Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

Ben awe jasiri tu badala ya kumuachia Mungu amuhukumu aseme tu wampeleke mbele ya mahakama na huko ndio aweze kujisafisha mbele ya watanzania wote ama sivyo atakufa kihoro!!

Au akiri na kutuomba radhi watanzania kuwa alikosea kutoa nafasi kwa Mramba na Mpenzi wake Anna kumtawala hadi kufikia hatua ya kumpiga na Situli. Hapo tutamwelewa na kumsamehe.
 
Kama aliiba hakumuibia Mungu alituibia watanzania come on! ajibu hoja aache kuchomeka udaku kwenye hoja za msingi. Nadhani Mungu ana nafasi ya kumuhukumu siku atayokufa lakini kwa leo atujibu!
Kwa wale wasio amini kuna Mungu je anawatendea haki?

NANYI MTAIJUA HIYO KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU
 
Mkapa%285%29.jpg

Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

Rais mstaafu Benjamin Mkapa, amesema yote yanayosemwa juu yake, anamwachia Mungu.

Watanzania wanadai kwanza sheria zifanye kazi alafu, ndio uanze ibada zako. Eti kungekuweko kwa Mungu leo hii we ungekua somewhere in Lupango.

Unfortunately he hasnt proven his existence leo hii unapeta na kujitetea kwa jina lake.
 
Kama kawaida, the clowning continues.Na huyu mungu anasingiziwa upuuzi wote kama kawaida, hakika angeweza kujitetea angesema masikini.

Mkapa chapombe kaidi leo mpaka kamjua mungu?

Kama kawaida, the mungu fabrication is used politically. Mkapa the proud, with his back to the wall, is trying to look humble and god fearing.

Tatizo ni kwamba hata anapojidai kuwa humble bado ugangwe wake unajionyesha pale aliposusa kusoma hotuba.

Huyu mtu si corrupt tu, ana matatizo ya kisaikolojia pia.
 
Watanzania wanadai kwanza sheria zifanye kazi alafu, ndio uanze ibada zako. Eti kungekuweko kwa Mungu leo hii we ungekua somewhere in Lupango.

Unfortunately he hasnt proven his existence leo hii unapeta na kujitetea kwa jina lake.

Very well put.
 
Duh! Mkuu I can tell you are a CCM supporter. I am also a fan of CCM although the party has irritated me after all the current scandals. Lakini ushabiki pembeni wewe una fikiri kweli uwanja wa mpira ni big deal? Kwa hiyo mtu awe raisi miaka kumi kwako utaona uraisi wake ulikuwa na mafanikio kwa uwanja mmoja wa mpira? You can't be serious mkuu na sidhani uwanja wa mpira una justify ujinga mwingine ulio fanyika chini ya uongozi wake.

You are right, sijui kama kweli uwanja wa mpira ni maendeleo, sawa Kibunango anaweza kuwa right, lakini je umewezesha wangapi kwenye huo uwanja wa mpira na nchi ina watu wangapi, kwanini kwanza usiwezeshe miundo mbinu ambayo kila mtanzania wa hali ya chini anahitaji kama afya, maji, barabara, shule, na tunapoongelea shule hatuongelei majengo au kata ina shule ngapi tunaongelea elimu yenye ubora na tija, and then mtu ndo aanze kuangalia kama je tunahitaji viwanja vya mpira? na kama tunahitaji tunataka kufanya navo nini, sio tu kuwa na viwanja vizuri halafu mpira hata hamjui, mna constructive ideas zipi za kuendeleza fani, and then mnaamua ok let start building up fantansy and good looking stadiums. Au sio kibunango, huu sio muda wa kukurupuka na kujenga tu vitu, you must have had a program and constructive ones.
Ok pamoja na kuwa sio fan wa CCM Mkapa kuna vitu vizurri alivifanya, lakini haimaanishi basi kama alikuwa mwizi basi aachiwe, kwani mtu akifanya dhambi basi siku nyingine akifanya kitu kizuri Mungu anamfutia dhambi aliyofanya jana yake, kama ni hivo basi hakuna mwenye dhambi duniani, we are all clean.

Rom
 
Na hilo ndio suala la msingi jinsi ninavyoona. Aseme ukweli kiungwana mambo yaishe.Tena kwa kufanya hivyo tunaweza kuwa na mwanzo mpya maana sasa hivi tumesahau agenda za maendelea tumezama kuhakikisha yale wanayoyafukia kwa lazima bila ustaarabu yanaendelea kuonekana bado yako vile vile.
Wote tunakosea. Na hawa wazee wengi ambao leo wamejikuta katika kashfa hizi na zile pia na wao waamue kuwa wanyenyekevu na kukubali makosa ya kiutendaji yaliyotokea ili tuanze upya.
Tatizo ni ego zao bwana.Wanajiamini kweli hata kama wanaonekana vituko kila wanakopita.
Na watanzania tusisahau pia kama anavyosema Lole kuwa yapo mengi mazuri mtu kama BWM ameyafanya. Dawa sio kulia chini chini. Ajivike ujasiri wa kusema sorry
Mara ngapi? Au ni kwa vile aliliomba taifa msamaha kwa maneno mazito sana kuhusiana na pale alipoteleza katika kipindi chake cha uongozi wa nchi. Mapema January 2006 alirudia tena kanisani Saint Joseph siku alipoomba misa ya kumshukuru Mungu kwa kumvusha salama katika madaraka aliyokuwa nayo.

Nakupa sehemu ambazo utapata ujumbe mzito kwa WaTZ toka kwa Rais, Nenda kwenye hotuba yake Mwisho akiwa mkuu wa nchi hii alipokuwa anaaga na kututakia kila heri katika awamu ya nne, waliomsikiliza Mkapa siku wanajua haya lakini sasa ni kama wanapata kuuona ukweli wa yote.

Tatizo ninaloliona ni timing yake imeendelea kuwasumbua watu wengi humu jamvini, media na baadhi ya wakuru. Wao walipenda wa break news then aombe msamaha nafasi ambayo Mkapa hakuwapatia hata sekunde, baada ya hapo tukaanza kuwasikia akina lowasa wakisema tatizo la umeme ni la awamu ya tatu na siyo wao walioleta mgao, mara Mengi yuko katika misafara ya JK na JK akimsifia kuwa ni mtu wa kupigiwa mfano ghafla KULIKONI, This Day na kadharika, Kubenea ..........mara wahindi online mara Kiwira na mengineyo.

Mara Butiku naye yumo........

Yeye ameishi maisha yake ya Kidunia vya kutosha kwahiyo siyo ajabu sasa kujiangalia mbele ya Mungu zaidi hususani unapopata fursa hiyo.

Kama hamumpeleki Mahakamani mnataka ajipeleke katika zama ambazo yeye keshazipita ? Kama kuna tuhuma ziende mahakamani, hao watamrejesha katika udunia ili ajibizane kidunia zaidi.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Watanzania rais tunaemtaka yupo dunia hii?, na je anaweza tokea?

Eda Sanga alimuuliza Nyerere swali hili, baada ya Nyerere kutoa criteria zake za rais.Nyerere akasema, kusema mtu mwenye sifa hizi hayupo katika nchi kubwa kama Tanzania ni kama kuwatukana watanzania.Kwa maana ya kwamba katika watu wote hatuwezi kukosa mtu mmoja mwenye sifa.

Nakubaliana na Nyerere katika hili. Lakini tumeona choice yake na ilipotupeleka, kama huyu Mkapa ndiye idea yake ya mtu anayefaa then swali la Eda Sanga liko relevant bado.

Tatizo linakuja, ili uwe mgombea wa urais ni lazima upitie machinery za vyama vya siasa.Hususan CCM. Machinery ya CCM inahakikisha kwamba itawachuja na kuwaacha wale wote wenye sifa na kuchukua mafisadi wenye kujua connections na kutafuta campaign money.

Kwa hiyo, at the end of the day Socrates prevails, wenye sifa na uwezo wa kuongoza hawaongozi, instead wenye visa na uozo ndio wanaongoza.

Ndiyo maana hili swali la Eda Sanga linakuwa muhimu, na linajirudia rudia.Si kwa sababu Tanzania wenye sifa hawako, bali hawawezi kuvuka hata ngazi ya kijiji huko. Huku mafisadi papa yanajitia ucha mungu feki.
 
Kama hamumpeleki Mahakamani mnataka ajipeleke katika zama ambazo yeye keshazipita ? Kama kuna tuhuma ziende mahakamani, hao watamrejesha katika udunia ili ajibizane kidunia zaidi.
Mungu Ibariki Tanzania

kaka mimi nafikiri katiba ya Tanzania unaijua na umewahi kuisoma, Mkapa mpaka sasa ana kinga na hawezi kushitakiwa mpaka hapo kinga yake itakapoenguliwa kama kutakuwa na any constitutional amendment, na ndo maana akina Dr. Slaa waliliomba Bunge la jamhuri limtolee kinga bwana Ben ili aweze kushitakiwa, sasa kutokana na tabia ya kulindana kuwa je yakinifika mimi itakuwaje ndo maana mpaka sasa Ben yupo mtaani, lakini angekuwa nchi zingine sasa ingekuwa Historia kuwa alikuwepo Bwana Ben na sasa yupo Lupango, kaka tuombe haya mambo yasibadilike wakati bado wapo, lakini ikitokea hayo mambo yakatolewa am telling you Ben na huyu predeccessor wake tutakuja kuwashitaki tu, labda wawe wamekufa.

Rom
 
Hakumjua Mungu alipokuwa anafanya biashara akiwa Ikulu kwa siri na kujilimbikizia mali kwa uroho aliokuwa nao, kusaini mikataba ya kuchimba madini isiyokuwa na maslahi, kukopa bilioni 7 toka NSSF ambazo hadi leo hajarudisha hata senti tano na baadaye kuamua kutuibia Kiwira eti sasa ndiyo anajidai kumjua Mungu! Fisadi mkubwa Wee!
 
Kama hamumpeleki Mahakamani mnataka ajipeleke katika zama ambazo yeye keshazipita ? Kama kuna tuhuma ziende mahakamani

FDR Jr....komredi umesahau tuna political tolerance! Hii ni sifa tunayoigwa na kusifiwa na wanasiasa wachanga!
 
kaka mimi nafikiri katiba ya Tanzania unaijua na umewahi kuisoma, Mkapa mpaka sasa ana kinga na hawezi kushitakiwa mpaka hapo kinga yake itakapoenguliwa kama kutakuwa na any constitutional amendment, na ndo maana akina Dr. Slaa waliliomba Bunge la jamhuri limtolee kinga bwana Ben ili aweze kushitakiwa, sasa kutokana na tabia ya kulindana kuwa je yakinifika mimi itakuwaje ndo maana mpaka sasa Ben yupo mtaani, lakini angekuwa nchi zingine sasa ingekuwa Historia kuwa alikuwepo Bwana Ben na sasa yupo Lupango, kaka tuombe haya mambo yasibadilike wakati bado wapo, lakini ikitokea hayo mambo yakatolewa am telling you Ben na huyu predeccessor wake tutakuja kuwashitaki tu, labda wawe wamekufa.

Rom
Sasa kama hata katiba yenyewe hatuiwezi yanini makelele haya?????

Let us vote for Christopher wa Tanu aah kumbe ni Dp!!!
 
Duh! Mkuu I can tell you are a CCM supporter. I am also a fan of CCM although the party has irritated me after all the current scandals. Lakini ushabiki pembeni wewe una fikiri kweli uwanja wa mpira ni big deal? Kwa hiyo mtu awe raisi miaka kumi kwako utaona uraisi wake ulikuwa na mafanikio kwa uwanja mmoja wa mpira? You can't be serious mkuu na sidhani uwanja wa mpira una justify ujinga mwingine ulio fanyika chini ya uongozi wake.

Pamoja na mabaya yote aliyofanya Mheshimiwa Mkapa kuna mazuri yake pia. Alikuwa rais wa pekee Tanzania kujenga barabara kwa kodi za watanzania, alilipa madeni ya nje ambayo nchi ilikuwa inadaiwa, alihakikisha uchumi wa nchi unakuwa na inflation inabaki a single digit. Uwanja wa mpira pia ni kipimo kizuri wamepita viongozi hapo kabla lakini uwanja wa mpira wa kisasa haukujengwa.
 
Mkapa kaiweka Tanzania kwenye ramani, alijua anafanya nini na kauli zake zilikuwa na mantiki siyo ubabaishaji. Ukisema Mkapa aliiba na hii inayotokea sasa hivi utasemaje?

Tujifunze kushukuru kwa madogo aliyofanya, siyo mwehu kwamba hakufanya chochote. Watanzania nyie vipi???

Kauli nyingine siyo jamani learn how to argue.
 
Ila katika kipindi chake Tanzania imebadilika kiuchumi...HILO HALINA UBISHI.Uchumi na science pamoja na technology vimekua.

hamna lolote hivi mmewahi kuangalia hizo economic data za wakati wa Mkapa na mtuambie zilibadilika vipi?
 
Mara ngapi? Au ni kwa vile aliliomba taifa msamaha kwa maneno mazito sana kuhusiana na pale alipoteleza katika kipindi chake cha uongozi wa nchi. Mapema January 2006 alirudia tena kanisani Saint Joseph siku alipoomba misa ya kumshukuru Mungu kwa kumvusha salama katika madaraka aliyokuwa nayo.

Nakupa sehemu ambazo utapata ujumbe mzito kwa WaTZ toka kwa Rais, Nenda kwenye hotuba yake Mwisho akiwa mkuu wa nchi hii alipokuwa anaaga na kututakia kila heri katika awamu ya nne, waliomsikiliza Mkapa siku wanajua haya lakini sasa ni kama wanapata kuuona ukweli wa yote.

Tatizo ninaloliona ni timing yake imeendelea kuwasumbua watu wengi humu jamvini, media na baadhi ya wakuru. Wao walipenda wa break news then aombe msamaha nafasi ambayo Mkapa hakuwapatia hata sekunde, baada ya hapo tukaanza kuwasikia akina lowasa wakisema tatizo la umeme ni la awamu ya tatu na siyo wao walioleta mgao, mara Mengi yuko katika misafara ya JK na JK akimsifia kuwa ni mtu wa kupigiwa mfano ghafla KULIKONI, This Day na kadharika, Kubenea ..........mara wahindi online mara Kiwira na mengineyo.

Mara Butiku naye yumo........

Yeye ameishi maisha yake ya Kidunia vya kutosha kwahiyo siyo ajabu sasa kujiangalia mbele ya Mungu zaidi hususani unapopata fursa hiyo.

Kama hamumpeleki Mahakamani mnataka ajipeleke katika zama ambazo yeye keshazipita ? Kama kuna tuhuma ziende mahakamani, hao watamrejesha katika udunia ili ajibizane kidunia zaidi.
Mungu Ibariki Tanzania
Mhh, Sidhani kama issue ni kutaka kupata breaking news. Huyu jamaa watu wana vitu specific wanavyoona inastahili kupata maelezo yake na sio maswala ya jumla jumla kama unavyodai alifanya.
Kuna mtu hapa amesema huyu jamaa ni kaidi na mkorofi.Yes! inawezekana akawa egotist pia kwasababu ya kudharau mambo anayoyaona hayaendi vile anavyotegemea kwake.
Kama alishaomba radhi watanzania basi aendelee kukaa kimya watanzania wataamua wenyewe lini wakae kimya maana nahisi hawajaipata vizuri hiyo omba msamaha yake.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, pamoja na kuibuliwa kwa uchafu wakati wa utawala wake ukweli unabaki pale pale mengi mazuri.

Wakati anaondoka madarakani bundle moja ya bati tulinunua 87,000/= lakini ilipofioka January 2008 ilishafika 280,000/=, nauli za daladala zilisimama kwa miaka yake yote ya utawala katika 100/=; haya ndiyo mambo sisi watu wa kawaida tunayoyaangalia;

Wakati wa Mkapa tulikuwa tuki budget, leo hii haiwezekani, tumebaki kuishi kwa matumaini tu.

Sio sahihi kabisa kumbeza mzee huyu kwamba hajafanya kitu, hapana amefanya makubwa kuliko hayo mabaya.

Kwanza mikataba ya madini ilianzia kwake, tuwe wakweli, IPTL nani alikuwa waziri wa madini na nishati na nani alikuwa rais!!!!

Mwacheni mzee wa watu apumzike.
 
Na serikali yake ilikua inafanya kazi, leo hii me hata ukinitajia baadhi ya mawaziri cwajui wanashika wizara gani kwani hata hawasikiki.....na ukitaka kujua hii awamu ilikua inamfanyia mchezo mchafu, sasa hivi wamegeukiana wenyewe kwa wenyewe basi wanatupa kero nchini kwelikweli. Mambo hayaendi na uchumi unazidi kushuka. Me huwa naangalia hali ya watanzania zaidi kuliko kuletewa data za IMF na WTO.
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, pamoja na kuibuliwa kwa uchafu wakati wa utawala wake ukweli unabaki pale pale mengi mazuri.

Wakati anaondoka madarakani bundle moja ya bati tulinunua 87,000/= lakini ilipofioka January 2008 ilishafika 280,000/=, nauli za daladala zilisimama kwa miaka yake yote ya utawala katika 100/=; haya ndiyo mambo sisi watu wa kawaida tunayoyaangalia;

Wakati wa Mkapa tulikuwa tuki budget, leo hii haiwezekani, tumebaki kuishi kwa matumaini tu.

Sio sahihi kabisa kumbeza mzee huyu kwamba hajafanya kitu, hapana amefanya makubwa kuliko hayo mabaya.

Kwanza mikataba ya madini ilianzia kwake, tuwe wakweli, IPTL nani alikuwa waziri wa madini na nishati na nani alikuwa rais!!!!

Mwacheni mzee wa watu apumzike.
Nakubaliana na wewe kabisa, ndo maana me sifwatilii data za TO na IMF, huwa naangalia real situation ya wa Tanzania. leo mfuko wa cement unalipa kiasi gani na wakati ule unalipa kiasi gani?, bei ya vyakula je?vipi tiba mahospitalini?.Ukiangalia hivyo vitu wiyhin four years vimepanda zaidi ya asilimia 200, tafteni nchi gani ukiondoa Zimbabwe kuna hali ya inflation kubwa kama kwetu, ukiona hivyo ujue kuna tatizo katika serikali hii. Mzee Ben alijitahidi....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom