Mkasa wa Dr. Ulimboka: Inawezekana Kabisa Sio "Inside Job"!, bali ni "Smear Campaign?!.

Hii nilitaka kuiposti kule Jamii Inteligence nikidhani ni theories za kiinteligensia, nikagundua kumbe kule huwezi kuposti mpaka kwa kibali cha mode, hivyo nimeileta huku jukwaa huru ambalo halihitaji ruhusa ya yeyote kuposti humu!.

Wanabodi,

Wakati tukiendelea kugumia kilichomkuta Dr. Ulimboka, kama kawaida lazima "conspiracy theories' ziwepo ili kujifariji kuwa kuwa aliyefanya hivyo ni nani na kwa malengo gani?.

'Conspiracy theory' Number 1: " It is an "inside job"!.
theory hii ambayo ndiyo ya walio wanaamini kabisa ile ni kazi ya serikali, kwa msingi kuwa yeye ndio chanzo cha mgomo toka mwanzo, kwa hiyo, akishughulikiwa, mgomo ndio utamalizika rasmi, hivyo serikali ikawatumia vijana wake waitwao "the oparatives" wamshughulikie vile wataona inafaa, na kweli vijana wakaingia kazini na kilichotokea ni motokeo ya kazi "nzuri" ya vijana wale ambao wameitekeleza vibaya (incomplete), hivyo sasa kui embarass serikali!.

Wanabodi, hakuna ubishi, "the oparatives wapo", na hizo ndizo kazi zao, lakini naomba kutofautiana na simple thinkers wanaoamini its an 'inside job', kwa sababu ili "oparatives" waingie kwenye any 'covert' oparation, lazima kwanza waweke malengo, "what do they want to achieve", ili kujaustify "the motive behind", na kabla ya utekelezaji, lazima wapime, "impact" na "consequences" ndipo huamua "the best way" ya utekelezaji, na kwa vile "they are proffessionals", siku zote hutekeleza with very high degree za 'precise' na leaving no trace behind!.

Kilichomtokea Dr. Ulimboka ni kazi ya "amateures" kwa kuacha loop holes kibao ambapo ukiwa "deep thinker", uta doubt kama ile ni kazi ya "professionals", hivyo inawezekana kabisa sio "inside job", unless kilichofanyika kiwe ni tactics za vijana wa "inside job" to carry out kihovyo hovyo ili ionekana ni amateures na huko kumuacha aishi pia ndio lengo na sio aliachwa kuishi kwa bahati mbaya!.

Normal comon sense inanishawishi nijiulize, kama Dr. Ulimboka ndie adui wa serikali, kama serikali hiyo hiyo imeamua kumshughulikia kwa njia hiyo ili iachieve nini?. Ule msemo wa mchawi, mpe mwanao akulelee kwa imani kuwa hawezi kumdhuru!, hivi inawezekana kweli serikali yetu ndio iliyomshughulikia Dr. Ulimboka na kwa nanma ile?!. Kama ni kweli, hii ni kazi ya "inside job", then for sure, "hii itakuwa ni serikali ya vichaa!".

Conspiracy Theory No. 2. Could it be just a "Smear Caipaign"?!.
Adui wa adui yako ni rafiki yako, kwa vile Dr. Ulimboka ndiye kiongozi wa hii migomo, na hii migomo imeishaipasua sana kichwa serikali, hadi rais Jakaya Kikwete, akautangazia umma kuwa mgomo ule ni wa mwisho, na kwa vile sasa mgomo umeibuka tena na kuwafanya wote waliojifanya kuuepusha tangu mwanzo kuonekana wajinga, akiwemo rais JK, its obvious Dr. Ulimboka ndie alishaonekana ni adui wa serikali na kila mtu anajua, hivyo jambo lolote litakalomtokea Dr. Ulimboka, automatically, fingers zitakuwa pointed kwa serikali kuwa sio mshukiwa bali ni mhusika mkuu!.

Kwa msingi kuwa, Dr. Ulimboka ni adui wa serikali, automatically atakuwa ni rafiki wa maadui wa serikali, hivyo sasa amegeuka target nzuri kwa maadui wa serikali waliomo within, ambao hawaitakii mema serikali yao, wakaamua kumshughulikia Dr. Ulimboka ili kuiembarass serikali kunyooshewa vidole vya lawama kwa utaratibu unaojulikana kama "smear Campagn"!.

Could it be?.
Conspiracy Theory Number. 3 Its an "Isolated event" as an "Oportunity to Gain"
For every problem, there is an "opportunity to gain", wakati watu wanalia kwa msiba wa mpendwa wao, kwa mjenga majeneza, its an opportunity to gain!. Zamani mtu akifiwa tulikwenda kulala kumfariji, na majirani ndugu jamaa na marafiki kuchangia chochote, huku kina mama wakijitanda kanga na tulikwenda kulala misibani kwa upendo!. Siku hizi misiba ni dili, watu wanashona sare, kutengeneza T-shitrs, mpampaji, caterer, Kwanya, PA, video, picha, MC hadi waliaji wakukodishwa wapo!, hizi zote ni opportunities, kama ilivyo kwa wenzetu wa traffic, gari lako likikuharibikia, kwao ni opportunity na ikitokea ajali, zile breakdown zinashindana mpaka wanapiganaga!.

Vivyo hivyo, huu mgomo wa madaktari, kwa wengine ni shida na vilio, lakini kwa wengine its an opportunity to geai more and more!. Hivyo ndiyo ilivyo hii posibility ya conspiracy theory ya 3, kuwa Waliomteka Dr. Ulimboka, could be paid up thughs, waliokuwa contaracted na mtu au kikundi cha watu, ambao kwao mgomo ni dili kubwa na kadri utakavyo endelea, ndivyo wao wanavyo stand to gain!, kwa vile Dr. Ulimboka ndie kiongozi wa madaktari, ukimpotezea kwa kipigo kile, utafanikiwa ku fuel madaktari wapandishe hasira na kugoma jumla if possible, ili wao wazidi kuneemeka. Hawa pia walifanya hivi ili ionekane wazi, aliyemshughuliki Dr. Ulimboka sii mwingine, bali ni yule yule adui yake ambaye ni "one and only" anayefahamika!. Kama theory hii ni kweli, then walidhamiria kumpotezea jumla, na survival yake ni kwa kudra ya Mungu tuu!. And if this is the case, then aliyemlipa mpiga zumari, ama atakuwa tayari, kulipa fungu kubwa zaidi ili kuikamilisha kazi hiyo, kabla Dr. Ulimboka asije kuwatambua!, au atakodi timu nyingine, kuhakikisha, anawanyamazisha wote waliomshughulikia Dr. Ulimboka kwa kuwapotezea!.

Salama ya hao waliolipwa ni ku confess the sooner the better ili wabaki salama, vinginevyo, they'll vanish into thin air within no time!.


Pole Dr. Ulimboka.

Get well soon!.

Pasco.
​
Hizi theories zako Mkuu zingekuwa valid kama Dr. Ulimboka angekuwa hayupo duniani..lakini Mungu hajampenda zaidi muda huu. Dr Ulimboka ana kumbukumbu na inavyoonekana Madaktari wanawajua mafedhuli hao katili. Tubule subira Dr Ulimboka apate nafuu na uzima ili aje kuujuza Umma. Hizo theories ungezituliza kwanza kapuni.
 
Ndugu katika Bwana fikiri mara mbili kabla ya Kushangilia huu udhalimu wa ma dktr Zidi ya wasionacho Kuwa na huruma ya kimungu hawo ma dk Ni wanyama wanaroho ngumu sana kwa pa moja tuiombee nchi yetu



hivi sisi watanzania tunamatatizo gani? madaktari hawa tunawaita wana roho ngumu leo lakini kwa muda mrefu wamekuwa wanatuhudumia pamoja na makasoro tele katika sekta ya afya na mazingira magumu ya kazi tuna nini?
 
View attachment 57744

Haya mkuu embu ona nani kaathirika hapo na nani anapaswa kuombewa mungu

Hiyo picha ya hao wamama ni kati ya mambo wanayopinga madaktari, hapo utatoaje huduma sasa? Au mgomo ndo umesababisha hao wasijifungue? Poa, Uli akiombewa mabaya na yakamkuta hao wamama watapata vitanda gafla na huduma kuboreka? Come on brother, the issue here is the government. If it was serious we wouldn't have reached here! Kumbuka kuwa madaktari hawadai nyongeza ya mshahara peke yake. How do you risk your life where you know you're not valued?
 
Hiyo picha ya hao wamama ni kati ya mambo wanayopinga madaktari, hapo utatoaje huduma sasa? Au mgomo ndo umesababisha hao wasijifungue? Poa, Uli akiombewa mabaya na yakamkuta hao wamama watapata vitanda gafla na huduma kuboreka? Come on brother, the issue here is the government. If it was serious we wouldn't have reached here! Kumbuka kuwa madaktari hawadai nyongeza ya mshahara peke yake. How do you risk your life where you know you're not valued?

Je njia waliyoitumia ni sahihi? Ingelikuwa Mama Yako ama Mke ama Mtoto wako amefariki kwa kukosa muhudumu wa kumtundukia tu drip leo hii ungekuwa unaandika huo ***** hapo juu?
 
Je njia waliyoitumia ni sahihi? Ingelikuwa Mama Yako ama Mke ama Mtoto wako amefariki kwa kukosa muhudumu wa kumtundukia tu drip leo hii ungekuwa unaandika huo ***** hapo juu?


ila hao uliowataja wangekufa kwa kukosa dawa ama kukosa huduma kwa kutokuwapo na vifaa fulanifulani wewe ungeandika huo up.............................. ulioandika hapo.
tafakari
 
ila hao uliowataja wangekufa kwa kukosa dawa ama kukosa huduma kwa kutokuwapo na vifaa fulanifulani wewe ungeandika huo up.............................. ulioandika hapo.
tafakari

Ebu penda kushirikisha hata akili yako ya kuzaliwa

Maana ulichoeleza sio nilichoeleza unaleta mambo ya kama kama
Zungumzia hali halisi acha UGAMBAGWANDA wewe
 
Mi naona kuna watu wametumwa kuvuruga akili za wengine na kujifanya kutengeneza conspiracy theory ambazo hazipo na kupima watu wana buy story gani
1. Kuna theory za Pasco
2. Kuna jina la Blandina Nyoni linatajwa kwa nguvu
3. Kuna "kikundi kinachofadhili"- Martha Mlata Mb
4. Wananchi wanye hasira

nk

Lakini wote hakuna anayesema cochcote kuhusu watu waliokuwa pamoja na Ulimboka wakati anakamatwa/tekwa
1. dr. Deo-amezungumza na magazeti, na olisi. Ndie alyeripoti tukio, bila shaka ametoa maelezo na jina la mtu waliyekuwa naye
2. Huyu mtu wa tatu ni nani (so far majina mawili yanatajwa-Abedi/Abduel). Kamanda Kova aliepuka kabisa kutaja chochote kama polisi inamtafuta huyu mtu ama la; hakuna chochombo chochote kilicho ripoti kujaribu kufanya nae mawasiliano, mtu huyu muhimu ambaye kwangu mpaka sasa ndie shahidi muhimu " ambaye hakuna anayependa kuongea naye" (which seems fishy). Tukumbuke huyu mtu hakuwa mgeni kwa Ulimboka na deo, wamekutana mara kadhaa (zipo habari pia aliambatana na Pinda Muhimbili katika kikao cha madaktari). The big qiestion is Kova ana mpango wa kumtafuta huyu jamaa ahoojiwe????
 
Hakunalolote Pasco anataka kutupeleka upande mwingine tofauti, Pasco inamaana unataka kusema wenye Hospital binafsi ndio wanausika na mchezo mchafu huu wa kumumiza Dkt Ulimboka? au wapinzani wa serikali ya JK ndio walio usika?
Si kubaliani na maelezo yako ya kutaka kunitoa kwenye mstali ambao ninausimamia kwa nguvu zote na ninauamini kwa 100% kuwa SERIKALI IMEUSIKA NA UTEKAJI WA Dkt ULIMBOKA full stop.
 
As a normal human being huwezi muombea binadamu mwenzio mabaya it is not ethical...., lets hope 4the best this matter can be resolved siasa pembeni maisha ya wenzetu ndo muhimu
 
Sidhani kama kuna mkono wa mtu ama chama ama serikali katika sakata la Dr. Ulimboka. Kilichompata nadhani ni hatua ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa 'kumgawia maumivu' kiongozi anayeogoza watu waliopewa dhamana ya kuangalia afya na uhai wa watu kwa niaba ya aliyewaumba na serikali. Na hapo naona somo pande zote mbili, serikali na madaktari. Madaktari watambue umuhimu wao, na km wamegoma kweli, Dr. Uli km mtanzania mwingine na mlipa kodi angeachwa km walivyoachwa wagonjwa wengine MOI.

Sikubaliane na kitendo walichonfanyia Dr. Uli, ila kitendo cha yeye kupewa huduma nzuri na sasa anaendelea vizuri kinaonesha kuwa madaktari wetu wanatuchezea pamoja na serikali kwa kuchagua watu wakuwahudumia kulingana na vyeo/nafasi/nk. Madaktari acheni ubabaishaji, hamuezi kutumia roho za watu kuichapa serikali! Watu wamechochwa na tabia zenu za kibabe na ukaidi.

Wavaa magwanda nanyi msiwe opportunists, kutumia tukio hili kujipatia umaarufu kwa 'kulaani'. How can you prove that you are innocent on this issue?

Labda hukujua kinachoendelea, madaktari wanafanya fundraising kupata pesa ya kumpeleka Dr Ulimboka India kwa matibabu zaidi.
 
Hizi theories zako Mkuu zingekuwa valid kama Dr. Ulimboka angekuwa hayupo duniani..lakini Mungu hajampenda zaidi muda huu. Dr Ulimboka ana kumbukumbu na inavyoonekana Madaktari wanawajua mafedhuli hao katili. Tubule subira Dr Ulimboka apate nafuu na uzima ili aje kuujuza Umma. Hizo theories ungezituliza kwanza kapuni.
tulimsubiri na kumuombea sana "Dr. Mwakyembe" apone na arudi katika afya yake ya kawaida huku tukiwa na shahuku ya kuujua ukweli. Mwisho siku tuliambulia kauli kama hizi, "....naomba mjadala wowote kuhusu afya yangu ufungwe"
"mi ni mzima na nipotayari kuitumikia serikali"
"yote yalitokea namuachia Mungu"
 
Kwani DR. Ulimboka ndio mgojwa peke yake?, hujaona watu wanataabika na kufa kwa kukosa huduma? kuna haja ya kuwaombea wagonjwa wote.
 
Back
Top Bottom