Mkasa wa kusikitisha Dodoma: Msaidizi wa kazi anyanyaswa na mwajiri wake, mtoto wake mchanga afungiwa ndani ya kabati kwa miezi 6

Chipukizi

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
2,884
2,000
Kama nilivyotumiwa
Ukhty leo nina mkasa nimeukuta hospitali ya mkoa wa Dodoma nilienda kusalimia wagonjwa,nikakuta binti wa kazi amelazwa kapigwa na boss wake mpaka kamjeruhi kisa alichelewa kuamka kumchemshia maji ya kuoga huyo mama ambae ni mwalimu wa shule ya msingi Mlimwa C iliyopo hapa mjini Dodoma.

Binti anaonekana kidogo ana matatizo ya akili japo anajielewa vizuri,alipata ujauzito boss wake akamwambia asiseme kwa yeyote kama ana mimba,mpaka kajifungua kamwambia asiwaambie hata majirani kama ana mtoto kwani hapo hakuja kuzaa bali alikuja kumlelea watoto wake.

Kwa hiyo huyo mtoto akawa anamfungia kwenye kabati lake la nguo huyo boss ili majirani wasisikie sauti ya mtoto kwa muda wa miezi mitano hadi Jana alipompiga hadi akazimia ndio siri ikagundulika.

Binti yupo Hospitali na mwanae,hali ya hako katoto ni ngumu mno,ukiambiwa ana miezi mitano huwezi kuamini.

Kwa kweli nimeumia hadi nimelia, sijaamini sisi wanawake kama ni wakatili kwa kiwango hiki.
 

Attachments

 • IMG-20181230-WA0006.jpg
  File size
  98 KB
  Views
  120
 • IMG-20181230-WA0007.jpg
  File size
  176.8 KB
  Views
  115
 • File size
  1.3 MB
  Views
  50

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,809
2,000
Hii sura inaonekana ameishawahi kuuwa maana linatishaa
Sura ya muuwaji inajulikana kwa kuangalia tu
Ukatili gani huo wa kufungia kichanga kabatini jamani.
Huyu achunguzwe ni psycho
Na huyo msichana masikini hana ugonjwa wowote wa akili bali ni mfadhaiko wa yaliyomkuta tu

Sent from my SM using Tapatalk
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Dec 14, 2018
2,182
2,000
Wanawake kweli mnafanya hayo
Kama nilivyotumiwa
Ukhty Leo Nina mkasa nimeukuta hospitali ya mkoa wa Dodoma nilienda kusalimia wagonjwa,nikakuta binti wa kazi amelazwa kapigwa na boss wake mpk kamjeruhi,,,kisa alichelewa kuamka kumchemshia maji ya kuoga huyo mama ambae ni mwalimu wa shule ya msingi mlimwa C iliyopo hapa mjini Dodoma. Binti anaonekana kidogo anamatatizo ya akili japo anajielewa vzr,alipata ujauzito boss wake akamwambia asiseme kwa yeyote km ana mimba,mpk kajifungua kamwambia asiwaambie ht majirani km ana mtoto kwan hapo hakuja kuzaa bali alikuja kumlelea watoto wake,kwahiyo huyo mtoto akawa anamfungia kweny kabat lake la nguo huyo boss ili majiran wasisikie sauti ya mtoto kwa muda wa miezi mitano had Jana alipompiga had akazimia ndo siri ikagundulika,,binti yupo Hosp na mwanae,hali ya hako katoto ni ngumu mnoooo,ukiambiwa anamiez mitano huwezi kuamini,kwakweli nimeumia had nimeliaaaa,,,sijaamini sisi wanawake km ni wakatili kwa kiwango hiki,nimeumia mnooo km utaona yafaa peleka kwa group wamama wengine waone unyama huu na wenye roho za kiuaji km hizi waache tafadhari

Sent using Jamii Forums mobile app
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
42,740
2,000
Haha mama taaluma yake ni mwalimu " ... anatufundishia watoto wetu " Ambao tunatarajia kupitia mafundisho yake " watakuja kuwa ni watoto bora walio elimika staarabika na ndio mfano bora wa baadae wakuigwa katika jamii (refer watoto ni taifa la kesho )

So kwa huu unyama alio utenda kwa huyo dada wa kazi " Ni wazi ya kwamba kuna haja ya sisi kuwatizama watoto wanaofundishwa na huyo mwalimu kuwa ni wahanga " wakuu wanao athirika kwa tabia mbovu za huyo mama " akiendelea kuacha basi tutaraji kujua kuwa na kizazi cha jamii iliyojaza wana taaluma mbali mbali wenye roho katili kama yake "

zinazo pelekea watoto wetu kuiga tabia zake mbovu za unyanyapaa na manyanyaso " Tabia ambazo huja kuchochea taifa letu kuja kuwa na kizazi cha watu katili waliokosa utu nastaha katika Jamie yetu " (kama jiwe)
Jamii yetu inamtambua mwalimu kuwa nimlezi wa pili baada ya mzazi " so tunataraji kuwa na kizazi cha namna gani hapo baadae" ikiwa mlezi huyu tuliye mkabidhi mamlaka ya kuwaelimisha watoto wetu maisha yake yamezungukwa na tabia hizi korofi zilizo kosa Utu " ...

Huyo hafai hata kuwa mwalimu tena kwa sababu watoto wetu watakuwa ni wahanga wa tabia zake so anapaswa kufukuzwa kazi na kuwajibishwa kisheria " ili iwe fundisho kwa wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
42,740
2,000
Hii sura inaonekana ameishawahi kuuwa huyu maana linatishaa
Sura ya muuwaji zinajulikana kwa kuangalia tu
Ukatili gani huo wa kufungia kichanga kabatini jamani.
Huyu achunguzwe ni psycho
Na huyo msichana masikini hana ugonjwa wowote wa akili bali ni mfadhaiko wa yaliyomkuta tu

Sent from my SM using Tapatalk
Hahaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom