Mkasa mzima kutenguliwa kwa Mkurugenzi wa NIMR

Magufuri mjanja...lazima atamfuta machozi mda si mrefu kwa kumpa posti kubwa kama kuwa mkuu wa hospital ya muhimbili kitengo cha mifupa kwani aliepo bado anakaimu.
Hapo ndipo huwa sielewi kabisaaaaa 'unamfukuza mtu kazi kwa kosa fulani kesho unamwajiri kazi kubwa zaidi' Sasa hapa nani anakomolewa aliyefukuzwa akaajiriwa au aliyefukuza akaajiri?!
 
Ambacho sikielewi...hivi kweli hilo kosa alilolifanya linahalalisha kufukuzwa kazi?

Hakuweza kupewa onyo tu la kiofisi kwamba 'hapa umechemsha, usirudie tena'?

Au labda alikuwa anatafutiwa sababu kwa siku nyingi na fursa ilipojitokeza tu ndo ikawa mwisho wake?

Mkuu najaribu kuwaza ukubwa wa hili kosa na lile la kununua MV Dar es Salaam ambayo hata sijui iko wapi...
 
Nilitegemea nikifingua nikutane na wingu kweli.

Nilitegemea tupate chanzo kamili cha kutenguliwa tofauti na habari za zika.

Anyway
Free mexencemelo
Hii kitu ndio imetumika "kumpiga panga/kumtumbua" Dr. Mwele.
Dr. alikuwa "mkweli" kupita kiwango kinachokubalika na mamlaka alipotoa taarifa ya utafiti.

Kweli hakuufuata ukiritimba wa kutoa ripoti za utafiti wa magonjwa ya binadamu lakini bado hakupaswa kuondoshwa kwa utaratibu huo, hapa uvumilivu ungetumika kwani hakuna alie mkamilifu.pia tafiti hii yapaswa kupingwa kitafiti si maneno tu kwani huyu mama nimsomi na ameonesha kuwa wataalamu wa ttanzania wanaweza,nyinyi mnakimbilia WHO tu.
 
Hili saga utalielewa vizuri zaidi ukisikiliza video ya Mkurugenzi (Mwele), halafu ya Kigwangala na mwisho ile ya Waziri ambamo na Mganga mkuu alizungumza. Kuna ile abstract pia iko kwenye nyuzi za jamii forum. Ukivichanganya hivyo na kama ukiamini ile abstract iko safi kisayansi basi utaona wapi kila aliyejaribu kuzungumza alijikanyaga. Communication ndo imekuwa tatizo kubwa yamesemwa ambayo hayakustahili kusemwa na pande zote mbili labda kama kuna paper nyingine zaidi ya ile iliyowekwa kwenye mtandao.
 
Mkuu nakubaliana na wewe, hata pesa za waathirika wa Bukoba, mimi na wewe tu twachemsha bongo, kupika na kupakia, who knows...Public office === Private matters... unataka kujiingiza kwenye mikasa isiyokua yako, aikuhusu Mkuu...

lakini nakuhakikishia, ukimtema mtu hata kazini kama uko kwenye employment yoyote ile, first kutakua na disciplinary process, warnings na mahashanga mengine halafu then unatemwa, munabaki na gossiping tu offisini ee bwana katemwa kwa sababu ya ulevi wake, kutwa yu maji na mipombe yake, at least you would know the reason.... unfortunately, this is different it is a just a style of leadership, so so refreshing!

na mimi nitajuaje kama wewe hujatumwa humu Mkuu, maana ugali kupatikana huku mtaani umeshakua mgumu, makazini pesa mbovu, na maisha kama mdundiko, unatafuta dagaa wa kukausha na donna la Mikoani, basi aa! aa!, life goes on... si unajua na wengine wanyongeke, we are all playing in the same field, yaani mpaka tunyongeke kweli kweli, basi safari hii ndio tutakaa sawa, one thing for sure I like the honesty of the style, look for the positive, ALWAYS i hope im clear..

kabla sijakuchosha...

I have actually hired and fired in my career. So, I understand that disciplinary processes that involve reprimand are standard. Ila ujue kwamba siyo kila kosa kazini linashuhulikiwa kwa kuanza na onyo. After all, mimi na wewe hatujui kama Dr. Mwele Malecela alikuwa amewahi kupewa onyo huko nyuma au hapana. Pia kumbuka kwamba nafasi yake ilikuwa ni ya kuteuliwa. Hakuna sheria inayomtaka Rais aanze na onyo kabla hajatengua uteuzi wako. This is a fact that we all have to live with under our current constitution. It may be sad, but it is a reality. Nafasi za kuteuliwa ni rahisi kuzipata, na wakati mwingine unaweza kuipata without being the most qualified person for the job, but also ni rahisi sana kuipoteza nafasi ya kuteuliwa. Tuishie tu kusema kwamba Dr. Malecela katenguliwa, sababu ya kutenguliwa kwake tunaweza tusije kuijua milele.
 
Nnamshangaa huyo Mwele, haelewi tofauti ya "research" na "sampling".

Suala ni kwamba je kuna Zika Tanzania au hakuna? Basically, she said Zika cases have been found in Tanzania, following a preliminary research. Kiafya ujumbe muhimu ktk taarifa yake ni kwamba mdudu Zika yupo nchini. Sasa Watanzania na wageni wanachohitaji kujua ni hicho tu kwamba mdudu Zika yupo Tanzania au hayupo. Tuanzie hapo. Kumbuka sample yote waliyoitumia kuja na hiyo conclusion ilipatikana Tanzania. Utaaminika angalau kidogo kama ukikosoa vifaa vilivyotumika kupima huyo mdudu Zika lakini siyo sample wala sampling methodology. A sampling error in this case would most likely indicate the presence of fewer or more cases than reported but not the absence of the disease. The only way you can debunk the findings of this study is by conducting a separate research testing the reported cases again to verify whether they really have the disease or not. Siyo kinadharia hivyo.
 
Ambacho sikielewi...hivi kweli hilo kosa alilolifanya linahalalisha kufukuzwa kazi?

Hakuweza kupewa onyo tu la kiofisi kwamba 'hapa umechemsha, usirudie tena'?

Au labda alikuwa anatafutiwa sababu kwa siku nyingi na fursa ilipojitokeza tu ndo ikawa mwisho wake?

Kwani kafukuzwa kazi?

Nadhani kilichofanyika ni kuondolewa tu ktk cheo cha ukurugenzi (demotion) ktk taasisi hiyo lakini anaendelea kuwa mwajiriwa wa Wizara ya afya na specific ktk taasisi hiyo...

Nadhani ndiyo maana ya "kutengua uteuzi" na si "kufukuzwa kazi" ama "kusimamishwa kazi......"

Kujibu swali lako sasa, tunaweza kusema, ndiyo linamfanya kukosa sifa za kuongoza taasisi na badala yake yeye anapaswa kuongozwa ili aendelee kujifunza taratibu na kanuni za uongozi iwapo tu kweli kakosea utaratibu wa utoaji wa taarifa kama hiyo aliyoitoa.....
 
Mwacheakanyeedebe
segerealeoo ujenzi Mkubwa unaendelea hofusina Kabisa NA atakapopumzika mtukama huyu
ha ha maisha ya kunyea debe ya kawaida kuna watanznia kibao facts has to be said nchi yetu baba
 
Babylata punguza hasira zinaweza kuwa mtego kwenye maisha yako bila wewe mwenyewe kufahamu.
Phillipo unanishangaza sana kwa nini unaona wewe upo sober ila wengine tunahasira kwa sabau ni metamka neon Magufuli kutumia hasira kwenye majibu ya sayansi badaala ya busara nauliza tena je anataka wananchi wa nchi hii tufe
 
Ambacho sikielewi...hivi kweli hilo kosa alilolifanya linahalalisha kufukuzwa kazi?

Hakuweza kupewa onyo tu la kiofisi kwamba 'hapa umechemsha, usirudie tena'?

Au labda alikuwa anatafutiwa sababu kwa siku nyingi na fursa ilipojitokeza tu ndo ikawa mwisho wake?
Halafu ukipata majibu ya swali hili, pia jiulize ni kwa namna gani katika muda mfupi ule imewezekana kuitisha cv ya mteule mpya na mapendekezo ya wataalam wa HR/leadership, kuipitia, kuomba ushauri wa kitaalam na kufanya screening na hatimaye kumtangaza mteule mpya. One size fits all? Unless, uteule siku hizi unafanywa kwa kurusha shilingi tu juu, ikionyesha H au T then mhusika anatangazwa. So interesting!
 
Phillipo unanishangaza sana kwa nini unaona wewe upo sober ila wengine tunahasira kwa sabau ni metamka neon Magufuli kutumia hasira kwenye majibu ya sayansi badaala ya busara nauliza tena je anataka wananchi wa nchi hii tufe
Unapochangia uwe mwangalifu
 
Suala ni kwamba je kuna Zika Tanzania au hakuna? Basically, she said Zika cases have been found in Tanzania, following a preliminary research. Kiafya ujumbe muhimu ktk taarifa yake ni kwamba mdudu Zika yupo nchini. Sasa Watanzania na wageni wanachohitaji kujua ni hicho tu kwamba mdudu Zika yupo Tanzania au hayupo. Tuanzie hapo. Kumbuka sample yote waliyoitumia kuja na hiyo conclusion ilipatikana Tanzania. Utaaminika angalau kidogo kama ukikosoa vifaa vilivyotumika kupima huyo mdudu Zika lakini siyo sample wala sampling methodology. A sampling error in this case would most likely indicate the presence of fewer or more cases than reported but not the absence of the disease. The only way you can debunk the findings of this study is by conducting a separate research testing the reported cases again to verify whether they really have the disease or not. Siyo kinadharia hivyo.

Ukisoma kuhusu ZIKA utafahamu kuwa ugonjwa huo ulivumbuliwa Uganda na muda mfupi baadae Tanganyika katika miaka ya 50s.

Kwa hiyo kama haujafanya tafiti za kina unaweza ukakumbana na "traces" za ugonjwa huo ukadhani kuwa ni ugonjwa wenyewe, hususan ukichukulia kuwa walikuwa wanatumia vipimia ambavyo havijawahi kutumika hapo swali.

Hata kama upo, tafiti zina "procedures" zake za kuhakiki na namna zake za kuwakilisha na hatua zake za kuchukuwa kabla hazijatangazwa Kimataifa.

Huyo Mwale hakuwa sahihi kabisa na nashangaa sana mtu kama huyo kuweza kupewa wadhifa kama huo. She is simply bogus, ZIKA iwepo au isiwepo.
 
Nimejaribu kusoma hii habari zaidi ya mara 5 sijaona sehemu ambayo wingu limetanda labda wenzangu mnisaidie kuhusu hilo wingu

Huyo mleta mada anaejiita BAK si mnafik na fataani wa siku nyingi humu JF. Hana zaidi ya ufataani na unafik.
 
Mtaisoma namba.

Walioisoma namba ni Yona na Mramba na sasa anaeisoma anaeitwa Sioi na tumeona Sumaye akisomeshwa juzijuzi na Mwale na mama'ke ndiyo kama ulivyoona.

Hatufanyi kazi kwa majina.

Ngoja tukianza kutumbuwa sehemu fulani, watu itabidi waeleze ranchi walizipataje.

Tumeanza taratibu kuwataka waliopo serikalini waorodheshe mali zao, za wake zao, za watoto zao na za ndugu, jamaa na marafiki zao.

Soon tutaanza na wastaafu wa serikalini wenye mali zisizo na hesabu.
 
Back
Top Bottom