Msaidizi wa kazi anyanyaswa na mwajiri wake, mtoto wake mchanga afungiwa ndani ya kabati kwa miezi 6

tujifunze kusikiliza na upande wa pili, na pia kuiachia mahakama kazi ya kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria, hii tabia ya watanzania kujichukulia sheria mkononi ndio imepelea nchi kuzalisha rais ambaye anaona katiba na sheria vinamchelewesha na anaagiza polisi wanaovunja sheria na kufanya uharifu dhidi ya binadamu wapandishwe vyeo!! akili kama hizi zinaanzia huko mitaani na haziibukii tu ikulu kwa bahati mbaya.
 
View attachment 982849
JESHI la Polisi limelazimika kumtia tena mbaroni Anitha Kimaro, ambaye anadaiwa kumfungia kabatini mtoto wa miezi sita.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake na kuanza kumtembezea kichapo huku wakipinga hatua ya polisi kumpa dhamana.

Anitha ambaye pia ni mwalimu wa Shule ya Msingi Chadulu mjini hapa, anatuhumiwa kumfanyia ukatili mfanyakazi wake wa ndani (jina linahifadhiwa), kwa kumpiga na kumjeruhi, huku akimfungia ndani ya kabati mtoto wake wa miezi sita Mtaa wa Makongoro, Kata ya Kiwanja cha Ndege.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema waliamua kumkamata tena Anitha kutokana na usalama wake uraiani kuwa mdogo.

Alisema awali walimkamata mtuhumiwa huyo, lakini ilibidi wamwachie kwa dhamana ambayo ni haki yake ya msingi.

“Tulimwachia kwa dhamana, lakini jana (juzi) tulilazimika kumkamata tena kutokana na usalama wake kuwa mdogo baada ya wananchi wenye hasira kuvamia nyumbani kwake,” alisema.

Kamanda Muroto aliitaja sababu nyingine ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kwamba anadaiwa kuharibu …
Hiyo ndo dawa kwa mijitu yenye roho mbaya Kama huyo mwalimu.
 
tujifunze kusikiliza na upande wa pili, na pia kuiachia mahakama kazi ya kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria, hii tabia ya watanzania kujichukulia sheria mkononi ndio imepelea nchi kuzalisha rais ambaye anaona katiba na sheria vinamchelewesha na anaagiza polisi wanaovunja sheria na kufanya uharifu dhidi ya binadamu wapandishwe vyeo!! akili kama hizi zinaanzia huko mitaani na haziibukii tu ikulu kwa bahati mbaya.
Embu tupatie story ya upande wa pili ili story I balance.
 
tujifunze kusikiliza na upande wa pili, na pia kuiachia mahakama kazi ya kutoa hukumu kwa mujibu wa sheria, hii tabia ya watanzania kujichukulia sheria mkononi ndio imepelea nchi kuzalisha rais ambaye anaona katiba na sheria vinamchelewesha na anaagiza polisi wanaovunja sheria na kufanya uharifu dhidi ya binadamu wapandishwe vyeo!! akili kama hizi zinaanzia huko mitaani na haziibukii tu ikulu kwa bahati mbaya.
Kweli mkuu,umeona mbaali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashauri akitoka huko ahame Jiji na sijui ni mji gani watampokea labda arudi kijijini kwao
 
Mwajili wake inabidi amchukulie hatua. Wazazi wanajiuliza watoto wao wako katika hali gani huko shuleni
 
Kweli kuna watu wana roho ngumu aisee, hapo si ajabu hata hiyo mimba aliipata kwa kubaka.
Najaribu kuvaa uhusika wa huyo dada, nashindwa kbs kupata picha ya alivyokuwa akjisikia wkt anasikia mtoto wake analia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama nilivyotumiwa
Ukhty leo nina mkasa nimeukuta hospitali ya mkoa wa Dodoma nilienda kusalimia wagonjwa,nikakuta binti wa kazi amelazwa kapigwa na boss wake mpaka kamjeruhi kisa alichelewa kuamka kumchemshia maji ya kuoga huyo mama ambae ni mwalimu wa shule ya msingi Mlimwa C iliyopo hapa mjini Dodoma.

Binti anaonekana kidogo ana matatizo ya akili japo anajielewa vizuri,alipata ujauzito boss wake akamwambia asiseme kwa yeyote kama ana mimba,mpaka kajifungua kamwambia asiwaambie hata majirani kama ana mtoto kwani hapo hakuja kuzaa bali alikuja kumlelea watoto wake.

Kwa hiyo huyo mtoto akawa anamfungia kwenye kabati lake la nguo huyo boss ili majirani wasisikie sauti ya mtoto kwa muda wa miezi mitano hadi Jana alipompiga hadi akazimia ndio siri ikagundulika.

Binti yupo Hospitali na mwanae,hali ya hako katoto ni ngumu mno,ukiambiwa ana miezi mitano huwezi kuamini.

Kwa kweli nimeumia hadi nimelia, sijaamini sisi wanawake kama ni wakatili kwa kiwango hiki.
Mwalimu ni huyo hapo Mayasa?? Liangalie kwanza...! Ukute hiyo mimba ni ya mtoto wake ama mdogo wake anayeishi naye ndio maana alitaka kupotezea..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom