Mkasa wa Atletico Madrid na Eibar

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
3,187
8,213
Wakati Eibar wanapanda daraja kushiriki La Liga 2014, Atletico Madrid walikuwa mabingwa wa Hispania.

Miaka saba baadaye, 2021, Eibar wameshuka daraja, Atletico wametwaa tena ubingwa.

Unaweza ukadhani Eibar wamefeli sana hadi kushuka daraja na Atletico wamefanikiwa sana kwa kushinda ubingwa.

Hutokosea ukiwaza hivyo kwa sababu kwenye mpira ubingwa ndiyo furaha ya juu zaidi na kushuka daraja ndiyo ya chini zaidi.

Lakini hii siyo kwa Eibar, kwao kushuka daraja siyo jambo la huzuni sana kwa sababu ndani ya nyoyo zao wanaamini fika kwamba wao siyo timu ya ligi kuu, siyo timu ya daraja kwanza na wala siyo timu ya daraja la pili.

Wao wanaamini kwamba timu yao ina hadhi ya kucheza daraja la tatu tu...basi!

Hii ni kwa sababu timu hiyo inatoka kwenye kamji kadogo ambako hakana uwezo wa kuhimili kuwa na timu za madaraja hayo ya juu.

Eibar inatoka kwenye mji wenye hilo hilo la klabu, ambao una wakazi 27,000 tu.

Uwanja wa nyumbani wa Atletico Madrid, Wanda Metropolitano, unachukua watu 68,456...wa Eibar ni watu 5200.

Ukiwachukua watu wote wa mji wa Eibar halafu ukawaweka kwenye uwanja wa Atletico, siti 41453 zitabaki wazi.

Hii inaifanya Eibar kuwa timu yenye uchumi mdogo zaidi kwenye La Liga, Segunda 1 na hata Segunda 2.

Mwaka 2014, wakati wakiwa kwenye kampeni zao za kupanda daraja, walikuwa kwenye hatari ya kushushwa hadi daraja la tatu kutokana na sheria ya kifedha kwenye michezo iliyopitishwa mwaka huo na kupangwa kuanza kutumika Agosti mwaka huo huo.

Sheria hii ilitaka kila klabu angalau iwe na mtaji wa hisa Euro milioni 1.7.

Kiasi hiki kilikuwa mtihani mkubwa kwa klabu hiyo hadi Xabi Alonso ambaye alikuwa Real Madrid wakati huo, alipoendesha kampeni ya kuchangisha pesa.

Alifanya hivyo kuisaidia klabu hiyo ambayo aliwahi kuichezea.

Bajeti yao ya mishahara ni Euro milioni 3.5 kwa msimu, wakati Atletico Madrid kwa wiki tu ni Euro milioni 2, 789,000.

Kikosi chao kimesheheni wachezaji wa mkopo tu au usajili huru, kasoro wawili.

Wakati Luis Suarez ndiyo anayelipwa zaidi Atletico Madrid, pauni 281,000 kwa wiki, kwa Eibar ni Gonzalo Escalante pauni 22, 000 kwa wiki.

Kubaki La Liga kwa misimu 6 mfululizo, ni muujiza kwao!
 
Back
Top Bottom