Dr Ulimboka ni raia kama raia mwingine na watu wengi washakumbwa na makubwa zaidi yake. Tanzania ina watu milioni 45 sasa itawezekana vipi mtu mmoja awashughulishe watu wa JAMII FORUMS namna hii? Kuna watu wamekufa na wameteseka zaidi ya huyu mtu mmoja, sasa sielewi kwa nini baadhi ya watu wanataka kuilaumu serikali kwa yaliyotokeaSerikali iko bize kushughulikia hii migomo na jeshi la polisi haliwezi kupeleka resources zake zote kushughulia kesi ya mtu mmoja wakati wengine wanapata taabu zaidi yake.Hoja za msingi hapa ni 2.1. Serikali haiwezi kulaumiwa kuwa ilimteka na kumpiga. Tanzania sio banana republic na ni nchi inayoendeshwa na sheria na kama hakuna mwenye ushahidi wa kutosha kuwa serikali ilimteka ulimboka then fikirieni conspiracy theories zingine lakini sio kumteka na kumpiga huyu jamaa. Kuna watu ambao wanaiendesha mbio serikali kama akina Issa Ponda wapo na hakuna aliyewateka wala nini.2. Jeshi la Polisi hawawezi kulaumiwa kwa lolote. Na sikuona sababu ya mkuu wa polisi kuitisha press conference juu ya Dr Ulimboka. wao wangesema kuwa jalada limefunguliwa na wataishughulikia kesi yake kama mtu mwingine.Just thinking outside the box
1. Kama Tanzania ina watu milioni 45 ina maana kwanza umetambua umuhimu wa mtu mmoja na ukimwondoa hutasema tena watu milioni 45.
2. Ili ionekane ni tukio muhimu, wewe ungetaka wapigwe watu wangapi kaa Dr Ulimboka? Kwa maneno mengine, inatakiwa ifike idadi gani ya watu ili tukio liwe muhimu?
3. Huwezi katika hatua hii useme: "serikali haihusiki na jeshi la polisi halihusiki". Nani anayehusika? Ili ionekane serikali haihusiki na jeshi la polisi halihusiki ndio maana wapenda haki wanashauri iundwe tume huru ili kufanya uchunguzi usio wa upendeleo.
4. Tukio la Dr Ulimboka ni muhimu kwa sababu kama halitafutiwi ufumbuzi basi hata hao Watanzania milioni 45 unaodai huenda nao wakawa wanatendewa kama Dr Ulimboka na hata wengine wakawa wanapotea au uliwa katika mazingira kama hayo na kwa kutumia 'reasoning' yako, kama atakuwa anauliwa mtu mmoja mmoja tu kwako haitakuwa issue hadi watu milioni 45 watakapotoweka maana hiyo ndiyo namba kubwa zaidi kwa hapa Tanzania.