Mkasa wa Dr. Ulimboka: Inawezekana Kabisa Sio "Inside Job"!, bali ni "Smear Campaign?!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkasa wa Dr. Ulimboka: Inawezekana Kabisa Sio "Inside Job"!, bali ni "Smear Campaign?!.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Jun 28, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,234
  Trophy Points: 280
  Hii nilitaka kuiposti kule Jamii Inteligence nikidhani ni theories za kiinteligensia, nikagundua kumbe kule huwezi kuposti mpaka kwa kibali cha mode, hivyo nimeileta huku jukwaa huru ambalo halihitaji ruhusa ya yeyote kuposti humu!.

  Wanabodi,

  Wakati tukiendelea kugumia kilichomkuta Dr. Ulimboka, kama kawaida lazima "conspiracy theories' ziwepo ili kujifariji kuwa kuwa aliyefanya hivyo ni nani na kwa malengo gani?.

  'Conspiracy theory' Number 1: " It is an "inside job"!.
  theory hii ambayo ndiyo ya walio wanaamini kabisa ile ni kazi ya serikali, kwa msingi kuwa yeye ndio chanzo cha mgomo toka mwanzo, kwa hiyo, akishughulikiwa, mgomo ndio utamalizika rasmi, hivyo serikali ikawatumia vijana wake waitwao "the oparatives" wamshughulikie vile wataona inafaa, na kweli vijana wakaingia kazini na kilichotokea ni motokeo ya kazi "nzuri" ya vijana wale ambao wameitekeleza vibaya (incomplete), hivyo sasa kui embarass serikali!.

  Wanabodi, hakuna ubishi, "the oparatives wapo", na hizo ndizo kazi zao, lakini naomba kutofautiana na simple thinkers wanaoamini its an 'inside job', kwa sababu ili "oparatives" waingie kwenye any 'covert' oparation, lazima kwanza waweke malengo, "what do they want to achieve", ili kujaustify "the motive behind", na kabla ya utekelezaji, lazima wapime, "impact" na "consequences" ndipo huamua "the best way" ya utekelezaji, na kwa vile "they are proffessionals", siku zote hutekeleza with very high degree za 'precise' na leaving no trace behind!.

  Kilichomtokea Dr. Ulimboka ni kazi ya "amateures" kwa kuacha loop holes kibao ambapo ukiwa "deep thinker", uta doubt kama ile ni kazi ya "professionals", hivyo inawezekana kabisa sio "inside job", unless kilichofanyika kiwe ni tactics za vijana wa "inside job" to carry out kihovyo hovyo ili ionekana ni amateures na huko kumuacha aishi pia ndio lengo na sio aliachwa kuishi kwa bahati mbaya!.

  Normal comon sense inanishawishi nijiulize, kama Dr. Ulimboka ndie adui wa serikali, kama serikali hiyo hiyo imeamua kumshughulikia kwa njia hiyo ili iachieve nini?. Ule msemo wa mchawi, mpe mwanao akulelee kwa imani kuwa hawezi kumdhuru!, hivi inawezekana kweli serikali yetu ndio iliyomshughulikia Dr. Ulimboka na kwa nanma ile?!. Kama ni kweli, hii ni kazi ya "inside job", then for sure, "hii itakuwa ni serikali ya vichaa!".

  Conspiracy Theory No. 2. Could it be just a "Smear Caipaign"?!.
  Adui wa adui yako ni rafiki yako, kwa vile Dr. Ulimboka ndiye kiongozi wa hii migomo, na hii migomo imeishaipasua sana kichwa serikali, hadi rais Jakaya Kikwete, akautangazia umma kuwa mgomo ule ni wa mwisho, na kwa vile sasa mgomo umeibuka tena na kuwafanya wote waliojifanya kuuepusha tangu mwanzo kuonekana wajinga, akiwemo rais JK, its obvious Dr. Ulimboka ndie alishaonekana ni adui wa serikali na kila mtu anajua, hivyo jambo lolote litakalomtokea Dr. Ulimboka, automatically, fingers zitakuwa pointed kwa serikali kuwa sio mshukiwa bali ni mhusika mkuu!.

  Kwa msingi kuwa, Dr. Ulimboka ni adui wa serikali, automatically atakuwa ni rafiki wa maadui wa serikali, hivyo sasa amegeuka target nzuri kwa maadui wa serikali waliomo within, ambao hawaitakii mema serikali yao, wakaamua kumshughulikia Dr. Ulimboka ili kuiembarass serikali kunyooshewa vidole vya lawama kwa utaratibu unaojulikana kama "smear Campagn"!.

  Could it be?.
  Conspiracy Theory Number. 3 Its an "Isolated event" as an "Oportunity to Gain"
  For every problem, there is an "opportunity to gain", wakati watu wanalia kwa msiba wa mpendwa wao, kwa mjenga majeneza, its an opportunity to gain!. Zamani mtu akifiwa tulikwenda kulala kumfariji, na majirani ndugu jamaa na marafiki kuchangia chochote, huku kina mama wakijitanda kanga na tulikwenda kulala misibani kwa upendo!. Siku hizi misiba ni dili, watu wanashona sare, kutengeneza T-shitrs, mpampaji, caterer, Kwanya, PA, video, picha, MC hadi waliaji wakukodishwa wapo!, hizi zote ni opportunities, kama ilivyo kwa wenzetu wa traffic, gari lako likikuharibikia, kwao ni opportunity na ikitokea ajali, zile breakdown zinashindana mpaka wanapiganaga!.

  Vivyo hivyo, huu mgomo wa madaktari, kwa wengine ni shida na vilio, lakini kwa wengine its an opportunity to geai more and more!. Hivyo ndiyo ilivyo hii posibility ya conspiracy theory ya 3, kuwa Waliomteka Dr. Ulimboka, could be paid up thughs, waliokuwa contaracted na mtu au kikundi cha watu, ambao kwao mgomo ni dili kubwa na kadri utakavyo endelea, ndivyo wao wanavyo stand to gain!, kwa vile Dr. Ulimboka ndie kiongozi wa madaktari, ukimpotezea kwa kipigo kile, utafanikiwa ku fuel madaktari wapandishe hasira na kugoma jumla if possible, ili wao wazidi kuneemeka. Hawa pia walifanya hivi ili ionekane wazi, aliyemshughuliki Dr. Ulimboka sii mwingine, bali ni yule yule adui yake ambaye ni "one and only" anayefahamika!. Kama theory hii ni kweli, then walidhamiria kumpotezea jumla, na survival yake ni kwa kudra ya Mungu tuu!. And if this is the case, then aliyemlipa mpiga zumari, ama atakuwa tayari, kulipa fungu kubwa zaidi ili kuikamilisha kazi hiyo, kabla Dr. Ulimboka asije kuwatambua!, au atakodi timu nyingine, kuhakikisha, anawanyamazisha wote waliomshughulikia Dr. Ulimboka kwa kuwapotezea!.

  Salama ya hao waliolipwa ni ku confess the sooner the better ili wabaki salama, vinginevyo, they'll vanish into thin air within no time!.


  Pole Dr. Ulimboka.

  Get well soon!.

  Pasco.
  ​
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Hapa Pasco sijakuelewa vizuri
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Pasco, unaonekana unajua sana mambo yanayofanywa na hao vijana unaowaita "operatives". Je, we ni mmoja wao? Maana unaandika kwa uhakika na kwa kujiamini sana. Unajua hata wasivyofanya makosa ktk utekelezaji wa "kazi" yao.
   
 4. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekuelewa vizuri asante kwa uchambuzi wako wa kimantiki!
   
 5. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Endelea kuchambua pasco tudadavulie kwa uwepesi usione uvivu kuandika
   
 6. M

  Moony JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  You have SOME points there. Pia kuna madaktari wenzake inawezekana kabisa wakawa wametumiwa na moja ya makundi uliyotaja.

  Keep it up 'Perry Mason'
   
 7. kinyoba

  kinyoba JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 1,238
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Naunga mkono hoja hasa hii "smear campaign "
   
 8. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa, wavaa khaki za mgambo wanahusika hapa !
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Pasco, smear campaign inajikita kwenye maneno -information ili kuharibu reputation ya mtu/watu fulani. Ni tofauti na sana na kidnapping and torture (inflicting physical pain/injury). Naona umetumia nguvu kubwa sana kujenga hoja ya kufanya watu 'pyscholigically' wakubali hiki ni something which is not.

  Kuna watu wana roho ngumu (wengine hupenda kusema roho ngumu kama paka) and Dr Ulimboka happens to be one of them. Waingereza wanasema, he lived to tell.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Haaahaaa! Why so many noises? I hate jumping into conclusions kwenye kitu ambacho mtu hajakifahamu. Anywey ndo demokrasia yetu ilivyo...we agree to disagree
   
 11. 1

  1st.Tanzanian Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lengo halikuwa kusababisha kifo, but to create a distraction with political headline
   
 12. d

  dmayola JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  K
   
 13. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Lengo kuu ni kuamisha fikra za madaktari,i think tanzania now its a hell,nafikiri tuwape wengine dola potelea mbali ntapiga kura zangu 2015 waibe wasiibe sio ccm,waligombea posho wananch wakakataa wakajipa kimya kimya kura zetu ah ,
   
 14. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,983
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  waliofanya hvy ni maadui wa serikali ya jk..
   
 15. K

  Kapeleka Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama kuna mkono wa mtu ama chama ama serikali katika sakata la Dr. Ulimboka. Kilichompata nadhani ni hatua ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa 'kumgawia maumivu' kiongozi anayeogoza watu waliopewa dhamana ya kuangalia afya na uhai wa watu kwa niaba ya aliyewaumba na serikali. Na hapo naona somo pande zote mbili, serikali na madaktari. Madaktari watambue umuhimu wao, na km wamegoma kweli, Dr. Uli km mtanzania mwingine na mlipa kodi angeachwa km walivyoachwa wagonjwa wengine MOI.

  Sikubaliane na kitendo walichonfanyia Dr. Uli, ila kitendo cha yeye kupewa huduma nzuri na sasa anaendelea vizuri kinaonesha kuwa madaktari wetu wanatuchezea pamoja na serikali kwa kuchagua watu wakuwahudumia kulingana na vyeo/nafasi/nk. Madaktari acheni ubabaishaji, hamuezi kutumia roho za watu kuichapa serikali! Watu wamechochwa na tabia zenu za kibabe na ukaidi.

  Wavaa magwanda nanyi msiwe opportunists, kutumia tukio hili kujipatia umaarufu kwa 'kulaani'. How can you prove that you are innocent on this issue?
   
 16. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jamani kama serikali haihusiki basi ni very simple watupe wahusika, maana hapa mtu kama mimi yaani hata nichapwe nasema serikali ina mkono wake kwa hiyo kunibadilisha nahitaji kabisaaaaa vielelezo tosha. na serikali ijue tu ikishindwa kutupa inamaanisha ndio ina mkono mia kwa mia tena wakichukua muda tutahisi wanapika kwa hiyo wafanya chapu tu
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Kapeleka, utasema nini kama Dr Ulimboka atatambua mmoja/baadhi ya watu waliomfanyia huo unyama. Ndio maana nadhani essay ya Pasco is very pre-mature. Well planned, badly excuted. He lived to tell!
   
 18. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Its kinda difficult kuangalia upande mwingine kutokana na facts japo tunajaribu ili kujiridhisha kwa ku "think outside the box, kila nikijaribu narudi palepale...............
  Sidhani kama lengo lilikuwa ku inflict pain tu indicators zote zilikuwa zinaelekeza kuwa jamaa auwawe na judging from yule mwanausalama aliyekong'otwa pale muhimbili ni vigumu kukubali kirahisi kuwa hakuna mkono wa Serikali
   
 19. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Duh, unaweza kuhisi kuwa kuna mkono wa wale walioachishwa
  baada ya kuvunjwa baraza la mawaziri au yale makundi yetu ndani
  ya Chama.
   
 20. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1:kuna idadi kubwa ya madoctor wa kutegemewa na wenye elimu ya kati wanamiliki zahanati(nyengine za nguvu)au maabara zao binafsi,na asilimia kubwa ya vyombo vinavyotumika humo sawa dawa zinazotolewa au vyombo vya kupimia na kuainishwa gonjwa,ni mali ya hospitali za serikali,zimefikaje humo,wakati kama wanavyodai kuna upungufu mkubwa wa dawa na vyombo mbali mbali(majina mengi sana yameorodheshwa mikoa na wilaya na ....)mbali mbali!
  2:madoctor hao hao unapokwenda hospitali za serikali hukwambia ili kuepuka foleni na kupata dawa za bei poa,nakuandikia vipimo nenda kwenye zahanati yangu upate huduma nafuu na ya fasta!!tupo pamoja hapo??!!
  3:madoctor wengi sana ni walevi na wazinzi wa kupindukia hata wakiwa kazini,na asilimia si mbaya ya madoctor hao ni waathirika wa h.i.v
  4:kuna idadi si ya kupuuzia ya madoctor wanaotumia madawa ya kulevya,na kuna wengine yameshawaathiri vibaya,hapo tunategemea nini??!!(data wahusika wanazo)
  5:madoctor wengi wananyumba za malaya wao za kutunza tu si chini ya tatu mpaka tano,wakati mjarisiamali mwenye kipato cha kati kutunza familia moja tu ni kazi!!!,hapa naona wanahaki ya kugoma!
  6:ni lazima madoctor wawe na jeuri kwa masikini wa hali ya chini kwani wenye fedha wakiwahonga hata usiku wa saa nane hukurupuka,na kusikiliza nini kimejiri,kwa kuwa wamezoeshwa hulka hii,asiekuwa na hela,kutibiwa hospitali za serikali ni ndoto,au atapasuliwa kwa makusudi kichwa badala ya goti.
  kuna mengi sana ya kuongeza hapo,tatizo mda!
  nimewasilisha hoja wana jf!!
   
Loading...