Mkasa wa Dr. Ulimboka: Inawezekana Kabisa Sio 'Inside Job'!, bali ni 'Smear Campaign'?!

Kama hii nchi ina watu wana mawazo mafupi kama yako wewe hans, basi watanzania wataendelea kuburuzwa milele... Hata mtoto wa darasa la tatu ukimuelezea hii senariao lazima ataelewa kinachoendelea.

Nakataa kukubali kuwa wewe ni kiziwi au kipofu wa kutokuona haya mambo au umetumwa kuja kuleta destraction humu JF, Tanzania haingozwi na walokole au watawa, au na wewe ni wale usalama wa taifa ambao kazi pekee wanayoijua ni kuua? Hizo fikira zako za nje ya boksi kaziweke kwenye dust bin....
 
Kuna raia na raia maarufu, mifano ipo mingi kwamba Steven Kanumba alikuwa rai wa kawaida lakini alikuwa maarufu(let the famous people be praised) Ndio Dr Ulimboka alikuwa raia wa kawaida lakini maarufu,kwa hiyo Kama ni maarufu lazima aenziwe hiyo ni kawaida ya binadamu wote,sasa Kama wewe sio maarufu ni bahati mbaya lakini utake usitake watu maarufu wataenziwa( kuheshimiwa) na sio kwa Ulimboka tu walikuwepo watu maarufu na dunia itaendele kutoa wangine lakini kila mwanadamu na wakati wake.

Kama wapo waliofia msalabani wakapata umaarufu,wapo waliofungwa Kama Nelson Mandela na kadhalika kwahiyo Hoja kusema ni raia Kama raia mwingine ni sawa lakini yeye ni maarufu,Kama wewe sio maarufu basi hiyo ni bahati mbaya tafuta kitu kikupe umaarufu na Ndio utakapo enziwa,
 
Mawazo ni haki haki ya mtu.Mtazamo wangu Serikali iweya kwanza kutajwa kwatika mkasa huu.
1. Serikali inavyombo vya usalama vyote ambavyo vinakusanya taarifa zote zinazoashiria kuhatarisha usalama wa Taifa kama migomo,hujuma ambazo zinaweza kufanywa kwa lengo la kuiabisha Serikali.Je nitaarfa zipi serikali ilishauriwa na wanausalama na ilichukua hatua gani,Kama vyombo hivyo havikufanya kazi hiyo serikali inatuambia nini?

2. Kama serikali haijahusika Wanausalama wanaishauri na kutabili nini mbele yetu ili
a.kuzui watu kutumia migogoro wake kutumiwa na magenge ya kulipiziana risasi
b.kuthibiti magenge ya uhasama yanayotokana na siasa chafu,ufujaji wa mali ya Umma,
c.kufuatilia magenge yanayoitwa walinzi binafsi.
d.kuthibiti uwezekano wa watu kuunda magenge yao yakuteka nyara watu kama la ulimboka limefanikiwa
e.mauaji ya askari halali ambayo watakuwa katika kazi halali kwa sas hata mimi kama nina silaha sitakubali kuchukukuliwa kizembe eti mtu amejitambulisha yeye polisi
f.Ili kuepusha vijana wengi wasio na ajira kutekwa na matajiri katika ajira za utekaji nyara kwani kuna watu wengi matariji lakini wanazungukwa na Malalamiko mengi ikiwamo kutumia vibaya utajiri wao
Kifupi Watanzani niseme chimbuko la mkasa wa ulimboka ni zaidi ya mgomo tatizo ni serikali kutokuwa makini katika ukusanyaji ripoti.

Wizi wa pesa za serikali hauvumiliki unasbabisha watu kujiuliza swali Je serikali haina pesa kweli.
pesa zinazoibwa ni matokeo mabaya ukusanyaji wa taarifa kwa watu wenye dhamana.
Hatua zinazochukuliwa dhidi ya matapeli wa mali za umma yanatia mashaka kwa wanaodai hali ngumu za maisha.

Kazi ya usalama wa nchi ni kazi zaidi ya kulinda viongozi kwani viongozi watakuwa salama kama haki na usawa vinatawala nchi.

BARAZA AU SHIRIKA HURU LA USALAMA WA TAIFA NI MUHIMU SANA KWA SABABU KILA MTU HATA RAIS ANAWABAYA WAKE CHOMBO HIKI KIWEZE KUKUSANYA TAARIFA ZA MTU HATA KABLA YA KUINGIA MADARAKANI
Ili kuepusha madhara ambayo hata wanaoyaandaa yatawarudi serikali IJIPAMBANUE WAZI WAZI KWAMBA HAIKUHUSIKA KWANI KUSEMWA KUWA IMEHUSIKA NI KUPOTEZA IMANI KWA WANANCHI NA HIVYO NI VIASHIRIA VYA KUTOWEKA AMANI NCHINI
MUNGU IBARIKI tANZANIA
 
dr ulimboka ni raia kama raia mwingine na watu wengi washakumbwa na makubwa zaidi yake. Tanzania ina watu milioni 45 sasa itawezekana vipi mtu mmoja awashughulishe watu wa jamii forums namna hii? Kuna watu wamekufa na wameteseka zaidi ya huyu mtu mmoja, sasa sielewi kwa nini baadhi ya watu wanataka kuilaumu serikali kwa yaliyotokea

serikali iko bize kushughulikia hii migomo na jeshi la polisi haliwezi kupeleka resources zake zote kushughulia kesi ya mtu mmoja wakati wengine wanapata taabu zaidi yake.

Hoja za msingi hapa ni 2.

1. Serikali haiwezi kulaumiwa kuwa ilimteka na kumpiga. Tanzania sio banana republic na ni nchi inayoendeshwa na sheria na kama hakuna mwenye ushahidi wa kutosha kuwa serikali ilimteka ulimboka then fikirieni conspiracy theories zingine lakini sio kumteka na kumpiga huyu jamaa. Kuna watu ambao wanaiendesha mbio serikali kama akina issa ponda wapo na hakuna aliyewateka wala nini.

2. Jeshi la polisi hawawezi kulaumiwa kwa lolote. Na sikuona sababu ya mkuu wa polisi kuitisha press conference juu ya dr ulimboka. Wao wangesema kuwa jalada limefunguliwa na wataishughulikia kesi yake kama mtu mwingine.

Just thinking outside the box

wewe mtanzania bwana, umenena. Liwalo na liwe. Heri yenu.
 
Plato aliwagawa watu katika makundi 3. Sijui ndugu yetu uko wapi. Nway, una uhuru wa maoni, tumekusikia, waliokutuma wamekusikia na wanasonga mbele.
 
Dr Ulimboka ni raia kama raia mwingine na watu wengi washakumbwa na makubwa zaidi yake. Tanzania ina watu milioni 45 sasa itawezekana vipi mtu mmoja awashughulishe watu wa JAMII FORUMS namna hii? Kuna watu wamekufa na wameteseka zaidi ya huyu mtu mmoja, sasa sielewi kwa nini baadhi ya watu wanataka kuilaumu serikali kwa yaliyotokea

Serikali iko bize kushughulikia hii migomo na jeshi la polisi haliwezi kupeleka resources zake zote kushughulia kesi ya mtu mmoja wakati wengine wanapata taabu zaidi yake.

Hoja za msingi hapa ni 2.

1. Serikali haiwezi kulaumiwa kuwa ilimteka na kumpiga. Tanzania sio banana republic na ni nchi inayoendeshwa na sheria na kama hakuna mwenye ushahidi wa kutosha kuwa serikali ilimteka ulimboka then fikirieni conspiracy theories zingine lakini sio kumteka na kumpiga huyu jamaa. Kuna watu ambao wanaiendesha mbio serikali kama akina Issa Ponda wapo na hakuna aliyewateka wala nini.

2. Jeshi la Polisi hawawezi kulaumiwa kwa lolote. Na sikuona sababu ya mkuu wa polisi kuitisha press conference juu ya Dr Ulimboka. wao wangesema kuwa jalada limefunguliwa na wataishughulikia kesi yake kama mtu mwingine.

Just thinking outside the box

nikusaidie kwa machache tu kwanza: baada ya kuchukuliwa pale leaders club, marafiki zake walienda kutoa taarifa kituo cha polis, kwanza wakaambiwa "anahojiwa". Sasa endelea na conspiracy theories zako.................
 
Dr Ulimboka ni raia kama raia mwingine na watu wengi washakumbwa na makubwa zaidi yake. Tanzania ina watu milioni 45 sasa itawezekana vipi mtu mmoja awashughulishe watu wa JAMII FORUMS namna hii? Kuna watu wamekufa na wameteseka zaidi ya huyu mtu mmoja, sasa sielewi kwa nini baadhi ya watu wanataka kuilaumu serikali kwa yaliyotokea

Serikali iko bize kushughulikia hii migomo na jeshi la polisi haliwezi kupeleka resources zake zote kushughulia kesi ya mtu mmoja wakati wengine wanapata taabu zaidi yake.

Hoja za msingi hapa ni 2.

1. Serikali haiwezi kulaumiwa kuwa ilimteka na kumpiga. Tanzania sio banana republic na ni nchi inayoendeshwa na sheria na kama hakuna mwenye ushahidi wa kutosha kuwa serikali ilimteka ulimboka then fikirieni conspiracy theories zingine lakini sio kumteka na kumpiga huyu jamaa. Kuna watu ambao wanaiendesha mbio serikali kama akina Issa Ponda wapo na hakuna aliyewateka wala nini.

2. Jeshi la Polisi hawawezi kulaumiwa kwa lolote. Na sikuona sababu ya mkuu wa polisi kuitisha press conference juu ya Dr Ulimboka. wao wangesema kuwa jalada limefunguliwa na wataishughulikia kesi yake kama mtu mwingine.

Just thinking outside the box

Siku ukijua jinsi serikali ya Tz inavyoendeshwa ndo utajua hoja zako hazina msingi juu ya suala la Dr Ulimboka
 
subiri siku utakavofanyiwa wewe ndo utajua kiazi wewe!!
 
Ungeweza kujenga hoja nzuri (ya kushawishi) kwamba Serikali haihusiki na kadhia hiyo lakini si jinsi ulivyofanya. Dr. Ulimboka katika habari ya sasa si mtu yeyote! Inawezekana Tanzania unayoifahamu wewe ni nzuri sana; hujawahi kukutana na adha za dola. Halafu usijidanganye, Tanzania ni banana republic kwa kila kigezo (ukiondoa wananchi wake wastaarabu walio wengi pia). Utawala wa sheria unaoendeshwa kwa kuangalia sura? Ambapo kuna wasiogusika (untouchables)? Wanaoiba mabilioni Benki Kuu na kuombwa kurudisha kiasi? Wanaochukua 100% kwenye rada lakini hawakamatiki pamoja na wauzaji/matapeli (BAE Systems) kulazimika kukiri dhulma na kurejesha? Hujasikia habari za watu kubambikiwa kesi au kuzimwa kwa vitisho na rushwa? Uko nchi ipi hasa?

Mwenyewe nilishangaa na sikutaka kuamini uhusika wa serikali katika hili. Kwa sababu hakuna manufaa yoyote ambayo serikali ingepata kwa kufa au kuumia kwa Dr. Ulimboka. Lakini serikali ya CCM ina hulka ya kufanya mambo mengi ya kijinga katika kuonyesha umwamba kwa wanyonge kiasi cha kujichimbia kaburi yenyewe. Kuna sera ya siri ya kutisha (terrorise) wale wote wanaoonekana tishio kwa maslahi ya viongozi. Sihitaji kutaja mifano. Hili la Ulimboka ni jaribio jingine la kutotumia busara katika serikali hii (a bungled case).

Of course, wako wanaoogopwa pia kwa namna moja au nyingine kama hao unaowataja - akina Ponda ongeza na kina Slaa, Lissu, n.k. Angalau jamaa wanajua mahali ambapo ukigusa ni kama bomu la atomiki. Walifikiri Ulimboka anaweza kupotezewa kirahisi kama unavyodhani wewe - mtu wa kawaida tu. Kwa bahati mbaya si katika context ya sasa!
 
Sababu zifuatazo ndiyo zinahusisha serikali na kipigo cha Dr. Ulimboka;-

Maelezo ya Dr. Ulimboka

Katika maelezo yake ya jinsi alivyokamatwa na kuteswa; Dr Ulimboka anasema waliomteka, walihitaji KUJUA tu NANI YUPO BEHIND YA MIGOMO YA MADAKTARI inayoendelea. Kwakua yeye ni kiongozi wa hiyo migomo, hao watekaji walitegemea kwavyovyote vile Ulimboka angewasaidia katika kuwapa hiyo habari.
-Je, ndugu Hans Rogers Dibagula, unadhani kibaka, jambazi au hata ndugu wa aliyempoteza mgojnwa wake fuatia migomo ya madaktari, habari za nani yupo nyuma ya migomo atazihitaji kwa ajili gani na ili azifanyie nini?...ni..PEKEYAKE SERIKALI NDIYO WANGEZIHITAJI habari hizi, au nani wengine?

Maelezo ya Dr . Deo, ambaye walikuwa pamoja na Ulimboka siku ya tukio, anasema; watu hao watano waliomteka Ulimboka walivaa nguo KAMA za kijeshi huku wakiwa wamebeba bunduki. Kwa hapa nchini, wanao vaa nguo zinazofana kama za jeshi, ni askari wetu wa TISS wanao linda mageti yakuingia ofisini, na kwenye hili, watakuwa wanaotoka eneo kati ya Victoria na Mwenge (fuatia maelezo ya Ulimboka).

Mazingira ya kukamatwa na alipoteswa.

Dr. Uliomboka anakumbuka; wakati akiwa kwenye gari, huku akiwa anachukua kipondo, na kabla hajaingia kwenye nyumba fulani nzuri hivi, alikumbuka kupita maeneo ya victoria (yaani walipita maeneo ya Victoria). Na wakati alipokuwa anaenda kutupwa huko mabwepande, alikumbuka pia kupita maeneo ya mwenge. Kwahiyo kwa hesabu nyepesi tu kabisa, sehemu aliyokuwa anakula kichapo ni eneo lolote kati ya victoria na mwenge, lenye nyumba nzuri.......ulimboka anaeleza pia kuwa; kuna wakati ali'attempt kukimbia wakati anakula mkong'oto ghafla, risasi ikapigwa hewani ili kumzuia asile kona..... Hivyo basi, inaonyesha kuwa eneo aliliopelekwa ili kula nakoz, risasi inaweza kupigwa anyhow na polisi wasiweze kuja kufuatilia mlio huo....
-Hans, ni sehemu gani kati ya mwenge na Victoria unayoweza kudhania ....?

Ufuatiliaji na ujihusishaji wa vyombo vya serikali

TBC1, haikutangaza kabisa katika taarifa yake ya habari ya saa mbili usiku tukio la kukamatwa na kupigwa Dr. Ulimboka, tofauti na vyombo vingine vyote vya binafsi vya TV nchini, vilivyotangaza, tena kama habari ya kwanza. ....Kusafirishwa kwa Dr. Ulimboka, hapo napo TV zote zilitangaza isipokuwa TBC1.
Magazeti mengi ya serikali yaliandika "....kinara wa migomo ya madaktari atekwa..." Lakini kifo cha Kanumba.... nadhani uliona TV yetu nzuri ya taifa TBC1 ilivyokava vyema msiba ule wa kusikitisha.

Katika kituo cha polisi cha kawe ambapo Ulimboka alipelekwa baada ya kuokotwa, polisi hawakufanya juhudi yeyote ya kumtafutia usafiri wa haraka ili akimbizwe hospitalini kuokoa maisha yake kutokana na kuvuja kwa damu nyingi. Polisi walipoulizwa kwanini hawakutoa msaada huo walisema; walikuwa wanawangoja ndugu zake.

".....kamanda shupavu HEMED, alikutwa faragha akiongea na Radio za ki'Police akiripoti;....bado hajafa....pale Muhimbili! Swali kwako ndgu Hans, Kwani alitakiwa afe? (fuatia mazungumzo ya hemedi na wenzie)..."

Tangu Jumanne hadi hii leo, hakuna aliyekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo.

Hitimisho

Kwa kumtocha vile ili kupata information za aina ile tu, ni kuonyesha ukihiyo na ukilaza wa maafisa waliofanya zoezi hili ulivyo mdogo, ukilaza na ukihiyo, ukizingatia uwepo wavyombo vingi vya kisasa vya kunasa mawasiliano ya email,text, voice call na kumfuatilia 24/7 kila atakapoweka mguu. Halikadhalika, kuna private compony nyingi za uchunguzi zipo nchini na zenye vyombo vya kisasa, in one week mngepata kila mlichotaka.

Intelijensia ya sasa hapa Tz, ni ile yakupeana bila kuangalia uwezo wa mtu na ndiyo inatufikisha hapa....! Tumchukue huyu kijana kwakua mzazi wake aliyekufa na alikuwa mfanyakazi mwenzetu hapa tiss ili kuisaidia familia ya marehemu.....aaah, hata kama ni ZUZU, tumchukue tu...?!! huyu kaletwa na mkuu, tumchukue tu. Matokeo yake, intelijensi haiwezi kujisafisha na kadhia hii mbele ya sura za nchi za kimataifa.....kama ilivyo kuwa kwa Owko jirani zetu, Sarowiwa huko NGA....!

Kibanga Msese.
 
Mwenye akili timamu hahitaji kujadili nani amehusika katika huu uharamia. Jibu liko dhahiri na Dr. Ulimboka alimtaja mmoja wao kwa jina na kumtambua kwa sura pindi alipofika MMH kumaliza kazi yake. Mwenyezi Mungu akamshushua! :wacko:
 
Tatizo lako ni kuwa, hujui kuwa Population ya watu milioni 45 Tanzania inasumbuliwa na mtu mmoja tu, ambaye ni Kikwete.Na Kwa sababu iyo hiyo ndo mana hao watu mil45 wamesahaulika anajadiliwa mkombozi wa afya ya watanzania mil45.Funguka.

Sigma hiyo avater yako ungejua inavyotema usingeikashifu Serikali ya Dr Ulli yameshatokeea mwacheni apone lakini mumi SIO ktk wa TZ anaowatetea hutto Dr na wenzake ndo maana nasisitiza Uluumboka sio Mwajiriwa wa Serikali ila ni Mkiti wa MaDr wasiopungua 400 na ukitoa walio Mafunzoni hawafiki MaDr 150 mfano mikoani km Dodoma walikuwa 10 tu kwa nini na mm uniweke ktk watu m45 SITAKI na waache wafukuzwe wote tutabaki na Ma-Medical na Manesi kuliko kumlipa mmoja 7.7m NO BIG NO Hospital si zao kwa nini Wasiondoke?

Sigme itokee vita au milipuko km ya hapo Kenya hao MaDr (wasio na Uzalendo) watasogea au ni hii .com inawadanganya mnatakajifananisha na Syiria au Somalia Acheni tukae kwa Amani mwenye ubavu akaulize yale majengo karibu na Victoria kwa nini wananccua nguo na kuacha bukta au kutoa kucha na meno mbona geti lipo wazi!!
 
Dr Ulimboka ni raia kama raia mwingine na watu wengi washakumbwa na makubwa zaidi yake. Tanzania ina watu milioni 45 sasa itawezekana vipi mtu mmoja awashughulishe watu wa JAMII FORUMS namna hii? Kuna watu wamekufa na wameteseka zaidi ya huyu mtu mmoja, sasa sielewi kwa nini baadhi ya watu wanataka kuilaumu serikali kwa yaliyotokea

Serikali iko bize kushughulikia hii migomo na jeshi la polisi haliwezi kupeleka resources zake zote kushughulia kesi ya mtu mmoja wakati wengine wanapata taabu zaidi yake.

Hoja za msingi hapa ni 2.

1. Serikali haiwezi kulaumiwa kuwa ilimteka na kumpiga. Tanzania sio banana republic na ni nchi inayoendeshwa na sheria na kama hakuna mwenye ushahidi wa kutosha kuwa serikali ilimteka ulimboka then fikirieni conspiracy theories zingine lakini sio kumteka na kumpiga huyu jamaa. Kuna watu ambao wanaiendesha mbio serikali kama akina Issa Ponda wapo na hakuna aliyewateka wala nini.

2. Jeshi la Polisi hawawezi kulaumiwa kwa lolote. Na sikuona sababu ya mkuu wa polisi kuitisha press conference juu ya Dr Ulimboka. wao wangesema kuwa jalada limefunguliwa na wataishughulikia kesi yake kama mtu mwingine.

Just thinking outside the box
so far namshangaa mtoa mada,mada yenyewe na hata hao waliomgongea like!!!!!!.hivi siku hizi wale watu wa kuchakachua thread wamepotelea wapi?
 
Sigma Mtu Mzima hatishiwi nyau Runguka
Soma hiyo ngoma imeisha chocheeni kingine na wanaharakati wenu

Breaking Nuuuuuuuuuz: JULAI 2, 2012Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012. Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo.

Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizoUpande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.

Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji.. KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.Imetolewa na;Aminiel Buberwa AligaeshaAfisa Uhusiano Mwandamizi Julai 2, 2012
Tatizo lako ni kuwa, hujui kuwa Population ya watu milioni 45 Tanzania inasumbuliwa na mtu mmoja tu, ambaye ni Kikwete.
Na Kwa sababu iyo hiyo ndo mana hao watu mil45 wamesahaulika anajadiliwa mkombozi wa afya ya watanzania mil45.
Funguka.
 
Sigma Mtu Mzima hatishiwi nyau Runguka
Soma hiyo ngoma imeisha chocheeni kingine na wanaharakati wenu

Breaking Nuuuuuuuuuz: JULAI 2, 2012Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa 16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizoUpande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji.. KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.Imetolewa na;Aminiel Buberwa AligaeshaAfisa Uhusiano Mwandamizi Julai 2, 2012
Duh, kweli JF imekuwa kokoro! Kuisema serikali ya Kikwete ni kama kufungulia bomba la maji machafu, wapuuzi na wachafu wote watajitokeza kuitetea. Kuteswa kama alivyoteswa Dr. Ulimboka kuna maana moja tu kuna kitu kilikuwa kikitafutwa na Dr. hakuweza kukitoa. Ni taasisi moja tu inaweza kumtaka Dr. Ulimboka ataje walioko nyuma ya mgomo wa Madaktari, nayo ni serikali na kwa kuwa kilichokuwa kikitafutwa ni nani wa kumbambikizia hizo tuhuma...na kwa mtu yeyote mwenye chembe ya uelewa, madai ya Stella Manyanya bungeni yamezidi kufichua lengo la hawa vilaza serikalini.

Lakini kwa kuwa jambo hili si kweli, Dr. Ulimboka ilibidi ang'olewe hadi meno na kucha lakini kwa ushujaa wa ajabu hakuwapa kile walichotaka. Vinginevyo leo hii TBC ingekuwa kila dakika inaimba wimbo wenye sauti ya Dr. Ulimboka akikiri kuhusika kwa chama cha siasa katika mgomo wao. Jambazi ama mlipa kisasi asingemvamia Dr. Ulimboka Leaders Club (of all the places!), na kumbeba mzobe mzobe na bila wasiwasi...Nachukia vilaza na theories zao za kijinga kama hii iliyoletwa hapa. Ona sasa wanavyozidi kujichanganya, eti breaking nu...uz, madaktari warejea kazini, Ukwaju kajipange upya!
 
Hem huyo jamaa afanye review ya waziri mkuu bungeni, alisema " Tume jaribu kufuata mkondo wa sheria,ila tunaona tumeshindwa, na inatulazimu tufanye jambo fulani, come what may" Sasa yeye hadhani jambo lolote nje ya ssheria ambalo serikali ingeweza kufanya ni kitu kama hicho? lets be realistic jamani kwenye vitu kama hivi. Remember peoples' lives are at stake here.
 
what a brilliant analysis! Members wa JF wanatakiwa kutoa hoja na uchambuzi wenye mashiko na uzito mantiki na mtiririko kama hizi na siyo kuoneshana umahiri wa matusi na mizaha kama wanavyofanya baadhi yetu.

Hans ametoa mchango wake, na mkuu huyu kamfungulia upande wa pili wa coin ambao naamini hata Hans kama ni makini ataukubali na kuobgeza uelewa wake kuhusu hili sakata la Dr. Ulimboka.

Hizi ndizo aina za hoja zinazojenga na kuelimisha.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom