#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

BAADA YA RUFAA KUWA YA DANADANA SANA: KITU KILICHOMJIA MHUSIKA KICHWANI KWA SABABU NA YEYE PIA NI BINADAMU SIYO MUNGU

Ikumbukwe kuwa mnamo mwaka 2006, dada yake na mhusika aliwahi kufika huku Dar es salaam akitokea mkoani, akiwa ana mtoto ambaye alikuwa na tatizo la moyo. Mtoto huyo alikuwa amepewa rufaa kutoka kwenye hospitali ya mtu binafsi tu na rufaa hiyo ilimleta kwenye hospitali ya mtu binafsi mwingine tena. Maelezo kamili kuhusiana na mtoto huyu, mhusika alishawahi kuyaleta humu jukwaani siku nyingi nyuma kupitia kwenye post hii hapa #189

Mtoto huyu hakuweza kufanikiwa kupona na ilipofika Septemba 2006, mtoto alipoteza maisha

Baada ya danadana ya rufaa ya safari hii kutokea, mhusika alipata mawazo kuwa pengine inabidi awaeleze wamlete tu mtoto bila rufaa kwa sababu kuendelea kusubiri rufaa iliyokuwa ya danadana, kungeweza kupelekea mtoto hyuo kupata matatizo zaidi.

Baada ya mhusika kuwa amefikiria hivyo, akakumbuka tena swala la mtoto kwenye post hii hapa #189 na kugundua kuwa kwa kufanya hivyo, LIABILITY ya usalama wa mtoto, angei-transfer kutoka kwa mtaalamu aliyetakiwa kuandika na kutoa rufaa hiyo na angeileta kwake yeye (mhusika) mwenyewe; LIABILITUY kutoka kwa MTAALAMU kwenda kwa LAYMAN

Baada ya mhusika kujikagua kila mahali ambapo huwa anakuwa yupo, akakumbuka pia kuwa Serikali ya Mama ipo pale mlangoni ofisini kwake imejaa tele; ipo pia mlangoni nyumbani kwake napo imejaa tele, na ipo kila mahali kama hewa.

Hayupo mtu mwoga duniani, kama mhusika na hiki kitu ndiyo mara zote huwa ananitia aibu sana mimi. Huwa siipendi kabisa tabia yake hiyo ya uoga wa namna hiyo

Baada ya kugundua hilo, mhusika alipiga simu nyumbani kwao akimweleza mdogo wake (ambaye ni mama wa mtoto) kuwa ni muhimu sana kwamba inabidi asubiri rufaa ya daktari, hata kama itachukua mwezi mzima

Mama mtoto aliendelea kusubiri rufaa hiyo na ilipofika J5 wiki hii kwa bahati nzuri alifanikiwa kuipata

UP NEXT

MPANGO WA USAFIRI ALIOKUWA AMEUNDAA MHUSIKA BAADA YA KUSIKIA KUWA MTOTO ANAUMWA NA ANATAKIWA ALETWE DAR ES SALAAM


Ni usafiri wa ndege, ila mara zote alikuwa anaongelea usafiri wa Basi ambao mabasi yake huwa yanaingia saa 6 usiku hapa Da es Salaam

……………..inaendelea
 
MPANGO WA USAFIRI ALIOKUWA AMEUNDAA MHUSIKA TOKA AWALI

Kilichokuwa kinampa bashasha mhusika kuhusiana na mtoto huyu ni kwamba alikuwa anatamani sana akutane naye hapa Dar es salaam akiwa bado katika hali ambayo ni in-stu; yaani kabla hajakutana na tiba nyingine ya aina yoyote ile katika sekunde zake za mwanzo kabisa za kuwasili kwake Dar es Salaam

Kwa usafiri wa Basi, isingekuwa rahisi kwa mhusika kufanya observation hii kwa sababu mtoto angeweza akazidiwa usiku baada ya kuwasili na kupelekea kupokea tiba mbadala kabla haijafika asubuhi

Kwa hiyo mhusika aliandaa plan ya usafiri wa ndege ila plan hiyo akawa ameifadhi rohoni kwake kama siri yake. Zaidi alimwelekeza mama wa mtoto kuwa atakapokuwa amepewa rufaa, asikate kwanza tiketi ya Basi kwa sababu kuna uwezekano wa kusafiri bure na gari ambalo liko huko Mwanza ambalo lina mpango wa kuja Dar es Salaam, kitu ambacho kilikuwa ni uongo

Mamtakiwa ajiandae kesho yake kwa ajili ya a wa mtoto alipopata rufaa J5, mhusika alimpa taarifa kwamba anatakiwa ajiandae kwa ajili ya usafiri wa ndege na si wa Basi

J5 hiyo mhusika alifika ofisi za ATCL Mlimani City na kufanikiwa kupata nafasi mbili za ndege ya saa mbili asubuhi

Mhusika alimjulisha mama wa mtoto kuwa takuwepo Airport kwa ajili ya kuwapoke

Ilipofika jioni saa moja; mhusika alibadilisha taarifa na kumjulisha mama wa mtoto kuwa hatakuwepo Airport

Hapo ililkuwa ni baada ya kuwa ameona pilika pilika za akina MR X J5 hiyo alipokuwa bado yupo ofisini na ambazo maelezo yake alikuja kuyatoa jioni hiyo kwenye post hii hapa #992

J5 mhusika alifika Aitport saa 3:10 asubuhi na ndege iliingia nusu saa baadaye na alimuona mtoto akiwa kwenye hali ambayo ni in-stu, kama alivyotamani tangu mwanzo

…………………..itaendelea
 
KUHUSIANA NA “SPECIALIST”………

TUKIO LA KWANZA KABISA LA MSIBA AMBALO MHUSIKA ALIWAHI KUHUDHURIA MAENEO JIRANI NA OFISINI KWAKE, NA PIA JIRANI NA MAHALI PALE ANAPOISHI YEYE NA KUKUTANA NA WATU WATATU TU ALIOWAFAHAMU; KWENYE MSIBA HUO


Ukiondoa tukio la msiba wa idarani kwake na mhusika ambalo aliwahi kuleta taarifa zake humu na lililotokea mwaka 2020; na ambalo mhusika alijulishwa taarifa zake na Kaimu Mkuu wa Idara (ambaye kwa sasa ndiye Mkuu wa Idara), kuna tukio jingine la aina hiyo ambalo tayari mhusika alikuwa ameshalishuhudia hapo kabla (nadhani mwishoni mwa mwaka 2016 au mwanzoni mwa mwaka 2017)

Kwa hiyo tukio hili la idarani kwake na mhusika LILIKUWA NI LA PILI, na lilishahibiana kwa kiasi na lile la kwanza la lililotokea nyumbani kwake na “SPECIALIST”; ila kwa wakati huo mhusika hakutaka kuuongelea mfanano wa matukio haya; ISIPOKUWA ALILLAZIMKA TU KULIONGELEA LILE LA IDARANI KWAKE (LA PILI) na kuliacha lile la “SPECIALIST” (LA KWANZA) baada ya kuwa ameona kwa mara nyingine tena kuwa hata lile la idarani nalo pia lilikuwa na namna ya mbinu fulani (tricks) hivi ambazo zilikuwa zimekusudiwa maalumu kwa ajili yake mhusika na zilizoshahibiana kwa namna fulani na za tukio lile la kwanza

NAMNA MHUSIKA ALIVYOTOKEA KUPATA TAARIFA ZA KILA MSIBA KWA MISIBA HII

Taarifa za tukio la msiba wa idarani kwake mhusika alizipata SIKU YA IJUMAA akiwa kwenye korido baada ya saa 6 mchana; maeneo ya ofisini. Ilikuwa ni baada ya kuwa amemaliza darasa alilokuwa nalo siku hiyo. Mhusika alijulishwa kuwa msiba wenyewe ulikuwa maeneo ya karibu kabisa na ofisini, nyumbani kwa mfiwa na ambapo pia ni jirani kabisa na mahali pale anapoishi mhusika.

TUKIO LA KWANZA LINALOFANANA NA HILO AMBALO MHUSIKA ALIKUWA TAYARI AMESHAKUMBANA NALO HAPO KABLA

Tukio la kwanza kabisa la namna hiyo mhusika aliwahi tayari ameshakumbana nalo kwa mara ya kwanza, nyumbani kwa “SPECIALIST”; hili la idarani kwake, lilikuwa la pili

Kwenye tukio la kwanza, mhusika hakupata taarifa kutoka kwa “SPECIALIST’ mwenyewe bali kwa binti msaidizi wake wa ofisini ambaye kwa bahati tu walikutana nje ya Ofisi ya Mkuu wa Idara ofisini kwa mhusika

  • Binti huyu alikuwa amefika ofisini pale kwa shida za kiofisi na wakati wanabahatika kukutana na mhusika, binti alikuwa tayari yuko njia moja anarudi ofisini kwake
  • Baada ya kusalimiana na mhusika, mhusika alimpa pia binti salaam za swahiba wake “SPECIALIST” ili amfikishie
  • Pale ndiyo binti alipomjulisha mhusika kuwa “SPECIALIST” hakuwepo ofisini kwake siku hiyo bali nyumbani kwa sababu alikuwa amepata msiba mkubwa. Siku hiyo ilikuwa ni SIKU YA IJUMAA wakiwa kwenye veranda iliyo mbele ya ofisi ya Mkuu wa Idara
Ilipofika kesho yake Jumamosi, mhusika aliamua kwenda kuhani msiba nyumbani kwake na “SPECIALIST”

Pamoja na kuwa ilikuwa ni Jumamosi, mhusika alikaa pale nyumbani kwa takribani masaa mawili, na katika muda wote wote huo watu pekee aliowaona na kuwafahamu msibani pale walikuwa ni watatu tu

  • “SPECIALIST” mwenyewe
  • Injinia mmoja kutoka miliki za nyumba ambaye alikuwa anasimamia ukarabati wa nyumba anayoishi “SPECIALIST”
  • Bwana Afya wa taasisi anayofanyia kazi mhusika
Hapakuwa na office-mate yeyote wa “SPECIALIST” kwenye msiba huo; yaani wale ambao anafanya nao kazi idara moja, hawakuwepo hata mmoja

Hawa office-mates wa “SPECIALIST” majority yake mhusika anawafahamu kutokana na interactions nao za kipindi kirefu kiasi cha takribani miezi mitatu; ambazo mhusika aliwahi kuwa nazo na wafanyakazi hao mwaka 2008.

Kwa hiyo walio wengi wa wafanyakazi wa idara hiyo mhusika anafahamiana nao na baadhi yake wamekuwa pia ni majirani zake kwenye mazingira ya makazi ya taasisi ambamo mhusika bado anaishi mpaka leo

Mfanano unaotokea hapa ni kwamba, kwenye matukio haya mawili; ni kwamba katika kila tukio

  • Mhusika alikuwa anapata taarifa za uwepo wa kila msiba, SIKU ZA IJUMAA aidha akiwa kwenye korido au kwenye veranda
  • Matukio yote mawaili yalitokea maeneo jirani kabisa na ofisini kwa mhusika na pia jirani na sehemu ya makazi yake
  • Taarifa zilizokuwa zinafikishwa kwa mhusika zilikuwa ni “second hand” kwa maana kuwa waliokuwa wanamjulisha mhusika kuhusiana na uwepo wa msiba walikuwa ni watu wengine na si wahusika wa msiba wenyewe pamoja na kwamba mawasiliano yake ya simu walikuwa wanayo
  • Bila kujali ukubwa wa msiba uliokuwa umetokea, kwenye msiba wa kwanza (2016/2017) alikutana na watu watatu aliowafahamu na ambao amewataja hapo juu
  • Vile vile, bila kujali ukubwa wa msiba uliokuwa umetokea, kwenye msiba wa PILI (2020) napo alikutana pia na watu watatu tu aliowafahamu. Hawa walikuwa ni jirani yake na mhusika pamoja na mke wake, pamoja na mama mwenye nyumba ambaye mume wake ndiyo alikuwa mfiwa
Staff-mates wengine wote kutoka idarani kwa mhusika hawakuwepo msibani, na mhusika aliondoka ofisini hai hai siku hiyo akiacha ofisi karibia zote zikiwa zimefungwa; huku akidhani kuwa wenzake wote watakuwa walikuwa wametangulia kwenye msiba kwa sababu yeye alikuwa amecchelewa kupata taarifa; alizipata siku hiyo hiyo

Siku hiyo, alipokuwa yupo nje kwenye parking za gari akiwa anajiandaa kuelekea msibani, pale ndiyo alibahatika kumuona SENIOR MSTAAFU WA KIUME (SMME), na akiwa anajiandaa kuwasha gari aondoke, na ndiye mtu pekee aliyekuwa amebaki ndani ya jengo muda huo, ukiondoa mhusika mwenyewe

  • Baada ya kumuona SMME, mhusika alidhani kuwa SMME naye alikuwa yuko njia moja kuelekea msibani kwa sababu ndiyo mtu pekee ambaye alikuwa ameabakia idarani siku hiyo
  • Baada ya kufika msibani, mhusika hakumkuta SMME
Aidha mhusika hakumkuta mtu mwingine yeyote yule kutoka idarani kwake, na wakati huo huo watu wote ofisini hawakuwepo wakati anaondoka idarani. Ofisi zote zilikuwa zimefungwa

Kabla hajaondoka ofisini siku hiyo, mhusika alikagua kwanza floor zote na alijiridhisha kuwa watu wote hawakuwepo idarani na alipotoka nje ndiyo alimuona SMME tu na hapo ndipo alipogundua kuwa huyo ndiyo alikuwa mtu pekee ambaye naye alikuwa amebakia ndani ya jengo muda huo

HITIMISHO

Tukirudi kwenye tukio hili la “SPECIALIST”, office mates wote kutoka idarani kwa “SPECIALIST”, hawakuwepo kwenye msiba huo, isipokuwa staff-mates hao wawili tu mhusika aliowataja hapo juu ikiwa ni pamoja na “SPECIALIST” mwenyewe ambaye ndiye aliyekuwa mfiwa

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE: MONNDAY 16TH MAY 2022

DOCUMENTS MUHIMU ZA MTOTO ALIYEPEWA RUFAA, MHUSIKA NAYE ANAZO PIA.
 
UPDATE: TUESDAY 17TH MAY 2022

FUNDI WA AC ARUDI TENA OFISINI KWA MHUSIKA AKIWA YUKO PEKE YAKE


Fundi wa AC amerudi tena ofisini kwa mhusika akiwa tena yuko peke yake. Kabla hajaja, kuna mtu alifika ofisini kwa mhusika kwanza, walikuwa wameambatana na mwingine wa pili isipokuwa yule wa pili hakuingia ofisini kwa mhusika; alidivert na kuingia ofisi nyingine, alikuwa kama msindikizaji

Huyu wa pili yeye alikuwa anatembea akiwa nyuma; nadhani ilikuwa ni kumkinga kwa nyuma na Kamera yule aliyekuwa mbele iliyopo kwenye korido ili asiweze kuonekana vizuri na Kamera kuwa alikuwa ni nani

  • Aliyekuwa mbele ni yule mfanyakazi mgeni ambaye mhusika hajawahi kutambulishwa kwake
  • Aliyekuwa nyuma akiwa amemkinga mfanyakazi mgeni ni yule mfanyakazi mwenyeji aliyehamia kutoka Dodoma, na ambaye Mkuu wa Idara na mhusika waliongozana kuelekea ofisini kwake siku kadhaa zilizopita kwa ajili kujadili swala la matengenezo ya AC
AC bado haijatengenezwa mpaka muda, na possi ly ndiy kitu ambacho kilikuwa kimelmleta tena fundi huyu.

Kwa bahati mbaya mhusika tayari alishamwogopa mno na hakumruhusu kabisa kuingia ofisini kwake

Details zaidi zitawajia kesho
 
UPDATE: WEDNESDAY 18TH MAY 2022

FUNDI WA AC AWASILI TENA OFISINI KWA MHUSIKA AKIWA YUKO PEKE YAKE

…………inaendelea

MAELEZO YA UTANGULIZI


Itakumbukwa kuwA siku kadhaa nyuma, mhusika aliwahi kulete taarifa kuwa Mkuu wa Idara (MWI) hakuwepo idarani na ilikuwa haijulikani alienda wapi kwa sababu hapakuwa na official notice iliyotoa maelezo ya wapi alipokuwa ameenda. Aidha ilikuwa haijulikani pia ni nani alikuwa anakaimu nafasi yake katika kipindi chote hicho ambacho MWI hakuwepo idarani.

Hata hivyo J3 ya wiki hii tarehe 16/05/2022; kwa mara ya kwanza ndiyo MWI alionekana tena idarani; na pia walibahatika kugongana na mhusika kwenye korido/veranda na kusalimiana

Kwenye siku kadhaa ambazo MWI hakuwepo idarani, kwenye mojawapo ya siku hizo Katibu Muhtasi wa MWI (KMMWI) alibahatika kufika ofisini kwa mhusika akiwa na wafanyakazi wageni wawili ambao aliwatambulisha kwa mhusika. Mmojawapo wa wageni hao alikuwa yuko destined kwenye idara nyingine; ila kwa wakati huo, alikuwa tayari ameshakuwepo kwenye idarani hii husika kwa cha siku kadhaa, kwa hiyo alikuwa tayari ameshakuwa mwenyeji angalau kwa siku kadhaa

Baada ya siku hiyo, mfanyakazi huyu mgeni ambaye alikuwa ameshaanza kuwa mwenyeji, hakuonekana tena idarani na alibaki yule mwingine mmoja na ambaye ndiyo yupo idarani mpaka muda huu

Siku wafanyakazi hawa wageni wanaletwa na KMMWI kuja kutambulishwa ofisini kwa mhusika

  • Yule ambaye kwa sasa hayupo na ambaye alikuwa destined kwenye idara nyingine, alikuwa tayari ameshaonekana kwa wiki chache idarani, isipokuwa alikuwa hajawahi kutambulishwa
  • Yule ambaye kwa sasa yupo idarani, ndiyo alikuwa mgeni kabisa na ilikuwa ni mara yake ya kwanza kabisa kuonekana idarani siku hiyo ya utambulisho
  • Kwa hiyo wa pili na ambaye yupo hadi sasa, ndiyo alikuwa mgeni kabisa machoni pa mhusika, wakati yule ambaye tayari ameshaondoka, alikuwa ameshakuwa familiar machoni pa mhusika, isipokuwa tu alikuwa hajawahi kutambulishwa kama mmojawapo wa wafanyakazi idarani
Hilo likapita

KILICHOTOKEA MCHANA JANA SIKU YA J4 TAREHE 17 MEI 2022 BAADA YA MWI KUWA AMESHARUDI OFISINI

Asubuhi yake mhusika alikuwa na pilikapilika na alijaribu kupita hapa na pale kwenye baadhi ya Benki na maduka zilizopo/ yaliyopo Mlimani City

Baada ya hapo alirudi ofisini akipitia nyumbani kwake kwanza

Akiwa yupo ofisini kwake, kwenye mida ya around saa 7 hivi, aliwaona watu wawili wakiwa kwenye korido wakiwa wanaonyesha kama kuja pale alipokuwa amekaa ofisini kwake. Watu hawa walikuwa wametangulizana, mmoja mbele (slim/ slender and a bit short) na mwingine (a bit tough and taller than the slim guy) alikuwa nyuma. Configuration hii ya namna walivyokuwa wanatembea kwenye korido, ilikuwa inapelekea yule wa nyuma kum-cover wa mbele; kiasi kwamba kwa kuwaangalia kutokea nyuma yao, mtu asingeweza kumuona yule aliyekuwa ametangulia mbele isipokuwa yule wa nyuma tu. Yule aliyekuwa mbele muonekanao wake ulikuwa unamezwa na yule aliyekuwa anamfuata kwa nyuma

Kule nyuma walikokuwa wanatokea watu hawa wawili, ndiyo kuna ile Kamera inayomulika kwenye korido inayoelekea ofisini kwa mhusika, na kwa wakati huo mlango wa ofisi ya mhusika ulikuwa wazi kwa sababu bado hajafanikiwa kupata AC inayofanya kazi

…………….inaendelea
 
…………….inaendelea

KILICHOTOKEA MCHANA JANA SIKU YA J4 TAREHE 17 MEI 2022 BAADA YA MWI KUWA AMESHARUDI OFISINI


Watu hawa wawili walivyokaribia ofisini kwa mhusika, aliyekuwa mbele alisogea kidogo anataka kuingia ofisini kwa mhusika halafu akarudi nyuma na kuingia kwenye ofisi nyingine jirani.

Mhusika hakumbuki ni ofisi ipi. Yule wa pili (aliyekuwa anatembea akiwa nyuma ya mwenzake) naye vile vile aliingia kwenye ofisi nyingine. Ni kwa sababu walimkuta mhusika akiwa anongea na simu.

Hatua hii ilikusudiwa kumjenga mhusika kisaikolojia kuwa mtu huyo atarudi baadaye ofisini kwake

Mpaka hapo wote wawili wakawa wamepotea kwenye korido

BAADA YA DAKIKA KDHAA KUPITA, TAKRIBANI KAMA NUSU SAA

Yule wa pili aliyekuwa anatembea akiwa mbele ya mwenzake, akawa ameibukia tena ofisini kwa mhusika akitokea ofisi jirani tu na ile ya mhsiika, na safari hii alifanikiwa kuingia ofisini kwa mhusika kwa sababu mhusika alikuwa haongei na simu tena

Ikumbukwe kuwa huyu ndiye yule mgeni ambaye hajawahi kutambulishwa na kiongozi yeyote yule pale idarani, na ndiye mgeni ambaye taaarifa zake ziliwajieni hivi humu jukwaani; siku kadhaa zilizopita

Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kabisa mtu huyu kuingia ofisini kwa mhusika

Hata hivyo, ilikuwa ni mara ya pili kwa mhusika kumuona mtu huyu akiwa kwenye sakafu ya korido hiyo ofisi ya mhusika ilipo. Ni kwa sababu kabla ya hapo, ni mara moja tu mhusika alikuwa amewahi kumona mtu huyu akiwa kwenye korido ya sakafu hiyo



BAADA YA KUINGIA OFISINI KWA MHUSIKA

Mtu huyu alidai kuwa anapita kwa ajili ya zoezi la stock taking ya vifaa ambavyo ni vibovu, kama vipo

Mhusika alimuonyesha mgeni huyu Analogue Seimograph moja tu (kifaa cha zamani kabisa cha kurekodia data za matetemeko ya ardhi) ambacho ndiyo ifaa pekee kibovu kilichopo ofisini kwake hadi muda huu

Hata hivyo kwa upande wake, mhusika hana tatizo kabisa na sababu zilizopelekea mgeni huyu kuonekana ofisini kwake (mhusika) isipokuwa ana tatizo na ule mchakato alioupitia mgeni huyu hadi kufikia hatua ya kuingia ofisini kwa mhusika

HITIMISHO

BAADA YA KUPITA TAKRIBANI SAA MOJA TENA


  • Fundi wa AC naye sasa ndiyo aliingia
  • Kwa bahati nzuri fundi huyu yeye alifanikiwa kumkuta mhusika anamalizia maongezi na simu nyingine
  • Akiwa bado yupo kwenye korido amekaribia kabisa karibu na mlango wa ofisi ya mhusika; mhusika alimshauri fundi arudi asiingie ofisini kwake na kwa bahati nzuri fundi huyu aliupokea ushauri huo bila tatizo lolote na hivyo muda huo huo kuanza kurudi kule alikokuwa ametokea
MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE: FRIDAY 20 MAY 2022

FUNDI WA AC ARUDI TENA OFISINI KWENYE JENGO ILIMO OFISI YA MHUSIKA NA KUBANA CHOONI KWA KIFICHO


Mhusika alimkuta fundi huyu akiwa amesimama kwenye washrooms za ground floor huku akiwa ameelekeza kisogo kwenye mlango wa kuingilia kwenye washrooms hizo. Kwa hiyo alikuwa amesimama katika namna ambayo ilikuwa inaonyesha kama alikuwa amejibanza

ILIKUWA JANA ALHAMIS SAA TISA KAMILI. KWA HIYO JANA SAA TISA KAMILI FUNDI HUYU ALIKUWA VYOO VYA GROUND FLOOR ZA JENGO ILIMO OFISI YA MHUSIKA

Baada ya mhusika kumuona, hakuingia kwenye washrooms hizo; aligeuza na kuelekea juu kwenye washrooms zilizoko floor ya pili

Details zaidi kuhusiana na fundi huyu zitawajieni muda siyo mrefu. Zaidi kwa sasa ni kuwa kuna watu wawili au watatu walikuja na kukaa kwenye ofisi jirani na ile ya mhusika, na wakati mhusika anatoka ofisini kwake kuelekea washrooms, watu hao walikuweno ofisini humo. Chances kubwa ni kwamba funguo za ofisi hiyo walipewa na huyu mfanyakazi aliyehamia kutoka Dodoma kwa sababu ni watu wawili tu ambao huwa wanamiliki funguo za ofisi; MR X pamoja na huyo bwana.


 
FUNDI WA AC AONEKANA TENA NDANI YA JENGO ILIMO OFISI YA MHUSIKA AKIWA KWENYE POSE YA AINA FULANI YA KIFICHO:

MACHACHE YALIYOJIRI KABLA YA FUNDI HUYU KUONEKANA TENA NDANI YA JINGO SIKU HIYO


  • Asubuhi siku hiyo (Alhamis ya tarehe 19/05/2022), mfanyakazi mgeni ambaye hajawahi kutambulishwa, alifika tena ofisini kwa mhusika
  • Safari hii ilikuwa sasa ni mara yake ya pili kuingia ofisini kwa mhusika
  • Mara ya kwanza ofisa huyu kuingia ofisini kwa mhusika ilikuwa ni kwenye siku ile ambayo alifika akiwa anafanya stock taking ya vifaa vibovu na kufanikiwa kurekodi kifaa kimoja cha kupimia matetemeko ya ardhi kinachojulikana kama seismograph au seismometer
Kwa hiyo Alhamisi ya wiki hii mfanyakazi huyu alifika tena ofisi kwa mhusika na safari hii alimjulisha mhusika kuwa alikuwa anapita kumsalimia tu. Mhusika alimshukuru kwa salaam hizo na alifurahi pia kumuona ofisini kwake kwa mara nyingine. Hapo sasa ilikuwa ni asubuhi mida ya kabla ya saa sita mchana

Baadaye kwenye mida ya baada ya saa 7 mchana, mhusika aliona watu watatu wakiingia kwenye chumba jirani na ilipo ofisi yake na ambao walionekana kuwa ni wanafanuzi

  • Watu hawa walikuja wakiwa na funguo ambazo walikuwa wamepewa na walifungua chumba hicho na kuingia ndani na kukaa humo wakiwa wanaendelea na kazi zao
  • Kawaida funguo hizo huwa wanakuwa nazo watu wawili tu ambao mmoja wao ni huyu mfanyakazi aliyehamia kutoka Dpodoma na ambaye taarifa zake zimekuwa ziki-trende humu kwa siku kadhaa sasa
  • Wanafunzi hawa waliingia na kukaa humo tangu kuanzia muda huo hadi mhusika alipoamua kutoka ofisini kwake akielekea washroom zilizopo grond floor
Akiwa anajiandaa kuingia ndani ya washrooms hizo huku mlango wake ukiwa umeachwa wazi kidogo, kabla ya kuingia aligongana na kisogo cha mtu aliyekuwa amekiekeza kwenye mlango wa kuingilia humo

Mhusika alimtambua mtu huyu kupitia kisogoni, kuwa ndiyo yule fundi wa AC

Fundi huyu alikuwa kwenye pose ambayo mhusika hata hakuweza kufahamu alikuwa anafanya nini humo washroom kwa wakati huo kwa sababu alikuwa haonyeshi hata dalili kuwa pengine alikuwa ni mtu aliyekuwa amemaliza kujisadia

Mhusika na fundi wala hawakuonana uso kwa uso, bali ni mhusika alimuona tu fundi na kuamua kutoingia ndani na kugeuza akielekea sehemu nyingine

Baada ya kumtambua fundi wa AC, mhusika aliamua kupandisha juu kwenye washrooms zilizoko sakafu ya pili, na baada ya hapo, alipitia chumba cha chai na kusabahiana na kundi la baadhi ya wafanyakazi wenzake kadhaa waliokuwa wamekusanyika kwenye chumba cha chai kwa ajili ya lunch ya siku hiyo.

Lunch hii ilikuwa imechelewa kidogo kwa sababu muda ulikuwa ni saa 9:00 kamili alasiri wakati kundi lililokuwa linapata lunch muda huo lilikuwa ni kubwa kiasi; kuonyesha kuwa ni watu wengi walikuwa wamechelewa kupata lunch yao siku hiyo

Hiyo ilikuwa ni jana Alhamis tarehe 19/05/2022 ambapo fundi wa AC alikuwa chooni muda wa saa 9:00 kamili mchana

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE: MONDAY 30 MAY 2022

ACCIDENTS, COINCIDENCES OR A PATTERN:

MFANANO WA KIPEKEE WA NAMBA ZA GARI LA MHUSIKA (TARAKIMU PEKEE) NA ZILE ZA LILE LA JIRANI YAKE ALIYEWAHI KUHAMIA KWENYE BLOCK LA MHUSIKA MWAKA 2012


  • Namba za gari la mhusika (tarakimu zake na siyo herufi zake) tuseme ni PAS, herufi hizi zote zikiwa zinawakilisha tarakimu ambazo zimefichwa zilizo kati ya 1 na 9
  • Wakati huo huo namba za gari la jirani yake (tarakimu zake na siyo herufi zake) zenyewe ni SPA, herufi hizi zote nazo pia zikiwa zinawakilisha tarakimu zilizofichwa ambazo ziko kati ya 1 na 9
  • Kwa hiyo kati ya tarakimu zile tatu zilizopo kwenye plate namba ya gari la mhusika, ukichukua tarakimu ile ya mwisho pekee (au ya tatu) ukaihamisha na kuiweka mwanzoni, unapata exactly namba za gari la jirani yake
  • Kwa maana nyingine ni kuwa ukichukua tarakimu ya kwanza ya gari la jirani ukaihamisha na kuiweka mwishoni (kwenye nafasi ya tatu) unapata exactly namba za gari la mhusika
  • Kwa hiyo tarakimu tatu zilizoko kwenye plate namba za magari haya mawili, zote zinafanana isipokuwa zinatofautiana mpangilio tu kama ilivyoelezwa hapo juu
  • Kwenye gari moja tarakimu ya tatu ni ya kwanza, na kwenye gari nyingine tarakimu ya kwanza ni ya tatu; A RARE COINCIDENCE?
  • Jirani alihamia kwenye block la mhusika mwaka 2012 akiwa anatokea block jingine jirani na lile la mhusika
  • Kabla ya hapo, mwaka 2010 mhusika aliwahi kuibiwa injini ya gari ambayo model yake ni similar na possibly exactly the same na injini ya gari ile inayomilikiwa na jirani aliyehamia kwenye block la mhusika
  • Jirani alinunua gari mwaka 2010, baada ya injini ya gari la awali la mhusika kuwa tayari ilishaibiwa
  • Mhusika alinunua gari mwaka 2013
Kwa hiyo jirani alitangulia kusajili gari mwaka 2010 halafu mhusika naye ndiyo akafuata mwka 2013; takribani miaka mitatu baadaye

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE: TUESDAY 31 MAY 2022

MATUKIO MUHIMU YANAYOONYESHA KUWA NA UHUSIANO WA NAMNA FULANI; YALIYOJIRI KWA MUDA WA SIKU MBILI KUANZIA JUMAPILI YA TAREHE 29/05/2022 (KANISANI) NA JUMATATU YA TAREHE 30/05/2022 (OFISINI)

MAELEZO YA UTANGULIZI


J2 ya tarehe 29/05/2022 Kiongozi Mkuu wa Kanisa A (KM-A) hakuwepo Kanisani, alikuwa na udhuru maalumu

Vile vile, kesho yake J3 ya tarehe 30/05/2022 Katibu Muhtasi wa Mkuu wa Idara (KMMWI) pamoja na yule mfanyakazi mwingine mgeni ambaye hajawahi kutambulishwa idarani waliye naye kwenye ofisi moja, nao vile vile hawakuwepo ofisini

Kutokuwepo kwa wawili hawa, ofisini kumepelekea uwepo wa mfanyakazi mwingine mgeni ambaye bado hajatambulishwa kuwa ni nani, ndiye anayeshikilia kiti cha KMMWI hadi muda huu

Kinachopelekea taarifa hizi kuletwa kwenu ni kutokana na tukio ambalo lilianzia Kanisani, na ambalo lilikuwa linahusisha familia ya MR X. Kulikuwa na tangazo maalumu Kanisani ambalo katika hali ya kawaida (mara nyingi, si mara zote) huwa linatolewa na KM-A na hilo ndiyo baadaye lilikuja kupelekea uwepo wa mlolongo wa matukio mengine tena ofisini kwa mhusika kesho yake J3 ya tarehe 30/05/2022

Picha ya matukio haya inaanza mara tu baada ya MR X kufika ofisini kwa mhusika asubuhi hiyo kwenye midaa ya kama ya saa 4 asubuhi hivi

MR X alikuja kwa nia njema tu ya kumshirikisha mhusika katika kile amabcho kilikuwa kimetolewa tangazo Kanisani, ambacho utekelezaji wake hasa aliulelezea kuwa unatakiwa kuwa August mwaka huu

………………..inaendelea
 
ALICHOONGEA MR X BAADA YA KUFIKA OFISINI KWA MHUSIKA

MR X hakuongelea tangazo lililotolewa J2, kanisani bali aliongelea utekelezaji wake ambao alisema utakuwa J2 ya mwisho kabisa ya mwezi wa 8

Hapa sasa wasomaji wanaombwa wazingatie mlolongo wa matukio haya kwa makini kwamba

Tangazo lilitoka J2 Kanisani, na J3 asubuhi MR X alikuwa tayari ameshafika ofisini kwa mhusika kwa ajili ya kumshirikisha kuwenye mkakati wa utekelezaji wa tangazo hilo ambao unatakiwa ufanyike August mwishoni, takribani miezi mitatu kuanzia sasa

Ukizingatia mazingira yao ya ofisiniwatu wawili hawa; yaani MR X na mhusika; kwamba muda wote wa siku zote tano za kazi kwa wiki huwa wanakuwa wapo pamoja, na ukiangalia window iliyopo kuanzia siku ya tangazo hadi siku ya utekelezaji wake; ujio wa MR X ofisini kwa mhusika ulionyesha uharaka mkubwa kiasi, ambao pamoja na uharaka huo, bado mhusika hakuona shida juu ya hilo ukizingatia umuhimu wa swala lenyewe lililompelekea MR X kufika ofisini kwa mhuiska. HILO MOJA

PILI: Tukirudi Kanisani, mhusika hakumbuki Kiongozi aliyelazimika kutoa tangazo lililohusisha familia ya MR X, (baada ya KM-A kuwa amepata udhuru wa kutokuwepo Kanisani) mara ya mwisho aliwahi kutoa tangazo la aina hiyo lini; ila uhakika tu ni kwamba ndani ya kipindi cha zaidi ya miezi sita iliyopita, Kiongozi huyo hakuwahi kusimama madhabahuni na kutoa tangazo la aina hiyo. Pamoja na uwepo wa matangazo ya aina hiyo kwa wingi sana, mara nyingi matangazo hayo yamekuwa yakitolewa na KM-A tu, na kwa kipindi kirefu sana, possibly cha zaidi ya mwaka mmoja au miwili hivi

Kwa hali hiyo, ukizingatia window hiyo iliyopo kati ya siku ya tangazo na siku ya utekelezaji wa tangazo, bado kunaonyesha uwezekano wa kuwa tangazo hilo lingeweza kumsubiri KM-A na akalitoa yeye J2 ya wiki hii yaani tarehe 04/06/2022. Na kwa jicho jingine, possibly, tangazo hili lingeweza kutolewa hata tarehe 11/06/2022 at the latest na bado utekelezaji wake ukabaki kwenye tarehe ile ile ya J2 ya mwisho wa mwezi August 2022

Kwa hiyo mhusika yeye anapata shida kidogo na uharaka huo uliofanyika kote kote, ofisini na Kanisani; ukizingatia matukio yaliyojiri BAADAYE ofisini siku ya J3 hiyo, baada ya MR X kuwa ametoka ofisini kwa mhusika.

Kwa upande mwingine, pasingejiri tukio lolote ofisini siku hiyo, mhusika asingekuwa na shida na uharaka huo wote, yaani ule wa Kanisani na ule wa ofisini uliofanywa na MR X

……………………inaendelea
 
YALIYOJIRI BAADA YA MR X KUWA AMEONDOKA OFISINI KWA MHUSIKA J3 HIYO

MR X na mhusika hawakubahatika kuonana tena J3 hiyo hadi mhusika alipoondoka ofisini majiraya saa 11:30 jioni.

  • Hiki kitu ni cha kawaida sana, na ni kawaida sana hata wakawepo ofisini wote wawili na wasionane kabisa siku nzima, ni kawaida sana.
  • Kisicho cha kawaida, ni wote kuwepo ofisini muda wote halafu wasionane muda wa wiki nzima, hicho ndicho siyo cha kawaida
Baada ya MR X kuwa ametoka ofisini kwa mhusika, baadaye tena SENIOR MSTAAFU WA KIKE (SMKE) naye aliingia, ila yeye hakufika ofisini kwa mhusika. Ndiyo alikuwa anafika ofisini siku hiyo

  • SMKE na mhusika walibahatika kusalimiana tu kwa sababu mlango wa ofisi ya mhusika ulikuwa wazi, bado hajapata AC
  • Baada ya takribani masaa kama mawili hivi, mhusika alimuona SMKE akifunga grill ya mlango wa ofisi, na baada ya hapo hakuonekana tena ofisini hadi mhusika anaondoka ofisini
Baada tena ya muda kuwa umepita tangu SMKE aondoke ofisini, binti aliyeonekana kama ni mwanafunzi, akiwa amevaa ushungi mweusi uso akiwa ameuacha wazi, alifika na kuingia ofisi iliyo jirani na ile ya mhusika, ambayo mara nyingi huwa inatumiwa na MR X

Binti huyu alliingia ofisini kabla ya saa saba mchana na aliendelea kukaa humo ofisini akifanya kazi zake na hadi anaondoka ilikuwa possibly kwenye muda baada ya saa tisa alasiri

KIINI HASA KILICHOPELEKEA HAYA YOTE KULETWA KWENU WASOMAJI: MZEE WA KIUME MGENI NDANI YA JENGO


Kwenye mida baada ya saa saba, mhusika aliamua kupandisha juu kwenye washrooms zilizoko sakafu inayofuata huku binti aliyekuwa amevaa ushungi akiwa yupo anafanya kazi chumba jirani na ofisi ya mhusika

Pale katikati kwenye veranda zilipo ngazi za kushuka au kupandisha juu, mhusika akagongana na mtu mgeni, mzee wa makamo, mrefu mwili umejengeka mithili ya askari mstaafu, umri possibly kati ya miaka 68-72

Mzee alionekana ana afya njema, na alikuwa amevaa smart

Mwonekano wa sura, mhusika alimfananisha sana na baba yake mkubwa (RIP), na possibly kama mhusika angeamua kumsemesha halafu watu wakawaona wako wote pamoja wanaongea, chances ni kwamba watu wangejua kuwa mhusika leo ametembelewa na ndugu yake mazingira ya ofisini

Mhusika anasema hivi kwa sababu anafahamu namna alivyokuwa anakuwa identified kirahisi sana na watu ambao walikuwa hawamjui, ila wale ambao walikuwa wanawajua wazazi; baba zake

Mhusika alihisi kuwa possibly ni mgeni wa SENIOR MSTAAFU WA KIUME (SMME), kwa sababu kwa kipindi hiki, wageni wa caliber na umri huo na ambao huwa wanaopnadisha sakafu ya juu mara nyingi huwa wanakuwa ni wageni wa SMME

Lakini sasa SMME hakuwepo ofisini siku hiyo na mara ya mwisho mhusika alimuona SMME mazingira ya ofisini ni kama wiki nzima iliyopita

Mzee alikuwa mbele kidogo ya mhusika na hivyo alibahatika kuzishika kwanza yeye ngazi za kupandisha sakafu ya juu, akawa yuko mbele na mhusika naye akawa yuko anamfuata kwa nyuma

Walipozimaliza ngazi wamefika sakafu ya juu, mzee akawa kama anataka kuelekea kulia ziliko ofisi za Mkuu wa Idara, halafu akasita kidogo na hatimaye kugeuka kushoto, akaanza kutembea akiwa anaelekea usawa wa kule ziliko washrooms za wanaume. Hapo sasa mhusika alikuwa amesimama kwenye veranda ya sakafu ya juu, akitka kujua kwanza uelekeo wa huyu mzee, halafu ndiyo nay eye aamue wapi pa kuelekea

Swala la mhusika kuelekea washroom halikuwepo tena, ila uelekeo wake ulianza kutegemea uelekeo wa huyu mzee kwamba ataelekea wapi

……………………inaendekea
 
MZEE WA KIUME MGENI NDANI YA JENGO

…………….inaendelea


Mhusika alisita kwanza kuelekea washrooms, akimuangalia kwanza huyu mgeni aliyeonyesha kusitasita akiwa mbele yake, kuwa alikuwa anataka kuelekea wapi

Baada ya mzee kugeuka kushoto, alinyoosha moja kwa moja hadi kwenye mlango wa washroom, akavuta kitasa na kuingia humo

Mhusika aliamua kusitisha kwanza zoezi la kuingia washroom, akavunga amwache kwanza ili atakapotoka, ndiyo na yeye ataingia

Kuna washrooms zingine ambazo ziko ground floor, ambazo siku kadhaa zilizopita aligongana humo na fundi wa AC hali iliyopelekea aahirishe zoezi la kuingia humo na kupandisha juu kwenye washrooms hizi ambazo sasa mzee huyu mgeni alikuwa ameingia

Safari hii, mhusika hakuamua mbadala wa kushuka chini kwenye washrooms zilizoko sakafu ya chini; kwa sababu hicho ndicho kilichokuwa kinatafutwa; angefanya hivyo, lingekuwa ni KOSA LA MILLENNIUM NA SI LA KARNE

  • Mhusika alisubiria muda wa kutosha na baadaye aliporudi washroom na kufungua mlango, hakuona dalili za mtu mwingine kuwemo humo; hata mwenyeji naye pia hakuwemo
  • Baada ya hapo alishuka chini kwenye sakafu inayofuata na kwenda kusimama kwenye veranda akiwa ana-face parking za magari
  • Pale kwenye RESERVED PARKING ya SMME kulikuwa na gari imepaki pale, rangi ya ORIGINAL BLUE, model ilikuwa ni LANDCRUISER, 8-seater
  • Gari hiyo haikuwepo kabla, kwa sababu mara zote mhusika anapopita kwenye veranda hiyo, huwa anapenda kupumzika pale kidogo kunyoosha viungo kwa sababu ya kutumia muda mwingi akiwa amekaa kwenye kiti ofisini
  • Mhusika ali-suspect kuwa pengine gari hiyo ndiyo ilikuwa ya mgeni aliyemuwahi kuingnia washroom
  • Hazikupita dakika nyingi, mhusika alimuona tena mzee mgeni akitoka sasa ndani ya jengo
  • Wakati huo alikuwa anatokea sakafu ya chini.
  • Mzee alipita karibu na pale ilipokuwa imepaki gari hiyo ya blue na kunyoosha akishika barabara inayoelekea juu maeneno ya utawala.
Mpaka hapo kwake yeye mhusika ikawa ikadhihirka kuwa gari hiyo haikuwa yake, na kama ilikuwa yake, basi alikuwa bado ana shughuli nyingine za kufanya, muda wake wa kuondoka ulikuwa bado au alitaka mhusika asijue kuwa gari hiyo ilikuwa ni yake

HITIMISHO: DHANA ALIYONAYO MHUSIKA KUHUSIANA NA TUKIO HILI

Baada ya mzee huyu kum-scare mhusika na kupelekea mhusika asiingie washroom, baadaye sasa mzee alishuka chini akiwa anajua kuwa possibly mhusika atakuwa alishuka huko kwenye washrooms ziilizoko sakafu ya chini

Mzee huyu alikuwa sakafu ya chini kwa sababu kama angekuwa ameendelea kubaki sakafu za juu, ilikuwa lazima mhusika angemuona wakati wa kushuka, kwa sababu yeye (mhusika) alisimama kwenye sehemu ambayo alikuwa anaweza kumuona kila mtu anayeshuka na kupandisha juu kupitia kwenye ngazi

Zaidi ni kuwa kwa maelezo haya, mhusika anafuta kila kitu walichoongea J3 hiyo na MR X, kumpa nafasi MR X ku-concentrate na vitu vingine vya maana zaidi.

Hata hivyo anamtakia kila la kheri na zaidi tu ni kuwa anawapenda sana rafiki zake; watoto wake na MR X, na hao ndiyo pekee ambao huwa wanamvuta na kumfanya mara zote kuwa humble na MR X pamoja na familia yake kwa ujumla. Mhusikahuwa hana sura mbili; kinachoonekana nje ndiyo kilicho ndani kwake

Wasingekuwa hao marafiki zake na mhusika, MR X na mhusika wasingeweza tena kuhusiana kwa lolote lile ukiachilia mbali mambo ya ofisini tu

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
NYONGEZA MUHIMU KUHUSIANA NA MR X

Katika yale yote waliyoongea na mhusika; MR X alisisitiza pia kumpatia kadi mhusika; kitu ambacho kilikuwa ni unnecessary kwa sababu huwezi ukampatia kadi mtu ambaye kila siku mnapishana kwenye korido. Mtu wa aina hii ukimpatia kadi na akaikubali, kuna uwezekano mkubwa akawa hana nia ya kushiriki kile ulichomshirikisha.

Hata hivyo, MR X alikusudia kuja kuitumia kadi hiyo huko mbele ya safari kama ushahidi wa mahusiano yaliyokuwa tayari yameshaboreka kati yake na mhusika; just in case of anything

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE: 7TH JUNE 2022

MAONI KADHAA ALIYONAYO MHUSIKA KUHUSIANA NA MATANGAZO YALIYOTOLEWA “KANISA A” NA VIONGOZI WAWILI; KIONGOZI WA ZAMU (KZ) PAMOJA NA KIONGOZI MKUU; JUMAPILI YA TAREHE 05/06/2022 WAKATI WA IBADA YA PILI


J2 hiyo Kiongozi wa Zamu (KZ) alisimama madhabahuni na kutangaza kuwa kuanzia J4 hadi Alhamis wiki hii; kutakuwa na maombi ambayo yataambatana na mfungo wa maji tu

Huu mfungo wa maji tu kwenye maombi ya Kanisa-A, umefululiza kwa takribani miaka mitatu sasa. Hata hivyo hili nalo ni swala jingine linalojitegemea mhusika atakuja kuliongelea peke yake kulingana na utafiti ambao tayari ameshauthibitisha pasipo shaka. Maombi karibia yote ambayo yamekuwa yakifanyika kwa takribani miaka mitatu iliyopita, ni ya mfungo wa maji tu.

Mbali na hayo, tangu waumini waanze kuabudu ndani ya KANISA JIPYA, hapajwahi kutokea maombi ambayo mfungo wake haukuwa wa maji

  • Baada ya KZ kutangaza maombi ya mfungo wa maji tu; aliendelea kwa na kudokeza kuwa maombi hayo angekuja kuyasemea hasa Kiongozi Mkuu wa Kanisa A (KM-A) na kwa hali hiyo KZ hakufafanua content ya maombi hayo na hivyo hakusema yatahusu nini
  • Baada ya KZ kushuka madhabahuni, KM-A alipanda madhabahuni aktoa matangazo mengine aliyokuwa nayo na hatimaye akaanza kufafanua content ya maombi ambayo KZ alikuwa tayari amewajulisha waumini kuwa yatakuwepo kuanzia J4 hadi Alhamis
KM-A alianza kwa kusema kuwa maombi hayo ni ya kuliombea Taifa.

  • Tangazo la kwanza lilihusu hali ya chakula kwa Taifa, ambalo mhusika hata kidogo hana tatizo kabisa na tangazo hili
  • Tangazo la pili lilihusu kuombea mambo machafu ambayo yameanza kujitokeza, na hapa ndipo tatizo la mhusika na ufafanuzi wa KM-A kuhisna na tangazo hilo la maombi ya kuanzia J4 hadi Alhamis, linapoanzia.
  • Katika hili KM-A alitaja ulawiti kwa watoto; kwamba wanakuwa katika hali ambayo si salama hata wanapokuwa na jamaa zao wa karibu
  • Hapa ndipo pale ambapo shida ya matanagazo haya ilipoanzia ukizingatia MATUKIO MENGINE ya hivi karibuni na na ya kusikitisha sana ambayo tayari yameshajitokeza; na ambayo yalionekana kuwa KM-A yeye hayo hakuyaona isipokuwa hili la ULAWITI
Kwa kifupi tu ni kwamba kila mtu anajua kabisa kuwa hivi karibuni, tumepoteza watu mfululizo kwa mauaji ya kikatili mojawapo likimhusisha mtoto anayesemekana kuwa amenyongwa na mfanyakazi wa ndani. Tukio hili limetikisa kwa kusikitisha mno watu kiasi kwamba ilikuwa wakati mwingine mtu unashindwa kuvumilia kusikiliza taarifa hiyo; inabidi ubadilishe channel ya TV kwa muda taarifa hiyo ipite kwanza halafu baadaye ndiyo urudishe tena kwenye channel hiyo. Mtoto huyu amesikitsiha watu sana. HILO MOJA

PILI, kule Mwanza, wanandoa wameuana, mme kamuua mke kwa kumpiga risasi 7, na hatimaye na yeye mwenyewe naye kujiua pia


Matukio ya mauaji ya kusikitisha na ambayo ni ya hivi karibu sana ni mengi mno na si haya tu; yapo mengi tu

  • Haya yote, kwa hekima yake aliyonayo, KM-A hakuyaona ila akaona tukio la ulawiti tu na ambalo bado ni tuhuma pending uthibitisho wa Mahakama
  • Mbali na hayo, ukiliangalia tukio lenyewe kwa jicho la ki-layman; unaona kabisa kuwa huyu mtuhumiwa hana wasiwasi wowote kabisa na wala hajifichi uso kutokana na kutuhumiwa kitendo cha aibu; kitu ambacho inawezekana ikawa hata akawa amesingiziwa
Still, amesingiziwa au hajasingiziwa, katika hali ya kawaida, KM-A kama mtumishi wa Mungu aliyejaa Roho, alitakiwa alione pia swala la mauaji ya watu yanayoendelea na si hili la tu ulawiti; na ambalo bado ni tuhuma tu ambazo inabidi Mahakama ijiridhishe kwanza kama ni za kweli

Ikumbukwe kuwa shida ya mhusika hapa si kwa KM-A kuliona tukio la ULAWITI hapana; shida ya mhusika ni KM-A kuliona tukio la ulawiti tu na pasipo kuyaona matukio mengine MAKUBWA ZAIDI YA HILO; kama haya ya mauaji na ambayo yamekuwa yakiendelea kutikisa nchi kuliko hata huo ulawiti, na ukizingatia ukeweli kuwa TUKIO LA ULAWITI NA AMBALO HALIJATHIBITISHWA, LIMETOKEA KWENYE MUDA MMOJA NA LILE LA MAUAJI YA KIKATILI YA MTOTO; NA AMBALO LIMESHATHIBITISHWA

Picha anayoitoa hapa KM-A ni kwamba yeye anaguswa na tukio dogo ambalo halijathibitishwa wakati lile kubwa ambalo limeshathibitishwa hana habari nalo


Unless kama kiongozi huyu wa kiroho, yeye jicho lake la rohoni huwa linaona madogo kabla ya yale ambayo ni makubwa

Katika hali ya kawaida kabisa, ni dhahiri kuwa KM-A alitakiwa alione tukio la mauaji kwanza kabla ya lile la ulawiti

Hii ni kutokana na ukweli kuwa mauaji yenyewe tayari yameshatokea na hayahitaji uthibisho wa aina yoyote ile. KM-A hata hivyo, hakuyaona kabisa mauaji isipokuwa ulawiti tu na ambao bado uko pending uthibitsho wa Mahakama; pamoja na kuwa tukio hilo linaweza hatimaye kuja kuthibitishwa kuwa ni la kweli

TANGAZO JINGINE LA NYONGEZA ALILOLITOA NA LILILOSHAHIBIANA NA LILE LA ULAWITI

Baada ya tangazo hilo, KM-A aliongezea tena tangazo jngine la kuwekwa huru muumini ambaye alikuwa amefungiwa; possibly kutokana na uzinzi

Kwenye mambo ya namna hii, mhusika ameshazifahamu sana mbinu ambazo KM-A huwa anazitumia kuishambulia madhabahu pindi anapoona kuwa madhabahu imekuwa ya moto kwake. Hii yote huwa anafanya ili kuhakikisha kuwa anaendelea kupanda madhabahuni

KANISA JIPYA LINALOENDELEA KUTUMIKA MPAKA MUDA HUU HALIJAWAHI KUWEKWA WAKFU

Kanisa jipya limeanza kutumika zaidi ya miezi sita sasa na halijawahi kuwekwa wakfu

Kanisa halijawahi kuwekwa wakfu, lakini limeshaanza ku-host Ibada za SECTION ambazo kawaida ina makanisa yasiyopungua kumi

Pilika pilika za KM-A sasa hivi zimekuwa nyingi sana

…………………….inaendelea
 
Kwa hiyo labda tuseme kwamba yeye KM-A ana sikio la kusikia matukio ya ulawiti tu na si ya mauaji kiasi kwamba hata hili lililotokea juzi tu la mtoto tuliyempoteza juzi anayeitwa ERICSSON, hata hilo yeye hakulisikia?
 
Back
Top Bottom