#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
10,269
6,836
Wanabodi:
Niwaletee mkasa huu wa kipekee unahusiana na pilika pilika za kujikinga na COVID-19 umemtokea jamaa yangu Jumapili ya tarehe 19/04/2020 akiwa Kanisani kwake

Muhimu: Uzi huu unawafaa sana hasa wale ambao tu huwa wana muda na wanapenda kuchambua mambo kwa kina, vinginevyio kama wewe siyo mmoja wao, unaweza ukaona kana unapoteza muda wako kuufuatilia.

Mhusika wa matukio, amenisimulia kwa kina akisema kuwa kuna matukio ambayo yamemtokea, na ambayo yalianza kuonyesha pattern kuanzia siku ya Jumapili ya tarehe 5/04/2020

Zaidi, anadai pia kuwa matukio haya, yanaweza kuwa ni pure coincidences tu, japo anakiri kuwa kuna baadhi ya maeneo ambayo yanadhihirisha patterns za kipekee, kama nitakavyoyaainisha ndani ya uzi huu kulingana na simulizi yake

Ni kwamba Jumapili hiyo ya tarehe tajwa hapo juu, AKIWA ANATOKEA NYUMBANI alifika mahali pake pa Ibada kwenye nyumba ya Ibada (tuiite jina Nyumba ya Ibada A), muda wa saa 12 kasoro asubuhi, akapaki gari na akapuliziwa sanitizer na Mlinzi A, (tumwite hivyo kwa sababu maaskari wapo wengi pale getini, nadhani zaidi ya wannne) aliyemkaribisha kwa kumfungulia geti. Baada ya hapo akaendelea kuelekea kwenye Ibada. Siku hiyo ikapita.

Jumatano ya tarehe 08/04/2020 alifika tena kwenye nyumba hiyo ya Ibada, akitokea ofisini, mishale ya dakika chache baada ya saa 10 alasiri. Hata hivyo, tofauti na siku ya nyuma yake aliyofika kanisani hapo, pakuwa na mlinzii aliyempatia Sanitizer, na hakumbuki kama ilikuwepo ndoo ya maji yanayotiririka sehemu ambapo yanatakiwa kuwapo, na kama yalikuwepo basi siku hiyo hakuyatumia, ila kumbukumbu zake kidogo zimefifia kuhusiana na siku hiyo

Vilevile siku ya Ijumaa Kuu (11/04/2020) kwenye mishale ya baada ya saa tano asubuhi, AKATOKA NYUMBANI kuelekea kwenye nyumba ya Ibada, kwa kusudi la kwenda kufanya maombi binafsi, huku akisubiria Ibada Kuu ambayo ilikuwa scheduled kuanza saa 10 kamili alasiri. Alipoingia getini, safari hii tena akamkuta Mlinzi A , akapuliziwa sanitizer halafu akaendelea na shughuli zake za maombi na hatimaye huduma ya Ibada, muda ulipofika. Siku hiyo nayo pia ikapita.

Jumapili ya Pasaka (12/04/2020) ilipofika, kwenye mida ya saa 12 kasoro asubuhi akawa tena amefika kwenye nyumba hiyo ya Ibada, AKIWA ANATOKEA NYUMBANI, kwa ajili ya Ibada ambayo ilikuwa inaanza kwa maombi saa 12, na hatimaye Ibada kamili kuanzia saa 1. Alipoingia getini, safari hii tena akamkuta Mlinzi A , akapuliziwa sanitizer halafu akaendelea na shughuli zake kwenye huduma ya Ibada muda ulipofika. Siku hiyo nayo tena ikapita pia.

Tukio muhimu la kipekee sana alilokutana nalo hapo Kanisani sku hiyo ni kuwa kwa mara ya kwanza tangu aanze kuhudhuria Ibada za asubuhi, takribani miaka miwili sasa, alikuwa hajawahi kukuta hakuna mtu Kanisani. Siku hiyo hapakuwa na mtu yeyote ila kulionyesha dalili kuwa kuna mtu alikuwepo ila alitoka kidogo, na akiwa amesahau feni mbili za pangaboy za kwenye madhabahu, zikiwa zinatembea. Kwa hiyo huyu bwana kuona hakuna mtu hapo kanisani na feni zinatembea, aakaona ni busara kwenda kuzizimama zile feni ili zisiendelee kula umeme wa bure wakati hapakuwa na mtu pale madhabahuni.

Alipofika kwenye panel ya switch za umeme, akakuta kuna siwitch moja tu iko ON na alipoizima, baadhi ya taa zikazima; akagundua kuwa siyo yenyewe. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake yote ya Ibada kwenye nyumba hiyo, akapandisha juu ya madhabahu ili aone kama kuna swich ziko pale, na kweli azlizikuta na akafanikiwa kuzima feni hizo.

Hapo kabla, asubuhi ya Jumapili siku hiyo wakati anatoka nyumbani ili aelekee kanisani, alikuta switch za kwenye parking kwenye jingo analoishii ziko OFF, na kwenye parking kulikuwa na giza. Aliamua akaziweka ON na kuondoka, na hakujali kuhakikisha kuwa zimewaka kwa sababu huwa zinaweza zikachukua muda wa hata masaa matatu kuanzia pale switch inapowekwa ON, hadi kufikia kuwaka; ni taa za aina yake. Mahali anapoishi ni ghorofa ambalo ni shared, lenye parking iliyo ground floor.

Vilevile, siku za Jumatano ya tarehe 15/04/2020 na Ijumaa ya tarehe 17/04/2020 nazo pia alifika kwenye Ibada za jioni za kuanzia saa 10 na nusu alasiri,siku zote hizo mbili akiwa ANATOKEA OFISINI ila hapakuwa na Askari kwa ajili ya sanitizer, na hata ndoo ya maji yanayotirirka haikuwepo, na kama ilikuwepo basi hakuiona. Hizo siku nazo pia zikapiata.

Siku ya mwisho katika mlolongo wa matukio haya, ikawa ni Jumapili ya tarehe 19/04/2020. Akiwa ANATOKEA NYUMBANI siku hiyo tena akafika Kanisani kwenye mida ya saa 12 kasoro asubuhi. Nyumbani alikokuwa ametokea, switch za parking ya magari hazikuwa zimewashwa tena, japo huwa yupo mlinzi. Safari hii hakuziwasha

Ailpofika kanisani Mlinzi A, hakuwepo ila alikuwepo mwingine ambaye alimchungulia kwanza kabla hajamfungulia geti ili aingize gari ndani. Kabla hajamfungulia geti, mlinzi akatoka na sanitizer ampulizie kwanza halafu ndiyo aingize gari ndani. Katika kujaribu kuongea huyu mtu akadai kuwa hajawahi kukatili kupuliziwa sanitizer na hivyo si haki kumfuata na sanitizer nje, akaomba aingize gari kwanza ndani halafu ndiyo apuliziwe sanitizer. Baada ya kuingia ndani, akagoma kwanza kupuliziwa sanitizer kutokana na hoja za msingi alizokuwa nazo , ila baadaye alikuja mlinzi mwenzake akamtishia kumtoa nje na gari lake, ndiyo akatii amri ya kupuliziwa tena. Angeweza kutumia maji ya bomba na sabuni ya maji kule men’s room.

Kwa hiyo kwa ufupi yeye anadai kuwa mgogoro uliotokea ni kutokana na mlolongo wa matukio hayo kama nilivyoyaeleza hapo juu, na kwa sababu ambazo yeye aliziainisha kwangu kuwa kama ifuatavyo:

MOJA: Hapakuwa na haja ya kumfuata kumpulizia sanitizer akiwa nje ya gate kwa sababu haijawahi kutokea akakatili kupuliziwa sanitizer, ni agizo la Serikali

MBILI:Ni siku za Ibada kuu tu (Ibada ya siku ya Ijumaa Kuu na zile za Jumapili asubuhi) na AKIWA ANATOKEA NYUMBANI, ndizo ambazo amekuwa akikuta mtu yuko standby kwa ajili ya kumpulizia sanitizer.

TATU: Siku za Ibada za jioni ambazo si Ibada kuu, na ambapo amekuwa akifika kanisani AKITOKEA OFISINI, hakuna mtu amabye amekuwa akikaa standby kwa ajili ya kumpulizia sanitizer, isipokuwa siku za Ibada kuu tu, na ambazo amekuwa akitokea nyumbani, kama iilivyoainishwa kwenye kipengele namba mbili hapo juu

NNE: Jumapili hiyo, ndoo ya maji yanayotiririka nayo pia ilikuwepo, kitu kinachoonyesha kuwa huyu bwana, baada ya kuingia ndani, angeweza kutoa hoja kwamba anatamani kunawa kwa kutumia maji yanayotiririka na si kupuliziwa sanitizer. Hivyo kilichofanyika ni kumuwahi akiwa nje ili apuliziwe sanitizer kwanza kabla hajayaona maji yanayotiririka. Kwa hiyo inaonyesha kama kulikuwa na mpango mahsusi wa kuhakikisha kuwa huyu bwana lazima apuliziwe sanitizer ili asije aka-opt kutumia maji yanayotiririka halafu sanitizer akaacha kuitumia

TANO: Mpuliziwa alidai kuwa sanitizer zinazotumika Kanisani ni tofauti na zinazoweza kutumika shehemu nyingine yoyote ile kama vile sokoni. Chochote kile kinachotumika Kanisani lazima kiwekwe wakfu kwanza, lakini hajawahi kuona hata siku moja sanitizer hizo zikiwekwa wakfu kwa ajili ya matumizi hapo Kanisani, tangu zianze kutumika

SITA: Siku alipokuta feni zinatembea pale madhabahuni, na hapakuwa na mtu, inaonyesha KAMA kuna mtu aliziacha zinatembea makusudi ili mpuliziwa atakapokuja, azizime. Inaonyesha KAMA vilitaIkiwa vidole vyake kugusa switch za feni hizo, ili kuzima feni hizo, baada ya kuwa vidole hivyo vimetoka kupuliziwa sanitizer.

SITA: Akiwa kwenye Ibada siku ya mgogoro wa sanitizer wa Jumapili ya tarehe 19/04/2020, kuna msamaria mwema ambaye pia ni shemasi, alikuja akamjulisha kuwa kioo cha mbele cha gari lake upande wa passenger kiko wazi. Hapo sasa tayari swala la sanitizer lilikuwa limeshapita, na Ibada ilikuwa imeshaanza. Cha kushangaza ni kwamba Jumamosi siku nzima ilinyesha mvua kubwa, na yeye gari hakuligusa Jumamosi yote mchana wala usiku. Kioo hiki cha passenger kingekuwa kimeachwa wazi kuanzia Ijumaa, gari ingelowana na mvua ya Jumamosi na usiku wa kuamkia Jumapili passenger seat ingekuwa bado imelowana. Lakini kioo cha gari kweli alikikuta kikiwa wazi na passenger seat ikiwa ni kavu. Jumapili asubuhi akiwa anaelekea Kanisani, hakufungua dirsha lolote, na wala hakuwa amewasha AC kwa sababu hali ya hewa ilikuwa nzuri na ya ubaridi kiasi. Hapa napo inaonyesha KAMA, sanitizer aliyolazimishwa kupuliziwa, baada ya pale alitakiwa aitumie vidole vyake kwenda kugusa kitu kingine, ambacho bado hajajua ni kitu gani hasa!

SABA: Huyu bwana anadai kuwa kipindi kabla ya Corona, wakati watu walikuwa wako huru kushikana mikono, kuna watu wachache ambao alikuwa ameshawaainisha, ambao walikuwa wana tabia ya kuhakikisha kuwa wame-shake hands naye kabla Ibada haijaanza, na kwa nia ambayo yeye anadai kuwa haikuwa njema. Hawa watu walikuwa wamejipanga randomly kiasi kwamba usipokuwa makini, huwezi kuwatofautisha na wengine ambao walikuwa wanakwenda ku-shake hands naye kwa nia iliyo njema. Inaonyesha KAMA hawa shaker hands, wameanza kutumia sanitizer kwake, kama substitute yao baada ya Corona kuingia, maana haiwezekani tena ku-shake hands kwa sasa.

NANE: Inaonyesha KAMA swich iliyokuwa inaachwa OFF kwenye parking ya jeingo analoishi kwa Jumapili mbili mfululizo, ina uhusiano wa ki-mantiki na switch za feni zilizokuwa zimeachwa zinatembea madhabahuni, bila kuwepo watu, ambazo ilimlazimu kupanda madhabahuni kwenda kuziweka OFF ili feni zisitembee. Hata hivyo uhusianao huo bado hajaweza kuujua, assuming utakuwa upo kweli

Huu ni uchambuzi wake na nitazidi kuwaletea updates kadri atakavyokuwa anani-update. Siku hizi napenda kiasi mambo ya umbea, siyo kama zamani.

Hata hivyo, kwa upande mwingine matukio haya yanaweza kuwa ni pure coincidences na ambazo hazina maana yoyote, au kukawa na kitu wachambuzi wa maswala yaliyojifichaficha wanaweza kuokota kitu kutoka kwenye cobweb ya matukio haya.

Naomba kuwasilisha.

UPDATE 22/04/2020

1 SWITCH ZA TAA ZA PARKING KWENYE JENGO ANALOISHI KUTOKUWA ZIMEWASHWA KWA JUMAPILI MBILI MFULULIZO, UKIHUSIANISHA NA SWITCH ZA FENI ALIZOKUTA ZIKITEMBEA KANISANI, PAMOJA NA ASKARI WA SANITIZER


Ikumbukwe kuwa Jumapili (ya Pasaka) ya siku ambayo alikuta Kanisani kuna feni zinatembea halafu akaenda akazima switch zake, kule nyumbani alikotokea kwenyewe nako aliacha amewasha switch za kwenye parking, ambazo nazo alizikuta ziko OFF. Jumapili hiyo alihudumiwa sanitizer na Mlinzi A, na ilikuwa mara ya 3 mfululizo kupata huduma kutoka kwa mtu huyu, kwenye siku za Ibada kuu ukiongeza na zile za Ijumaa Kuu, na Jumapili ya wiki kabla ya Jumapili ya Pasaka

Lakini pia vilevlie, Jumapili hii iliyopita (wiki jana), switch za kwenye parking alizikuta tena zikiwa OFF, lakini safari hii hakuziwasha, aliziacha kama alivyozikuta. Alipofika Kanisani akapokelewa na Mlinzi mwingine nje ya gate, akiwa anajiandaa kumpulizia sanitizer na hatimaye malumbano kidogo baada ya kuingia ndani ya gate la Kanisa

Yeye hypothesis yake kwenye matukio haya anadai kuwa kama ifuatavyo:

Inaonyesha KAMA alivyoweka ON switchi za kwenye parking asubuhi ya Jumapili ya Pasaka, halafu tena akaenda akaweka OFF switch za feni kule Kanisani, ambazo kwa sasa yeye anadai kuwa ziliachwa ON makusudi, kitendo cha yeye kutorudia tena kuziweka ON switch za kwenye Parking ya jengo analoishi Jumapili ya wiki jana, ziliashiria kuwa inawezekana tayari ameshajenga dhana kuwa kitendo cha kuwa anakuta switch zimeachwa katika position ambayo siyo sahihi halafu unazirekebisha, ni kitendo malicious, na si cha bahati mbaya. Kwa hali hiyo siku ya Jumapili hiyo aliyoacha kuweka ON switch za kwenye parking, inaonyesha KAMA kuna information zilikuwa relayed kule alikokuwa anaelekea, yaani Kanisani, kwamba jamaa ameshastuka na issue ya switch. Na kwa sababu switch alizowasha Kanisani zilikuwa connected na issue ya Sanitizer, ikaonekana sasa kuwa kuna uwezekano asubuhi ile angeweza kutoa resistance namna ya kupokea huduma hiyo ya sanitizer, pindi atakapokuwa amefika Kanisani. Kwa hiyo mkakati ukapangwa sasa wakati akiwa bado yuko njiani kwamba:

Mlinizi A asitumike tena siku hiyo kumpa huduma ya sanitizer kwa sababu kuu mbili
  • amekuwa akimpa kwa mara 3 mfululizo, na siku hiyo ingekuwa mara ya nne.
  • kulikuwa na uwezekano wa mhudumiwa kutoa upinzani wa huduma hiyo, na kama mhudumu angekuwa yuleyule, pengine upinzani ungekuwa mkubwa zaidi ikiwa ni pamoja na maswali mengi
Kwa hiyo inaonyesha KAMA mamlaka zikawa zimeafiki mtu mwingine ajiandae kwa kumpa huduma ya Sanitizer na kwa kumfuata nje kabla hajaingia ndani ya gate ili kama pengine kutatokea mgogoro, umalizikie huko huko nje ili waliomo ndani ya gate wasije wakaunusa.

Mbali na hilo, kwenye sehemu ya parking ,hivi karibuni kumewekwa Kamera. Kwa hiyo inaonyesha pia KAMA mhudumu wa sanitizer alishauriwa hivyo ili kukwepa uwezekano wa tukio lake na mhudumiwa, kukamatwa kwenye Kamera, kwa sababu kama nilivyosema hapo awali kuwa, baada ya kuwa ameingia ndani, aligundua kuwa kulikuwa pia na ndoo ya maji yanayotiririka. Assuming angeingia ndani halafu tukio likawa limekamatwa kwenye Kamera, la mhudumu anampelekea mtu sanitizer halafu mhudumiwa anaanza kuuliza maswali ya kumhoji mhudumu, mojawapo likiwa tuseme KWA NINI KILA MARA MUNANILETEA SANITIZER WAKATI LEO YAPO PIA MAJI YANAYOTIRIRIKA? ,…., na maswali mengine ambayo yangeweza kufana na hayo

Kama hypothesis hii ya switch haitakuwa sahihi, uwezekano mwingine ni kuwa Jumapili ya wiki jana, switch ziliwekwa OFF ili kuwe na giza kwenye parking, kuruhusu ufunguaji wa kioo cha gari upande wa passenger seat, ambalo mhusika hakuwa ameliacha wazi. Uhakika alionao ni kuwa kioo hicho kilifunguliwa gari likiwa nyumbani, alfajiri ya Jumapili, na kwa sababu huwa anaondoka ikiwa bado giza kidogo, na pia Kanisani si mbali sana kiasi kwamba anaweza akahitaji kukimbia mwendo mkubwa, kioo hakukiona hadi anafika Kanisani na kupaki gari na kuiacha.

Alternatively, hypotheses zote mbili zinaweza pia ku-apply, kwamba mambo hayo yote mawili yanaweza kuwa yalikuwa yamekusudiwa kutendeka kwa pamoja.

2. TRIP ZA KUTOKEA NYUMBANI NA ZILE ZA KUTOKEA OFISINI KUELEKEA KWENYE IBADA, NA UHUSIANO WAKE NA SANITIZER

Anadai kuwa amekuwa akipata huduma ya Sanitizer pindi anapokuwa anaelekea Kanisani kutokea nyumbani na kwa siku ambazo ni za Ibada Kuu tu. Hapati huduma hiyo akiwa anatokea ofisini kuelekea kwenye Ibada za katikati ya wiki ambazo huwa zina kawaida ya kuanza baada ya saa 10. Yeye hapa anadai kuwa kunaweza kukawa na mambo makuu mawili ambayo ni:
  • Inaonyesha KAMA huwa anatoa upinzani mkubwa kwenye Ibada Kuu hasa zile zinazoanza asubuhi kwa sababu huwa anafika Ibadani asubuhi akiwa anatokea nyumbani, na akiwa haja-interact na mtu yeyote siku hiyo. Mbali na hivyo, huwa anaanza kwa maombi kwanza pamoja na kusoma maandiko matakatifu, alfajiri kabla hajanza safari ya kuelekea Kanisani. Kwa hiyo akiwa anatokea nyumbani kuelekea Ibadani, inalazimika afanyiwe udhibiti wa kipekee, na hivyo huduma ya sanitizer, anapokuwa tu amefika Ibadani akiwa anatokea nyumbani
  • Inaonyesha pia KAMA huwa hatoi upinzani mkubwa kwenye Ibada za katikati ya wiki, anapokuwa ametokea ofisini, au kama anatoa basi bado kunakuwa na nafasi ya kuudhibiti kabla ya siku ya Ibada Kuu, yaani Jumapili. Aidha kunaweza pia kukawa na mtandao saidizi mwingine ofisini kwake ulio kinyume naye, ambao huwa unahakikisha kuwa umemdhibiti kabla muda wa Ibada kuwa umefikakiasi kwamba huwa anaondoka ofisini akiwa tayari hana ule upako wa kutoa upinzani unaoweza kuleta athari. Kwa hali hiyo kwa siku kama hizi, inakuwa hakuna haja ya kumpa huduma ya Sanitizer, itapelekea huduma hiyo iwe monotonous kwake halafu ipelekee aje aigomee kwenye siku ambayo ni ya muhimu huko mbele ya safari

3 COINCIDENCE INAYOMHUSU KIONGOZI ALIYESEMEKANA KUWA NI MHUSIKA WA MANUNUZI YA CORONA
  • Mhusika anadai kuwa baada ya kupuliziwa Sanitizer kwa lazima, alipitiliza moja kwa moja mpaka men’s room, akanawa kwa sabuni na maji yanayotiririka. Kuna bomba moja tu la maji kwenye chumba hicho
  • Baadaye alirudi ofisini kwa walinzi, akawa anahoji mawili matatu kuhusiana na baadhi ya mambo ambayo alikuwa anayaona hayaendi sawa, mojawapo ikiwa ni kujua kama Sanitizer hizo zimewekwa wakfu kwa ajili ya matumizi ya Kanisani
  • Hatimaye mtu mmoja alijibu akasema muulize fulani (akamtaja kiongozi ambaye inaonyesha ndiyo mhusika wa manunuzi ya vifaa hivyo)
  • Baadaye wakati Ibada inaendelea, mhusika alitoka tena kuelekea men’s room. Alipofika huko akamkuta mtu aliyetajwa kuwa mhusika wa manunuzi, men’s room, akiwa ananawa kwenye bomba la hilo la maji. Umbali kutoka pale lilipo bomba hilo na pale alipokuwa amekaa kiongozi mhusika wa manunuzi wakati wa Ibada, hauzidi mita kumi na tano, na umbali kutoka kule alikokuwa mhusika wa tukio hadi kufika kwenye bomba hilo, shortest distance inaweza kuwa mara 3 ya umbali huo, lakini pia ali-opt kutumia njia mbadala kukwepa kuwabughudi watu kwa sababu Ibada ilikuwa inandelea, na njia aliyotumia inaweza kuwa na urefu wa takribani mita 60
  • Mhusika wakati anatoka men’s room, (kiongozi alikuwa tayari ameshaondoka) alirudi kwa kutumia njia ile ile aliyoijia. Njiani tena akakutana na binti wa karibu sana na kiongozi aliyetajwa, yeye naye alikuwa anaelekea kule alikokuwa anatoka mhusika. Configuration ya sehemu ile namna ilivyokaa ni uchochoro ambao uwezekano wa mtu mwingine kumuona mwenzake ni lazima uwe maeneo yale na si Kanisani au kwingine. Kwa hiyo hayupo mtu ambaye anaweza kuwa alituona wakati tunapishana, labda satellite iliyo juu!
Scenerio hii nayo ilionekana kama rare coincidence kwake, japo anakiri kuwa inaweza kuwa haina maana yoyote!

Nitarudi kwa ajili ya sehemu ya mwisho ambayo mojawapo ya habari zake ni hii hapa chini, mbarikiwe tena na Bwana

4. MAMBO MENGINE AMBAYO HAYAHUSIANI MOJA KWA MOJA NA TUKIO LA MHUSIKA, LAKINI AMBAYO ANASHAURI KAMA KUNA UWEZEKANO, UONGOZI UWEZE

Anadai kuwa pembezoni mwa nyumba ya Ibada wanayoabudia kwa sasa kuna chamber za majitaka umbali wa si zaidi ya mita moja, upande wa kushoto wa Kanisa. Kanisa ni Banda ambalo halina kuta, na Kanisa jipya bado liko kwenye ujenzi. Chambre hizi zimekuwa zikiachwa zinafurika na kutoa nje maji yaliyochanganyikana na kinyesi, halafu maji hayo yanaanza kutirirka kupitia njia ambayo waumini huwa wanapita na watoto kucheza. Kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni, anadai hakuona mafuriko hayo, ila pia hana taarifa kama chemba hizo zimefanyiwa kazi, ila pengie hazikuvuja tu kwa bahati nzuri. Pia anadai kuwa kuna mtu alimdokeza kuwa mapepo huwa yana uwezo wa kukaa hata kwenye harufu ya kitu tu, au kwenye kitu kinachotiririka, kama nilichokitaja

NITARUDI

UPDATE 04/05/2020

SABABU ZILIZO NYUMA YA PAZIA ZINAZOPELEKEA KANISA JIPYA LILILOJENGWA ALMAARUFU KAMA “JENGO JIPYA” KUTOKUTUMIKA MPAKA MUDA HUU

  • Kanisa jipya ambalo liko kwenye stage ambayo lingekuwa limeshaanza kutumika, halitumiki na uongozi mzima ulishalibatiza jina JENGO JIPYA.
  • Inaonyesha KAMA ni marufuku kuliita “KANISA JIPYA” na huwezi ukamsikia kiongozi YEYOTE pale Kanisani analitaja kuwa ni KANISA JIPYA, bali JENGO JIPYA
  • Haya majina yana implications zake kubwa sana kwenye ulimwengu war oho, kwa maana kuwa PEPO anaweza akakaa kirahisi tu ndani ya JENGO lolote lile, lakini ni vigumu sana kwake kukaa kwenye KANISA na ndiyo maana haliitwi KANISA JIPYA bali JENGO JIPYA, ili kutoa mwanya wa mapepo kuweza kupata hifadhi humo
  • Si kwamba hawezi kabisa kukaa kwenye kanisa, kama kuna jitihada za kumuwezesha afanye hivyo, ila ni vigumu kwake kukaa ndani ya kanisa na hasa kufanya makao permanent
  • Tofauti na ilivyo sehemu zingine, kwenye jengo la kawaida pepo anaweza akafanya makao permanent kirahisi tu, unless zimefanyika jitihada za kumwondoa
Sababu za kutokutumika Kanisa hilo jipya, yeye anaziona kama ifuatavvyo:
  • MADHABAHU YA KANISA LA ZAMANI (ambalo ni banda na huwa liko vulnerable sana na manyunyu ya mvua hata iwe ni ndogo tu) iko karibu na vyoo, na huko vyooni ndiko kuna hifadhi ya washiriki wa ziada (mapepo) wa Ibada zinazofanyika Kanisani hapo na hivyo kuna BAADHI ya wahudumu ambao huwa wanaanzia huko kwanza halafu wakitoka huko wanapanda moja kwa moja madhabadhuni na kuanza kuhudumu
  • Kawaida huwa wanapanda madhabahuni kupitia ubavuni mwa madhabahu wakiwa wanatokea vyooni, na si kwenye ngazi zilizoko upande wa mbele wa madhabahu
  • Washiriki hawa wa ziada (mapepo) huwa ni lazima wakae chooni, huko ndiko wanakopata hifadhi, hawawezi kukaa permanently Kanisani, sehemu ambapo Ibada huwa zinafanyika
  • Washiriki hawa huwa wanapatikana wakati wa maombezi ambayo huwa yanafanyika kila siku za wiki kuanzia Jumanne hadi Ijumaa
  • Kuna watu huwa wanakuja kutoka nje, wanatolewa mapepo, halafu mapepo hayo baadaye yanafanyiwa utaratibu wa kuhifadhiwa vyooni
  • Kazi ya kuyahifadhi vyooni huwa inafanyika na kikundi maalumu ambacho huwa kinajichanganya na waumini waaminifu, katika siku za maombi ya kuanzua saa 12.00 mpaka saa 2.00 usiku, pamoja na zile za maombi ya mkesha, ambazo ni Ijumaa usiku kuanzia saa 3.00 usiku na kuendelea Ndiyo maana ratiba ya maombi kwa nyumba hii ya Ibada huwa ni lazima kuanzia saa 12.00 jioni tu, na hakuna siku ambayo maombi yake huwa yanaanza kabla ya muda huo.
  • Isipokuwa tu kwa kipindi hiki cha Corona, ndiyo kumekuwepo na session nyingine mpya kabisa ya maombi yanayoanza saa 10:30 mpaka saa 12:00
Washiriki hawa ambao makazi yao maalumu (permanent) ni vyooni, huwa wanachukuliwa, na kuletwa kwenye Ibada kwa kutumia njia mbili:
  • MOSI: huchukuliwa kitaalamu kwa makusudi na wahusika wanaojua kuwa wamehifadhiwa humo na kuletwa kwenye Ibada
  • PILI: Wanaweza pia kuambatana na mtu mwingine yeyote anayeweza kuingia humo kwa shida yoyote ile, na kwa namna ile pasipo mhusika kuwa anajua, huweza kuambatana naye mpaka kwenye Ibada
Kazi yao kubwa kwenye Ibada ni kuhakikisha kuwa Ibada haifanyiki kama ambavyo waumini wa kweli na walio wengi, wangependa ifanyike.
  • Na kwa sababu waumini walio wengi hawako kwenye mpango huo na wala hawaujui, Ibada zinapokuwa zinaendelea wakati mwingine mapepo huzidiwa nguvu kutokana na upako wa watu wanaofanya Ibada, hivyo hulazimika kukimbia kwa muda
  • Inapotokea kuwa yamekimbia, kundi linalohusika hufanya tena jitihada ya kuyarudisha, kwa wiki inayofuata, Mbinu zinazotumika ni kwa kutumia aidha maombezi, maombi ya usiku au maombi ya mkesha. Kundi linalofanya haya ni dogo ila linashirikiana na uongozi, kiongozi mkuu wa kanisa akiwa mmoja wao, na washiriki walio wengi inaonyesha KAMA hawana taarifa ya kinachoendelea, na walio wengi huwa wanashiriki vizuri tu Ibada hizo ila pasipo kuwa na taarifa ya uwepo wa vitu vingine ambavyo huwa viko tofauti na Ibda.
  • Kwa hiyo cycle ya kuwa-restore washiriki hawa, yaani mapepo, huwa inafanyika kwa mtindo huo, na ndiyo maana maombi ni mengi zaidi kuliko mafundisho, ni kwa sababu kwenye maombi huwa kuna kazi ya ziada inayofanyika kisirisiri na ambayo wengi hawaijui
  • Tuchukulie kwa mfano kwa mwaka huu tangu uanze, kwa mara ya kwanza mafundisho yamefanyika J5 ya tarehe 15 April 2020, na kuanzia pale yameanza kufululiza kila j5 kwa sababu ya Corona. Kabla ya tarehe hiyo, tangu mwaka huu uanze, hapakuwahi kuwepo j5 ya mafundisho, isipokuwa maombi au kitu kingine ila si mafundisho
  • Sehemu nyingine inayotumika kuwahifadhi hawa washiriki ni kwenye “JENGO JIPYA” na ndiyo maana haliitwi KANISA JIPYA kwa sababu ukishaliita KANISA, kiroho unakuwa automatically umemu-deny pepo uhalali wa kupata hifadhi humo, japo si lazima kuwa ndiyo hawezi kabisa kukaa humo. Jitihada inayopaswa ikifanyika, bado anaweza kukaa humo pia
  • Na kwa mtindo uleule, kwenye JENGO JIPYA, namo pia pepo hawa huwa wanafikia hatua ya kutaharuki siku za Ibada halafu wanakimbia, na kazi ya kuwarudisha inafanyika tena wiki inayofuata kwa kutumia mkakati na mbinu zile zile kama nilizozieleza hapo juu
  • MHUSIKA ANADAI KUWA KUNA UWEZEKANO ZIPO PIA SEHEMU ZINGINE ZINAZOHIFADHI HAWA VIUMBE, NDANI YA NYUMBA HIYO YA IBADA. Kwa mfano, utafiti wake mpaka muda huu ameshajiridhisha kabisa kuwa kinyesi kilichokuwa kinatirrirka kutoka kwenye chemba za maji machafu, ilikuwa ni mojawapo ya hifadhi ya hawa viumbe. Walikuwa wanakaa kwenye harufu, na kwenye maji yaliyokuwa yamechanganyikana na kinyesi hicho, na ndiyo maana kinyesi hicho kilikuwa kinaachwa kitiririke makusudi!
SABABU ZINGINE ZINAZOPELEKEA KANISA LA ZAMANI KUENDELEA KUTUMIKA MPAKA MUDA HUU
  • Uchunguzi wa mhusika wa taarifa hizi unadai kuwa kuna kipindi washiriki hawa (mapepo) walionekana wamepotea kabisa, kanisani hapo, hasa kwenye Kanisa la zamani
  • Hali hiyo ilipelekea kiongozi mkuu kutengeneza utaratibu wa kufanya test ya kuhamia kwenye JENGO JIPYA, kwenda kuona kama kwenyewe labda kutakuwa kuna ahueni
  • Kwa hiyo Ibada za J2 mbili mfululizo zliifanyika kwenye JENGO JIPYA, lakini ikaonekana kwenyewe ndiyo hali ilikuwa mbaya zaidi, hawakwuwepo kabisa, Ibada zikawa almost haziendesheki
  • Baada ya kuona hivyo, ukatengenezwa utaratibu kupitia mafundi mitambo wa vyombo vya sauti na muziki, ikafanywa trick kiongozi mkuu akiwa amesimama madhabahuni anaongea, baadhi ya washiriki wakawa hawamsikii
  • Baadaye zikatolewa sababu kuwa kuna mwangwi kwenye jeingo jipya, na hivyo inabidi lisitumike kwanza.
  • Mbinu hii ndiyo ikasababisha kurudi tena kwenye kanisa la zamani, lakini ukweli ni kwamba hakuna mwangwi unaoweza kuwashibda mafundi mitambo kuurekebisha, tena kwenye kanisa ambalo hata kuta bado hazijawekwa.
Ni mchezo ulifanyika hapa na sababu zilizopelekea kufanyika mchezo huu ni kama ifuatavyo:
  • KANISA JIPYA, kama ambavyo yeye huwa analiita, kutokana na jinsi lilivyo, wakati wa Ibada za majaribio zilizofanyika kwa J2 mbili mfululizo, wakati wa Ibada, lilianza kutoa sauti zinazoimba (melody), ya hali ya juu sana; melody ambayo hata kichaa akiisikia, anajua kuwa kuna watu wa MUNGU wako kwenye Ibada. Melody hii ilichangia kwa kiwango kikubwa kusababisha mapepo yakimbie mbali zaidi, kitu ambacho hakikuwa kimetarajiwa
  • Pia BAADHI ya wahudumu wa Ibada (Praise and Worship) zinazohusiana na uimbaji, walikosa option ile ya kuanzia chooni halafu ndiyo mtu anapanda moja kwa moja madhabahuni, na kama ilivyo hadi sasa kwa madhabahu ya kanisa la zamani. Ni kwa sababu madhababu ya Kanisa jipya iko mbali na vyoo, na hata wale ambao wangetamani kufanya hivyo, with time wangeweza kuja kujulikana, kwa sababu ingebidi waonyeshe pattern fulani ambayo hata mtu ambaye hakuwa makini nao, angeweza kuiona; madhbahu ya Kanisa jipya iko mbali na vyoo, na wale ambao wangekuwa na tabia ya kuanzia chooni kwanza halafu ndiyo waelekee madhbabahuni, ingebidi waonekane na kila mtu
SABABU NYINGINE INAYOPIGILIA MSUMARI KU-SUPPORT KWAMBA KANISA JIPYA LIMETELEKEZWA KWA SABABU LINATOA MELODY NZURI SANA WAKATI WA IBADA, AMBAYO HAITAKIWII NA MAPEPO YANAYOHIFADHIWA HUMO
  • Kutokana na tahadhari ya ugonjwa wa corona, siku ya Ibada ya Ijumaa kuu tarehe 10/04/2020 ndiyo siku ya kwanza ambayo viti vilianza kupangwa umbali wa mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine, na hivyo ilibidi visambae hadi sehemu karibia yote ya kanisa jipya pia
  • Kutokana na hali hiyo, ilibidi spika za muziki na sauti zisambazwe hadi kwenye eneo hilo la Kanisa jipya
  • MELODY ya Ibada ya siku ya Ijumaa kuu ilikuwa nzuri muno, watu walikuwa wakiimba unasikika mziki mtamu utadhani unatokea mbinguni
  • Baada ya siku hiyo, Jumapili ya Pasaka ghafla zikaongezwa ngoma pamoja na sahani kwenye kikundi cha waimbaji wa Praise and Worship, vyombo ambavyo mhusika hakuwa amewahi kuviona vikitumika pale tangu aanze kuabudu pale mwaka 2011
  • Drums hizi zilizoongezeka zina tabia ya kusababisha kelele na kuchuja utamu wa mziki, na ndiyo maana zimeongezwa ili kuchuja ile melody ya mziki inayotokana na sauti ya waumini pamoja na vyombo vya muziki vinavyokuwemo ndani ya Kanisa jipya
  • Drums na sahani zimeongezeka kwa sababu JENGO JIPYA inabidi liendelee kutumika lote kwa ujumla wake mpaka pale Corona itakapoisha. Kabla ya hapo, lilikuwa linatumika sehemu tu, ambayo ilikuwa haihitaji sana mafundi mitambo kusambaza vyombo vya sauti na muziki ndani ya jengo hilo
  • Zaidi ni kuwa mpigaji drum ni mgeni, inaonyesha amehamishwa kutoka sehemu moja kuhamia pale kwa ajli ya kazi hiyo tu, hata hivyo cha kushangaza zaidi ni kuwa HAJAONEKANA AKIWEKEWA MIKONO MBELE YA MADHABAHU NA MBELE YA WASHIRIKI, KWA SABABU WAHUDUMU WOTE WANAOHUDUMU KWENYE KIKUNDI HICHO NI LAZIMA WAWE WAMEWEKEWA MIKONO. Huyu mgeni aliyekuja hajaonekena akipitia hatua hiyo, kwa sababu ameibuka ghafla siku ya J2 ya pasaka, na kabla ya hapo hakuwahi kuwepo Kanisani hapo
  • Kwa kumbukumbu zake za mbali sana mhusika wa taarifa hiii, yeye anadai kuwa kipindi cha nyuma kwenye miaka kati ya 2011-2013, aliwahi kuona drum hizo zimenunuliwa ila hakuwahi kuziona zimetumika. Zililetwa madhabahuni na kuonyeshwa na mhusika wa manunuzi mbele ya kanisa zima, lakini hakuwahi kuziona zimetumika tangu pale
  • Mbali na haya yote, Kanisa hili lilitakiwa kuwa limeshaanza kutumika mwaka jana, possibly muda kama huu, kama sikosei. Hela kwa ajili ya ujenzi wa madhabahu zilishachangwa nadhani zaidi ya mil 300. Baada ya hela kuchangwa ilifanyika kaziya kujenga kwanza ngazi za madhabahu kwa kutumia tofali tu na baada ya hapo pilika pilika zote zikasita hadi leo. Na kama madhabahu ilitakiwa kuagizwa kutoka China, bado kulikuwa na muda wa kutosha, kwamba madhabahu hiyo ingekuwa imeshawasili Dar es salaam hata kabla ya kuanza kwa gonjwa hili la Corona.
  • Mhusika wa taarifa hii anadhani kuwa pengine sasa hivi mtu akiuuliza uongozi kwa nini madhabahu bado haijakamilika, anaweza akaambiwa kuwa ni sababu ya Corona
Kwa hiyo KANISA JIPYA, almaarufu kama JENGO JIPYA, halitakiwi kutumika kwa sababu kuu mbili, noja ikiwa ni melody nzuri inayotokana na Kanisa hilo, kiasi kwamba imesababisha hadi drums za muziki ziongezeke kwenye timu ya waimbaji na pili ni kwa sababu linatumika kama hifadhi ya washiriki wengine wa kisirisiri ndani ya nyumba hiyo ya Ibada

Mhusika anatoa wito kuwa kama kweli kuna mwangwi umesababisha kanisa jipya lisitumike, anashauri iletwe timu huru ya wataaalmu wa vyombo vya muziki, ije iverify kama kweli kutna tatizo hilo. Nyumba ambayo haina hata kuta bado haiwezi kuwa na mwangwi ambao ni complicated kiasi cha kuwashinda wataalamu kuudhibiti. Nyumba zingine zina kuta na mwangwi hazina. Anadai kuwa ni rahisi zaidi kupata mwangwi kwenye nyumba iliyo na kuta, kuliko ile ambayo haina. Waletwe wataalamu waje wathibistishe hilo, kama upo uwezekano huo

KANISA JIPYA, ALMAARUFU KAMA JENGO JIPYA NA UHUSIANO AMBAO UMEKUWEPO KATI YAKE NA KIPINDI CHA KILA J2 CHA SOMO LA UANAFUNZI NA MAANDIKO

  • Inapotokea kuwa kuna somo la uanafunzi na maandiko, ambalo kawaida lilitakiwa kuwepo kila j2 ila huwa linakuwepo kwa mara chache sana, kiongozi mkuu huwa anasimama kidete kuwapanga watu kuhakiksha kuwa wamekaa kwa kusogeleana na kuenea ndani ya kanisa la zamani, wasije wakafikia hatua ya kusambaa hadi kwenye kanisa jipya, kiasi kwamba washiriki wa somo hilo inabidi wawe ni wale tu waliokaa na kuenea kwenye kanisa la zamani
  • Huwa anahakikisha anafanya hili kwa umakini mkubwa halafu baadaye anaondoka kwenda kunywa chai, yeye huwa siyo kawaida yake kushiriki somo hilo.
  • Pia huwa anahakikisha kuwa waumini walioko kwenye kanisa jipya ambao hawashiriki somo hilo, wamekaa mbali kiasi cha kutoweza kuwa wanasikia kinachofundishwa kwenye kanisa la zamani, ili isije kwa namna moja ama nyingine, mafundisho hayo yakawafikia halafu wakaambukiza upako kwenye JENGO JIPYA, na kusababisha washiriki wa akiba, kukimbia ndani ya jengo hilo
PEPO MAARUFU ANAYETAMBA KANISANI HAPO KWA SASA, ANAYETUMIA SAUTI ZA WATU NA ZA VYOMBO VYA MUZIKI, ALIYERUSHWA J5 YA TAREHE 15/04/2020 WAKATI WA IBADA YA JIONI YA MAFUNDISHO YA MAANDIKO MATAKATIFU
  • Alirushwa kwa kutumia “secret code” inayotumia neno “UZINZI”(Secret code hii ina maelezo yake ya kina na itafafanuliwa peke yake katika sehemu itakayofuata)
  • Ana uwezo wa kurushwa kwako kwa kutumia njia ya mtu kukusemesha, kukusalimia au kusemezana naye tu
  • Alirushwa na kiongozi yule yule aliyesemekana kuwa ni mhusika wa manunuzi ya Sanitizer, kwenye Ibada ya mafundisho ya maandiko matakatifu J5 ya wiki iliyofuata wiki ya pasaka
  • Kiongozi huyo alikaribishwa kuchangia kwa sababu somo liliendeshwa kwa mjadala, na kama kawaida yake, akataja neno UZINZI, ambalo tayari mhusika alishaling’amua kuwa huwa ni secret code ambayo huwa anaitumia kuita mapepo, na kipindi fulani nyuma amewahi kuitumia kwa karibia mwaka mzima
  • Wakati pepo huyo anarushwa, Ilikuwa j5 ya kwanza (kwa mwaka huu tangu uanze), kwa somo la maandiko matakatifu kufundishwa kanisani hapo. J5 zingine zote zilizopita tangu mwaka huu uanze, zilikuwa zinatumika kwa maombi kwa mara zilizo nyingi na au/semina/ibada za shukrani kwa mara chache sana
  • Kawaida siku zote, mafundisho ya j5 huwa yanaendeshwa na mtumishi mmoja wa Mungu kusimama mbele na kuanza kufundisha, wengine wakiwa wasikilizaji
  • Hata hivyo, KWA MARA YA KWANZA utaratibu siku hiyo ulibadilika, na ikabidi uwe wa majibizano, na kwa kutoa majibu ya maswali ambayo mchungaji mhusika alitoa maswali yake
  • Inaonyesha KAMA pepo huyu ana-operate vizuri zaidi katika mazingira ambayo sauti za watu wengi zinahusika, especially sauti moja kwa wakati na si kwa sauti ambazo ni za jumla kama vile za watu wanaoimba kwa pamoja au wanaofanya maombi kwa pamoja
  • Kuanzia pale sasa, hata vipindi vingine vilivyofuata vya mafundisho ya j5 imebidi sasa viwe kwa mtindo huo wa majadiliano. Maelezo yalitolewa kuwa utaratibu huo ni agizo kutoka ngazi za juu, kutokana na ratiba za J2 kuingiliwa na ugonjwa wa corona
  • Ukiangalia kuiuhalisia, agizo hili linapingana na tahadhari ya corona kwa sababu inabidi sasa mic moja ya kuongelea ishikwe na mikono isiyopungua kumi ndani ya lisaa limoja, na mouth piece itumike na midomo isiyopungua idadi hiyo hiyo na ndani ya muda huo huo. Sasa mtu hapa atajiuliza maswali, hii ngazi ya juu iliyotoa agizo hili, yenyewe haikuona hoja hii ya wazi juu ya tahadhari ya Corona, hoja iliyo wazi namna hii wala haijajificha?
  • Inaonyesha KAMA “test signal” ya J5 ya tarehe 15 siku ambayo somo la kwanza lilifundishwa kwa mwaka huu ilizaa matunda bora zaidi na yaliyokusudiwa na hivyo sasa kuanzia pale ikapendeza kuwa mafundisho yote ya siku za J5 yawe ya majibizano
  • Kuanzia pale sasa hata siku zingine zote za j5 mafundisho ni kwa njia ya majibizano mpaka pale corona itakapoisha
  • HATA HIVYO MHUSIKA ANAOMBA KUSHAURI KINYUME CHAKE. MAFUNDISHO HAYA YA J5 YAFUATE UTARATIBU KAMA ILIVYOKUWA ZAMANI KABLA YA CORONA, YAANI MTU MMOJA KUSIMAMA MBELE YA HADHIRA, NA KUFUNDISHA, NA PASIWE NA MAJIBIZANO MPAKA PALE CORONA ITAKAPOISHA
  • Pepo huyu anayejadiliwa hapa, ana uwezo wa kusambaa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia maongezi
  • Ana uwezo wa kushambulia kupitia sauti ya mtu unayemsikiliza akiongea redioni, anaweza kupitishiwa kwenye sauti ya redio kwenye mita band ulizotune radio yako
  • Ana uwezo wa kushambulia sauti ya chombo chocote pia. Nyumbani kwake mhusika wa habari hii, tayari ameshaharibu micro-wave oven kupitia alarm ile ya micro-wave ambayo huwa inapigwa muda wa kupasha/ kupika chakula ukishatimia. Alishambulia micro wave kupita alarm hiyo ambayo huwa inaita ili mtu akatoe chakula kwenye micro-wave kikishakuwa tayari kimeshapata joto
  • Pia ameshaunguza pasi ya kunyooshea nguo, alikuwa akisikiliza mahubiri redioni wakati akiwa ananyoosha nguo
  • Kwa hiyo anaweza pia kushambulia sauti za vyombo vya muziki vitumikavyo kanisani wakati wa Ibada, na hasa vile ambavyo vinakuwa havijawekwa wakfu, au vile ambavyo vinaweza kuwa viliwekwa wakfu kwa kuegesha, ili baadaye vitumike kwa kusudi jingine
  • Na hapa mhusika pia ana wasiwasi sana na drums zilizoongezeka kwenye vyombo vya Ibada kuanzia J2 ya pasaka
  • Ana uwezo pia wa kurushwa kwa kutumia sauti ya mtu aliyesimama madhabahuni akitoa neno au mahubiri
Mwisho kwa sehemu hii:

Mhusika wa tukio anadai kuwa yeye si mtaalamu sana wa mambo haya ya kiroho na hivyo kuna sehemu pengine anaweza kuwa ametoa maelezo ambayo hayako sawa, especially kuhuisana na sehemu ambazo mapepo wanahifadhiwa, lakini UHAKIKA NI KUWA HAWA MAPEPO WAPO KANISANI HAPO NA PIA WANAHIFADHIWA. Kama kuna sehemu atakuwa amekosea, basi itakuwa ni sehemu ambapo mapepo wanahifadhiwa, ila utakatishaji au urutubishaji wa mapepo hayo upo hilo hana shaka nalo!

NITARUDI

SEHEMU INAYOFUATA

POPULAR KEY WORDS AU POPULAR SECRET CODES ZINAZOTUMIKA KUWAITA MAPEPO NA /AU KU-ACKNOWLEDGE UWEPO WAO, WAKATI WA IBADA

UPDATE: TUESDAY 05/05/2020

POPULAR KEY WORDS AU POPULAR SECRET CODES ZINAZOTUMIKA KUWAITA MAPEPO NA /AU KU-ACKNOWLEDGE UWEPO WAO, WAKATI WA IBADA


Zaweza kuwa zipo nyingi, ila yeye mpaka muda huu ameshaainisha njia mbili ambazo ni

  • Njia ya kupiga makofi maalumu, ambapo makofi haya nayo yamegawanyika katika makundi mawaili kama alivyoyaanisha hapa chini
  • Kutumia secret code inayotumia neno “UZINZI”
MAKOFI MAALUMU

Makofi haya yamegawanyika katika makundi mawaili, na anaposema makofi maalum, anamaanisha kuwa si makofi yote yanayopigwa kanisani, yanaangukia katika kundi hili la makofi kwa ajili ya mapepo, hapana. Pia ieleweke kuwa makofi ni sehemu mojawapo ya shamrashamra za shangwe kwa waumini wanapokuwa wapo kwenye Ibada Kanisani kama ilivyo sehemu zingine za mikusanyiko ya watu wengi

Hata hivyo mhusika hapa anapenda kuongelea aina fulani ya makofi maalum ambayo huwa yanapigwa kwa namna ya kipekee sana, wakati wa (kuzindua /au mara baada ya kuhitimisha) ibada ya kusifu na kuabudu, aidha kufuatia “OMBI MAALUM” kutoka kwa mtumishi wa Mungu anayetoa sala madhabahuni au kufuatia “OMBI AUTOMATIC” ambalo huwa analitoa mtumishi huyo, kama itakavyofafanuliwa hapa chini

“OMBI MAALUM” LA MAKOFI

Hili hutolewa na mtumishi akiwa amesimama madhabahuni, mara baada ya kuwa ameongoza sala ya kuhitimisha Ibada ya Kusifu na Kuabudu. Akishahitimisha sala kwa kusema “…… NA WOTE TUSEME AMINA” na watu wote kujibu wito huo kwa kuitikia AMINA, mtumishi huyu huendelea mbele na kuwaomba wale ambao hawakuweza kustahimili kusimama katika kipindi chote cha Ibada ya kusifu na kuabudu (ambao wakati huo huwa tayari wameshakaa), nao pia wasimame, halafu watu wote kwa ujumla wao huombwa kupiga makofi mengine kwa ujumla wao. Ukiona hivi kwenye Ibada, ya J2 ujue kuwa kwenye maombi ya ijumaa iliyopita kuna kitu kilifanikiwa, mhusika anarudisha acknowledgement kwa mapepo waliofanikiwa kuhifadhiwa usiku huo na wanakuwa wako active kwenye Ibada ya J2 hiyo. Huu ni utafiti wa muda mrefu na ana uhakika nao zaidi ya 100%

“OMBI AUTOMATIC” LA MAKOFI

Hili ni ombi ambalo huwa linaunganishwa kwenye sala na mtumishi wa Mungu, sala ambayo inaweza kuwa aidha ni ya kufungua Ibada ya kusifu na kuabudu au ya kufunga Ibada hiyo. Mtumishi anayetoa sala madhababhuni akishafikia hatua anataka kuhitimisha sala hiyo, (lakini bado akiwa anaendelea nayo), automatically anaanza kutamka maneno kama haya “… TWAINUA MIKONO YETU, TWASIMAMA WIMA WIMA MUNGU WETU, TWAKUPIGIA MAKOFI YA SHANGWE.

Hapa mtumishi akishasema tu maneno “TWAKUPIGIA MAKOFI YA SHANGWE” tayari makofi yanakuwa yameshaitika kwa kasi ya ajabu muno, sababu watu wanajua wapo Kanisani kwa ajili ya kumshangilia Mungu, wakati kumbe kuna vingine wanazungukwa pasipo wao kuwa wanajua

Tofauti na yale ya mwanzo, nakofi haya ya aina hii ya pili huwa yana sifa zifuatazo

  • Hupigwa kabla neno “AMINA” (neno kwa ajli ya kuhitimisha sala), halijatamkwa
  • Kwa hiyo neno “AMINA” huwa linakuja kutamkwa baada ya makofi kuwa yameshapigwa tayari
  • Baada ya hapo, hakuna tena makofi yanayopigwa, japo kwa mara chache sana inaweza ikatokea, mtumishi akaomba tena kwa kusema ‘TUMSHANGILIE TENA BWANA YESU” na hivyo makofi mengine hupigwa tena KWA MARA YA PILI, ambayo sasa haya ndiyo yale makofi ya kawaida yasiyokuwa na ila
Kwa hiyo mhusika anachojaribu kusema hapa ni kwamba, wakati wa kuhitimisha sala yoyote ile wakati wa Ibada, makofi ya kawaida ni yale tu yanayopigwa baada ya neno AMINA, na kunakuwa hakuna makofi mengine yaliyotangulia kupigwa kabla ya neno hilo

Hata hivyo kuna kundi jingine la tatu la makofi ambayo bado mhusika anayafanyia utafiti, bado hajajua kama yako kawaida ama la. Haya huombwa kupigwa baada ya mtu mgeni kupita mbele madhabahauni na kumkiri Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wake

  • Kawaida mtu akishapita mbele na kuongozwa sala ya Toba, kanisa zima huwa linaombwa pia kumuombea katika muda ule ule ambao anakuwa anaongozwa sala ya toba
  • Mgeni huyu, huongozwa sala hiyo na mtumishi wa Mungu, kwa kutumia kipaza sauti na Kanisa zima huwa linasikia maneno anayoelekezwa atamke
  • Hata hivyo kumeshawahi kujitokeza scenario ambazo mtu anayeongozwa sala ya toba akiwa mbele madhabahuni, kwa sala anayoongozwa kutokusikika na waumini, yaani muongozwa sala na muongozaji wanakuwa wanasikilizana wao wawili tu pale mbele ya madhabahu
  • Pia, wakiwa wanaongozana sala hiyo ya toba, Kanisa linakuwa halijaambiwa kumuombea muongofu mpya, linakuwa liko kimya tu linasubiria wamalizane kwanza
  • Wakishamaliza kuongozana sala hiyo, ndipo sasa Kanisa zima huombwa lisimamame na kushangilia kwa makofi mengi, kwa mantiki kuwa mtu mmoja akiokoka malaika mbinguni hufrahi na hushangilia
Makofi haya ya mtindo huu siyo popular sana, japo na menyewe yana mshikeli, kwamba mwongofu mpya anaongozwa sala ya toba kimyakimya halafu badala ya kanisa kuombwa limuombee kama ilivyo kawaida, linaombwa kusimama na kupiga makofi

Vinginevyo makofi mengine Kanisani ukiondoa haya yaliyotajwa hapa, inaonekana ni ya kawaida na ni kwa ajili ya Utukufu wa Mungu kama ambavyo waumini walio wengi wanakuwa wamekusudia. Kama yapo mengine ambayo yana kasoro, basi kasoro hizo ziko juu ya uwezo wa kirho wa mhusika, na kwa sababu tayari ameshachochea mada, wataalamu zadi lazima watajitokeza na kuendelea kurekebisha pale ambapo pataonekan kuwa yeye bado hana uwezo wa kupafikia

NITARUDI

SEHEMU INAYOFUATA

Neno “UZINZI” kutamkwa wakati wa Ibada na mtumishi wa Mungu kama njia ya kuita mapepo

  • NENO UZINZI KUTAMKWA NA MTUMISHI ESPECIALLY AKIWA AMESIMAMA KWENYE MADHABAHU kwa nia ya kuita mapepo
  • NENO UZINZI LILIVYOTUMIWA NA NABII AKIWA AMEPEWA RIDHAA NA KIONGOZI MKUU, KUSIMAMA KUHUBIRI MADHABAHUNI NA KUTAMKA MANENO YA NGUONI KWA WANAUME WOTE KANISANI HAPO AKISEMA “MNAWAGEUZA NYUMA WAKE ZENU”
  • Watoto walikuwa na wazazi wao siku hiyo kwenye Ibada
  • Wazazi walikuwa na wakwe zao wa kike na wa kiume, kwenye Ibada
  • Wazazi walikuwa na familia zao kwenye Ibada
Hata hivyo, baada ya neno hili UZINZI kuwa decoded, imeonekana kuwa ilikuwa ni secret code ambayo ilibidi kutengenezwe mazingira ambayo ni exaggreted, ili code hiyo ipate uhalali wa kutamkwa mbele ya waumini, na ili iweze kufanya kazi yake kama iliyokuwa imekusudiwa. In fact, uchunguzi ulikuja kubaini kuwa hapakuwa na uzinzi wa aina hiyo kama ilivyokuwa inadaiwa

UPDATE: WEDNESDAY 05/05/2020 (NYONGEZA MUHIMU)

UHUSIANO WA NCHI YETU NA MATETEMEKO YANAYOENDELEA KUTOKEA HASA KATIKA KIPINDI HIKI


Mhusika wa taarifa hizi anaomba awarudishe nyuma kidogo kuanzia mwaka 2005

Tanzania ipo kwenye ukanda wa matetemeeko, kutokana na ukweli kwamba baadhi ya sehemu zake ziko ndani ya Bonde la Ufa, likiwemo ziwa Tanganyika. Hata hivyo, kabla ya mwaka 2005 kurudi nyuma, matatemeko makubwa (au hata madogo) na yenye madhara yamekuwa ni nadra sana.

Kwa hiyo kwa ufupi anaomba muangalie matukio haya matatu hapa chini
  • Desemba 2005 lilitokea tetemeko ndani ya Ziwa Tanganyika lenye ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo cha Ritcher
  • Mwaka 2012 (April au June) lilitokea tetetemeko likatikisa majengo yote marefu Dar es Salaam na kusababisha taharuki kubwa jijini siku hiyo. Lilitokea ndani ya bahari takriban kilomita 70 kutoka pwani ya Dar es Salaam, na kwenye uelekeo wa Mafia. Hata hivyo, hii ni sehemu ambayo haitarajiwi sana kwa tetemeko kutokea, japo uwezekano pia upo lakini kwa baadhi ya wataalamu waliosomea maswala ya Jiolojia, walidai kuwa “is almost geologically impossible” kwa tetemeko kutokea sehemu hiyo na ilikuwa mara ya kwanza kwa sehemu hiyo kutokea tetemeko katika Historia ya nchi yetu
  • Pia Septemba 2016 lilitokea tetemeko na kusababisha maafa Kagera, na lilitokea kwenye maji ndani ya ziwa Victoria
Yapo pia matetetemeko mengine ambayo yameshatokea na kusababisha madhara pia, tukianzia huo mwaka wa 2005 lakini mhusika angeenda kwa sasa kuyamulika haya matatu tu aliyoyataja hapo juu

Awali ya yote, anapenda kuujulisha umma wa wa-Tanzania kuwa mtaalamu aliyekuwa anasomea haya mambo ya matetemeko, alirudi kutoka masomoni Ulaya mwaka 2003, na matetemeko yote yaliyotokea baada ya 2003, yametokea akiwa tayari yupo kazini.

Ukiyaangalia matetemeko matatu yaliyotajwa hapo juu, utakuta kuwa yana sifa kuu nne zinazofanana, kwamba yote
  • Yametokea kwenye maji (Baharini, Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria)
  • Yametokea kwenye sehemu ambazo kuna uwezekano wa kupatikana Oil na Gas
  • Data za matetemeko hutumika kwa ajili ya utafiti wa Oil na Gas. Kwa hiyo matetemeko haya kutokea sehemu kama hizi, yaliashira pia uwezekano wa kutoa mwanga wa kuweza kujua hilo
Ikumbukwe kuwa kabla ya Serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani, umeme uliokuwa unatiliwa mkazo zaidi ni ule wa Oil na Gas, ukilinganisha na umeme wa maji, na kuna siku niliwahi kumsikia mwanasiasa maarufu akithibitisha kuwa msomi mmoja nadhani Profesa mstaafu kutoka UDSM, aliwahi kufanya utafiti ulioonyesha kuwa haiwezekani kujenga bwawa la kuzalisha umeme wa maji, bwawa ambalo ndiyo linajengwa sasa hivi huko kwa kutumia maji ya mto Rufiji
  • Kwa hiyo inaonyesha KAMA umeme wa maji ulikuwa hautakiwi kuwepo kwa sababu ungeweza kuziba ule wa Oil na Gas
  • Inaonyesha KAMA mpango wa Oil na Gas ulikuwa ni mkakati uliaonza kuandaliwa siku nyingi nyuma, na unaweza ukawa unahusisha wasomi kwenye taasisi maarufu na nyeti, walio bado ofisini muda huu na wengine ambao tayari wanaweza kuwa wameshastaafu kwa sasa
  • Inaonyesha KAMA mpango huu ulikuwa na wafadhili wenye uwezo wa kutoa pesa nyingi kwa ajili ya utafiti wa Oil na Gas, pesa ambazo zisingepatikana just in case Tanzania wange-opt kuzalisha umeme wa maji kabla
MAELEZO MAFUPI NAMNA AMBAVYO DATA ZA MATETEMEKO HUTUMIKA KWENYE UTAFITI WA OIL NA GAS

Kwa waliosoma Fizikia, mawimbi yanayosababishwa na tetemeko, husafiri ardhini na kupita kwenye miamba, kwa kufuata kanuni za namna mwanga ambavyo huwa unasafiri kwenye kitu chchote kile. Kawaida mwanga:

  • Husafiri kwenye mstari ulioonyooka, pale unapokuwa unasafiri ndani ya kitu husika (media)
  • Huakisiwa (reflected) na au /husharabiwa (refracted) pindi unapokuwa unasafiri kutoka kwenye media moja na kuingia kwenye media nyingine tofauti
  • Mwanga unaposharabiwa na media fulani, media hiyo inaweza kujulikana ni kitu gani, kwa kutumia kanuni ya refractive index. Refractive index ya mwanga inajulikana na hivyo chochote kile kinacchoweza kuusharabu mwanga, refractive index yake lazima nayo ijulikane pia, na ikishajulikana, lazima kitu hicho kijulikane ni nini
Tukirudi sasa kwenye mada yetu, mawimbi ya matetemeko nayo vilevile husharabiwa na media iliyoko ardhini, pindi yanapokuwa yanasafiri ardhini, na yakishasharabiwa, kitu kilichoyasharabu lazima kijulikane ni nini, na hivyo kama yamepita sehemu ambapo kuna Oil au Gas, watafiti sasa wanaweza kujua kuwa hapa kuna Oil na au Gas. Kwa hiyo nadharia rahisi kabisa ya uhusiano uliopo kati ya matetemeko na utafiti wa oil na gas, iko namna hiyo

Kwa mantiki hiyo basi, unahitaji uwe umepima matetemeko kwanza sehemu yako ya utafiti wa Oil na Gas halafu ndiyo uweze kujua kama ipo ama la. Kama sehemu ambayo unahitaji kufanya utafiti huo haina matetemeko ya asili ambayo yameshawahi kutokea na yakapimwa, njia pekee unayoweza kutumia ni kusababisha tetemeko, yaani unatengeneza tetemeko la kibinadamu

HYPOTHESIS ALIZONAZO MHUSIKA WA TUKIO HILI KUHUSIANA NA MATETEMEKO MATATU ALIYOYATAJA HAPO JUU
  • Inaonyesha KAMA matetemeko aliyoyataja hapo juu ( na si hayo tu, yanaweza kuwepo na mengine pia), yalikuwa ni ya kutengeneza (hayakuwa ya asili), kwa ajili ya utafiti wa Oil na Gas
  • Inaonyesha KAMA mhusika alijikuta kwa bahati mbaya akiwa miongoni mwa wahusika wa mtandao huo ambao ulikuwa ni wa siri, lakini mtandao huo ukawa umeshindwa namna ya kumchuka ili awe mmoja wao, ili aweze kutunza siri kama kuna chochote cha ajabu kinaweza kutokea huko mbele ya safari. Kwa mfano, makosa yangefanyika kwa tetemeko lile lililotokea baharini na kusababisha maghorofa kutikisika jinni Dar es salaam. Tuseme tetemeko hili lingeangusha baadhi ya majengo makubwa jijini Dar es salaam na kuua maelfu ya watu! Alitakiwa awe mmoja wao ili aweze kutunza siri kama hizi!
  • Baada mtandao huu kuona kuwa hauna namna ambayo unaweza ukamfanya akawa mmoja wao, ndiyo vikaanza sasa vitimbi hivyo, network ikawa imesukwa kuanzia ofisini, nyumbani anapoishi, Kanisani na sehemu zingine zote ambazo huwa anatokea kuwepo.
  • Uhakika mkubwa kabisa alionao ni kuwa kiini cha mtandao huo kilianzia ofisini
  • Kanisani sasa nako kukatafutwa watumishi wale amabao wapo kwa ajili ya MBESA TU, WACHUMIA MATUMBO, na kukawa na mwitikio mzuri tu na ndiyo sasa ilipofika kipindi hiki cha Corona, zikaanza kutumika mbinu mpya kwa kutumia ubunifu wa Sanitizer.
Unfortunately kumbe tayari alishachoka sana na upumbavu huu, kwa hiyo akasema ENOUGH IS ENOUGH, akasema sasa safari hii come sun come rain, public lazima ijue ni nini kilichoko nyuma ya pazia

ANADHANI SASA KWA MAELEZO HAYA MAFUPI, MNAWEZA KUENDELEA NAYE PASIPO MASWALI MENGI KICHWANI. Maana watu wamekuwa wakiulza maswali sana.

HATA HIVYO BADO ANAKARIBISHA SANA MASWALI TENA KWA WINGI KWA WALE AMBAO WANAYO

Muhimu tu anachopenda kuwausia wa-Tanzania ni kuwa inabdi wawe waelewa, na wenye kupima mambo kwa jicho hata la kumi, kama inawezekana. You can just imagine “a mere layman” kama huyu bwana anakumbana na mambo kama haya, ije iwe mtu ambaye mmemkabidhi Nchi na anamiliki vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Nchi yenu? Mtu anapowaambia kuwa DIESEL imetest POSITIVE kwa Covid-19 inabidi muelewe!

Kumbukeni kuwa huyu bwana anachowakilisha kwenu kwa sas bado ni HYPOTHESIS, ila na nyie mtazipima na kuona kama kweli hizi bado ni hypothesis tu au pengine you at least need to ratify them to a single, unified theory

ATARUDI KWA AJILI YA KUENDELEA NA MADA ILIYOPO HEWANI SIKU ZOTE.

UPDATE NO 2: WEDNESDAY 05/05/2020

NENO UZINZI KUTUMIKA KAMA SECRET CODE YA KUITA MAPEPO


Kuna scenerios kama tatu au nne hivi zinazothibitisha hili
  • Neno hili lilitokea kutawala matukio kwa karibia mwaka mzima, mwanzilishi wake akiwa ni kiongozi yule ambaye anasemekana kuwa ndiye mhusika wa manunuzi ya Sanitizer
  • Akiwa ametoka safari kwenye mikutano ya Injili, alisimama madhabahuni na kuanza kuhubiri kuhusiana na uzinzi
  • Mwishoni mwa Ibada alitoa wito kwa wale wote ambao ni wazinzi wapite mbele madhabahuni kwa ajili ya msaada
  • Pia alitoa wito kwa wale ambao wamekuwa wakipatwa na tatizo la kufanya mapenzi wakiwa usingizini/ ndotoni nao wapiti mbele
  • Kosa pekee alilofanya siku hiyo ya kwanza, akiwa anaendelea na mahubiri yake alipitiwa akatamka maneno haya (siyo exact quote, ya kile alichosema) kuhusiana na wale ambao wamekuwa wakiwa na tatizo la kufanya mapenzi usingizini. “Wakati mwingine jitu liko usingizini linafanywishwa mapenzi hadi linafikia hatua ya kupiga kelele,……., Mungu atusaidie sana wapendwa”
  • Statement hii ilitoa taswira kuwa kumbe wanaofanyishwa mapenzi usingizini, kwake ni majitu, na si kwamba ni watu ambao anawaonea huruma yeye kama mtumishi wa Mungu
  • Ilitoa picha pia KAMA waathirika wa kufanyishwa mapenzi usingizini ni maadui zake
  • Kosa la pili lililofanyika ni kuwa baada ya wahusika kuitwa madhabahuni, binti mkubwa wa kike wa Kiongozi Mkuu wa Kanisa, pamoja na binti wa kike wa kiongozi aliyekuwa anahubiri, nao pia walipita wakiwa mojawapo ya wahusika/ waathirika
  • Kosa la tatu, kati ya waliopita pale mbele madhabahuni, zaidi ya asilimia 90 zilikuwa ni sura ngeni kabisa, wengi wao wakiwa watoto ambao ni teenagers! Teenagers wenyeji kawaida huwa wanakuwa wako sehemu yao kwenye Ibada yao, huwa hawachangayikani na wakubwa. Cha kushangaza siku hiyo kulikuwa na utitiri wa teenagers wengi sana pamoja na sura zingine mpya kabisa kanisani hapo
  • Mhusika anadai kuwa hapa watu ianbidi wakubaliane na fact hii kwamba: sura ngeni ambayo mtu hajawahi kuzoea kuiona mahali pa mkusanyiko wa watu wengi ambapo yeye ni mwenyeji siku zote, lakini sura hiyo nayo ipo pale siku zote sema tu hajazoea kuiona kwa sababu ya uwingi wa watu, INA MUONEKANO TOFAUTI USONI, ukilinganisha na sura ngeni ambayo yenyewe imevamia mahali pale kwa siku hiyo tu, kwa kuamini kuwa haiwezi kujulikana kuwa ni sura ngeni pale kwa sababu ya uwepo wa watu wengi. Hawa watu wawili mionekano yao usoni huwa iko tofauti.
  • Kwa maana nyingine ni kuwa sura ngeni ambayo huwa inafika kwenye Ibada kila j2 ila kwa bahati mbaya tu hamjatokea kufahamiana, ina muonekano tofauti sana na sura nyingine ngeni kabisa ambayo inaweza kuwa imefika kanisani hapo kwa mara ya kwanza, au ambayo huwa inahudhuria Kanisani hapo mara chache sana na kwa matukio maalum tu. Hawa watu wawili kwa mtu anayejua kuangalia nyuso za watu kisaikolojia anaweza kuwatofautisha kirahisi tu
  • Kwa hiyo ilionyesha wazi kabisa siku hiyo kulikuwa na wageni waliokuwa wamealikwa kwa ajili ya kuja kupita mbele ya madhabahu, na sura zao zilikuwa zinasema hilo kuwa ni wageni pale na ambao huwa hawafiki pale mara kwa mara au walikuwa wamefika pale siku hiyo kwa mara ya kwanza
  • Wakati haya yanafayika siku hiyo, kiongozi mkuu alikuwa tayari ana wiki kdhaa bila kupanda madhabahuni, yaani alikuwepo pale kanisani ila hakuwa akipanda madhabahuni kwa ajili ya kuhubiri
  • Baada ya J2 hiyo kupita, IMMEDIATELY J2 ILIYOFUATA, Kiongozi Mkuu alirudi tena madhabahuni na kuanza kuhubiri tena
Baada ya wiki kadhaa tena kupita
  • Ikatokea tena kiongozi mkuu akapotea madhabahuni, yaani akawa hapandi madhabahuni kutoa huduma
  • Akatokea tena mhubiri yuleyule na akiwa amerudi kutoka safari ile ile ya kwenye mkutano wa Injili
  • Mahubiri yaleyale ya uzinzi na kufanya mapenzi ndotoni
  • Wahusika wale wale waliopita madhabahuni, sura nyingi ngeni za teenagers pamoja na baadhi za watu wazima na binti yake mhubiri akiwa tena mmojawao
  • Tofauti ni kuwa sfari hii binti wa kiongozi mkuu hakujitokeza, na hakuwahi kujitokeza tena kwa safari zote zilizofuata
Maswali yakawa yanaanza ku-click kichwani kwamba hawa mabiinti wa viongozi, hata kama kweli ni wazinzi, wanashindwa kuwa na aibu kwamba kila siku mzazi wao anasimama madhabahuni kuita wazinzi na wao wanajitokeza bila aibu? Sababu kuu zilizosababisha mhusika ajiulize maswali haya ni kama ifuatavyo
  • MOSI: Binti ambaye ni mzinzi lakini ambaye wazazi wake ni watumishi wa Mungu, lazima awe na tabia ya kujificha ficha kuanzia kwa mtu mmoja mmoja hadi kikundi, na hivyo ni ngumu sana kwa mtu kama huyo kushindwa kujificha hasa akiwa kwenye kundi la watu wengi kama Kanisa zima. Hawa mabinti kama kweli walikuwa wazinzi, lazima wangetafuta namna ya kukwepa kuonekana mbele ya madhabahu.
  • PILI: Baadaye ilikuja kuonyesha KAMA hawa watoto walikuwa na ujasiri wa kupita mbele bila aibu kwa sababu walijua hawako hivyo na walipita kwa ajli ya kitu kingine ambacho wao walikuwa tayari wanakijua, ambacho siyo uzinzi
Ilionyesha wazi kuwa kama hawa mabinti kweli wangekuwa ni wazinzi, wasingekuwa na courage hiyo ya kupita mbele ya umati wa kanisa, baba yao akiwa ni mtoa wito. Mhusika alibaki mdomo wazi akijiuliza kuwa labda pengine wanapata mashambulio ya kufanya mapenzi ndotoni, lakini hilo nalo baadaye akaliondoa, kwa sababu mhubiri tayari alishaponda wale wanaofanyishwa mapenzi ndotoni, ingekuwa hivyo kwa binti yake angekuwa na huruma. Kwa hiyo hatimaye picha aliyokuja kuipata mhusika na ikakubalika ni kuwa hawa watu walikuwa upande ule wa wazinzi.
  • Baada ya J2 hiyo kupita tena, IMMEDIATELY J2 ILIYOFUATA, Kiongozi Mkuu alirudi tena madhabahuni kwa ajli ya mahubiri
Matukio haya yakapita na wiki kadhaa zikapita tena. Lakini mpaka hapa kukawa tayari kumeshaanza kujionyesha pattern kama ifuatavyo

  • Inaanza na kiongozi mkuu kupotea madhabahuni kwanza, kwa angalau wiki 2-3
  • Kiongozi mkuu akishapotea, hatimaye anakuja kiongozi mwingine anapanda madhabahuni akiwa ametokea kwenye mikutano ya injili
  • Kiongozi huyu anahubiri kuhusu uzinzi na mwishoni anatoa wito wa waumini kupita mbele, wale ambao ni wazinzi pamoja na wanaosumbuliwa na tatizo la kufanya mapenzi wakiwa usingizini
  • Baada ya J2 hiyo, IMMEDITELY J2 INAYOFUATA Kiongozi Mkuu anarejea tena madhabahuni
Kwa hiyo inaonyesha wazi kabisa kuwa:
  • Kila J2 aliyopanda madhabahuni mhubiri wa uzinzi, J2 ya nyuma yake, pamoja na J2 zingine kadhaa nyuma ya hiyo, mhubiri wake HAKUWA Kiongozi Mkuu; lakini
  • Kila J2 aliyopanda madhabahuni mhubiri wa uzinzi, J2 iliyofuata mbele yake na pengine na J2 zingine kadhaa mbele ya hiyo, mhubiri wake ALIKUWA Kiongozi Mkuu
Mhusika anapenda kutoa challenge kwa Kiongozi Mkuu kama anaweza kukanusha hili
  • Baadaye ikatokea tena kiongozi mkuu akapotea madhabahuni, safari hii kwa mara ya tatu sasa
  • Hata hivyo, safari kukawa na mabadiliko kidogo, katikati ya wiki kabla ya J2 ya Ibada
  • Ikatokea siku ya J5 ya mafundisho ya maandiko matakatifu, Nabii wa Kike akatoa unabii wakati somo bado halijaanza, waumini walikuwa bado wako kwenye Ibada ya kusifu na kuabdudu
Unabii wake ulihusu mambo mawili yafuatayo, kulingana na mpangilio wa namna nabii mwenyewe alivyoyataja:
  • Ibada za sanamu- watu wanafanya Ibada hizo
  • Uzinzi na uasherati
Baada ya hapo, kiongozi mkuu akasimama na kubadilisha program ya siku hiyo kutoka kuwa mafundisho na kuwa maombi, akisisitiza kuwa nabii ametaja jambo zito la uzinzi na uasherati, watu wakemee hilo. BAHATI MBAYA KIONGOZI MKUU AKAWA AMELISAHAU LILE LA IBADA ZA SANAMU, HAKULITAJA. Kwa hiyo kwa J5 hiyo waumini wakajikita kwenye swala la kukemea pepo la uzinzi na uasherati

Kwa hiyo hapa utaona kuwa
  • J5 ya mafundisho iligeuka na kuwa ya maombi
  • Nabii alianza kwa kutoa unabii wa Ibada za sanamu na hatimaye uzinzi
  • Kiongozi mkuu yeye akakamata kwenye uzinzi na kubadilisha Ibada kuwa ya maombi na si mafundisho tena
  • Kiongozi mkuu akang’ang’ania hoja ya uzinzi, ibada ya sanamu akaiweka pembeni
  • Jumapili iliyofuata nabii akapewa madhababhu kuhubiri juu ya unabii alioutoa J5 ya wiki hiyo
  • Nabii akaogopa kupanda madhabahuni alitaka ahubiri akiwa amesimama chini lakini watu wakamlazimisha apande juu
  • Nabii naye akajikita kwenye uzinzi, NAYE AKASAHAU TENA UJUMBE WAKE JUU YA IBADA ZA SANAMU
NITARUDI

UPDATE TUESDAY 12 MAY 2020

MAHUBIRI YA NABII KUHUSU UZINZI, KWENYE IBADA YA J2 ILIYOFUATIA J5


  • Nabii alisimama madhabahuni siku hiyo kwa ridhaa ya Kiongozi Mkuu. Akatamka maneno makali/ matusi kwa wanaume wote kanisani pale akiwaambia MNAWAGEUZA NYUMA WAKE ZENU”, ‘mbele ya waumini wote wakiwa na watoto, na wengine wakiwa na wakwe zao
  • Jioni ya J2 hiyo tena wasio kwenye ndoa wote wakakusanywa kwa maelekezo ya kiogozi mkuu
  • Kanisa lilikaribia kujaa hasa vijana, hali iliyoonyesha wazi kabisa kuwa kuna watu wengine wageni walikuwa wamepewa signal ya kuhudhuria kusanyiko hilo, ambao si washiriki wa Kanisa la hilo
  • Kanisa lilifurika na mahubiri yakawa ni yale yale ya uzinzi, likaongezewa kidogo na swala la wizi wa Zaka.
  • Wahusika walitakiwa kupita mbele madhabahuni na hatimaye Ibada hiyo ilihitimishwa na Kiongozi Mkuu akilalamika kuwa waliopita mbele si wote, isipokuwa kuna wengine wameamua kujificha
  • Huwa anafurahi zaidi wakipatikana watuhumiwa wengi wa kupita mbele ya madhabahu, hilo kabisa huwa halimsikitishi bali humpa furaha sana
Mpaka hapa mhusika wa tukio akawa amepata kitu kingine cha nyongeza kwamba haikuwa secret code tu ya neno uzinzi ambayo effect yake iklikuwa imekusudiwa kufanya kazi kupitia kusanyiko hilo, isipokuwa pia kitendo cha watu kupita mbele ya madhabahu nacho pia kilikuwa na mchango wake. Watu hawa walivyokuwa wanapita mbele, kulikuwa na kitu cha kiroho pia kilikuwa kinafanyika kwenye sehemu ya sakafu ile iliyoko mele ya madhabahu, ambapo watu hawa walikuwa wanakwenda kujipanga na kukanyaga kwa miguu yao pale. Yaani kuna watu ambao miguu yao ilikuwa inatakiwa ikanyage kwenye sakafu hiyo iliyoko mbele ya madhabahu hiyo, na hicho kitendo kilikuwa na maana yake kubwa

Baada ya hapo, wiki kadhaa zilipita tena na mtumishi mwingine alitumwa kusimama madhabahuni kwa ajili yak u-arrest roho ya uchawi na uzinzi Kanisani hapo. Kikubwa kingine alichofanya mtumishi huyo siku hiyo ni kitendo cha kukiri kuwa KUNA UCHAWI UNAENDELEA KANISANI HAPO KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU SANA, na siku hiyo aliiita watu wapite mbele wakiwemo wachawi na wazinzi

Mpaka hapa, mhusika anazidi kutoa hoja kuwa hata kama kweli hoja ya uzinzi ilikuwa ni genuine, inaonekana kuwa ilikuwa exaggregretd ili ku-save kusudi jingine tofauti na hoja yenyewe. Hii ni kwa sababu mtindo uliokuwa unatumika katika kutafuta ufumbuzi wa tatizo, haukuwa muafaka. Ulikuwa ni mtindo wa zimamoto na usiojali kuchambua wahusika halisi na wasiokuwa wahuiska. Hii inamaanisha kuwa assuming kweli uzinzi ulikuwepo, bado kilichokuwa kinafanyika hakikuwa na mlengo wa kutatua tatizo hilo.

TANGAZO LA KUFUKUZWA USHIRIKA MTU ALIYEKUWA AMEBADILISHA IMANI (AKAHAMIA DINI NYINGINE) NA KUFUNGA NDOA HALALI, KWA KUDAIWA KUWA NI MZINZI

Baada ya hapo, ilipita miezi kadhaa, ikatokea tena Kiongozi Mkuu akasimama madhabahuni kutangaza tangazo ambalo lilikuwa na utata ambao haukuhitaji mtu makini sana kuweza kuuona. Kiongozi huyu alisismama madhabahuni J2 moja na kutangaza kuwa amemtenga binti ambaye alikuwa muumini wake lakini amebadilisha imani na kufunga ndoa na mwanamme wa dini nyingine. Hili nalo tayari likawa ni tatizo kwa sababu mtu aliyebadilisha imani hakustahili kutangazwa kuwa ni mzinzi kwa sababu hakuwa tena kondoo wa zizini kwa kiongozi huyu

Mpaka hapa, hali bado inazidi kudhihirisha kuwa kulikuwa na “specially vetssed interest” kwenye issue hii ya neno uzinzi kwa sababu kiongozi huyu:
  • alianza tena ku-cross-cut na kuingia kwenye dini nyingine na kuepeleka mamlaka yake huko
  • angekuwa yuko sahihi tu kama angechukua hatua za kumtenga binti huyu wakati akiwa kwenye mahusiano na mwanamme wake NA KABLA HAJABADILISHA IMANI WALA KUFUNGA NDOA
  • kwa kipindi hicho, hakustahili tena kumgusa kwa lolote binti huyu. Ni kwa sababu alikuwa tayari ameshabadilisha inani, na zaidi kwamba, alikuwa tayari yuko KWENYE NDOA HALALI kupitia dini nyingine. Kwa hiyo iwe ni kwa itikadi za kanisa lolote lile, au dini yoyote ile, binti huyu hakuwa mzinzi kwa sababu tayari alikuwa kwenye mahusiano ya ndoa halali na kwa kufuata taratibu za dini ya kule alikokuwa amehamia
Mpaka hapa, inaonyesha KAMA kiongozi mkuu alikuwa anatafuta kila namna ya kupata nafasi ya kuhalalisha neno uzinzi na kulitamka akiwa amesimama madhabahuni.

Pia kitu kingine cha msingi kuangalia hapa ni kuwa kwa sababu Kanisani hapo huwa kuna mambo mengi sana ya ajabu ajabu yanaendelea, kuna uwezekano pia kuwa binti huyu alikuwa amenunuliwa na alijua kuwa tukio hilo litatokea. Vinginevyo kama haikuwa hivyo, basi nadhani atakuwa hata alishachukua uamuzi wa kwenda mahakamani, kama siyo kusamehe

NENO “JEINGO JIPYA” NALO KUTUMIKA PIA KAMA SECRET CODE

Utafiti umekuwa ukiendelea ambao mpaka mda huu, umethibitisha kuwa mbali na neno hili “JEINGO JIPYA” kutumika kama mlango wa kuruhusu mapepo waweze kuweka makazi yao kwenye “KANISA JIPYA”, neno hili pia limekuwa likitumika kama “SECRET CODE” ya kuita mapepo, na hiyvyo limekuwa likitumika DOUBLY.

Tukirudi nyuma kidogo, utafiti wa mhusika umeonyesha pasipo shaka kabisa kuwa ili neno liweze ku-qualify kama secret code, lazima liwe na sifa kuu mbili. Ni lazima liwe na tabia ya kutamkwa tamkwa mara kwa mara na watumishi wa Mungu:
  • Wakiwa (mara nyingi, japo si zote) wamesimama madhabahuni
  • Kwa kutumia sababu ambazo ni za kutengeneza na ambazo hazina ulazima sana wa kulifanya neno hilo liendelee kukaa linatamkwa tamkwa
Tukirudi sasa kwenye neno hili “JENGO JIPYA’ tunaona tena kwamba:
  • Ni neno ambalo lilitakiwa liwe linatamkwa “KANISA JIPYA’ lakini kwa makusudi limekuwa likitamkwa “JENGO JIPYA’
  • Ni neno ambalo angalau kila J2 lazima litamkwe na mtumishi wa Mungu akiwa amesimama madhabahuni
  • hutamkwa wakati watumishi wa Mungu wanapokuwa wanatoa matangazo; matangazo ambayo baadhi yake huwa ni mahitaji ya watu ambao ni wahitaji na wanahitjai Kanisa liwaombee
  • Kwenye mchakato huo wa kuombea wahitaji, badala ya Kanisa zima kuombea mahitaji yote kwa ujumla wake, kiongozi mhusika huamua kutengeneza makundi ya waumini kwa ajili ya kuombea mahitaji hayo (kitu ambacho siyo lazima na ambacho huwa hakileti tofauti yoyote) kulingana na mpangilio wa namna walivyokaa waumini Kanisani hapo
  • Kwa hiyo kiongozi huyo hulazimika kutamka maneno kwa mojawapo ya makundi aliyoyatengeneza akisema kwa mfano “waliokaa kushoto kwangu pamoja na walioko JENGO JIPYA, tutaomba kwa ajili ya……..”
  • Mtindo huu huwa unafanyika kila J2, na neno hili huwa linatamkwa kila j2, mwaka mzima
Inaonyesha wazi kabisa KAMA neno hili “JENGO JIPYA“ lilishatengenezewa mazingira ya kutamkwa tamkwa na watumishi wakiwa wamesimama madhabahuni, na kwa kutumia sababu ambazo hazina ulazima wowote wa neno hilo kukaa linatamkwa tamkwa, na hivyo linatumika kama secret code. Hii ni kwa sababu maombi ya wahitaji yangeweza kuwa yanatajwa tu halafu kanisa zima kwa ujumla wake linaingia kwenye kuyaombea pasipo kuwa limegawanywa gawanywa kwenye makundi

NENO UZINZI LAIBUKA TENA HIVI KARIBUNI KWENYE IBADA YA JIONI J5 YA TAREHE 15/04/2020

J5 ya tarehe 15/04/2020 ilikuwa ni siku ya kwanza tangu mwaka huu wa 2020 uanze, kwa Ibada ya mafundisho ya maandiko matakatifu kufanyika; na kwa mara ya kwanza Ibada hii ilifanyika kwa majibizano/ majadiliano, badala ya ilivyo kawaida siku zote, ya mtumishi mmoja kusimama na kufundisha somo wengine wakiwa ni wasikilizaji. Hata hivyo, baada ya utaratibu wa siku hiyo kuwa umetangazwa kabla ya mafundisho kuanza, mhusika wa taarifa hizi alitarajia kuwa lazima neno uzinzi litapata nafasi ya kutamkwa kwenye Ibada hiyo, na hasa baada ya kumuona mhubiri wa Ibada za uzinzi, akiwa miongoni mwa washiriki wa somo la siku hiyo

  • Ibada ilianza kwa majabdiliano. Kwa kuanzia waumini wa kawaida wakikaribishwa kuchangia kwanza halafu kule mwiashoni, wakapewa nafasi viongozi
  • Karibia mwisho wa Ibada, mhubiri wa uzinzi alikaribishwa na katika mchango wake, kweli alitamka neno uzinzi, sawia kabisa na matarjio ya mhusika wa taarifa hizi.
Labda kwa kukumbushia tena kwa kifupi tu kuhusu mtumishi huyu ni kwamba, ndiyo yule:
  • Aliyesemekana kuwa ndiye mnunuzi wa sanitizer
  • Ambaye mhusika wa taarifa hizi aligongana naye kwenye bomba la maji kunawa siku ya tukio la sanitizer
  • Binti yake walipishana uchochoroni na mhusika wa tukio hili siku ya tukio la Sanitizer na binti huyu ndiyo yule ambaye amekuwa kinara wa kupita mbele ya madhabahu pindi wazinzi wanapotakiwa kupita mbele, kwa j2 zote ambazo mahubiri ya uzinzi yamekuwa yakifanyika
NITARUDI

UPDATE: THURSDAY 14/05/2020

WANAUME WAOMBWA KUKUSANYIKA KWA DHARURA J2 ILIYOFUATA; BAADA YA ILE YA MAHUBIRI YA NABII
  • Wanaume wote waliombwa kukusanyika kwa muda, mara baada ya Ibada ya kwanza kuisha
  • Ilikuwa ni katika muda ambao huwa linafanyika somo la uanafunzi na maandiko, lakini siku hiyo halikuwepo
  • Wanawake na watu wengine wasiokuwa katika rika linalohusika, waliombwa kukaa mbali ili wasisikie kile kitakachojiri katika mazungumzo hayo
  • Mwenyekiti wa chama cha wanaume alisimama kwa ajili ya kukaribisha ushuhuda wa namna jinsi wanaume WALIVYOBARIKIWA NA UJUMBE WA NABII JUMAPILI ILIYOPITA, YAANU ULIOHUSU UZINZI
  • Alichangia mtu mmoja tu ambaye alionyesha kusikitishwa sana na ujumbe huo NAMNA ulivotolewa pasipo kuzingatia maadili, akionyesha kuwa hakuwa na tatizo na UJUMBE, bali alikuwa na tatizo na nama ujumbe ulivytolewa.
  • Baada ya mtu huyo mmoja kuchangia, maongezi yaliishia pale
KERO YA KUTOKUWA NA SIKU MAALUMU KWA AJILI YA KUSANYIKO LA WANAUME KANISANI HAPO, TOFAUTI NA ILIVYO KWA MAKANISA MENGINE
  • Mhusika anadhani kuwa nyumba hii ya Ibada ni kanisa pekee (kwa makanisa ya aina hii) ambalo wanaume hawana siku yao ya kukusanyika kwa ajili ya Ibada
  • Makanisa mengine ya aina hii, yana siku maalum katikati ya wiki kwa ajli ya wanaume kukusanyika na kufanya Ibada yao muda wa jioni
  • Kwa hiyo wanaume ni kundi pekee Kanisani hapo, ambalo halina siku maalum ya kukusanyika katikati ya wiki kwa ajlii ya Ibada. Makundi mengine yote yanazo siku kwa ajli ya Ibada za jioni katikati ya wiki
  • Mpaka hapa, inaonyesha KAMA kiongozi mkuu ameamua kwa makusudi kuzuia wanaume kuwa na siku yao ya Ibada, kuepuka uwepo wa mikusanyiko ya wanaume Kanisani hapo kwa sababu ni watu pekee ambao wakishakuwa pamoja, wana uwezekano mkubwa wa kuwa wanabadilishana mawazo pamoja na kujadil maswala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuhoji kama wataona kuna chochote ambacho kinaonekana kutokwenda sawa Kanisani hapo

KIKAO KINGINE CHA DHARURA CHA WANAUME KILICHOFANYIKA HIVI KARIBUNI TAREHE 26/04/2020
  • Tangazo la kikao hicho baada ya kutolewa na kiongozi mhsika, liliongezewa msisitizo na Kiongozi Mkuu kwamba wanaume wote wanatakiwa wakusanyike mara baada ya Ibada ya kwanza
  • Tofauti na kusanyiko nilililotaja hapo juu ambalo lenyewe alifanikiwa kuhudhuria kiongozi mmoja tu ukiondoa mwenyekiti wa wanaume, hili la sasa lilihudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo Kiongozi Mkuu na mwenyekiti pia
  • Kusanyiko hili lilifanyika katika mazingira sawa kabisa na ya lile la mwanzo ambalo mhusika amelielezea hapo juu
  • Mwenyekiti wa chama cha wanaume alisimama tena na kabla hajaanza kueleza ajenda ya kusanyiko, alianza kwa kurusha lawama nyingi sana kwa wanaume, kama siyo kuwafokea, akidai kuwa ni wazembe, hawa-respond kwenye utekelezaji wa program mbalimbali kanisani hapo pindi wanapokuwa wameitwa
  • Hoja hii haikuwa kweli kwa sababu kama nilivyotaja hapo juu, wanaume hawajatengewa siku yao kwa ajli ya Ibada na hivyo kama kweli ipo siku waliitwa na hawakuonekana, ni kwa sababu wanajua kuwa chama chao kinaendeshwa kisiasa, kwa hiyo watakuwa waliona ni ujinga
  • Kwa hiyo chama hiki cha wanaume, kinaoknekana KAMA kipo si kwa ajli ya IBADA, isipokuwa kwa ajili ya michango mbalimbali ya fedha pindi zinapokuwa zinahitajika, pamoja na kusherehekea sikukuu ya wanaume ambayo huwa inafanyika mara moja kwa mwaka
Vikao vyote hivi vya wanaume, vilikuwa ni vya dharura

MWANDISHI ATARUDI TENA

UPDATE NO 2: THURSDAY 14/05/2020

Kikao cha dharura cha wanaume kilichofanyika hivi karibuni kinaonekana kugongana sawia kabisa na mambo mawili makubwa
  • Kilifanyika J2 iliyofuatia ile ya mgogoro wa Sanitizer
  • Klilifanyika katika wiki ambayo J3 ya wiki hiyo, mhusika wa taarifa hizi aliamua kuanza kutoa rasmi taarifa za matendo anayofanyiwa yasiyomridhisha na mengine pia yanayoendelea Kanisani hapo, kupitia mtandao huu
Kwa hiyo ukizingatia mambo hayo mawili hapo juu, ukiunganisha na mood aliyokuwa nayo mwenyekiti wakati anafungua kikao, inaonyesha KAMA:
  • Mwenyekiti aliamua kutumia lugha ya ukali na kufoka sehemu ambayo haistahili, yaani kanisani, na kwa sababu ambazo hazikuwa za msingi, akiwa na lengo la kutafuta targets ambao alijua huwa hawawezi kuvumilia kusikiliza ujinga, mhusika wa taarifa hizi akiwa mmoja wao
  • kwa vile mhusika wa taarifa hizi alikuwa tayari ameshaazisha kitu ndani ya wiki hiyo, inaonyesha pia KAMA mojawapo ya potential targets zilizokuwa zimekusudiwa alikuwa ni yeye
Na kama ni kweli kwamba yeye alikuwa ni potential target:
  • haina shaka kuwa kulikuwa na kitu kikubwa kilikuwa kimeandaliwa kwa ajili yake nyuma ya pazia, ambacho yeye alikuwa hakijui, na ndiyo maana hata viongozi karibia wote walikuwepo, akiwemo kiongozi mkuu mwenyewe.
  • Kuna kitu kikubwa kilkuwa kimendaliwa nyuma ya pazia, yawezekana hata fujo ambazo zingelazimu hata vyombo vya dola kuwasili mahali pale kwa ajili ya kuja kuituliza ghasia
Kwa hiyo iwapo kungeweza kutokea fujo mahli pale, uwezekano mkubwa ni kwamba fujo hiyo ilikuwa imepangwa, na possibly kuna watu ambao tayari walikuwa wameandaliwa kwa ajili ya kuianzisha

Mhusika anadai kuwa hawa viongozi ni wa hatari mno na huko nyuma wameshawahi kupanga matukio mengi tu ya hatari kwake ambayo baadhi atayaleta kwenu kadri habari hizi zitakavyokuwa zinawajia. Karibia mara zote wamekuwa katika mipango yao, wakishirikiana na staff mate wake ambaye naye huwa anaabudu mahali pale. Huyu mtu siku hiyo ghafla alionekana amekaa pembeni ya mhusika ila wakati wa Ibada hakuwa amemuona. Mhusika anadai ataleta angalau tukio moja kuthibitisha hatari iliyoko mahali pale

Hata hivyo, mhusika siku hiyo aliamua kuondoka kikaoni hapo baada ya kuona kinaelekea kule ambako yeye hakuwa ametarajia, akarudi nyumbani

UPDATE 18/05/2020

MATUKIO YASIYOKUWA YA KAWAIDA AMBAYO MHUSIKA AMEKUMBANA NAYO KUTOKEA KANISANI NA AMBAYO YANAONEKANA KAMA YANA UHUSIANO NA STAFF MATE/ OFFICE MATE WAKE, (TUMWITE MR. X ) AMBAYE WANAABUDU WOTE KANISANI HAPO


  • Staff mate huyu (Mr. X) ni mtu ambaye wanafanya naye kazi idara moja, jengo moja ila ofisi tofauti, kwa takriban miaka 20 sasa
  • Pia wanaabudu wote kwenye nyumba moja ya Ibada tangu mwaka 2011. Ni kwamba mhusika wa taarifa hizi alimkuta mwenzake akiwa tayari aliashaanza kuabdudu kwenye nyumba hiyo ya Ibada tangu mwaka huo, ila hakuwa amekaribishwa na Mr. X, wala mhusika hakuwahi awali kujua kuwa Mr. X alikuwa anaabudu kwenye nyumba hiyo ya Ibada
  • Mhusika anapenda kuwaletea matukio ambayo anayaona KAMA huyu mwenzake alihusika, na ambayo kwake yeye anayaona kuwa si ya kawaida na baadhi yake yanaweza kuwa / yaliikuwa ya hatari kwa usalama wake
  • Mhusika anapenda kuwaletea matukio haya (ni baadhi yake tu na machache sana, na si yote) kuanzia na la hivi karibuni kabisa na kurudi nyuma
1: MASHAMBULIO MATANO YA KIAFYA

A: SHAMBULIO LA KWANZA
  • Mhusika alipata kwa mara nyingine tena, shambulio la koo siku ya kikao cha dharura cha wanaume Kanisani, kilichoitishwa J2 ya tarehe 26/04/2020
  • Shambulio hilo liliendelea hadi wiki iliyofuata, akatumia tiba stahiki na hatimaye kupona
  • Haikuwa mara yake ya kwanza kupata shambulio la aina hiyo (kutokea Kanisani), ni mara nyingi tu amekuwa akipata shambulio la aina hii
  • Kawaida huwa linaanza J2 akiwa Kanisani au baada ya kuwa ametoka kanisani J2 husika, na huendelea mpaka pale tiba stahiki inapokuwa imefanya kazi yake
  • Hata hivyo, mengi kati ya matukio ya shambulio hili, inaonyesha KAMA: matano (5) kati yake yanamhusisha moja kwa moja Mr. X, na kama siyo basi tunaweza kusema kuwa ni hali ambayo ni “just a rare coincidence”
  • Siku ya tukio, mhusika anadai kuwa alikuja akastukia ghafla Mr. X amekaa jirani naye kwenye kiti kilichokuwa kulia kwa mhusika
  • Anadai kuwa alimuona ghafla kwa sababu hakuwa amemuona Kanisani siku hiyo, kabla ya hapo. HILI SASA TULIITE SHAMBULIO LA KWANZA kufuatana na mlolongo uliopo kwenye maelezo haya
Kwa hiyo kwenye matukio yote matano ya sahambulio la aina hii na ambayo yanaonekana KAMA kumhusisha Mr. X pekee, mhusika anadai kuwa MARA ZOTE huwa yanatokea pale tu Mr X anapotokea kuwa / kukaa karibu na mhusika kwenye Ibada Kanisani

B: SHAMBULIO LA PILI
  • Kwa kuanzia; kawaida Mr X huwa hana kawaida ya kuhudhuria kipindi cha Morning Glory kanisani, (ambacho sasa hivi kimesitishwa sababu ya ugonjwa wa Corona), na safari ya mwisho ambayo mhusika walikuwa wote kwenye kipindi hicho na kukaribiana karibu kabisa na Mr X, (Mr X alikuwa akimfuata fuata mhusika kila alikokuwa akielekea, na hatimaye walisalimiana kwa kushikana mikono) ilikuwa ni kwenye kipindi cha Morning Glory, zaidi ya mwaka mmoja au miwili iliyopita.
  • Siku hiyo nayo pia mhusika alipata shambulio la koo (halikuwa s la kwanza) , sawa na hili alilopata mwezi jana. HILI TULIITE SHAMBULIO LA PILI, kufuatana na mlolongo uliopo kwenye maelezo haya
Tangu pale mhusika hakuwahi tena kumuona Mr X kwenye kipindi cha morning glory, na kama aliwahi kuhudhuria tena kwenye Ibada ya aina hiyo, basi itakuwa ni katika siku ambazo mhusika naye hakuwa amehudhuria na hivyo wawili hawa watakuwa walipishana

C: SHAMBULIO LA TATU
  • Vilevile mwaka jana mwezi May siku ya sikukuu ya wanaume, mhusika alipata tena shambulio la koo isipokuwa hakumbuki vizuri kama walikaa karibu na Mr X, au pengine labda walikaribiana na kusalimiana kwa kushikana mikono tu
  • Anachokumbuka siku hiyo ni kwamba alibahatika kuwa karibu na watoto wadogo wawili ambao ni rafiki zake, baada ya kuwa amepishana nao kwa wiki kadhaa bila kuonana nao Kanisani hapo
  • Marafiki hawa wa mhusika pia ni watoto wake na Mr. X
  • Aliwaona baada ya kipindi cha Morning Glory Kanisani hapo wakiwa wawili wamekaa peke yao, akawafuata na kuwachukua na kwenda kukaa nao pale alipokuwa amekaa yeye
  • Namna alivyoachana nao marafiki hawa ndiyo kitendo ambacho hana kumbukumbu nacho vizuri, ila anadhani KAMA hatimaye Mr X alikuja kuwachukua, na possibly wali-shake hands wakati wa tukio hilo
  • Na kama Mr X hakuja kuwachukua bali mtu mwingine, au pengine waliondoka wao wenyewe, chances ni kwamba kuna namna ambayo mhusika na Mr. X walibahatika kuwa karibu siku ya J2 hiyo
  • Kwa hiyo siku hiyo nayo pia mhusika alipata shambulio la koo. HILI TULIITE SHAMBULIO LA TATU, kufuatana na mlolongo uliopo kwenye maelezo haya
D: SHAMBULIO LA NNE

Tukio la nne lilitokea J2 moja ambayo mhusika alibahatika tena kukaa karibu na Mr. X
  • Wawili hawa walikaa karibu kwenye kipindi cha somo la uanafunzi na maandiko, mara baada ya Ibada ya kwanza kuisha
  • Kama ilivyo kawaida, Kiongozi Mkuu alianza kwa kuwapanga waumini, namna walivyotakiwa kukaa kwenye Ibada hiyo, na baada ya kuhakikisha kuwa wamekaa katika mfumo aliouhitaji, aliondoka kwenda kunywa chai
  • Wakati huo huo mhusika alifanikiwa kukaa kwenye kiti kilichokuwa pembezoni mwa korido ya katikati ya Kanisa
  • Mhusika akiwa amekaa (safu ya nyuma), hatimaye Mr. X naye alikuja na kukaa kwenye safu ya viti vilivyokuwa mbele ya safu ya mhusika, ila kwenye mstari uleule ambao mhusika alikuwa amekaa
  • Kwa ufafanuzi mwingine ni kwamba hawa watu walikaa jirani kwenye safu mbili tofauti za viti na zilizokuwa jirani, ila kwenye viti ambavyo vilikuwa kwenye mstari mmoja kwenye safu hizo, assuming mtu anatembea kutoka safu moja moja kwenda nyingine
  • siku hiyo nayo pia mhusika alipata tena shambulio la koo. HILI TULIITE SHAMBULIO LA NNE, kufuatana na mlolongo uliopo kwenye maelezo haya
E: SHAMBULIO LA TANO

Tukio la TANO na la mwisho (katika yale tu yanayoonekana kuhusiana na Mr. X), lilitokea siku ya uchaguzi wa viongozi Kanisani, wanaoitwa mashemasi, takribani mwaka mmoja uliopita.

Siku hiyo nayo pia Mr. X na mhusika walikaa karibu na kwa pamoja kwenye kundi dogo maalumu la waumini waliokuwa wamejitenga kwa ajili ya shughuli hiyo ya uchaguzi. Kwa hiyo siku hiyo nayo pia mhusika alipata shambulio la koo. HILI SASA TULIITE SHAMBULIO LA TANO NA LA MWISHO, kufuatana na mlolongo uliopo kwenye maelezo haya

Hata hivyo, matukio haya yamekuwa yakitokea katika nyakati ambazo zina umbali mrefu kiasi (miezi kadhaa) kutoka tukio moja hadi jingine.

Nia kubwa hasa ya mhusika kuleta kwenu matukio haya ni ili yaweze kupata public opinions na watu waweze kuona kama pengine yanaangukia kwenye “rare coincidence” cases ama la

Baada ya shambulio la hivi karibuni lililotokea mwezi uliopota, J3 iliyofuata mhusika alihudhuria kwenye Kituo cha Afya kwenda kumuona Daktari kwa ajili ya matibabu. Baada ya kueleza tatizo lake, Daktari alimuuliza mhusika kama aidha yeye ni mhubiri au ni mwimbaji kanisani, kitu ambacho alikanusha. Kwa hiyo inaonyesha KAMA ingetokea kwa bahati nzuri akapata nafasi ya kuongea kwenye kikao cha wanaume (kama asingeamua kuondoka) kuna uwezekano sauti yake ingesikika mara ya mwisho siku hiyo, isingesikika tena baada ya pale, koo lingekwama

F: KUHUSIANA NA SHAMBULIIO LA HIVI KARIBUNI LA J2 YA TAREHE 26/04/2020: MHUSIKA ANACHODHANI KUWA NI ADDITIONAL MOTIVE BEHIND MR X’,s ACTION, ASSUMING NI KWELI ALIHUSIKA KWENYE SHAMBULIO HILO

  • Nia ya mhusika hapa ni kutaka kuonyesha uhusiano uliopo baina ya kitendo cha anayeweza kuwa ni mshambuliaji wake kwa tukio tajwa hapo juu, yaani Mr. X, na namna kinavyoweza kuwa kinahusiana na matendo ya hivi karibuni ya Mr. X ambayo amekuwa akiyafanya kwa mhusika
  • Yaani kitendo cha Mr. X cha J2 hiyo, kinavyoweza kuwa kinahusiana na matendo yake ya kabla, na ambayo ni ya hivi karibuni
  • Matukio mengine manne aliyoyayaelezea hapo juu. nayo pia yalikuwa na motives zake na anazijua, lakini si nia ya mhusika kuziongelea motives hizo
  • Kwa hiyo anataka kuongelea motive ya shambulio hili la hivi karibuni, na kwa kuanzia mbali kidogo
MHUSIKA ABAHATIKA KUWEPO KWENYE VIKAO VIWILI VILIVYOFANYIKA KWA NYAKATI TOFAUTI, VILIVYOMHAKIKISHIA KUWA MASLAHI YAKE AMBAYO HAJALIPWA NA ANAYODAI TANGIA JUNE 2014, YATALIPWA

Awali ya yote kabla hajaenda kwenye details za vikao, mhusika angependa kuweka wazi mambo kadhaa yafuatayo
  • Ni kwamba mhusika ana madai halali ofisini ambayo hayajaweza kulipwa mpaka leo
  • Si nia ya mhusika kuleta jukwaani humu swala la maslahi yake ya ofisini isipokuwa analazimika kutoa taarifa hizi kwa sababu matukio ambayo inabidi ayaelezzee, yanalazimisha agusie swala la maslahi hayo; vinginevyo haiwezekani namna ambavyo anaweza akatoa ufafanuzi na mtu yeyote aliye na akili timamu akapata kuelewa
  • Kwa hiyo kwa takribani miaka mitano iliyopita, mhusika amekuwa akifuatilia ili alipwe maslahi hayo lakini haikuwezekana, na zaidi akaendelea kuona kuwa kulikuwa na mitego mingi tu iliyokuwa inawekwa katika jitihada zake hizo, ambayo ni ya hatari kwake, kwa hiyo kufikia MWAKA JANA MWANZONI aliamua kusitisha kwanza ufuatiliaji wa maslahi hayo.
  • Kwa taarifa fupi tu ni kwamba mara ya mwisho alipanda daraja mwaka 2012, na kufikia June 2014, mshahara wake ulikatwa T. Shs 700,000/= , makato yasiyostahili na pasipo ridhaa yake
  • Pia tangu mwaka 2011/2012 anakatwa 25,000/=kila mwezi kwa ajili ya maji, nayo pasipo idhini yake wala pasipo kuwa na official notification juu ya makato hayo. Hata hivyo maji hayo kwa sasa yalishakatwa na huwa anachota maji kupandisha ghorofa ya kwanza. Yalikatwa tangu mwezi Novemba 2018, ila makato ya 25,000/= yenyewe bado yapo yanaendelea kila mwezi
  • Desemba 2014 alianza tena kukatwa asilimia 3% (na zinaendelea kukatwa hadi leo) kwa ajili ya uanachama wa mfuko ambao si mwanachama wake hadi leo nazo pia pasipo ridhaa yake;
  • Asilimia nyingine 7% ilianza kukatwa tena tangu Februari 2018 hadi leo, nayo pia ikiwa ni makato ambayo hastahili kukatwa na pasipo ridhaa yake
Yeye anaona kuwa makato haya mapya yaliyoanza Februari 2018, ni kama yalianzishwa kwa makusudi ya kumfanya aongeze zaidi jitihada zaidi za kufuatilia maslahi yake kwenye ofisi husika
  • Kwa ujumla, mpaka muda huu, mshahara wa mhusika unakatwa kiasi KISICHOPUNGUA T. Shs 1,100,000/= na kwa makato ambayo si halali, ilhali mshahara huo uliongezeka kwa mara ya mwisho Julai 2012
Kwa hiyo kabla ya vikao atakavyovielezea maudhui yake hapa chini, taarifa za awali zilizokuwepo ni kwamba mhusika alikuwa ameamua kuuacha kwanza mchakato wa kudai maslahi hayo kwa sababu ulionekana kuwa unakuwa ni wa hatari kwa usalama wake. Zaidi ni kuwa amekuwa akidai maslahi hayo kwa mfululizo kwa kipindi kisichopungua miaka minne lakini, pasipo mafanikio yoyote

KIKAO CHA KWANZA
  • Hiki hakikuwa kikao rasmi, na wala hakuwa amekaribishwa isipokuwa alikifumania tu kwa bahati nzuri na yeye akawa amejiunga katika maongezi yake, kwa kusikiliza zaidi kuliko kuongea
  • Yalikuwa ni maongezi ya kawaida tu ambayo watu wawili au watatu huwa wanafanya wakiwa ofisini, na ambayo hayakuwa na hadhi ya kuitwa kikao
  • Ilikuwa ni MWANZONI MWA MWAKA HUU, yaani JANUARI 2020
  • Maongezi yalikuwa ni ya watu wawili (mmoja tumwite Mr.T ,wakati yule wa pili alikuwa ni Mkuu wa Idara ambaye mhusika wa tukio hili, yuko chini ya mkuu huyo)
  • Mr.T alikuwa anasifu utendaji wa Serikali ya Awamu ya tano, kwa utendaji wake mzuri wa kazi kiasi kwamba imefanikiwa kulipa malimbikizo ya wafanyakazi kwa kuwaingizia fedha nyingi kwa mkupuo kwenye akaunti zao Benki
  • Mr.T alidai kuwa amekuta malimbikizo ya zaidi ya T.Shs million 50 zikiwa zimeingizwa kwenye account yake Benki
Hata hivyo, mhusika wa taarifa hizi alitilia shaka kidogo maongezi hayo, japo hakusema lolote juu ya malipo hayo kwa sababu Mr. T:
  • Alishastaafu miaka kadhaa nyuma (zaidi ya miaka miwili iliyopita)
  • Alishalipwa maslahi yake yote na kwa wakati huu anafanya kazi kwa mkataba, kitendo ambacho kinamfanya asiwe na madai ya malimbikizo yoyote yenye uwingi huo wa fedha
  • Alikuwa anaongea mbele ya Mkuu wa Idara, ambaye naye alionyesjha dalili za wazi kabisa kuwa taarifa hizo anazijua na ni sahihi
Tukirudi nyuma kidogo KWA UFUPI SANA, juu ya mahusiano yaliyopo kati ya Mr. T na mhusika wa taarifa hizi;
  • Ni kwamba mwaka 2008 (August/ Septemba), mhusika alikuwa anaishi peke yake kwenye nyumba ambayo ni ghororfa, na kuna wakazi wengine pia aliokuwa anaishi nao mahali pale, ila yeye nyumbani kwake alikuwa anaishi peke yake
  • Miezi hiyo ya August/ Septemba mhusika aliamua kuchukua likizo na wakati huo wageni wawili ndugu zake wa karibu, walimtembelea kutoka kijijini kwao, japo mmoja alikuwa pia na mahitaji ya tiba
  • Zaidi ni kuwa Mr. T na mhusika wanayo mahusaiano ya karibu tangu kipindi kirefu nyuma, kiasi kwamba Mr. T alikuwa na taarifa zote kwamba mhusika yuko likizo
  • Na katika kujaribu kusaidiana, Mr. T aliamua kumsaidia mhusika kwa kumtafutia kazi ya kuingiza kipato cha ziada wakati huo akiwa yuko likizo, bila mhusika kujua
  • Baada ya kazi hiyo kuwa imepatikana, Mr. T alimuita ofisini mhusika na kumwambia kuwa kuna kazi ya kufanya kama anaweza basi aende akaifanye, na mhusika alikubali
  • Baada ya mhusika kukubaliana na ofa hiyo nzuri, Mr. T. alimuunganisha na mhusika wa kazi hiyo, na baada ya mawasiliano kati yao, walikubaliana kukutana ofisini kwa mwenye kazi, ofisi zilizokuwa pale Namanga karibu na Ubalozi wa Marekani
  • Baada ya mhusika kukutana na mwenye kazi, waliongea na wakaachana kwa makubaliano kuwa watawasiliana tena ndani ya siku chache sana, kwa sababu siku ya kuondoka kuelekea kazini ilikuwa ndani ya wiki hiyo
  • Safari kuelekea kazini ilikuwa ni kwa usafriri wa ndege, na kazi ilikuwa ifanyike mkoani nje ya Dare s Salaam
  • Baada ya maongezo kuisha, wakati mhusika anatoka ofisini hapo, na akiwa pia ametambulishwa kwa baadhi ya watu kwenye timu atakayokwenda nayo, baadhi ya watu wa timu hiyo walianza kusisitiza kuwa afanye hima kwa sababu hata ticket yake ya ndege walikuwa tayari wameshabook
  • Mhusika alipotoka ofisi hiyo alirudi moja kwa moja ofisini na kuonana na Mr. T, akampa feedback za kule alikoenda na zaidi akamsisitiza Mr. T kuwa ajaribu kumkumbusha mwenye kazi atume haraka barua ya mkataba wa kazi, ili mhusika aitumie kuomba ruhusa kazini na waweze kuondoka kuelekea kazini kwa sababu ofisi husika kwa ajili ya kazi hiyo ilikuwa inaonyesha kuwa iko kwenye rush hour
Baada ya hapo, kukawa kimya kila mahali, wenye kazi wakawa kimya, vilevile Mr. T. Kwa hiyo mhusika hakufanikiwa kwenda kufanya kazi hiyo, mchakato wake ukawa umeishia hapo

Hat hivyo, baada ya miaka kdhaa kupita (nadhani ilikuwa mwaka 2014) tangu ofa hiyo ya kazi kutolewa, na matukio mengine kadhaa kuwa yamejitokeza, hatimaye mhusika alikuja kubaini mtego katika mpango mzima wa kazi hiyo ambayo ililetwa kwake na Mr. T.

Mhusika aligudua mambo kadhaa, baadhi yake ikiwa ni:
  • Wote Mr. T pamoja na mwenye kazi, walitarajia kuwa mhusika angeenda kufanya kazi hiyo pasipo kuomba ruhusa kazini kwake, kwa sababu alikuwa yuko likizo
  • Mhusika angeondoka kwenda kufanya kazi hiyo bila kuomba ruhusa kwa mwajiri wake, pamoja na kwamba alikuwa likizo, just in case of anything unexpected, mwajiri wake angemchukulia kuwa alikuwa ni mtoro kazini kwa sababu kisheria alitakiwa aombe ruhusa ya kwenda kufanya kazi hiyo, na mkataba wake auweke wazi kwa mwajiri wake. Zaidi ni kuwa alikuwa likizo lakini akiwa bado anaishi kwenye mazingira ya mwajiri wake, na kwenye nyumba ya Serikali
  • Na kwa sababu nyumbani alikuwa anaishi pake yake, mahali alipokuwa anaishi watu walikuwa na mazoea ya kujua kuwa yupo nyumbani kwa kuangalia gari lake kama lipo kwenye parking; kama ni mchana, na kwa kuangalia taa za nyumbani kwake kama zinawaka, ikiwa ni usiku
  • Na kwa sababu katika kipindi chicho alicholetewa kazi hiyo, kuna wageni walikuwa wameshakuja nyumbani kwake, utaratibu huu wa watu kujua kuwa yupo kwa kuangalia gari au taa za nyumbani kwake usiku, usingeweza kufanya kazi tena kwa sababu kama angeondoka, alikua haondoki na gari lake
  • Kwa hiyo watu wangeendelea kuona gari lipo kwenye parking, na wale walioozoea kuona taa za nyumbani zinawaka usiku, wangeendelea kuziona zinawaka, lakini yeye wakati huo angekuwa hayupo, ameenda kufanya kazi mbali
Kwa hiyo by 2014, mhusika alikuja kubaini kuwa aliachwa asiende kufanya kazi hiyo kwa sababu alitaka kuiweka kiofisi zaidi, kitu ambacho kilikuwa hakiatkiwi Kilichokuwa kinatakiwa ni kwamba alitakiwa asafiri, pasipo watu kujua kuwa amesafiri

MWANDISHI WENU ATARUDI

UPDATE 19 MAY 2020

Mwendelezo kuhusiana na kazi ambayo mhusika aliletewa na Mr. T


Zaidi ni kuwa safari hiyo ilikuwa na ughafla wa aina fulani uliokuwa unaashiria KAMA mhusika alitakiwa aondoke pasipo watu wengi kujua. Akakumbuka pia mwaka 1999 aliwahi kukumbana na hali ya namna hiyo wakati akiwa anasaka ajira ya kudumu.

Kumbuka kuwa maelezo haya ameyaleta kwa ajili ya kugusia kidogo tu uhusiano uliopo mpaka sasa, kati yake na Mr. T, ambaye alimthibitisha kuwa tayari yeye ameshapokea malipo zaidi ya million 50 kama malimbikizo.

Msomaji inabidi akumbuke pia kuwa hapa mhusika yeye alikuwa tayari ameshasimama kudai maslahi yake miezi kadhaa nyuma, baada ya kuona kuwa mchakato huo unakuwa wa hatari kwake.

Hata hivyo, pamoja na taarifa hizi za Mr. T, mhusika:

  • Yeye bado hajalipwa malimbikizo hayo mpaka leo
  • Kwa hiyo inaonyesha KAMA wote Mr T pamoja na Mkuu wa Idara walikuwa na nia ya kum-trigger aanze tena kufuatilia maslahi hayo, na ndiyo maana hajaweza kulipwa mpaka leo
  • Na kama ni kweli kwamba walikuwa na nia ya kumuanzisha ili aanzishe tena mchakato wa kudai masslahi hayo, basi obviously kulikuwa na set-up ya mitego mingine mipya kwenye mchakato wa kudai maslahi hayo
Hata hivyo, mhusika pamoja na kupata taarifa hizo nzuri kutoka kwa Mr T, bado hakuweza kuwa tempted kubadilisha msimamo wake, aliendelea na msimamo wa kuendelea kuusitisha kwa muda mchakato huo

KIKAO (CHA PILI) CHA DHARURA NA AMBACHO KILICHOITISHWA NA MR X
  • Tofauti na kile cha mwanzo ambacho kilimhusisha Mr T, hiki cha pili kilikuwa ni rasmi
  • Kilikuwa ni cha dharura, na kilifanyika mwezi wa pili mwishoni au wa tatau mwanzoni
  • MR X alimfuata mhusika ofisini kwake na kumkaribisha mhusika kwenye kikao hicho kikiwa na agenda ya moja tu ya kumthibitishia kuwa atarekebishiwa maslahi na mshahara wake March 2020 na hatimaye malimbikizo ya mshahara huo mwezi unaofuata; maslahi ambayo amekuwa akiyadai kwa takribani miaka mitano (5) sasa
  • Kikao hicho kilihudhuriwa na watu takribani 6 wenyeji pale ofisini, na mtu mwingine mmoja mgeni kutoka nje ya ofisi, na ambaye ni mstaafu wa pale, ila alikuwa akifanyia idara nyingine
  • Kwa hiyo, Mr X alimfuata mhusika ofisini kwake siku hiyo na kumuomba ahudhurie kikao hicho cha dharura akimweleza kuwa yeye ndiye alikuwa ni mdau mkubwa wa kikao hicho
  • Mhusika alikubali na alihudhuria kikao hicho na ambacho kiliweka wazi kuwa mwezi huo huo, ambao ulikuwa ni March 2020, angelipwa mshahara uliorekebishwa na kwamba malimbikizo ya mshahara huo uliorekebishwa, yangefuata mwezi unaofuata, yaani baada ya ule wa malipo ya mshahara mpya
  • Mkuu wa Idara hakuwepo kwenye mkutano huo ila ilionyesha wazi kabisa kuwa waliokuwa waki-coordinate mkutano huo walikuwa na mandate yake, yaani alikuwa amewa-authorise kuendesha kikao hicho
  • Hata hivyo hadi leo, hali haijatokea sawasawa na minutes za kikao hicho
Pamoja na kwamba hali haijatokea hivyo mpaka leo (May 2020) kwa maana kuwa hakuna malipo yoyote ambayo yameshafanywa kwa mhusika kulingana na minutes za kikao hicho, bado mhusika hana sababu yoyote ya kutilia shaka kilichojadiliwa kwenye kikao hicho

HATA HIVYO: Mhusika anaona KAMA Mr X alimpeleka mhusika kwenye kikao ambacho pengine

  • HAKIKUWA SHAHIHI na wala taarifa zake hazikuwa sahihi, nia ikiwa ni kum-trigger mhusika aanze kupita pita tena kwenye ofisi ambazo huko mwanzo alikuwa ameamua kuacha kupitapita kwa sababu alikuwa tayari ameshaona hatari katika mchakato huo
  • KILIKUWA SAHIHI isipokuwa taarifa zake kwamba malipo yake yangeweza kufanyika mwezi huo hazikuwa sahihi, nia yake ikiwa ni ile ile ya kum-trigger mhusika aanze kupita pita tena kwenye ofisi ambazo huko mwanzo alikuwa ameamua kuacha kwa sababu alikuwa tayari ameshaona kuna hatari katika pita pita hizo
  • Alifanya hivyo baada ya trigger ya Mr. T (aliyedai kulipwa zaidi ya million 50) kuwa imeshindwa kufanya kazi
Hii inatkna na ukweli kwamba vikao vyote viwili vinaonekana kuwa na taarifa ambazo haziko sahihi sana, na hivyo kumfanya mhusika kuwa na notion kwamba wote Mr X na Mr T walikuwa na nia ya kum-trigger ili aanze tena kupita pita kwenye maofisi ya watu ambao tayari ameshayaogopa.

Zaidi ni kuwa mahusiano yaliyopo kati ya mhusika na watoa taarifa hizi njema, na kama alivyoyaainisha kwa kifupi sana hapo juu, hayako sawia sana kiasi cha kumfanya mhusika asiwe katika hali ya kiwango ambacho angeweza kuendelea kuwaamini tena, kama ambavyo anaweza kuwaamini binadamu wengine wa kawaida. Ni kwa sababu muda wote wako tricky na kwa ndani siyo watu ambao anaweza akasema kuwa ni marafiki kwake

Kwa hali hiyo basi, assuming sasa mhusika angepata shauku ya kutaka kujua ni nini kinaendelea kuhusiana na maslahi yake, halafu akaamua kuyafuatilia kwenye ofisi husika, na kwa bahati mbaya katika kupita pita kwenye maofisi ya watu, kukatokea chochote kile ambacho ni cha madhara kwake, picha ya haraka haraka ambayo ingejitokeza ni kuwa mhusika angekuwa responsible kwa madhara yale ambayo yangempata, kwa sababu lazima watu wangehoji, kama huyu mtu alikuwa ameamua kusitissha mchakato wa kufuatilia maslahi hayo, na akatangaza hivyo hadharani , je kilichomfanya auanzishe tena ni nini? Wengine wangeweza hata kufikia conclusion kuwa kwa vile alikuwa anadai maslahi, possibly ameshafrustrate na hivyo alikuwa katika mchakato wa kuwadhuru wengine, isipokuwa kwa bahati mbaya madhara yakamrudia yeye mwenyewe

MWANDISHI WENU ATARUDI KWA MATUKIO ZAIDI YASIYO YA KAWAIDA, YANAYOMHUSISHA MR X NA WASHIRIKA WAKE

UPDATE 20/05/2020

TUKIO LA PILI: TUKIO LILILOPANGWA NA MR X KWA KUSHIRIKIANA NA KIONGOZI MKUU, SIKU YA (J5) IBADA YA JIONI KANISANI


MAELEZO YA UTANGULIZI KUHUSIANA NA TUKIO LENYEWE
  • Tukio hili lilipangwa na Mr X (possibly pamoja na mke wake Mr X pia) akishirikiana na Kiongozi Mkuu wa Kanisa ambalo mhusika ni muumini wa pale mpaka muda huu (tuliite Kanisa A kwa sasa)
  • Plan ilikuwa ni kwamba mhusika atengenezewe mazingira ya kum-trigger ili aweze kuomba appointment ya kuongea na Kiongozi Mkuu, ofisini kwa kiongozi huyo
  • Kama angefanya hivyo, tukio hilo la hatari lingemtokea, na ambalo lingeonyesha kuwa Kiongozi Mkuu hakuhusika nalo
  • Tukio hilo lingeonyesha pia kuwa mhusika aliomba appointment ya kuongea na kiongozi mkuu akiwa hana nia njema naye, alitaka kumdhuru ila kwa bahati nzuri likampata mhusika na kumkosa mlengwa
  • Kulingana na Saikolojia ya mhusika, yeye anadai kuwa anaona kwamba tukio hilo (lililokuwa limepangwa kwa ajili yake), lingempata katika muda ambao angeachwa peke yake kwa muda mfupi ofisini kwa kiongozi huyo, na kwa wakati ambao maongezi yangekuwa bado hayajamalizika/ yanaendelea, baada ya mwenye ofisi kuwa amepata udhuru wa kutoka kidogo nje ya ofisi hiyo
  • Mhusika anadai pia kuwa MFUMO wa tukio hilo ambalo ni aina ya shambulio la hatari sana, ulibuniwa na KIKUNDI KIDOGO cha waumini wa Kanisa B, ambako aliwahi kukimbilia kipindi fulani nyuma, akiwa anatokea Kanisa A, ambako alidumu akiwa muumi kwa takribani muda wa miaka mitatu,
  • Baada ya miaka hiyo kupita akiwa huko, mhusika alikimbia tena kutoka Kanisa B na kurudi tena Kanisa A, ambako ndiko aliko mpaka muda huu
Mhusika anadai kuwa kwa uchambuzi wake kuhusiana na makanisa haya mawili, yaani Kanisa A na Kanisa B
  • Kikundi sumbufu cha Kanisa A (mhusika aliko mpaka sasa) KINA WATU WENGI ILA WAOGA KIASI, ukilinganisha na kile cha Kanisa B; kwa maana kuwa kikundi sumbufu cha Kanisa B (alikowahi kuhamia halafu nako akakimbia tena) KINA WATU WACHACHEI ILA MAJASIRI SANA, na ndiyo maana hata kiliweza kubuni mfumo wa shambulio hilo la hatari, na ambalo mtego wake bado unaendelea kutumika hadi leo, katika mazingira yote ambayo mhusika huwa anakuwepo, KAMA VILE OFISINI.
  • Kwa kifupi sana, maelezo kuhusiana na hama hama hii yako kama ifuatavyo hapa chini:
Mhusika aliamua kuhama kutoka Kanisa A, kwenda Kanisa B, baada ya kikundi kidogo cha watu fulani kuwa kimemubugudhi kikiwa kinashirikiana na viongozi karibia wote wa Kanisa A. Wakati anakimbia kutoka A na kwenda B, wengi wa waumini aliowaacha A waliamini kuwa yeye ndiyo ana matatizo, kwa sababu haiwezekani viongozi wote washiriki kukuhamisha halafu bado uwe wewe ndiyo msafi. Alipofika Kanisa B akitokea A, alipokelewa vizuri halafu baadaye na huko nako ukaundwa mtandao uliokusudiwa kumhamisha akimbie Kanisa B, akitarajiwa safari hii kuwa angekimbilia Kanisa jingine, possibly Kanisa C. Baada ya takriban miaka mitatu hivi akiwa huko Kanisa B, akachoshwa na hila hizo pamoja na ujinga aliokuwa akiendelea kutendewa, na hivyo akaamua kurudi tena Kanisa A, tofauti kabisa na matarajio ya mtandao uliokuwa ukimbugudhi.

Alifanya hivyo ili kuthibitisha kuwa alihama wakati yeye akiwa si mwenye bugudha, bali baada ya yeye kuwa amebugudhiwa

Akiwa yuko Kanisa B (baada ya kutoka A), mambo mengi sana yalimtokea, baadhi yake yakiwa ni haya yafuatayo
  • Baada ya takribani miezi sita hivi tangu kuhama kwake, Kiongozi Mkuu wa Kanisa A, (kule alikohana) alitembelea Kanisa B (kule alikokuwa amehania) kwa ajili ya kutoa huduma Kanisani pale
  • Kabla ya Kiongozi huyu kutembelea Kanisani hili B, nyuma yake watoto wake waliwahi kufika Kanisani hapo kwa ajili ya huduma ya Ibada na hivyo kufanikiwa kuonana na mhusika, japo hakuwapa salaam kumpelekea Kiongozi huyo
  • Kwa hiyo ni wazi kabisa kuwa Kiongozi Mkuu kutoka Kanisa A, alifika Kanisa B akiwa ana taarifa kuwa mhusika alikuwa anaabudu pale
  • J2 hiyo, kabla ya muda wa huduma kuanza, mhusika alibahatika kuonana na kiongozi huyu mgeni kwa ghafla nje mlangoni; mhusika akiwa anatoka nje ya Kanisa na Kiongozi mgeni naye akiwa anajaribu kutaka kuingia ndani
  • Ilikuwa ni mpishano wa ghafla tu na hivyo walisalimiana na hawakuweza kuongea, isipokuwa Kiongozi mgeni alibahatika kupata nafasi ya kumwambia mhusika kuwa hakujua kuwa alihamia kwenye nyumba hiyo ya Ibada, kwa sababu wakati anaondoka kanisani kwake hakumuaga
  • Kiongozi huyu mgeni, alimwambia mhusika maneno hayo mbele ya Kiongozi mwingine mwenyeji wa Kanisa B, ambaye walikuwa wameambatana naye wakiwa katika harakati za kutaka kuingia ndani ya nyumba ya Ibada
  • Kabla mhusika hajajibu chochote, KWA HARAKA SANA kiongozi mwenyeji alidakia kwa kusema “AAH KUMBE HUYU MTU ALIONDOKA KANISANI KWAKO BILA HAKUAGA”?
  • Wakati huo viongozi hao tayari walikuwa wameshaanza kukanyaga ngazi za mlango tayari kwa kuingia ndani
  • Mhusika hakupata nafasi ya kujibu chochote na maongezi yao yaliishia hapo, mhusika akaelekea kule alikokuwa anaelekea, na viongozi hao nao wakaingia ndani ya nyumba ya Ibada
  • Zaidi ni kuwa, hakuna mtu mwingine yeyote Kanisani hapo J2 hiyo, aliyeshuhudia mhusika na Kiongozi mgeni wakikutana na kusalimiana, isipokuwa Kiongozi mwenyeji ambaye alikuwa ameambatana na mgeni huyo wakati wa kupishana mlangoni
Baada ya huduma ya siku hiyo kuisha na ambayo iliongozwa na Kiongozi mgeni, waumini walitawanyika na wengi wao wakiwa na matarajio ya kumuona mhusika akienda kumpa mkono wa salamu, Kiongozi mgeni kwa sababu walikuwa awanajua kuwa mhusika alifika Kanisani hapo akiwa anatokea kule anakohudumu Kiongozi huyo mgeni.

Hata hivyo walishangaa kumuona mhusika akiondoka Kanisani hapo pasipo kwenda kumpa mkono wa salamu kiongozi mgeni. Na kwa vile walikuwa wanajua kuwa kule alikotoka aliondoka katika mazingira yasiyo ya kawaida, waumini hawa wa Kanisa B wakawa na dhana kichwani kwamba mhusika amemkimbia Kiongozi wake wa kule alikotokea na hivyo ikaoenekana kuwa
  • Yeye ndiyo alikorofisha huko na kukimbia kwa sababu isingewezekana asiende kumpa mkono wa salamu Kiongozi wake wa zamani
  • Alikuwa anamkwepa Kiongozi huyu mgeni kwa sababu alijua kuwa ana hatia, akiogopa kuhojiwa maswali mbele ya Viongozi wake wapya wa Kanisa B
  • Kuanzia pale, Kiongozi mwenyeji aliyekuwa na mgeni wakati wanakutana na mhusika mlangoni , alianza sasa kutumika kama shahidi wa kuonyesha kuwa mhusika alitoroka Kanisani kwa Kiongozi mgeni, na Kiongozi mgeni alikuwa hata hajui kama alikuwa anaabudu hapo, sawasawa kabisa na maneno aliyoyatamka kiongozi mgeni akimlalamikia mhusika, walipokuwa wakipishana mlangoni J2 husika
  • Kwa hiyo tangia pale, ikajulikana kuwa mhusika ndiyo ana matatizo, alikorofisha kwa kiongozi mgeni halafu akaondoka na kukimbilia Kanisa B
Hata hivyo, mhusika baadaye alikuja kubaini kuwa huu ulikuwa ni mchoro uliokuwa umechorwa kwa ushirikiano wa Kiongozi mgeni na Kiongozi mwenyeji
  • Ni kwamba Kiongozi mwenyeji alikuwa ame-predict pattern ya movement za mhusika J2 hiyo na baada ya hapo akawa ameiwasilisha kwa Kiongozi mgeni
  • Kiongozi mgeni akiwa tayari amewasili Kanisa B, wawili hao wakaamua kukaa karibu kabisa na mlango wa kutokea nje, katika namna ambayo ilionyesha kama wanajadili kitu Fulani
  • Walikaa upande ule ambao mhusika huwa anapenda kuchoropokea akiwa anatoka nje ya Kanisa, wakiwa wame-predict kuwa lazima tu ndani ya mda Fulani mfupi, mhusika atatoka nje
  • Na kweli ilitokea hivyo, na wawili hao kwa haraka sana, wakamzonga mhusika pale mlangoni kwa maongezi mafupi na ya haraka sana ili watu wengine wasije wakaona wala kusikia
  • Viongozi hawa wawili walijua pia kuwa kama itatokea kama walivyokuwa wamepanga, baada ya Ibada kuisha, mhusika hataona tena haja ya kwenda kuongea na kiongozi ambaye tayari wameshasalimiana na ambaye anashikilia rekodi ya kumsababisha mhusika akimbie Kanisani kwake huku akiwa na kinyongo
  • Vilevile, viongozi hawa walijua pia kuwa picha itakaoyotokea kwa waumini wengine baada ya pale itaonyesha dhahiri kabisa kuwa mhusika aliogopa kukutana na Kiongozi mgeni, na hivyo kuamua kumkimbia pasipo hata kusalimiana naye na hivyo yeye ndiyo ana matatizo na si Kiongozi wake
Kwa hiyo baada ya matukio haya yote kutokea, Kiongozi mgeni baada ya kuwa ameondoka siku hiyo, akawa kuanzia pale tayari amewajenga waumini pamoja na viongozi wote wa Kanisa B kuwa mhusika aliondoka Kanisa A akiwa na hatia, na ushahidi ulionekana J2 hiyo kwamba alimkimbia Kiongozi wake wa Kanisa kule alikokuwa ametokea, mchana kweupe na waumini na viongozi wote wa kanisa B wakiwa wanashuhudia.

Zaidi ni kuwa Kiongozi huyu tayari alikuwa ameshapata refa Kanisani hapo wa kuendelea kumpigia filimbi; huyu si mwingine bali ni kiongozi mwenyeji wa kanisa hilo ambaye alikuwa ameshuhudia alicholalamikiwa mhusika na Kiongozi wake wa zamani, pindi walipokuwa wanapishana mlangoni

Hata hivyo, kila kitu hatimaye kilikuja kubadilika ghafla takribani miaka mitatu baadaye. Mhusika baada ya kuona bugudha zimezidi sana tena akiwa Kanisa B, aliamua kurudi tena Kanisa A, huku akitoa taarifa Kanisa B kuwa wakimubugudhi tena Kanisa A (ambacho ndicho wanachofanya tena sasa), atarudi tena Kanisa B, na hivyo kazi yake itakuwa ni ku-shuttle between churches A and B forever, mpaka pale bugudha zitakapokoma

Hatua hii ya kurudi Kanisa A iliwashangaza wengi kwa sababu:
  • Tayari waumini wa makanisa yote haya mawili walikuwa wamesha-stabilize kwenye ukweli kwamba mhusika ndiye alikuwa na matatizo
  • Waumini wa makanisa yote mawili walikuwa na taarifa za uhakika kuwa mhusika aliwahi kumkimbia Kiongozi wa kanisa A (ambako ndiko aliko sasa), pindi alipokuwa ametembelea Kanisa B (ambako ndiko alishahama tena, hayupo huko tena kwa sasa)
  • Wengi walitarajia kuwa mhusika atakapoamua kuhama tena kutoka Kanisa B, ataenda Kanisa jingine ambalo siyo Kanisa A (possibly ataenda Kanisa jingine C)
Baada ya haya yote kuwa yametokea na mhusika kuwa amerudi tena Kanisa A, jitihada sasa za kurekebisha uelewa wa waumini waliokuwa wameujenga mwanzo zikaanza kufanyika kwa jitihada kubwa, lengo ikiwa ni Kiongozi wa Kanisa A kujisafisha., Jitihada hizo zilihusisha mambo mengi, kubwa zaidi ikiwa ni mitego iliyokusudiwa kusababisha hatari kwa mhusika. Kwa hiyo mmojawapo ya mitego hiyo ndiyo mhusika anapenda kuuleta kwenu wasomaji. Ni mtego ambao uliundwa kwa ushirikiano wa MR X (possibly na mke wake MR X pia) na Kiongozi Mkuu wa Kanisa A.

Maelezo yake bado ni marefu kidogo na hivyo mhusika anazidi kuwaomba wasomaji waendelee kuwa wavumilivu kidogo

MWANDISHI WENU ATARUDI TENA

UPDATE 21/05/2020

TUKIO LA PILI: TUKIO LILILOPANGWA NA MR X KWA KUSHIRIKIANA NA KIONGOZI MKUU, SIKU YA (J5) IBADA YA JIONI KANISANI

……Inaendelea


MWANYA ULIOJITOKEZA NA KUSABABISHA MAANDALIZI YA TUKIO LENYEWE

Kabla ya kuendelea mbele mhusika anapenda kuleta kwenu kwa kifupi mlolongo wa tarehe za matukio haya muhimu:

  • Mr X alianza kuabudu kwenye nyumba ya Ibada Kanisa A mwaka 2005 na hajawahi kuhama
  • Mhusika alianza kuabudu kwenye nyumba ya Ibada Kanisa A tangu May 2011 na ameshawahi kuhama
  • Mhusika alihama kwa mara ya kwanza kutoka Kanisa A kwenda Kanisa B, tarehe 8 June 2014
  • Kiongozi mkuu kutoka Kanisa A alitembelea Kanisa B kwa ajili ya kutoa huduma kanisani hapo, J2 moja ambayo tarehe yake ilikuwa ni kati ya Septemba na Oktoba 2014
  • Mhusika alihama tena kwa mara nyingine kutoka Kanisa B (alikohamia mwanzo) na kurudi Kanisa A (alikohama mwanzo), tarehe 14 April 2017 na mpaka muda huu, bado anaabudu kwenye nyumba hiyo ya Ibada
Mhusika baada ya kuwa amerudi Kanisa A, alikuta utaratibu mpya wa kufanya usafi ambao wakati anaondoka hakuuacha. Kulikuwa na ratiba ya waumini wote kuhudhuria usafi Kanisani hapo kila wiki kwa siku za Jumamosi tu.

Hata hivyo, baada ya wiki kadhaa kupita pasipo kuwa ameweza kuhudhuria huduma hiyo, akapata wazo ambalo aliamua kumshirikisha mmojawapo wa mashemasi kanisani hapo. Wazo lenyewe ni kwamba alipendekeza kama kuna uwezekano, (kwa wale waliokuwa watoro kwenye huduma hiyo), kufidia shughuli hiyo ya usafi kwa kutoa sadaka, yaani kuwe na sadaka maalumu ya usafi kwa yule atakayejisikia kutoa kwa ridhaa yake, kama fidia ya kutoweza kufika kila Jumamosi Kanisani hapo kwa ajili ya usafi huo.

Baada ya maongezi hayo kufanyika
  • Shemasi alipokea ombi hilo na kuahidi kuwa atalifikisha kwenye ngazi husika na atarudisha majibu kwa mhusika
  • Baada ya siku kadhaa, kweli shemasi alirudisha majibu kuwa ombi la mhusika lilikubaliwa, na kwamba alitakiwa afanye kibinafsi tu kama yeye, kwa kuwa utaratibu wa kiujumla wa kufanya hivyo usingekuwepo
  • Mhusika alipokea majibu na hakuona kasoro yoyote kwenye majibu hayo.
Baada ya siku kadhaa kupita (kama wiki hivi na siku kadhaa) tokea siku mhusika apokee majibu ya ombi lake, ikatokea siku moja kwenye Ibada ya J5 jioni kwa ajli ya kujifunza maandiko matakatifu
  • Mwalimu wa somo (siku hiyo) alikuwa ni Kiongozi Mkuu
  • Akiwa anafundisha somo hilo, alifika sehemu akatoa mfano uliohusiana na kile alichokuwa anaendelea kufundisha
  • Mfano huu ulikuwa unaonya juu ya tabia ya waumini kujisikia wako juu kuliko watu wengine, na aliendelea mbele kwa kusema kuwa WAKATI MWINGINE MTU ANASHINDWA HATA KUJA KUFANYA SHUGHULI ZA USAFI WA JUMAMOSI KANISANI, KWA SABABU YEYE ANAJIONA YUKO JUU KULIKO WENGINE’
  • Kipindi somo hili linafundishwa, mhusika alikuwa hajamaliza hata nusu mwaka tangu arudi kutoka Kanisa B alikokuwa amekimbila
  • Zaidi ni kuwa alikuwa hajapata hata nafasi ya kuongea na Kiongozi Mkuu, na hakuwa na mpango wa kufanya hivyo isipokuwa tu pale ambapo pengine angeombwa na Kiongozi huyo, kufanya hivyo
  • Siku hiyo mhusika alikuwa amekaa kwenye safu ya mbele kabisa wa viti ambayo hufuatia ile ya viongozi, kiti cha kwanza jirani na korido ya katikati ya Kanisa
  • Nyuma yake mhusika (kama safu moja au mbili kutoka kwa ile ya mhusika), upande ule ule aliokuwa amekaa mhusika, walikaa Mr X na mke wake, nao kwenye viti vilivyokuwa jirani kabisa na korido hiyo ya kanisa
Labda tu kwa angalizo kidogo hapa kuhusu Mr X ni kwamba mhusika anadai kuwa muumini huyu huwa hana kawaida ya kuhudhuria Ibada za katikati ya wiki, au zile za asubuhi sana J2 (morning glory) na mara nyingi (japo si mara zote) anapokuwa ameonekana kwenye Ibada hizo, lazima awe ana jukumu maalumu kichwani kwake ambalo liko nje kabisa na mambo ya Ibada
  • Kwa hiyo, mhusika alikaa jirani sana na viti walivyokuwa wamekaa viongozi na mara baada ya Ibada kuisha, alisogea mbele kwenye safu ya viti vyao na kuanza kuwasalimia mmoja baada ya mwingine, akiwemo Kiongozi Mkuu
  • Baada ya hapo alianza kurudi akipita kwenye korido, ambapo umbali si mrefu alisimama tena kusalimiana na Mr X na mke wake
  • Kabla mhusika hajaendelea mbele, ghafla Kiongozi Mkuu naye akawa amewasili mahali pale na kupelekea mahali pale kuwepo na kundi dogo la watu wanne
  • Mhusika hakuongea tena na Kiongozi Mkuu kwa sababu walikuwa tayari wameshasalimiana, na aliondoka hapo akawaacha wenzake wakiendelea na maongezi na Kiongozi Mkuu
Muda mfupi baadaye, mhusika katika kujaribu kuchambua kilicotokea kwenye Ibada siku hiyo, akaja akakutana na mambo kadhaa ambayo hakuyaona kuwa ya kawaida sana. Mambo hayo ni kama yafuatayo
  • Huko nyuma kabla, hakuwahi hata siku moja kumuona Kiongozi Mkuu amemuongeela mtu yeyote kimafumbo fumbo akiwa amesimama mbele ya madhabahu, lakini siku hiyo alifanya hivyo.
  • Kutokana na hali hiyo, mhusika aliamua kuweka akiba rohoni KWAMBA, KAMA ITATOKEA HIVI KARIBUNI KIONGOZI HUYO AKAMUHITAJI KWA AJILI YA MAONGEZI, BASI ATAJUA KWA UHAKIKA KABISA KUWA KILA ALICHOKUWA ANAFANYA (KIONGOZI HUYO) SIKU HIYO YA IBADA, ALIKUWA AMEKIPANGA KWA MAKUSUDI NA HAKIKUTKEA KWA BAHATI MBAYA TU
Hata hivyo, kitu ambacho mhusika alikuwa ameshawahi kumuona kiongozi huyo akifanya pindi anapokuwa amekumbana na kero fulani, ni kuitisha mkutano wa dharura wa Kanisa zima na kutaja kero yake mbele ya Kanisa zima, na alishawahi kumuona akifanya hivyo kwa takribani mara mbili, kipindi kirefu nyuma kabla hajahamia kanisa B

Baada ya kuwaza na kuwazua jambo hili, mhusika pia alibaini mambo mengine kadhaa yafuatayo
  • Baada ya Ibada, Kiongozi Mkuu alipita njia ya korido la katikati ya Kanisa, njia ambayo mara zote huwa hapiti. Kawaida, awe anaingia au anatoka kwenye huduma ya Ibada, njia hiyo huwa hapiti, hadi leo
  • Kwa kuzingatia ukweli huo hapo juu, kiongozi huyu alionekana kuwa siku hiyo alipanga kupita njia hiyo
Vile vile, mafumbo ya malalamiko aliyoyatoa kiongozi huyu kuhusiana na usafi wa Jumamosi, na ambayo yalimlenga moja kwa moja mhusika: yalikusudiwa kum-dissappoint mhusika na kumfanya aone kuwa kumbe kulikuwa na unafiki ulikuwa unaendelea juu ya ombi alilopeleka kwa kiongozi huyo

Disappointment hiyo nayo ililenga tena aidha
  • Kum-prompt mhusika aondoke bila kuwasalimia viongozi waliokuwa wamekaa karibu kabisa mbele yake AU
  • Kum-prompt mhusika kwenda kusalimiana na viongozi hao na hatimaye kumuomba appointment ya maongezi Kiongoozi Mkuu, viongozi wenzake wakiwa wanashuhudia ombi lake hilo
Kwa ujumla Kiongozi huyu alikuwa anatengeneza mazingira ya kumlazimisha mhusika (pasipo yeye kujua), aombe appointment ya kuongea na kiongozi huyo na MBELE YA MASHAHIDI waliokusudiwa kuja kuwahakikishia wengine kuwa ni mhusika aliyeomba appointment kwa Kiongozi Mkuu na si kwamba Kiongozi Mkuu alimuomba mhusika wakutane na kuongea, ukizingatia pia kuwa mhusika aliondoka Kanisani hapo kwa kukimbia, na sasa amerudi tena na katika kipindi ambacho siyo kirefu, bugudha zimeanza tena. Kwa hiyo ilitarajiwa kuwa kwa namna yoyote ile yeye angekuwa wa kwanza kuanzisha mazungumzo na kuomba appointment ya kukutana na kiongozi huyo, na si Kiongozi Mkuu mwenyewe

Kinyume chake, baada ya mhusika kusalimiana na viongozi hao na akaondoka pasipo kuongea chochote, ikabidi sasa PLAN B itumike. Kiongozi Mkuu akaamua kumuwahi sasa akiwa bado anasalimiana na akina Mr X na mke wake, akitarajia kuwa pengine mhusika angeweza kupata wazo hilo la kuomba appointment, Mr X na mke wake wakiwa ni mashuhuda wa ombi lake hilo

ITAENDELEA

UPDATE 26/05/2020

TUKIO LA PILI: TUKIO LILILOPANGWA NA MR X KWA KUSHIRIKIANA NA KIONGOZI MKUU, SIKU YA (J5) IBADA YA JIONI KANISANI

……Inaendelea


MWANYA ULIOJITOKEZA NA KUSABABISHA MAANDALIZI YA TUKIO LENYEWE

Kwa hiyo mpaka muda huu, tunaona kuwa mwanya pekee uliojitokeza na kusababisha shambulio hili kwa mhusika ni kile kitendo cha mhusika kushauri utaratibu wa sadaka maalumu kwa wale ambao wanakuwa watoro kwenye usafi Kanisani siku ya Jumamosi asubuhi

Kumbuka maneno haya kwenye mwendelezo wa mada hii, yamendikwa mahali fulani kwenye sehemu iliyopita hapo juu

Kutokana na hali hiyo, mhusika aliamua kuweka akiba rohoni KWAMBA, KAMA ITATOKEA HIVI KARIBUNI KIONGOZI HUYO AKAMUHITAJI KWA AJILI YA MAONGEZI, BASI ATAJUA KWA UHAKIKA KABISA KUWA KILA ALICHOKUWA ANAFANYA (KIONGOZI HUYO) SIKU HIYO YA IBADA, ALIKUWA AMEKIPANGA KWA MAKUSUDI NA HAKIKUTKEA KWA BAHATI MBAYA TU
  • Mhusika aliondoka kwenye ibada hiyo ya jioni (J5), akiwaacha Mr X na mke wake pamoja na Kiongozi Mkuu, wakiendelea na maongezi
  • Mhusika pia hakudiriki kuomba appointment yoyote ya maongezi kutoka kwa kiongozi huyo
Hata hivyo, Jumapili ya wiki hiyo hiyo mara baada ya Ibada ya kwanza kuisha, Kiongozi Mkuu alimfuata mhusika na kumuomba kama ana nafasi ili waonane ofisini kwa ajili ya mongezi, na mhusika alikubali.

Baada ya Kiongozi Mkuu kuwa amefanya hivyo
  • Mhusika alihakikisha pasipo shaka kabisa kuwa kile alichokuwa ameki-predict kwenye Ibada ya J5 kilikuwa kiko sahihi
  • Siku ilipofika aliitikia wito na maongezi yakafanyika japo hayakumalizika, ilionekana kuwa kiongozi Mkuu alikuwa na appointment nyingine tena siku hiyo
  • Maongezi yalianza kwa sala, yakamalizika kwa kuachana ghafla bila sala kwa sababu kuna kiongozi mwingine alikuwa anakaa anachungulia chungulia mlangoni kuonyesha kumhitaji mwenzake aliyekuwa anafanya maongezi na mhusika
  • Wakati wa maongezi ya wawili hao, mhusika pia aliweka wazi kwa kiongozi huyo aina ya mashambulio ambayo kipindi fulani huko nyuma, yaliwahi kuelekezwa kwake kwa kutumia simu ya mkononi aina ya smartphone.
  • Wiki iliyofuata baada ya maongezi hayo, mhusika alitumiwa salio la T. Shs 1 kwenye aacount yake ya pesa za kwenye simu (siyo kwenye salio)
  • Ni akaunti ambayo mhusika alikuwa ameacha kuitumia kwa takribani zaidi ya miaka miwili, kwa sababu mara nyingi ilikuwa ainambatana na mashambulio
  • Ni akaunti ambayo wala haikuwa na salio lolote, ila ilikuwa ina-exist
  • Pesa hii ilisababisha SHAMBULIO JINGINE LA KOO, (hili sasa tuliite shambulio la sita, katika mlolongo wa mashambulio ya aina hii)
  • Ni shambulio sawa kabisa na yale matano ambayo mhusika ameshayaelezea hapo juu, na yanayomhusisha Mr. X
  • Kufikia siku ya J2 wakati anatoka kwenye Ibada, sahambulio likawa limekuwa severe, kiasi kwamba sauti yake ilikuwa karibia inakata ashindwe kabisa kuongea (Na hii ndiyo maana juzi ali-predict kuwa sahambulio la hivi karibuni lililofanyika J2 ambayo kikao cha wanaume kilifanyika, lilikuwa limeelnga kumfanya akate kauli na asiweze kuongea tena)
  • Hatimaye J2 hiyo aliamua kwenda Mlimani City na kuwaomba wahusika wafunge kabisa akaunti hiyo ya simu, kitu ambacho walifanya
  • Baada ya hapo koo lilipona, ila akaunti hiyo alishaifunga kimoja haifanyi kazi hadi leo
Kwenye shambulio hili, mhusika aliona mambo makubwa mawili ambayo mojawapo ni sahihi

Ni kwamba kuna taarifa muhimu za mashambulio alizomshirikisha Kiongozi Mkuu huyo siku hiyo ambazo yeye anadhani kuwa AIDHA:

  • Taarifa hizo baadaye zilitumika vibaya pengine baada ya Kiongozi huyo naye kuwa amezi-share na watu wengine ambao hakujua kuwa si wazuri, na ambao hatimaye waliamua ku-launch mashamabulizi kwa mhusika kwa kutumia taarifa hizo AU
  • Kiongozi Mkuu mwenyewe alihusika katika shambulizi hilo, na iwapo taarifa hizo alizishare na watu wengine, basi ilikuwa ni kwa makusudi hayo
Hii ni kutokana na uwiano au ukaribu wa muda ulijitokeza kati ya kutokea kwa sahambulio hilo na kutolewa kwa taarrifa za siri zinazohusiana na matukio ya nyuma, yaliyofanana na tukio hilo (providing confidential information to a confidant, who them turns on you by using them (such information) against you)

Kwa kifupi kwenye tukio hili tunanona kuwa
  • Mhusika alitakiwa aombe appointment, ila hakufanya hivyo
  • Kabla hajarudi tena Kanisa A, waumini wa makanisa yote mawili, Kanisa A na Kanisa B, walijua kuwa mhusika ndiyo chanzo cha matatizo
  • Baada ya Mhusika kurudi Kanisa A, ikabidi sasa Kiongozi Mkuu aanze kutafuta mbinu za kujinasua kutoka kwenye kile ambacho waumini wa makanisa yote haya mawili alikuwa amewapelekea wakiamini.
Na kama mhusika angefanya uamuzi usio sahihi wa kuhama tena kutoka Kanisa B na kwenda Kanisa Jingine tuseme C, (badala ya kurudi Kanisa A kama alivyofanya), picha pekee ya mhusika ambayo ingejitokeza kwa makanisa yote haya matatu(yaani Kanisa A, Kanisa B na Kanisa C) ingekuwa kwamba yeye ndiye ana matatizo kwa sababu:
  • Aliwahi kuhama kutoka Kanisa A na kwenda Kanisa B, pasipo kuwa ameuaga uongozi wa Kanisa A
  • Alihama kwa matatizo yake mwenyewe, hakuhamishwa na mtu yeyote
  • Aliwahi kumkwepa Kiongozi wa Kanisa A pindi alipokuwa ametembelea Kanisa B, Kanisa ambalo mhusika alihamia baada ya kutoka Kanisa A
  • Waumini wote pamoja na viongozi wote wa makanisa A na B wanajua kuwa mhusika ndiyo ana matatizo na si viongozi wake
  • Waumini wa Kanisa C nao pia sasa wangejumuika na uelewa wa waumini wenzao wa makanisa hayo mawili, kujua kuwa mhusika ndiyo ana matatizo na si viongozi wake
AMBACHO MHUSIKA HATIMAYE ANGEKUJA KUVUNA KAMA MATOKEO YAKE YA HAMA HAMA KUANZIA KANISA A MPAKA KANISA C

Kwa hiyo mwisho wake ingekuja kueleweka kuwa mhusika aamekuwa akihama hama makanisa kwa sababu anazozijua mwenyewe binafsi na pasipokuwa amebugudhiwa na mtu yeyote, ila akiwa na lengo la kuwachafua viongozi wa makanisa anakokuwa ametokea
  • Uelewa wa waumini wa makanisa yote haya matatu, ulikuwa na nguvu kubwa mno na kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa ungechukuliwa kuwa ndiyo uelewa wa PUBLIC
  • uelewa wa PUBLIC, ni uelewa wa DOLA
  • DOLA sasa hapa lazima ingeingia kazini kutaka kujua kwa nini huyu mtu anafanya mambo kama anavyotaka yeye, na ambayo yanaashiria jinai ndani yake
Kumbuka pia kuwa, hapa kulikuwa na uwezekano wa DOLA kutojijishughulisha na kuhoji sana isipokuwa ingechukua uelewa wa PUBLIC tu na kuanza kuufanyia kazi

MWANDISHI WENU ATARUDI KWA AJLI YA MATUKO MENGINE MAWILI ZAIDI, LA TATU NA LA NNE

UPDATE 27/05/2020

TUKIO LA TATU: FIRE EXTINGUISHER YA MAJI, ILIYOLETWA NA MR X NDANI YA JENGO LA OFISI, HALAFU BAADA YA SIKU CHACHE, TRANSFOMA YA UMEME ILIYO NYUMA KARIBU KABISA NA OFISI YA MHUSIKA IKALIPUKA


Ilikuwa ni mwaka 2015. Ilitokea ghafla siku moja mhusika akaona mtungi wa Fire Extinguisher uko njiani chini kwenye floor ya korido ya kuelekea mlango wa dharura, ambayo ofisi ya mhusika ipo. Kipindi cha miaka yote huko nyuma, mtungi huo kawaida ulikuwa ulikuwa haukai sehemu hiyo, bali ulikuwa unakaa kwenye attachment yake ndani ya chumba kingine ndani ya jengo hilo, na kwenye ghrorofa (floor) nyingine tofauti. Kwa hiyo mtungi huu ulihamishwa kutoka ghorofa moja kwenda ghorofa nyingine

Katika kutaka kujua mtungi huo ulilwekwa pale na nani, mhusika alipewa taarifa kuwa aliyeuweka pale alikuwa ni Mr X
  • Kitu cha muhimu ambacho msomaji inabidi akumbuke hapa ni kuwa mhusika na Mr X. ofisi zao ziko jengo moja, ghorofa moja
  • Mtungi huu ulikuwa katika sehemu ambayo mhuiska huwa mara zote anapita, akiwa anaelekea au anatoka ofisini kwake
  • Hata hivyo, mtungi huu pia ulikuwa katika sehemu ambayo Mr X huwa hapiti pindi anapokuwa anelekea au anatoka ofisini kwake, isipokuwa tu pale anapolazmimika kueelekea sehemu nyingine ndani ya jengo hilo, iliyo tofauti na ofisi yake, na kwa shida maalumu
  • Baada ya siku kadhaa kupita tangu uwepo wa mtungi mahali pale, ilitokea ajali ya mlipuko mkubwa sana wa Transformer la umeme ambalo liko sehemu inayotizamana na dirisha mojawapo la nyuma la ofisi ya mhusika
  • Kwa hiyo hapa mhusika anchojaribu kueleza ni kuwa ujio wa mtungi wa gas unaonekana KAMA kuhusiana na kulipuka wa Transfoma, kitu ambacho kinaonekana KAMA kilikuwa kimepangwa
  • Mlipuko huo uliambatana na cheche za moto pamoja na moshi mzito kuashiria kuwa lilikuwa linataka kuwaka moto
  • Na kwa sababu mlipuko huo ulionekana wazi kusababishwa na hitilafu ya umeme, mhuiska alianza kukimbia akitokea ofisini kwake kuelekea nje
  • Alipofika usawa wa korido pale ulipokuwa mtungi wa Fire Extinguisher, mhuiska akakutana na mtu mwingine akiulliza, HIVI HATUNA MTUNGI WA FIRE EXTINGUSHER JENGO HILI?
  • Mhuiska alimjibu mtu huyo kwa kumwambia kuwa TUNAO ULE PALE
  • Baada ya jibu hili, mtu huyo alienda na kuushika mtungi huo halafu akamuuliza, unajua namna ya kuutumia? Mhusika alijibu akasema hajui
  • Wakati huo mhusika alikuwa ameshafika sehemu ulipokuwa mtungi huo, na kuanza kuugeuzageuza akiungalia
  • Akiwa katika hati hati ya kujadili rohoni aidha auchukue au auache, aliamua kuuacha na kutoka nje
  • Hatimaye watu husika (siyo zimamoto) walikuja na kuuzima moto uliokuwa umeanza kufuka kwenye Transfoma hilo, baada ya kuwa wamepewa taarifa.
Kipindi pilikapilika hizo zilipokuwa zinaendelea kabla moto huo haujazimwa, Mr X alifika ghafla ofisini kwa mhusika na kumjulisha kuwa AMESHAWAPIGIA SIMU TANESCO ILI WAZIME UMEME. Hii ilionyesha wazi kuwa
  • Wakati mhusika anahangaika na mtungi wa gas, umeme ulikuwa bado haujazimwa na wala hakuwa na taarifa hizo
  • Wakati huo huo, Mr X alikuwa hajulikani alikuwa wapi kipindi hicho kwa sababu hakuwahi kumuona popote wakati kulikuwa na taharuki ndani ya jengo na karibia kila mtu alikuwa ameshatoka nje ya ofisi yake kama tahadhari ya kwanza
  • Kwa hiyo inaonyesha KAMA Mr X alikuwa ametegea kwanza kuona kama mhusika atachukua hatua za kwenda kuuzima moto kwa kutumia Fire Extinguisher hiyo
  • Kama mhusika angeenda kuuzima moto, Mr X asingewapigia TANESCO kwa ajili ya kuzima umeme huo
  • Na kwa sababu Fire Extinguisher ilikuwa ya maji, kujaribu kuzima nguzo ya Transfoma inayowaka moto kwa kutumia mtungi wa maji, kungesababisha mlipuko mwingine mkubwa kuliko ule wa Transfoma lenyewe
  • Umeme ungefuata mkondo wa maji na mhusika angepigwa shoti ya umeme na kufa palepale, na pengine na mtu mwingine yeyote ambaye naye angejisahau na kuwa karibu naye
  • Hata hivyo, baada ya mhusika kutochukua hatua hizo, na hivyo kupelekea watu wengine kuitwa kuja kuzima moto huo, ndiyo ikabidi sasa Mr X awapigie TANESCO ili wazime umeme, kwa sababu mlengwa alikuwa mhusika na si watu wengine
ALICHOKUWA MR X AMEPANGA KATIKA TUKIO HILI

Hapa matarajio ya Mr X yalikuwa ni kwamba mhusika angechukua hatua ya kwenda kuuzima moto huo kwa kutumia Fire Extinguisher hiyo iliyokuwa ni ya maji, halafu baada ya hapo, mlipuko wa moto wa umeme ungemfuata kwa kufuata mkondo wa gas ya maji. Na kama kweli angefanya hivyo, mlipuko ambao ungetokea pale, possibly ungeweza kulingana na ule wa Lori la Mafuta ya Petroli. Lakini kwa bahati nzuri, mhusika hakufanya hivyo hali iliyopelekea baadaye Mr X akapaniki na kuanza kuongea mambo ya ajabu. Ilikuwa salama zaidi kwake Mr X kama asingefanya kosa la kusema kuwa NIMEWAPIGIA TANESCO WAZIME UMEME.

Blunders za namna hii huwa mara nyingi zinafanyika pale tu ambapo mtu anakuwa ametumia nguvu za giza katika kupanga CRIME yake, na ndiyo yaliyotokea kwa Mr X.

MWANDISHI WENU ATARUDI KWA AJILI YA TUKIO JINGINE MOJA ZAIDI, NALO PIA LIKIWA LINAMHUSISHA MTU YULE YULE MR X

UPDATE 28/05/2020

TUKIO LA NNE:

LILIPANGWA NA MR X NA KIONGOZI MWINGINE (TUMWITE KIONGOZI X) J2 YA KWANZA YA/ SIKU YA UZINDUZI WA MABADILIKO YA MUDA WA IBADA ZA HARUSI KANISANI


Ikumbukwe kuwa mpaka muda huu, mada yetu bado inashughulika na matukio ya ajabu ambayo Mr X amewahi kuyafanya kwa mhusika. Kwa hiyo bado tuko kwenye matukio yanayomhusu Mr X akiwa anashirikiana na watu tofauti tofauti.

Sasa tukirudi kwenye tukio ambalo kichwa chake kimeelezwa hapo juu
  • Ni kwamba kwenye Kanisa linalohusika na habari hii, huko nyuma, tofauti na ilivyo kwa sasa, kulikuwa na kawaida ya kuwa na Ibada tatu pale tu ilipotokea kuwa J2 husika kuna wanandoa wanaunganishwa; yaani Ibada ya kwanza, Ibada ya pili na baadaye kufuatiwa tena na Ibada ya ndoa
  • Kwa J2 zingine zote ambazo hazikuwa na Ibada za ndoa, Ibada zilikuwa zinakuwa mbili tu, yaani Ibada ya kwanza na ya pili
Mhusika wa taarifa hizi kawaida yeye alikuwa na utaratibu wa kushiriki Ibada zote mbili, ya kwanza na ya pili pia. Hata hivyo, hakuwa na utaratibu wa kushiriki Ibada za harusi, baada ya kuwa amebaini mambo kadhaa kama atakavyoyaainisha hapa chini.
  • Kipindi kirefu huko nyuma, kabla hajahama kwenda Kanisa B, mhusika aliwahi kuhudhuria Ibada ya ndoa mara moja na kugundua kuwa ni Ibada iliyokuwa inaendeshwa kisherehe zaidi kuliko ki-Ibada
  • Kwa hiyo kuanzia pale mhusika akawa hapendelei tena kuhudhuria Ibada za aina hiyo
  • Mifano mingine mingi anayo kwa kuangalia Ibada zingine zinazofanana na hiyo kama vile zile ambazo huambatana na sikukuu kama vile sikukuu ya watoto, sikukuu ya vijana, sikukuu ya akima mama, n.k.
  • J2 zote za sikukuu hizo Ibada zake huwa zinafanywa kisherehe zaidi, viongozi huwa wanajisahau wanapelekea zinaendeshwa kama waumini wako kwenye ukumbi wa harusi
  • Vilevile, Ibada ya asubuhi inayoitwa morning Glory, mara nyingi huwa inafutwa kimya kimya kwenye siku kama hizi, yaani watu wanastukia haipo tu pasipo tangazo lolote rasmi
  • Na pale ambapo huwa inatokea ikawepo, basi inakuwepo kwa kusuasua sana, tofauti na ambavyo huwa inaendeshwa siku ambazo si za sikukuu
  • Kwa hiyo mhusika yeye kwa uzoefu wake alishaona KAMA siku za sikukuuu huwa zinatumika kama kkisingizio cha kuchakachakua Ibada hali inayopelekea kuendeshwa Ibada zilizofubaa, kitu ambacho huwa anona ni afadhali akawa yuko nyumbani akijifunza maandiko matakatifu, kuliko kuendelea kuwepo kwenye Ibada ya aina ile
  • Mfano halisi mwingine ni kwamba mwaka juzi Desemba 2018 siku ya kuwapongeza watumishi wa Mungu, kulikuandaliwa ma-MC wawili, mmoja wa kike na mwingine wa kiume
  • Mwaka jana pia 92019) kwenye siku kama hiyo hiyo, mbele kwenye madhabahu kulibandikwa bango refu la nguo lililoenea sehemu yote ya madhabahu (kutoka kulia kwake kwenda kushoto) lililokuwa na na picha ya Kiongozi Mkuu, akiwa amemkumbatia mke wake. Sasa watu hapa wajiulize, unawezaje kubandika picha ya hadhi ya mtu amekumbatia mke wake, kwenye madhabahu ya Mungu? Katika kipindi chote ambacho mhusika amekuwa pale, anakiri kabisa kuwa hajawahi hata siku moja kuona hata picha za Malaika, achilia mbali ya Yesu, imebandikwa kwenye bango la aina hiyo
  • Zaidi pia ni kwamba J2 hiyo Ibada pia ilifanya kitu kinaitwa procession, Kiongozi Mkuu nadhani alitembea akiwa amefuatwa na msululu wa wafuasi nyuma yake. Hiki kitu kilitangazwa halafu kabla hakijaanza kufanyika, mhusika aliondoka na kwenda kuabudu Kanisa jingine kwa kujua kuwa hapangekuwa na Ibada ya kawaida siku hiyo mahali pale
  • Ibada ya siku hiyo ilikuwa na viashiria vyote vya kugeuka kutoka kumwabudu Mungu na kumwabudu Kiongozi Mkuu
MWANDISHI WENU ATARUDI

UPDATE 01/06/2020

TUKIO LA NNE:

LILIPANGWA NA MR X NA KIONGOZI MWINGINE (TUMWITE KIONGOZI X) J2 YA KWANZA YA/ SIKU YA UZINDUZI WA MABADILIKO YA MUDA WA IBADA ZA HARUSI KANISANI


  • (inaendelea)

  • Baada ya kuwa amehamia Kanisa B na hatimaye tena kurudi Kanisa A, alikuta utaratibu ule ule wa zamani ukiwa bado unatumika, yaani Ibada tatu pindi inapotokea uwepo wa J2 ya wanandoa wanaounganishwa
  • Mhusika yeye aliendelea kuhudhuria Ibada mbili tu, ya kwanza na ya pili na pale zilipokuwa zinajitokeza Ibada za ndoa, hizo kabisa alikuwa anaziweka pembeni
KIONGOZI X ASIMAMA MADHABAHUNI NA KUTANGAZA MABADILIKO YA IBADA ZA NDOA KWAMBA ZITAKUWA ZINAFANYAIKA IBADA YA PILI

Baada ya takriban mwaka mmoja hivi kupita, Ilitokea J2 moja Kiongozi X akasimama madhabahuni na kutangaza kuwa kuanzia siku hiyo, Ibada zote za ndoa zitakazojitokeza tena, zitakuwa zinafanyika Ibada ya Pili. Kwa hiyo Ibada zitaendelea kuwa mbili tu kwa kila J2, bila kujali kuna ndoa ama la. Wakati Kiongozi X anatoa tangazo hili, J2 iliyokuwa inafuata kulikuwa na Ibada ya ndoa ya watu ambao hawakuwa wenyeji wa Kanisa hilo, mmojawapo wa wanandoa hao alikuwa ni mtu wa kutoka Msumbiji. Kifupi ni kwamba viongozi wa wanandoa hao watarajiwa walikuwa wameuomba uongozi wa Kanisa A uweze kutoa huduma hiyo kwa wanandoa hao watarajiwa.

Mpaka hapa, kabla hajaendelea zaidi, mhusika anaomba kwa kifupi sana agusie kidogo kuhusiana na WASIFU WA KIONOZI X
  • Ndiyo yule aliyekuwa akifungua fungua mlango kuchumgulia siku ambayo mhusika alikuwa na maongezi na Kiongozi Mkuu ofisini kwa kiongozi huyo, hali iliyopelekea maongezi yao kusitishwa na Kiongozi Mkuu kwa udhuru kuwa alihitajika kwenye commitment zingine (ambazo zilikuwa zinamfanya Kiongoz X achungulie mara kwa mara)
  • Ni kiongozi ambaye katika maisha yake yote, na kwa miaka takriban saba (7) sasa ya uwepo wa mhusika katika mazingira ya Kanisa analoendelea kuhudumu kiongozi huyo,, hajawahi kuonekana amesimama akiwa anaongea na mhusika hata kwa angalau dakika moja tu. Mara zote huwa wanasalimiana naye tu huku wakiwa wanapishana
  • Huwa hawezi kusimama kuongea na mhusika, licha ya kuwa huko nyuma, mhusika mwenyewe alikuwa na tamaa hiyo
  • Still, inapotokea mhusika yuko katika mazingira ambayo ni ya peke yake, au si ya peke yake ila yanatoa mwanya ambao Kiongozi X anaweza akapenyeza neno kwa mhusika na pasipo wengine walio karibu au mbali kuyasikia, ataongea maneno kwa chini chini katika namna ambayo watu hao hawawezi kujua kuwa ameongea naye neno lolote isipokuwa wataona tu hali ya kuwa wawili hao wamepishana huku wakisalimiana kwa kushikana mikono
  • Maneno ambayo Kiongozi huyu amekuwa akiyaongea kwa siri sana na kwa tahadhari kubwa sana, akiwa ANAMNONG’ONEZA mhusika, mara nyingi yamekuwa ni kama “NJOO OFISINI TUONGEE”; NJOO OFISINI NIKUTAMKIE MIBARAKA
  • Kumbuka kuwa maneno haya huwa anayaongea na kuhakikisha kuwa yamesikika na mhuiska tu na ni pale tu anapokuwa anapishana na mhusika huku akiwa anatembea pasipo kusimama
Baada ya kuona hivyo, mhusika alianza kuifanyia kazi hali hii kwamba kiongozi huyu anajitahidi kuongea naye kwa siri sana na kwa jambo ambalo halihitaji usiri. Hii ni kutokana na ukweli kuwa swala la muumini kuwa na appointment ya maongezi na Kiongozi wake siyo la siri; na kwa sababu Kiongozi ndiyo alikuwa anatamani sana kuongea na muumini wake ofisin kwakei, haikutakiwa kumpa shida Kiongozi huyo kumjulisha muumini wake juu ya hilo na alitakiwa alifanye wazi na watu wengine wakiwa wanashuhudia, au kuona. Badala yake haikuwa hivyo kabisa kwa kiongozi huyu

J2 YA KWANZA KABISA YA IBADA YA HARUSI KUFANYIKA IBADA YA PILI YAWADIA; MR X NA KIONGOZI X WAONYESHA AINA FULANI YA MAWASILIANO YA SIRI KUHUSIANA NA MHUSIKA
  • Kama ilivyoelezwa hapo awali, Ibada hii ilihusisha watu ambao hawakuwa wenyeji wa Kanisa A, mmojawapo akiwa ni mgeni kutoka Msumbiji
  • Kutokana na rekodi ambayo alikuwa ameiweka mhusika, hadi siku ya J2 hii inafika, alikuwa hajawahi kukosa Ibada ya pili hata siku moja, tangia pale alipoanzisha utaratibu wake huu wa kuabudu kwa namna hiyo
  • Kwa hiyo mpaka siku hiyo alikuwa hajawahi kukosa Ibada ya pili
  • Sku hiyo, ilitokea coincidence kwamba Mr X alikuwa amepaki gari lake jirani na la mhusika
  • Mhusika ndiyo alitangulia kupaki gari lake pale alipokuwa amepaki siku hiyo, kwenye muda wa saa 12 asubuhi, na hatimaye katika muda ambao mhusika hawezi kujua, Mr X naye alikuja akapaki gari lake jirani ubavuni kwake
  • Katika kumbukumbu zake hafifu, mhusika anadai kuwa siku hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza (na ya mwisho pia) kwa Mr X kupaki gari ubavuni jirani na la mhusika
  • Mpaka leo, coincidence ya namna hiyo haijaweza kujitokeza tena
  • Baada ya Ibada ya kwanza kuisha, mhusika hakuwa amepanga kuhudhuria Ibada ya ndoa, ambayo sasa kwa J2 hiyo, ilikuwa inafanyika wakati wa Ibada ya pili kwa mara ya kwanza
  • Alichofanya baadaye ni kutoka na kuelekea kwenye parking, ili akachuke gari lake na kuondoka
  • Kabla hajaondoka akawa mekutana pale na Mr X, na wakaanza kubadilishana mawili matatu
  • Huku kwingine nako sasa pilika pilika za watu waliokuwa wanatoka Ibada ya kwanza na wale waliokuwa wanaingia kwa ajili Ibada ya pili zikawa zinaendelea
  • Muda si muda mhusika akiwa yuko bado amesimama na Mr X hapo kwenye parking, akamuona Kiongozi X anapita kwa umbali kidogo huku akiwa hai hai, akawapungia mikono wote wawili na kutamka maneno “ NJOO OFISINI NIKUTAMKIE MIBARAKA”
  • Watu hawa wote watatu, Kiongozi, mhusika pamoja na Mr X walijua kuwa ujumbe huo ulimhusu mhusika
  • Hata hivyo haikuwa hivyo kwa watu wengine ambao walikuwepo maeneo yale na ambao waliusikia ujumbe wa Kiongozi huyo kwa sababu alionekana akiuelekeza kwa watu wawili waliokuwa wamesimama wakiongea, yaani Mr X na mhusika
ITAENDELEA
UPDATE 02/06/2020

TUKIO LA NNE:

LILIPANGWA NA MR X NA KIONGOZI MWINGINE (TUMWITE KIONGOZI X) J2 YA KWANZA YA/ SIKU YA UZINDUZI WA MABADILIKO YA MUDA WA IBADA ZA HARUSI KANISANI

  • (inaendelea)
J2 YA KWANZA KABISA YA IBADA YA HARUSI KUFANYIKA IBADA YA PILI YAWADIA; MR X NA KIONGOZI X WAONYESHA AINA FULANI YA MAWASILIANO YA SIRI KUHUSIANA NA MHUSIKA

Kwa hiyo kuna watu waliokukwa wamesimama maeneo yale karibu na pale walipokuwa wamesimama mhusika na Mr x, na ambao walifanikiwa kumsikia Kiongozi X akitamka maneno NJOO OFISINI NIKUTAMKIE MIBARAKA, ila uhakika ni kuwa watu hawa hawakuweza kujua wito huo ulimhusu nani kati ya wawili hao, yaani mhusika na Mr X, isipokuwa wao wenyewe (mhusika na Mr X) walijua pasipo shaka kuwa ujumbe huo ulikuwa unamhusu nani

Baada ya ujumbe huo, mhusika aliwasha gari na kuondoka kurudi nyumbani. Kwa hiyo J2 hiyo hakuweza kushiriki Ibada ya pili kwa mara ya kwanza tangu kipindi aanzishe utaratibu wake wa kuabudu Ibada mbili

Mpaka hapa, kutokana na mlolongo wa tabia ya matendo (siyo matukio) yaliyokuwa yakionyeshwa kwake na Kiongozi X, inaonyesha KAMA
  • Kiongozi X alikuwa anatamani sana akutane na mhusika kwa appointment ambayo haikutakiwa ijulikane kuwa ni yeye Kiongozi X aliyehitaji kukutana na mhusika
  • Ilitakiwa kuwa ni appointment ambayo ingeonyesha kuwa ni yeye mhusika aliyeomba appointment ya kuonana na kiongozi X ofisini kwa kiongozi huyo
  • Hitaji la kuwepo usiri wa hali ya juu kwenye appointment kati ya Kiongozi X na mhusika liliashiria kitu ambacho si kizuri na ambacho Kiongozi X alikuwa amekipanga kwa mhusika
  • Wakati haya yote yanatokea, tayari (siku nyingi nyuma) maongezi ya appointment ya kwanza na Kiongozi Mkuu, yalikuwa yameshapita/ yameshafanyika
  • Mtego ambao mhuiska aliubaini kuwepo kwenye appointment ya kwanza na Kiongozi Mkuu, ndiyo ule ule alioubaini wepo wake kwenye appointment hii ya pili na Kiongozi X
Kwa hiyo, hapa tena Inaonyesha KAMA:
  • Kiongozi X aliingia kazini kujaribu kufidia/ kutafuta kile kilichokuwa kimeshindikana kupatikana kama matunda kutoka kwenye appointment ya kwanza iliyofanyika kati ya mhusika na Kiongozi Mkuu
  • Kiongozi X aliamua kubadilisha utaratibu wa awali kutoka Ibada tatu na kuwa mbili, akitarajia kuwa pengine mhusika angeweza kuwa anashiriki Ibada za Harusi kwenye Ibada ya pili. Hii ni kwa sababu mhusika alikuwa na kawaida ya kushiriki Ibada zote mbili
  • Wahusika wa ndoa hiyo ambao mmoja wao alikuwa anatokea Msumbiji, walikuwa wanafahaniana zaidi na Kiongozi X kwa sababu kwa kipindi hicho, kiongozi huyo alikuwa ameshafanya mikutano ya Injili miwili au mitatu nchin Msumbiji
J2 hiyo, baada ya mshiriki kuonyesha dalili za wazi (siku hiyo ya kwanza), kuwa hakuwa na mpango wa kushiriki Ibada hiyo, ndiyo sasa Plan B ikabidi itumike; plan ambayo ilitekelezwa na Mr X aliyekuwa amepaki gari lake ubavuni kwa mhusika. Kwa hiyo Kiongozi X alipita haihai akisema NJOO OFISINI NIKUTAMKIE MIBARAKA, akitarajia kuwa pengine mhusika angebadilisha mawazo siku hiyo na kuamua kushiriki Ibada hiyo ya harusi, na possibly hatimaye kwenda kumuona Kiongozi X ofisini kwake.

Kwa hiyo mpaka hapa tena tunaona kuwa kulikuwa na jitihada pekee sana zilizokuwa zikifanywa na Kiongozi X kuhakiksha kuwa mhusika anshiriki Ibada siku hiyo. Na, assuming angeamua kutokuondoka na kubaki ashiriki Ibada ya pili siku hiyo halafu kule mbele likaja kutokea lolote la kutokea, kuna uwezekano kuwa:
  • Mr X angekuwa shahidi wa kwanza, na angeweza kusema kuwa mimi aliniambia kuwa atakuwepo kwenye Ibada ya pili kwa sababu baada ya hapo alikuwa ameomba appointment ya kufanya maongezi na Kiongozi X
  • Hii point ingeleta mantiki kwa sababu siku za mwanzoni wakati mhusika akiwa ndiyo amerudi kutoka uhamishoni Kanisa B, aliwahi kumuomba Mr X namba za simu za Kiongozi X kwa minajili ya kupanga appointment naye ili amuone ofisini
Wakati huo mhusika alikuwa bado hajapata picha kamili ya kiongozi huyo, kwa sababu wakati anaondoka kwenda uhamishoni (Kanisa B) alikuwa ni mgeni kiasi na akiwa bado hajamjua vizuri kiongozi huyo. Hata hivyo, baada ya kurudi uhamishoni, taratibu picha ya Kiongozi X ilianza kujifunua na akawa amebahatika kumjua baadhi ya maeneo yake ambayo yalianza kumuweka kwenye tahadhari kubwa, ukizingatia kuwa tayari alikuwa na tahadhari pia kwa Kiongozi Mkuu, tena kubwa tu
  • Kutokana na hali hiyo, hatimaye mhusika alijiridhisha kuwa tahadhari zake juu ya Kiongozi X nazo pia ni sahihi. Kwa hiyo alichofanya baada ya hapo ni kufuta kabisa namba zake zote (alipewa na Mr X wakiwa ofisini, zilikuwa mbili au tatu)
  • Baada ya Kiongozi X kuona mhusika ha-respond tena kama alivyotarajia, ndiyo akaamua kutumia sasa mbinu nyingine ya kumnong’oneza pindi wanapokuwa wanasalimiana, NJOO OFISINI NIKUTAMKIE MIBARAKA, NJOO OFISINI TUONGEE,.. ili kumuanzisha upya, wakati huo kiongozi huyo akiwa hajui chochote kama mhusika tayari alishaweka tahadhari kubwa juu yake
Kwa hiyo negative response ya mhusika juu ya appointment yake na Kiongozi X ndiyo ilipelekea sasa yatokee haya yote yanayoelezwa hapa kwenye tukio hili la nne

HITIMISHO JUU YA TUKIO HILI:

MFANANO WA KIPEKEE ULIOJITOKEZA KATI YA APPOINTMENT YA MWANZO (KATI YA MHUSIKA NA KIONGOZI MKUU) NA APPOINTMENT AMBAYO INGEWEZA KUWA YA PILI (KATI YA MHUSIKA NA KIONGOZI X)


Kwa hiyo, ukiangalia kwa undani zaidi utakuta kuwa kuna mfanano wa kipekee sana unajitokeza kwenye appointment ya mwanzo, iliyofanyika kati ya mhusika na Kiongozi Mkuu, na hii iliyokuwa inatafutwa kati ya mhusika na Kiongozi X, (ambayo haikuwahi kuwepo).

Ni kwamba mikakati iliyotumika kwenye appointments hizi mbili ina mfanano wa kipekee sana hasa kwenye mambo kadhaa yafuatayo, kwamba appointment zote mbili zinaonekana KAMA:
  • Ziina mazingira yaliyokuwa yakim-prompt mhusika kuomba appointment wakati si upande wake uliokuwa unahitaji maongezi, isipokuwa ule wa pili, yaani upande ule wa viongozi wake
  • Zote zina Plan B ambayo Mr X ametumika, baada ya Plan A kuwa haikufanikiwa kufanya kazi. Kwenye tukio hili la sasa, Plan A ilikuwa ni kwamba mhusika angeendelea kubaki na kushiriki Ibada ya pili; na ofauti tu ni kwamba lile la mwanzo walitumika wawili yeye na mke wakati kwa hili la sasa ametumika akiwa peke yake
  • Zinamhusisha Mr X kama cover ya kuwaziba watu wengine waliokuwa karibu, wasiweze kujua nini kilikuwa kinaendelea kati ya maongezi ya mhusika na viongozi waliokuwa wanatamani kufanya appointment na mhusika
  • Zililenga kumfanya Mr X awe shahidi wa kile kilichokuwa kinaendelea kati ya mhusika na viongozi hao kabla, wakati na baada ya appointment zao, na hata baada ya mazungumzo yao halisi kuwa yamefanyika na kumalizika
Kwa tukio hili, tuseme sasa pengine Kiongozi X alikuwa na nia ovu juu ya mhusika na kwamba kungeweza kutokea chochote mbele ya safari. Kwa hiyo, kwa namna Mr X alivyotumika kwenye tukio hili, hakuna shaka kabisa kuwa angekuwepo bega kwa bega kwa ajili ya kuokoa jahazi la upande wa Kiongozi X.

MWISHO WA TUKIO HILI

MWANDISHI WENU ATARUDI TENA KWA AJILI YA KUONYESHA RARE COINCIDENCE NYINGINE ILIYOTOKEA HIVI KARIBUNI SIKU ZA JUMAPILI YA TAREHE 24/05/2020 NA JUMATANO YA TAREHE 27/05/2020; NAYO PIA IKIMHUSISHA TENA MR X (Kumbukeni kuwa hili bado siyo tukio, isipokuwa ni rare coincidence tu ambayo ina viashiria vinavyoweza kuepelekea uwezeekaano wa kuwepo tukio)

UPDATE WEDNESDAY 03/06/2020

HITIMISHO LA MATUKIO YOTE MANNE YALIYOELEZWA HAPO JUU, NA AMBAYO YANAMHUSU MR X PIA


Katika kujaribu kuhitimisha mada hii ambayo imekuwa hewani kuhusiana na matukio haya ya ajabu manne bila kuwapoteza wasoamji, na kabla ya kuingia kwenye COINCIDENCE ya mambo mengine yaliyojitokeza kwenye siku kati ya J2 ya wiki juzi na J5 ya wiki jana, mhusika anapenda kukumbushia mambo kadhaa yafuatayo, kabla hajahamia kwenye jambo lingine
  • Kwamba mada iliyokuwepo hewani mpaka muda ilikuwa inahusiana na matukio manne ya ajabu ambayo mhusika alishawahi kuyashuhudia
  • Matukio haya, ni machache sana kati ya mengi sana ambayo mhusika ameshawahi kukumbana nayo mpaka muda huu
  • Kati ya matukio haya manne, matatu yalitokea Kanisani na moja ambalo linahusiana na Fire Extinguisher, ni la ofisini
  • Matukio ya ofisini ni mengi mno ukilinganisha na yale ya Kanisani, kwa sababu mzizi wa mtandao wa matukio haya upo ofisini
  • Na kwa sababu nia haikuwa kuongelea matukio ya ofisini, ndiyo maana mhusika ameamua kuleta kwenu matukio mengi ya Kanisani, possibly panapo nafasi huko mbele ya safari, na ya ofisini nayo atayongelea pia
  • Katika matukio haya mannne, tukio moja la ofisini ameliunganisha kwa sababu nalo pia ni kati ya yale matukio mengi ya ofisini ambayo yanayomhusisha Mr X
Mbali na hayo, maelezo ya matukio haya manne, yalichochewa pia na ukweli kwamba J2 ya tarehe 26/04/2020 kwenye mkutano wa dharura wa wanaume:
  • Ilionekana kama kulikuwa na fujo ilikuwa imepangwa kufanyika Kanisani, iwapo mhusika angeamua kunyanyua ulini wake kutoa hoja kwenye mkutano huo
  • Na ili kuthibitisha wasiwasi wake huu kwa wasomaji, mhusika alilazimika sasa kutoa taarifa kwa wasomaji, ya baadhi ya matukio machache sana ambayo yalishawahi kumpata huko nyuma., nia yake ikiwa ni kuwapa mwanga wasomaji waweze kupima juu ya wasiwasi wake huo kwamba, HAWA VIONGOZI AMBAO MHUSIKA ANADAI KUWA WANAWEZA KUWA WALIKUWA WAMEPANGA KUFANYA FUJO SIKU HIYO YA MKUTANO; FUJO AMBAYO INGEWEZA HATA KUPELEKEA VYOMBO VYA DOLA KUSOGEA KANISANI HAPO KWA AJILI YA KUTULIZA GHASIA, JE NI KWELI KWAMBA VIONGOZI HAO WANAWEZA KUWA WANA DALILI ZA UELEKEO WA MASHAKA YA MHUSIKA, AU ANAWASINGIZIA? JE, NI KWELI VIONGOZI HAO WANAFANANAFANANA NA MATENDO YA NAMNA HIYO?
Kwa hiyo kwa kukumbushia tu ni kwamba, kipengele hiki cha mwisho chenye maswali ndiyo kilichopelekea mhusika alete kwenu baadhi tu ya matukio (machache sana) kati ya mengi ambayo taarifa zake anazo, na ambayo haupo hata muda wa kutosha kuweza kuyaleta kwenu moja baada ya jingine. Kikubwa alichozingatia hapa ni kuchagua yale ambayo Mr X anahusika kwa sababu yeye ni mtu pekee kati ya watu wachache sana ambao wana-operate kwenye INTERSECTION ya set zote mbili za mitandao, yaani ule wa ofisini na wa kanisani pia. Hii pia inamaanisha kuwa si Mr X peke yake anaye operate kwenye mitandao miwili, wapo wengine pia ofisini, japo ofisi zao haziko jengo moja na la mhusika kama ilivyo kwa Mr X

N
Update 2: WEDNESDAY 03/06/2020

RARE COINCIDENCE ILIYOTOKEA KATI YA SIKU ZA JUMAPILI YA TAREHE 24/05/2020 NA JUMATANO YA TAREHE 27/05/2020; NA AMBAYO INAMHUSISHA MR X TENA

MAELEZO YA AWALI KUHUSIANA NA MATUKIO YANAYOUNDA COINCIDENCE YENYEWE


Go to page 8

UPDATE THURSDAY 04/06/2020

RARE COINCIDENCE ILIYOTOKEA KATI YA SIKU ZA JUMAPILI YA TAREHE 24/05/2020 NA JUMATANO YA TAREHE 27/05/2020; NA AMBAYO INAMHUSISHA MR X TENA


Inaendelea………………..

MAELEZO KUHUSIANA NA MATUKIO YANAYOUNDA COINCIDENCE YENYEWE

PDATE THURSDAY 05/06/2020

RARE COINCIDENCE ILIYOTOKEA KATI YA SIKU ZA JUMAPILI YA TAREHE 24/05/2020 NA JUMATANO YA TAREHE 27/05/2020; NA AMBAYO INAMHUSISHA MR X TENA


Inaendelea………………..

MAELEZO KUHUSIANA NA MATUKIO YANAYOUNDA COINCIDENCE YENYEWE

UPDATE MONDAY 08/06/2020

MAELEZO MAFUPI YA MWISHO KUHUSIANA NA MR X

A: MAHUSIANO YA MR X NA MHUSIKA KAMA WATU WANAOFANYA KAZI MAHALI PAMOJA
 
Kwamba kuliwa na lengo povu la kumuambukiza COVID-19?

Je, muumini huyu anamgogoro wowote na viongozi wa kanisa hilo?

Amesema ni miezi miwili tangu uanze kusali kanisani hapo, he katika kanisa lake la awali alikuwa kiongozi? Je, aliondoka huko kwa amani bila mgogoro na mtu?

Kwa mtizamo wangu kama hakuna hayo mamambo, basi huyo rafiki yako awe na amani tu, yaliyoyokea yametokea lakini si kwa makusudi ya kumdhuru.

Mshauri afanye fullybody sanitizer kama ile ya Rostam na Makonda!

Pia achukue tahadhali zaidi juu ya CORONA.
 
Kwamba kuliwa na lengo povu la kumuambukiza COVID-19?

Je muumini huyu anamgogoro wowote na viongozi wa kanisa hilo?.....
Ni mao ya kiroho zadi. Zingatia kipengele hiki hapa:

SABA: Huyu bwana anadai kuwa kipindi kabla ya Corona, wakati watu walikuwa wako huru kushikana mikono, kuna watu wachache ambao alikuwa ameshawaainisha, ambao walikuwa wana tabia ya kuhakikisha kuwa wame-shake hands naye kabla Ibada haijaanza, na kwa nia ambayo yeye anadai kuwa haikuwa njema.

Hawa watu walikuwa wamejipanga randomly kiasi kwamba usipokuwa makini, huwezi kuwatofautisha na wengine ambao walikuwa wanakwenda ku-shake hands naye kwa nia iliyo njema.

Inaonyesha KAMA hawa shaker hands, wameanza kutumia sanitizer kwake, kama substitute yao baada ya Corona kuingia, maana haiwezekani tena ku-shake hands kwa sasa.
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom