Mkapa: Yote yanayosemwa juu yangu namuachia Mungu

Kama hatuko tayari kumpeleka mheshimiwa BWM mahakamani ili ukweli wa tuhuma uthibitishwe na hatua stahili zichukuliwe, basi tumuache apumzike kwa amani.

Hizi tabia za watu wazima kupoteza mda kusengenya wengine (hata kama ni kwa maslahi binafsi) ni kiashiria cha taifa la watu wenye mdumao wa akili.
 
kuna mazuri mkapa kafanya, makosa ni sehemuya uongozi.

Hebu niambien huyu tulie nae nini cha maana kinaonekana amefanya?!
Hata yeye akitoka mtaponda tu. Wengine humu hata mambo ya familia zenu yanawashinda kazi kunyooshea vidole wengine.
Hata msemeje mkapa ndo kafanya mengi mazuri na nchi imepata heshima.

Kimya!!!
tatizo ni aliyemrithi anayetuhumiwa ku join hand na mengi kupitia magazeti yao kumdharirisha na kuipa kisogo legacy yake kwa kila linalowezekana na kusifia kila jambo la awamu hii as if bwm alikuwa angel michael /gabriel na akiwaongoza wale saints waliodondoshwa tanzania!!!!!!!

All in all, he did what alichoweza kama presidaa ktk term yake, kuyakubali na kupokea madhaifu yote kama mkuu wa nchi wa awamu husika.

Binafsi ninamshukuru kwa msimamo wake wa dhati kwa umma na mungu wake.
 
atoke hapa! Angefanya kazi yake mambo mengine wala yasingefika hapa. Anataka tumsifie kwa uwanja wa mpira?

Kwani dogo hilo?

Duh! Mkuu I can tell you are a CCM supporter. I am also a fan of CCM although the party has irritated me after all the current scandals. Lakini ushabiki pembeni wewe una fikiri kweli uwanja wa mpira ni big deal? Kwa hiyo mtu awe raisi miaka kumi kwako utaona uraisi wake ulikuwa na mafanikio kwa uwanja mmoja wa mpira? You can't be serious mkuu na sidhani uwanja wa mpira una justify ujinga mwingine ulio fanyika chini ya uongozi wake.
MF
Soma kejeli ya Mwanakijiji kwanza...
 
Kama isingekuwa tamaa (bila shaka kutokana na kuwa na washauri wabovu), huyu jamaa alifanya mambo mazuri mengi kwa maendeleo ya nchi. Mpaka sasa sielewi kwa nini alikubali kununuliwa na makaburu walioitwaa NBC yetu. Sijui ilikuwaje pia akapata kichaa cha kutumia vibaya madaraka yake na kununua Kiwira. Ukiondoa dosari hizo na kiburi chake cha Kimachinga, alifanya vizuri.

Ni tamaa yake na siyo kushauriwa vibaya- alipouza NBC alijenga/alijengewa hotel kubwa south africa (Huko si kushauriwa bali ni tamaa), kumbuka wakati huo Nyerere alikuwa hai lakini hakumsikiliza!
Kujiuzia Kiwira ni ukichaa, nakubaliana nawe, ila kukomesha ukichaa huu kwake, kwa waliopo na kwa wajao, dawa si kumuachia Mungu - ni kuwafikisha mahakamani.

Hata kupanda kwa uchumi lazima tukuangalie kwa makini. Uchumi ulipanda kwa kuuza raslimali tulizokuwa nazo? Tuliuza lakini uzalishaji haukuendelea kufanyika ndani, na hata huo kidogo ulioendelea kwenye madini ni wizi mtupu - je uchumi ulipandaje? Hata Mkapa mwenyewe anakiri hivyo

"Ex-president of Tanzania Benjamin Mkapa nicely summed up his experience and that of many other countries: “We privatized everything the state had. Everything was bought by foreign capital because we had no national capital to compete. The foreign companies almost always closed local businesses, which were not competitive, transforming them into distributors of foreign products and driving up unemployment. The experts of the World Bank and the IMF predicted that this would happen, but they told us: Now the influx of foreign investment will lead to the creation of new, competitive and technologically current businesses that will provide the foundations for a lasting, modern development. None of this happened for us.”

Written by Roberto Savio / Inter Press Service
Wednesday, 19 August 2009 21:16

Chukulia mfano mdogo - wewe una shamba lakini unakosa hela ya matumizi, unaamua kumuuzia mtu hilo shamba anakupa hela halafu unajidai sasa hali yako ni nzuri kwa kuwa unazo hela za kutumia? Mpumbavu wewe hela hizo zitakapoisha unakuwa maskini zaidi ya hapo mwanzo kwa kuwa hata shamba sasa huna. Utabaki kumuomba huyo uliyemuuzia akuajiri katika shamba hilo hilo - akikataa akaamua kuleta ndugu zake wewe si utakuwa umekwisha kabisa?
Haya ndiyo yaliyotokea TZ na yanaendelea kutokea - hata wafagiaji wanaletwa na wawekezaji!

Mkapa kuna mazuri alifanya; ni wazi huwezi kuongoza miaka kumi na usifanye hata moja zuri, ila wadanganyika tunapaswa kujua kuwa rais anapaswa kufanya mazuri tu na kwa mazuri hayo tunamlipa mshahara mzuri na maslahi mazuri anapostaafu hadi kufa kwake; hapaswi kuwa na tamaa kwani maisha yake yako-guaranteed hadi kifo na kuzikwa!
Kama kwa mazuri tunamlipa je kwa mabaya tena ya maksudi, tumfanyeje? Tumwachie Mungu tu? HAPANA, Hata wana dini wanasema "Mungu nisaidie huku nawe ukiweka nguvu zako"; nguvu zetu ni kumpeleka mahakamani, huko ndiko atatueleza vizuri 'wivu tuliokuwa nao wa kijinga'
 
- kumbe anamjua mungu? Makubwa haya.

fmes!
rejea siku aliporejea saint joseph cathedral aliposoma misa yake ya shukrani kwa mungu mkuu.

Ukiipata hiyo maneno haya ya kejeli usingaliyatamka maana hata muumba hapendezwi nayo daima.
 
Ana mengi ya kusifiwa si uwanja wa mpira tuuu...

Makosa pia kiuongozi anayoo ila mfumo huchochea kwa kiasi kikubwa kuyafanyaa..Anayakubali makosa ila ajadiliwe kwa haki pia.

Ulikuwa ni uongozi wa pamoja ambao mafanikio ya awamu yake yametumika sana kuhalalisha awamu iliyopooo...

Kumjadili Mkapa bado hakuisadiii jamii zaidi ya kunufaisha waliopo kuendeleaa kuwepo madarakani..Hata kampeni za kumchafua ni mikakati kwa masilahi binafsi.

angetakiwa kujibu hoja/tuhuma na sio kutoa blanket excuse
 
Hata aliyemweka madarakani (Mwl Nyerere), Aliwahi kutuhuniwa na akina Kambona kuwa ana kiwanda cha magari India, sina kumbukumbu ila nafikiri yale yalisuluhishwa mahakamani!
Sasa kama raisi mstaafu hawezi kushtakiwa, hawezi kushtaki pia???
Awapeleke akina Dr Slaa Mahakamani, Atapata fidia kubwa ya kupanua hiyo taasisa yake!!
Kwa sasa naamini hatapata wafadhili, kwa sababu ameshsonekana ni mwizi/mlafi!
 
enheeeeee...NIMEFURAHI KUSIKIA MZEE BEN UNAMWACHIA MUNGU YOOOOOTE YANAYOSEMWA JUU YAKO...fine and very good...NI KITENDO CHA KIUNGWANA WA ROHO KUMKABIDHI MUNGU KILA JAMBO LITOKEALO MBELE YAKO....sasa mkuu ben huoni kama ni BUSARA SANA ukatuomba radhi na msamaha wa kweli watanzania wote kwa yale mabaya machache tunayolalamika kuwa ulitukosea ili sadaka yako IKUBALIKE MBELE ZA BWANA...(hata andiko linasema kuwa kabla ya kutoa sadaka kwa bwana fanya patano na wote uliowakosea)....

Hii janja ya kumwachia mungu kitu ambacho hujakitolea utetezi ni uhuni mheshimiwa wetu....UNATAKIWA UJIBU TUHUMA HIZO ILI WATU WAJUE UN ASIMAMA KATIKA HAKI IPI...(hata yesu kimsingi alijibu tuhuma zake kabla ya kusulibiwa mbele ya pilato)...kwahiyo mkuu tunaomba ujibu tuhuma unazokabiliwa nazo kisha Majibu yako tuyakabidhi kwa MUNGU ajuaye haki kati yetu watanzania na wewe mkuu kiongozi wetu wa zamani.....USIWE MWOGA MHESHIMIWA SIKU ZOTE MUNGU HAWATUPI WATU WAKE...KAMA NAWE NI M1 WAO HAKI ZAKO MUNGU ATAZISIMAMIA
 
Mkapa alipoupata urais alisahau kwamba cheo ni dhamana ambayo amepewa na wananchi na alipaswa kuwatumikia na kuwaheshimu. Lakini, alijisahau akaona kwamba ni Rais kwa hiyo yuko juu ya kila mtu na kila kitu. Akajaa kiburi na mbwembwe. Twakumbuka ambavyo aliwahi kusema Watanzania ni wavivu kufikiri (shujaa wa kufikiri alikuwa ni yeye tu!)

Tukumbuke pia kwamba alifika mahali akawa anambeza hata yule aliyembeba mgongoni akamtembeza nchi nzima kumnadi hadi akaupata huo urais - Mwalimu Nyerere. Mkapa kwa hulka yake ya kujiona kwamba kwa kuwa ni Rais basi anajua sana kuliko mtu mwingine na hapaswi kuingiliwa, huenda Mwalimu alipokuwa akimshauri kuhusu mambo mbali mbali na hasa lile la kuuza/kubinafsisha NBC; huko pembeni alikuwa akilalama: "Mzee huyu naye...."

Na fedha za Kagoda je? Ni yeye aliyeidhinisha watu wachote mahela ya EPA kwa ajili ya uchaguzi wa CCM. Wapo wanaosema kwamba alifanya hivyo akiwa na mtu wake aliyemtaka awe Rais lakini Kikwete akamzidi maarifa. Halikadhalika, si ni yeye aliyepindisha utaratibu wa mchakato wa kupata mgombea urais pale Dodoma kwa shinikizo la wana Mtandao? Na ya Kiwira je, kwa kuwa Pinda amemsaidia kwa hiyo sasa ndo ameona anaweza kuanza kusema?

Kafanya mengi ndio, lakini hayo mengi aliyoyafanya kama yalikuwa ni kwa manufaa ya taifa ni wazi alikuwa anatimiza wajibu wake kama Rais hakuwa anawafanyia wananchi hisani!

Sasa asitafute sympathy. Kwa nini hawezi akakiri makosa na kuwaomba radhi wananchi kwa yale aliyoyakosea wakati wa uongozi wake? Asimtumbukize Mungu kwenye hayo. Anachohitaji kufanya ni kuwaomba wananchi wamsamehe kwa makosa aliyoyatenda akiwa Ikulu. Wananchi wakimsamehe hapo ndipo Mungu naye atamsamehe.
 
Jamani wakuu kuna useme wa wahenga unasema myonge mnyogeni lakini haki yake mpeni,Mh.Rais wa awamu ya tatu amefanya mengi mazuri na ya kuleta tija na maemdeleo kwa wanachi na taifa letu la tanzania kwa ujumla.

Tabia ya sisi viumbe binandamu tunaangalia sana upande mmoja wa maisha ya mwanandamu hasa upande mbaya,na ubaya unaenea haraka kuliko wema hii ndiyo hulka ya wanadamu tangu enzi hizo.

mimi binafsi pamoja na mambo yote yanayoemwa kuhsu rais mstaafu wa awamu ya tatu bado nakubali utendaji kazi wake uliyotukuka kwa maslahi ya nchi yetu changa ya Tanzania

labda watakuelewa kaka
 
Du shemeji tena? Mkuu Ben na admire sana kazi aliyofanya Ben. No doubt ni kiongozi bora aliyewahi kutokea kwenye "modern" Tanzania. Kuna kila evidence ya kufanya vizuri kwenye karibu kila litu alichofanya wakati wa urais wake, lakini hii haina maana tukae kimya kwa kitendo chake cha kututosa kwenye mdomo wa Simba, am sure alikuwa anajua wazi kabisa kuwa nchi inachukuliwa na kina nani na inakwenda kwa kina nani, hakuonesha effort yoyote ya kutusaidia.

Even worse alitudanganya kuwa atahakikisha kuwa tunapata rais mzuri, look at what he has done to us.

Kwangu mimi Ben Alifanya makosa mawili ya msingi wakati wa urais wake, mosi ni kule kuamini sana urafiki wake na Balozi Ruhinda ambaye ndiye aliyemfanya Rostam Akawa karibu na urais wake and hence the EPA scandal na pili; Kubadilisha kanuni za chama single handedly wakati wa uchaguzi wa mgombea URAIS and hence kumpata Rais wa sasa; bila ya kubadili zile kanuni Kikwete asingepata urais na balaa na aibu tunayoipata sasa isingekuwepo!! Mimi nadhani Ben awe jasiri tu badala ya kumuachia Mungu amuhukumu aseme tu wampeleke mbele ya mahakama na huko ndio aweze kujisafisha mbele ya watanzania wote ama sivyo atakufa kihoro!!
 
Ana mengi ya kusifiwa si uwanja wa mpira tuuu...

Makosa pia kiuongozi anayoo ila mfumo huchochea kwa kiasi kikubwa kuyafanyaa..Anayakubali makosa ila ajadiliwe kwa haki pia.

Ulikuwa ni uongozi wa pamoja ambao mafanikio ya awamu yake yametumika sana kuhalalisha awamu iliyopooo...

Kumjadili Mkapa bado hakuisadiii jamii zaidi ya kunufaisha waliopo kuendeleaa kuwepo madarakani..Hata kampeni za kumchafua ni mikakati kwa masilahi binafsi.

Jamani Mkapa leo ni mnyonge, myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Mkapa pamoja na kufanya makosa mengi ambayo inaelekea "alijisahau", kuna mengi vilevile aliyafanya mazuri kabisa.

Kosa kubwa la Mkapa ni kuingia tamaa,watu wanaomfahafu vizuri wanashindwa kueleza ibilisi huyu katoka wapi, maana Benjamin hakuwa na unyonge huo.

Kati ya makubwa yaliyofanyika na yatendelea kuliendeleza Taifa hili ni Restructuring ya Ukusanyaji kodi na kuanzisha TRA.Tusisahau kuwa Idara ya Kodi na Mapato wakati huo ilikuwa inakusanya around 15-25bil kwa mwezi.TRA ilipoingia ikaanza kukusanya over 150bil hadi 200bil.Haya si mambo madogo.Kabla ya mabadiliko haya wafanyakazi serikalini walikuwa wanyonge kwa mishahara midogo leo suti na mashangingi kila kona.

Vile vile mafanikio makubwa ya Mkapa ni kule kuRestructure Idara ya ujenzi wa Barabara na kuanzisha TANROADS.Miaka ya kabla ya hapo ilikuwa haingii akilini hata kwa viongozi wakuu kuwa ujenzi wa barabara ni lazima ufanywe na makampuni ya nje na kwa hela za nje.

Leo kwa hela zetu ni kawaida naimeingia akilini kuwa tunaweza kujenga barabara zetu kwa HELA ZETU WENYEWE. Haya ni mabadiliko makubwa katika fikra za watanzania na kiutendaji.

Pamoja na mafanikio haya namhurumia sana Mzee Mkapa maana katika awamu yake kukaingia CONSPICUOUS MORAL DECAY AND CONSUMPTION katika uendeshaji wa Serikali na hata Chama.

Sasa hivi si wakati wa kulia lia, Watanzania ni waelewa na wengi wanahuruma.Kuomba radhi wananchi bado liko katika uwezo wa Mkapa.

Akifanya hivyo pengine atarudisha heshima yake na kusaidia kuendeleza yale mazuri mengi aliyoyajenga.
 
Mkapa should know better. Yeye alimsoma Shakespear ambaye alisema “ The good things men do get interred with their bones once they die but the bad ones live long after them”. Yaani ukifa unazikwa na mazuri uliyofanya hapa duniani lakini mabaya uliyoyafanya hukumbukwa muda mrefu baada ya kifo chako.
 
Alisema lakini yeye (Mkapa) katika siku za karibuni, hajawahi kusemwa kwa mazuri wala kusifiwa lakini yote anamwachia Mungu.
Nimekuja kugundua kila mtu ana maana tofauti anavyo refer Neno Mungu. Kwa wengine ni yule mungu wanayemsujudia makanisani na misikitini, wengine ni vitu kama mawe, miti etc na wengine ni yule wanayemuita supreme being ambaye kwao suala kubwa ni kujenga eternal mansion on high(Climbing the pyramid).

Sasa BWM anatushakia kwa mungu gani maana kuna mkanganyiko mkubwa hapo?

Ukweli ni kuwa kuna mema aliyoyafanya. Ila akumbuke aliwaongoza binadamu ambao wanapata wakati mgumu kumuamini pale tuhuma nzito zinapoelekezwa kwake halafu yeye ameamua kukaa kimya tu as if hazimuhusu.

Hapo sasa ndio panaleta matatizo maana inakuwa ngumu kujua nini ilikuwa nia yake. Nafikiri ilitakiwa awe jasiri kutuelimisha bila kudanganya au kuficha ukweli yale yote anayotuhumiwa nayo ilikuwaje kuwaje yanaelekezwa kwake. Kwa ujasiri huo atatuondoa mashaka.

Vinginevyo kama inakuwa ngumu kutuambia watu tuliompa dhamana ya kuongoza,basi hakuna namna ya kumsaidia. Aendelee tu kumlilia Mungu wake.
 
In otherwords he is saying ...''Guys leave me alone for God knows what I did and so you have no right to judge me'' Shabbash!!!!!!!!!
 
Kumjadili Mkapa bado hakuisadiii jamii zaidi ya kunufaisha waliopo kuendeleaa kuwepo madarakani..Hata kampeni za kumchafua ni mikakati kwa masilahi binafsi.

Aaaah wapi. Hana jipya zaidi ya kujenga misingi imara ya ufisadi
 
Jamani Mkapa leo ni mnyonge, myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Mkapa pamoja na kufanya makosa mengi ambayo inaelekea "alijisahau", kuna mengi vilevile aliyafanya mazuri kabisa.

Kosa kubwa la Mkapa ni kuingia tamaa,watu wanaomfahafu vizuri wanashindwa kueleza ibilisi huyu katoka wapi, maana Benjamin hakuwa na unyonge huo.
Kati ya makubwa yaliyofanyika na yatendelea kuliendeleza Taifa hili ni Restructuring ya Ukusanyaji kodi na kuanzisha TRA.Tusisahau kuwa Idara ya Kodi na Mapato wakati huo ilikuwa inakusanya around 15-25bil kwa mwezi.TRA ilipoingia ikaanza kukusanya over 150bil hadi 200bil.Haya si mambo madogo.Kabla ya mabadiliko haya wafanyakazi serikalini walikuwa wanyonge kwa mishahara midogo leo suti na mashangingi kila kona.

Vile vile mafanikio makubwa ya Mkapa ni kule kuRestructure Idara ya ujenzi wa Barabara na kuanzisha TANROADS.Miaka ya kabla ya hapo ilikuwa haingii akilini hata kwa viongozi wakuu kuwa ujenzi wa barabara ni lazima ufanywe na makampuni ya nje na kwa hela za nje.
Leo kwa hela zetu ni kawaida naimeingia akilini kuwa tunaweza kujenga barabara zetu kwa HELA ZETU WENYEWE. Haya ni mabadiliko makubwa katika fikra za watanzania na kiutendaji.

Pamoja na mafanikio haya namhurumia sana Mzee Mkapa maana katika awamu yake kukaingia CONSPICUOUS MORAL DECAY AND CONSUMPTION katika uendeshaji wa Serikali na hata Chama.

Sasa hivi si wakati wa kulia lia, Watanzania ni waelewa na wengi wanahuruma.Kuomba radhi wananchi bado liko katika uwezo wa Mkapa. Akifanya hivyo pengine atarudisha heshima yake na kusaidia kuendeleza yale mazuri mengi aliyoyajenga.
Na hilo ndio suala la msingi jinsi ninavyoona. Aseme ukweli kiungwana mambo yaishe.Tena kwa kufanya hivyo tunaweza kuwa na mwanzo mpya maana sasa hivi tumesahau agenda za maendelea tumezama kuhakikisha yale wanayoyafukia kwa lazima bila ustaarabu yanaendelea kuonekana bado yako vile vile.
Wote tunakosea. Na hawa wazee wengi ambao leo wamejikuta katika kashfa hizi na zile pia na wao waamue kuwa wanyenyekevu na kukubali makosa ya kiutendaji yaliyotokea ili tuanze upya.
Tatizo ni ego zao bwana.Wanajiamini kweli hata kama wanaonekana vituko kila wanakopita.
Na watanzania tusisahau pia kama anavyosema Lole kuwa yapo mengi mazuri mtu kama BWM ameyafanya. Dawa sio kulia chini chini. Ajivike ujasiri wa kusema sorry
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom