Wood Stone
JF-Expert Member
- Jul 11, 2018
- 647
- 1,007
Hiyo inatokea ila nimeandika kwa kujikita na uzi. Kiufupi usioe mwanamke anayekuzidi kipato wala elimu. Nazungumzia unapotaka kuoa na siyo ndani ya ndoa.
Hapo kwenye nyekundu mkuu!!
Haitekelezeki kwani kuna mwanamke unaoa umemzidi elimu na kipato ila inatokea bahati nzuri au mbaya anaajiriwa katika kampuni binafsi au hizi za kimataifa ghafla anakuzidi mshahara mara 2 au hata 3 ....
je utamwacha uende ukaoe ambaye hajakuzidi kipato?
Mimi nacho amini ni kuwa :- hata mwanamke awe na kipato cha namna gani hawezi kukudharau kama na wewe unakipatoo chako na unafanyia vitu vya msingi na kikubwa kuliko vyote .... JIAMINI, KUWA NAMSIMAMO NA TEKELEZA MAJUKUMU YAKO KAMA MWANAUME..
Mwanamke akishakuwa na kipato anakua anajiamini na unaweza kuona anakiburi ila ni anakujaribu kuona kama unaweza kumwongoza na kumpa maelekezo bila kujali kipato chake.
KIKUBWA KINACHOTUTESA WANAUME WENGI NI KUTOKUJIAMINI( inferiority )
Ila nawashauri wanaume wanzangu swala la kuzidiwa kipato na mwanamke ni jambo lisilo epukika ...kwa dunia ya leo hivyo tusahau mambo ya zamani (it's a new world)