Mkapa: tume tangazeni matokeo CCM imeshinda muuwaache waende mahakamani

Kama ni hivyo basi yawezekana kweli anahusika na kifo cha Mwalimu.
Ila kabla hajasababisha mauaji mengine, atoe ufafanuzi wa kifo cha Mwalimu kwanza.
 
Slaa anazeeka vibaya naona.
OTIS

Nimemsahau jina.. Ila nilichosikia ni kuwa wana-CCM wengi huko Arumeru East walimtaka yule mwingine,na si Siyoi....

Na kwamba wamechukia mgombea wao kuachwa... Na zaidi ni kuwa hawako tayari kumpa Siyoi..
 
NEC wawe makini na ningeshauri wafutulie mbali ushauri wa Mkapa. Hamtakii mema Sioi kwa sababu kama watu hawakumchagua ataongozaje? Nani atampa ushirikiano? Tofauti na sehemu nyingine Meru watu wakisema hapana wanamaanisha hapana. NEC wana option ya kudumisha amani Meru au kuleta machafuko. Ushauri wa Mkapa utaleta balaa Meru.
 
Huyu muasisi wa ufisad mkapa unategemea ataongea nini?yaani ukiwa msomi ukiwa ccm gambaz akili inahama toka ubongoni hadi masaburini.tumsamehe so kosa lake anatamani urais tena huyo,zee zima halioni aibu dawa yake kulizomea kila lipitapo hili fisadi papa.
 
Dr mkapa ni mtu makin sana hawezi kuwa na myopia vision kama weewe.mwandishi wa thread hii muongo ,maana ametoa mfano wa amosi makala kupitishwa kwa nguvu, makala amekuwa mbunge mwaka 2010 wakati mkapa ame retire 2005 ! Wapi na wspi?
Wacha uwongo wewe! angekuwa makini angeongea pumba wakati wa uzinduzi wa kampeni kule Arumeru, ati Vincent Nyerere sio wa ukoo wa nyerere! Mtu makini asingekuja na hoja mfilisi kama hiyo. Kwani kuwa na nasaba na Nyerere ni dili?
 
hivi mna uhakika gani na haya maneno? je, Dr Slaa akisema jambo kila mtu lazima aamini bila source? angalia tusije onekana wambea!!!
 
Jana Dr. Slaa amedai kuwa ktk vikao vya siri vya ccm anekaririwa rais mstaafu BWM akiishinikiza tune ya uchaguzi kuitangaza ccm imeshinda uchaguzi wa Arumeru hata kama wameshindwa kwa sababu wataenda mahakamani na kesi itafia huko.

Napata picha kuwa ccm ni wezi, wanyang'anyi na wauwaji mbinu kama hii ndio iliyompa ubunge Makala baada ya mkapa kumtishia maisha mbunge wa cdm aliyekuwa ameshinda Mvomero baada ya kushindwa kumhonga

Tusikubali ushenzi huu cz wanajua fika tume na mahakama ni wateule wa mwenyekiti wao


Unachosema ni kweli, nimeshiriki katika research ya post election violence, na msimamizi wa uchaguzi Mvomero katoa ushuhuda kuwa Mkapa alimpa milioni 60 na kwamba kama angakataa kumtangaza makala mshindi kibarua kingeota nyasi. Hata tape za sauti za huyu jamaa bado zipo
 
BWM ni miongoni mwa viongozi bora barani AFRIKA,chuki zenu weka kapuuuuuuuuuuuuuuni a.k.a trashhhhhhhhhhhhhhhhhout.Kusema Vicent Nyerere si mtoto wa Mwl. JK Nyerere alikuwa sahihi.Japo kuwa ni ndugu yake ! Hilo suala limegeuzwa kama ni kosa kwa MKAPA ambaye amefanya mambo mengi makubwa na yanaonekana.Mfano barabara na madaraja yamejengwa kwa wingi wakati wa utawala wake.Tuhuma ambazo azithibitishwa si vizuri kuzitumia kuwachafua viongozi wastaafu.
 
Mzee mkapa alianza kupata umaarufu fulani watu walipoanza kujua kwamba JK ndio ziro kabisa, sasa kinachofanywa na magamba ni kumrudisha majukwaani ili achafuke na asiweze kabisa kuinfluence kwa namna yoyote uchaguzi mkuu ujao
 
BWM ni miongoni mwa viongozi bora barani AFRIKA,chuki zenu weka kapuuuuuuuuuuuuuuni a.k.a trashhhhhhhhhhhhhhhhhout.Kusema Vicent Nyerere si mtoto wa Mwl. JK Nyerere alikuwa sahihi.Japo kuwa ni ndugu yake ! Hilo suala limegeuzwa kama ni kosa kwa MKAPA ambaye amefanya mambo mengi makubwa na yanaonekana.Mfano barabara na madaraja yamejengwa kwa wingi wakati wa utawala wake.Tuhuma ambazo azithibitishwa si vizuri kuzitumia kuwachafua viongozi wastaafu.

Angekuwa kingozi bora Afrika angepata zawadi ya MO Ibrahimu mbona alipigwa chini?

BTW, kiongozi gani anayechaguliwa ili afanye mabaya?

Tuhumu zisizothibishwa?! Acha UTANI basi Unataka Mkapa tumpeleka kwa Ocampo ICC ndiyo ujue kwamba aliua watu Pemba na kuzalisha wakimbikizi kwa mara kwanza katika historia ya nchi hii?

Au unataka mpaka David Cameron aseme kwamba Mkapa kwa kushirikiana na Chenge walikula MLUNGULA kwenye ununuzi wa rada kutoka BAES?

Na huo mgodi wetu wa Kiwira aliojimilikisha kwa bei chee akiwa IUKULU, kabla ya kurudishwa kwa wananchi kwa shinikizo la People's Power au hata Hansard za bunge letu huliamini?

Hiyo Sheria unayotaka kutufundisha hapo duniani popote, kwamba mtu akifanya mambo mengi mazuri, basi akifanya makosa (JINA)machache asishitakiwe au ahurumiwe ni YAKO MWENYEWE, vinginevyo kusingekuwa na MTU hata mmoja Magereza.
 
hakuna cha mahakamani utakuwa muda mzuri wa JK kuondoka na genge lake na makatili na wauaji wa kubwa wa watanzania masikini.
 
Inafahamika ya kuwa ccm wameishiwa sera. Maovu yote yanayotokea leo hii ni matokeo ya uongozi mbovu wa ccm. Awali chama cha TANU kilikuwa kina mwelekeo wa kuwasimamia na kuwaendeleza wananchi wa Tanzania. Baada ya CCM kuzaliwa sera za awali za kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Tanzania ziliendelezwa kwa miaka michache 1977-1985.

Tangu CCM ilipovaa magamba na kuwa ccm, walipoondoa miiko ya viongozi, walipoliasi Azimio la Arusha na misingi yake ya Binadamu wote ni Sawa, walipoacha kuitana ndugu na kujipa cheo cha waheshimiwa, waliporuhusu viongozi kuwa na hisa kwenye makampuni na kuingiza wafanyabiashara kwenye siasa, ile dhana ya watu wote kuwa sawa ambayo ilikuwa msingi wa utanzania wetu ikapotea. ccm ya sasa sio CCM aliyoianzisha Mwalimu. ccm ya sasa sio tena chama cha wakulima na wafanyakazi. Ndiyo sababu wakubwa wakiugua wanapelekwa Afrika ya Kusini, India au Ujerumani, mlala hoi analala sakafuni Muhimbili. Ndiyo sababu wakubwa wanajiongezea posho wakati wafanyakazi wa kawaida hata mishahara yao halali kwa kazi waliyoifanya ya mwezi hawalipwi. Ndiyo sababu wakubwa wanadiriki kutamka hadharani kuwa dola 4000 ni vijipesa. Ndiyo sababu wako tayari kufanya lolote, hata kutumia vyombo vya dola vikiwemo polisi wenye silaha kuzima vuguvugu la mabadiliko. Ndiyo sababu hawatakuwa tayari kuona chama kingine chochote kinachukua madaraka!

Watasema na watafanya mengi, lakini hata utawala wa Warumi ulifika mwisho!
 
Back
Top Bottom