Mkasa: Katika ndoa kuna fimbo nyingi sana za kuchapiana

alubati

JF-Expert Member
May 29, 2016
4,134
2,000
Ni kweli mkuu hio hali ilishanikutaga kipindi flani sina ramani. Hakuna rangi niliacha kuona hapo mtoto anaenda job na kurudi muhuni naganga njaa mtaani. Siku akijisikia kukuchamba anakuchamba vizuri tu, sometime nilikuwa namzibua ila nachoshukuru tu hakuwahi kuniletea pigo za usaliti maana nahisi tungeuana mjengoni.

Sishauri mtu aanzishe mahusiano serious na mwanamke ikiwa hana shughuli ya kueleweka mjini. Utateseka sure im telling you. Wanawake wana masimango sana wakiwa na nafasi kiuchumi na wepesi sana kujisahau. Ikiwa yeye hana unamfanyia vyote kama binadamu kwa wema na upendo ila wao sasa ni ngumu sana.
Aisee...
 
Wood Stone

JF-Expert Member
Jul 11, 2018
647
1,000
Wqnaume wanakwamba wapi jaman
Wanaume tunapitia mengi sana tunapokuwa hatuna kitu kwa wake zetu. Baadae baada ya jamaa kufanikiwa kimaisha na kuamua kuoa mke mwingine utasikia. Nilimkuta hana mbele wa nyuma, mtaji nimempa mimi. Kwa dharau hizo? Hayupo mwanaume yoyote anayependa kudharauliwa na mwanamke. Huyo jamaa ningekuwa mimi, najifanya mjinga sana, mnanyenyekea hata akinikosea nitamuomba msamaha ili niweze kutumia pesa yake vizuri kuinvest. Nikaweka mambo yangu vizuri kiuchumi. Nikupiga chini wala hakuna kuangaalia nyuma na oa mke mwingine maisha yanaendelea.
 
miss_blossom

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,613
2,000
Mwanaume ukikosa kazi ujue umepatikana.
Wanawake wengi wana roho mbaya huwezi kuamini, yeye akiwa hana kazi utaishi nae na kwao itasaidia kama kawaida, sasa ukose mishe utakiona cha moto, mpaka kwao wanakusimanga
Ni kwa sababu hio sio nature na mwanaume kuhudumiwa. Mwanaume anatakiwa kuwa provider sio tegemezi ndio maana inapotokea mwanaume analelewa inakuwa issue kubwa....
Mwanaume anapopata mwanamke wa kumbeba anatakiwa abebeke japo apigane apate kitu kidogo ila sio kutegemea msaada wa mwanamke siku zote.
Inachosa sana.
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
42,806
2,000
Wanaume tunapitia mengi sana tunapokuwa hatuna kitu kwa wake zetu. Baadae baada ya jamaa kufanikiwa kimaisha na kuamua kuoa mke mwingine utasikia. Nilimkuta hana mbele wa nyuma, mtaji nimempa mimi. Kwa dharau hizo? Hayupo mwanaume yoyote anayependa kudharauliwa na mwanamke. Huyo jamaa ningekuwa mimi, najifanya mjinga sana, mnanyenyekea hata akinikosea nitamuomba msamaha ili niweze kutumia pesa yake vizuri kuinvest. Nikaweka mambo yangu vizuri kiuchumi. Nikupiga chini wala hakuna kuangaalia nyuma na oa mke mwingine maisha yanaendelea.
Hii inawakumbaga wanawake wengi sana wenye vidomodomo ambao huishia kutoswa bila huruma.

Wazee iko hivi,,,Kuwa na mtu ambaye hana kitu ni jambo moja ila kuishi nae vizuri ni jambo lingine.

Kuna mwanamke anaweza akawa na mwanaume ambaye hana kitu ila akam support working together as a team daily anamjaza energy kwa maneno mazuri ya faraja na kumsitiri kadri awezavyo. Words like unaweza baba, i believe in you...hebu try this naamini it will workout, hebu fanya vile tutasogea tu...go for it babaa na kwa baraka na moyo tu kidume unafanikiwa. Mwanamke wa aina hii kuolewa na jamaa na kuja kufanyiwa makubwa maishani kama shukurani ni jambo ambalo litastaajabisha wengi sana ils kiukweli she will be deserving the best out of the planet.

Aina nyingine ndio wale ambao heshima na upendo ni wa nyakati flani tu. Wakati wa raha ndio utajaliwa kama mfalme, pesa ikiwepo kurahisisha maisha utaitwa Handsome na majina yote mazuri. Ila siku hela zikipungua au kukatika uhusiano unageuka kuwa ni jehanamu. Utaitwa mpumbavu, mjinga huna lolote huna maana.
Hata kama pale mwanzo wa mahusiano alikuheshimu na kukuonesha upendo ila ukishaonekana hali yako ya kiuchumi ni duni mwendo wa dharau na kejeli na masimango kwamba huwezi mfanyia hiki wala kile ila yupo na wewe basi tu.

"We upo upo tu mbaba mzima huna kazi...huangalii hata vijana wenzio wamechangamka", "Jamani mi ningepata mwanaume mwenye uwezo tungekuwa mbali sana...ungekuta hata hatukai kwenye kanyumba haka kama choo!"

Kiukweli mwanamke wa aina hii ukitusua ni rahisi mno kumuacha solemba maana hana utu hata kidogo. Mwisho ni lawama tu oh, nilimpenda yule mwanaume nikamsaidia hili na lile ila deepdown ulimsaidia kwa masimango mengi mno. Ubongo wa mwanadamu ni mwepesi kukumbuka mabaya kuliko mema.

So inategemea na uliishi vipi na mtu, kama ulifanya manyanyaso kutokana kwamba mtu ana hali duni hatokaa asahau hilo hata kidogo. Mtu atasepa zake akafanye maisha mbele huku utaishia kuwa mtu wa lawama tu. Tujifunze kuishi na watu vizuri!
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
1,677

Wise msg ever!
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,457
2,000
Jamani mwanamke unapopata kazi unatakiwa kuipenda na kuwa na heshima kazi yako isiwe fimbo ya kuchapia watu..

jamani kuna dada mmoja ameolewa yeye anakazi ya ofisini ameajiriwa mumewe kazi hana yani yule kaka naona hana tu bahati ya kupata kazi japo amesoma mpaka diploma kutokana na maisha kuwa magumu kabla ya kuoa huyu kaka alipata kazi katika kampuni ya ulinzi ambayo ilikuwa inamsaidia anapata hela za kulipa kodi na kufanya mambo yake mengine

yule kaka akafanya kazi hapo kwa muda tu ila kipindi cha kati hapa tukagundua kunamabadiliko sana yani kijana anazidi kunawiri alikuwa amepanga chumba kimoja mara akamuomba mama mwenye nyumba yake anataka chumba na sebule kwakuwa kunampangaji mmoja alikuwa anahama kwenye hiyo nyumba

na akavilipia, mara tukaona ndani kunaletwa makochi, firji na makapeti mmhhh watu wakaanza kujiuliza jamaa kapandishwa cheo???? siunajua uswahilini tena

heeeee mara tukawa tunaona mwanamke anakuja siku za weekend anapika na kupakua na kufanya usafi ndio watu wakaanza sasa maneno ya chini chini mwanaume kabebwa kapata mwanamke mwenye hela ndio maana kamfanyia hivyo vyote, lakini yule kaka hakuacha kazi yake akawa bado anaendelea nayo masikini sema tu ndio mabadiliko kwa mtu aliyemjua tokea zamani anayaona na kushangaa ikaenda hivyohivyo mpaka yule kaka kuamua kuoa sasa kumuoa yule msichana kweli harusi zetu za ubwabwa simnazijua tukaenda kuoa ndugu na majirani tukachukua mwali wetu akaja uswazini

shoga mwanamke tena naona akaanza kuona aibu kwamba yeye anafanya kazi ofisini mumewe analinda tena kazi zenyewe za kurudi asubuhi akaona isiwe tabu akamwambia mumewe acha kazi nakufungulia biashara na kila mwezi nitakuwa nakupa laki moja

ukiangalia ndoa ndio kwanza changa jamaa atafanyaje akaamua kweli kuacha na kusubiri mkewe atakapo mfungulia biashara kweli yule dada akamfungulia duka yule kaka la kuuza vitu vya nyumbani mchele,sijui sabuni etc

maisha yakasonga lakini siunajuwa siye wanawake tena ni wachache hata baada ya kugombana ukamuheshimu mume wako ukiangalia wewe ndio unayeshika maisha ya nyumbani

basi jana usiku sijui waligombana nini jamani aibu hii yule dada alitushangaza mtaani pale alimtukana mumewe matusi na kumdharilisha sote tukajua kumbe yeye ndio alimuachisha kazi na anamlipa kila mwezi laki

yule kaka wa watu kama mwanaume akawa anafoka yule dada anamtukuna na akamwambia anafunga na duka lake kweli yule dada akachukua kufuli akafunga duka akaondoka zake akamuacha yule kaka pale kwa aibu watu kibao wamejaa

jamani watu roho ziliwauma...yule kaka akaondoka na kuingia ndani sasa sijui mpaka sasa hivi kama yule dada alirudi nyumbani kwake au vipi bado sijarudi mtaani ila kwa habari zaidi nitawaahadithia nikirudi uswahilini
Ati watu roho ziliwauma! Roho kuuma unakuja kuelekea yasiyokuhusu? Na hao wengine ndio hivyo hivyo wamepata ya kusimulia.
 
winlicious

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
888
1,000
Ni kwa sababu hio sio nature na mwanaume kuhudumiwa. Mwanaume anatakiwa kuwa provider sio tegemezi ndio maana inapotokea mwanaume analelewa inakuwa issue kubwa....
Mwanaume anapopata mwanamke wa kumbeba anatakiwa abebeke japo apigane apate kitu kidogo ila sio kutegemea msaada wa mwanamke siku zote.
Inachosa sana.
Kabisa tena hawana shukrani, ukimwambia huna ananuna na lawama juu
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
11,895
2,000
Mwanaume ukikosa kazi ujue umepatikana.
Wanawake wengi wana roho mbaya huwezi kuamini, yeye akiwa hana kazi utaishi nae na kwao itasaidia kama kawaida, sasa ukose mishe utakiona cha moto, mpaka kwao wanakusimanga

Yaani hawa wee wagegede tuu hawana maana kabisa. Hawajawai kupenda wanaangalia maisha tuu so na wewe angalia papuchi zao tuu... Mwanaume naye bwege kweli toka lini ukamtegemea mwanamke...ujinga mtupu.
 
mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
11,895
2,000
Ni kweli mkuu hio hali ilishanikutaga kipindi flani sina ramani. Hakuna rangi niliacha kuona 🤣🤣🤣 hapo mtoto anaenda job na kurudi muhuni naganga njaa mtaani. Siku akijisikia kukuchamba anakuchamba vizuri tu, sometime nilikuwa namzibua ila nachoshukuru tu hakuwahi kuniletea pigo za usaliti maana nahisi tungeuana mjengoni.

Sishauri mtu aanzishe mahusiano serious na mwanamke ikiwa hana shughuli ya kueleweka mjini. Utateseka sure im telling you. Wanawake wana masimango sana wakiwa na nafasi kiuchumi na wepesi sana kujisahau. Ikiwa yeye hana unamfanyia vyote kama binadamu kwa wema na upendo ila wao sasa ni ngumu sana.

Unaweka ndani mwanamke wa nini bwana... Kamata gegeda tupa kule. Hawana maana hawa ni chombo cha starehe tuu.
 
kedekede

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
4,668
2,000
Ni kwa sababu hio sio nature na mwanaume kuhudumiwa. Mwanaume anatakiwa kuwa provider sio tegemezi ndio maana inapotokea mwanaume analelewa inakuwa issue kubwa....
Mwanaume anapopata mwanamke wa kumbeba anatakiwa abebeke japo apigane apate kitu kidogo ila sio kutegemea msaada wa mwanamke siku zote.
Inachosa sana.
Wanawake mkitoa roho zinauma Sana, Si mume wake, si mnasema mwili mmoja? Au? Si anauza dukani?
 
Emmado

Senior Member
Dec 2, 2010
193
250
Mnatukanana halafu mnarudiana. Mtaa wote wanawaona wajinga. Ni vizuri kama umekosana na mpenzi wako muongee kistaarabu kama itashindikana basi kila mmoja achukue 50 zake. Kama hauna kazi au hela usije ukaoa mwanamke anayekuzidi pesa. Oa wa chini yako. Hawa viumbe siyo

Hapo kwenye nyekundu mkuu!!
Haitekelezeki kwani kuna mwanamke unaoa umemzidi elimu na kipato ila inatokea bahati nzuri au mbaya anaajiriwa katika kampuni binafsi au hizi za kimataifa ghafla anakuzidi mshahara mara 2 au hata 3 ....

je utamwacha uende ukaoe ambaye hajakuzidi kipato?

Mimi nacho amini ni kuwa :- hata mwanamke awe na kipato cha namna gani hawezi kukudharau kama na wewe unakipatoo chako na unafanyia vitu vya msingi na kikubwa kuliko vyote .... JIAMINI, KUWA NAMSIMAMO NA TEKELEZA MAJUKUMU YAKO KAMA MWANAUME..

Mwanamke akishakuwa na kipato anakua anajiamini na unaweza kuona anakiburi ila ni anakujaribu kuona kama unaweza kumwongoza na kumpa maelekezo bila kujali kipato chake.

KIKUBWA KINACHOTUTESA WANAUME WENGI NI KUTOKUJIAMINI( inferiority )

Ila nawashauri wanaume wanzangu swala la kuzidiwa kipato na mwanamke ni jambo lisilo epukika ...kwa dunia ya leo hivyo tusahau mambo ya zamani (it's a new world)
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom