Mkapa to miss Sullivan Summit

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Tuanze kubeba mabango ili kumshinikiza fisadi Mkapa katika mikutano anayohudhuria nchi za nje ili ajibu tuhuma nzito za ufisadi dhidi yake.

Mkapa to miss Sullivan Summit
DEOGRATIAS MUSHI in Arusha
Daily News; Sunday,June 01, 2008 @00:03

Former President Benjamin Mkapa will not attend the 8th Sullivan Summit due to begin here tomorrow, as he leaves today for London to attend Investment Climate Facility for Africa (ICF) meeting.

A Press statement released yesterday by his personal assistant Dr. Aziz Ponary Mlima said that Mr Mkapa, will Co-Chair the Board of Trustees and the Annual General Meetings of ICF on Tuesday.

The Investment Climate Facility for Africa (ICF), whose headquarters is in Dar es Salaam, seeks to help Africa to create a more attractive business environment and realize its potential as global player and trading partner.

The ICF works toward removing real and perceived obstacles of domestic and foreign investment by assisting Africans to prepare and promote the continent as an investment destination.

Dr Mlima said that ICF recently signed an agreement with the judiciary to expedite and facilitate court process in the country, mentioning priority areas as property rights and contract enforcement, business registration and licensing, taxation, customs, financial markets, infrastructure facilitation, labour markets, and competition.

ICF is funded by governments, international institutions and corporate donors, among them are Germany, United Kingdom, Ireland, Norway, France, Africa Development Bank, International Finance Corporation, Unilever, Standard Bank, Shell Foundation, Celtel, among others.

European Union and other governments are in discussion phase to become donors. After the ICF meeting, Mr Mkapa will travel to Boston in the United States to attend a strategic meeting of the Board of the Aga Khan International University, of which he is a member.
 
Tuanze kubeba mabango ili kumshinikiza fisadi Mkapa katika mikutano anayohudhuria nchi za nje ili ajibu tuhuma nzito za ufisadi dhidi yake.

This si right!

Alafu what si the big deal Mkapa akikosa kuhudhuria SS?

Kuna kitacho haribika? walikuwa wa ongelee Kukiuka maadili ya uogozi ?

Nimesoma the whole story sijui walitaka kutueleimisha nini kuhusu BEN kutokupo assit please!
 
Kuna trend inayojitokeza ya fisadi Mkapa kuanza kuingia mitini kwenye shughuli mbali mbali muhimu zinazofanyika nchini. Hakuhudhuria sherehe za uhuru December 9, 2007 zilizofanyika kitaifa pale Dodoma. Pamoja na kuwa mjumbe wa kamati kuu, hakuhudhuria kikao cha kamati kikuu kilichofanyika Butiama na sasa anaikimbia SS ili kuhudhuria mikutano mingine nje ya nchi.

Watanzania walio nje nao wakianza kumshinikiza kwa mabango ili ajibu tuhuma nzito za ufisadi dhidi yake basi atakuwa hana jinsi ama akubali kuhojiwa kwa kirefu kuhusu tuhuma hizo au aendelee kujificha ili kutohudhuria shughuli muhimu ndani na nje ya nchi.
 
kwa nini msingeenda na mabango kwenye arobaini ya ditto maana alikuwepo huko !
 
This si right!

Alafu what si the big deal Mkapa akikosa kuhudhuria SS?

Kuna kitacho haribika? walikuwa wa ongelee Kukiuka maadili ya uogozi ?

Nimesoma the whole story sijui walitaka kutueleimisha nini kuhusu BEN kutokupo assit please!

Jamani Che-Nkapa tunaweza kumtafutia angle nyingi lakini hii ya kutohudhuria Sullivan summit mi naona ni sawa tu. Maana ni utapeli mtupu, mwache anedelee kupalilia shamba lake huko nje [snark]! Maana Sullivan summit ni bustani la JK . Daily News nayo imekosa story, wanataka kufanya kama vile hiyo Sullivan summit ina umuhimu wowote! Tumbane Mkapa kutohudhuria sherehe za uhuru etc lakini hili hapana.
 
kwa nini msingeenda na mabango kwenye arobaini ya ditto maana alikuwepo huko !

Watanzania ni waungwana sana, pamoja na kutaka sana kusikia fisadi Mkapa akijibu tuhuma nzito dhidi yake, lakini siku zote tutaheshimu sehemu ya msiba. Sehemu ya msiba hakistahili kufanywa chochote kile kingine zaidi ya kuwafariji wafiwa. Na ndio maana Watanzania wengi tunamshangaa Waziri Simba alipoamua kumtetea fisadi Mkapa mahali penye msiba. Kuna sehemu chungu nzima ambazo Waziri Simba angeweza kufanya hivyo na kuwaheshimu wafiwa katika kuadhimisha arobaini ya msiba wao.
 
Tuhuma ameshajibu tatizo lenu mnataka ajibu manavyotaka ninyi. Na kama hamjalizika nadhani hayo mabango yenu myapeleke kwa hao wanaotakiwa kumchukulia hatua. By the way, mtanzania yeyote anaweza kufungua kesi unaweza kujinyoshea bango mwenyewe kwa kutomchukulia hatua.
 
Jamani Che-Nkapa tunaweza kumtafutia angle nyingi lakini hii ya kutohudhuria Sullivan summit mi naona ni sawa tu. Maana ni utapeli mtupu, mwache anedelee kupalilia shamba lake huko nje [snark]! Maana Sullivan summit ni bustani la JK . Daily News nayo imekosa story, wanataka kufanya kama vile hiyo Sullivan summit ina umuhimu wowote! Tumbane Mkapa kutohudhuria sherehe za uhuru etc lakini hili hapana.

Kwa hiyo angeudhuria sherehe ya uhuru matatizo ya huduma za afya yangeisha? Sherehe yenyewe haina manufaa yoyote cha umma zaidi ya kutumia gharama kubwa kuiandaa. Do you know how much is going to cost you kumpeleka Mkapa uwanja wa taifa? Wewe shukuru tu hakwenda.
 
Haya tusahau huo mkutano wa SS, lakini bado kuna trend inayojitokeza ya fisadi Mkapa kuingia mitini kwenye shughuli muhimu nchini kama nilivyoeleza hapo juu, hili halipingiki.
 
Tuhuma ameshajibu tatizo lenu mnataka ajibu manavyotaka ninyi.

Sam ,

Kitu ulichosema hapo hakimake sense hata kidogo . Ni tuhuma gani ambazo Mkapa amezijibu mpaka sasa ? Yeye si alisema policy yake ni uwazi na ukweli , kwa nini sasa hataki kuzungumzia in detail jinsi alivyotumia ikulu kujilimbikizia mali . Usije ukafikiri watu wanamchukuia Mkapa kama Mkapa bali watu wanachukia wizi alioufanya akiwa ofisini . Wewe kama unakunwa kool -aid yake sawa , lakini hii aitozuia watu wengine kuongea.
 
Najua kwa watanzania wengi haki make sense ndiyo maana mnafanya hii kuwa national debate. Mkapa amejibu in general kwamba tuhuma zote mnazosema na uongo kwa hiyo chukua tuhuma zote jibu lake ni uongo sasa hapo unataka details za nini. Kama amejilimbikiza mali kinyume cha sheria au utaratibu sisi siyo ngedere wanaoishi bila sheria chukueni sheria. Kwa mfano mtu akakutuhumu kwamba tunaomba utueleze ni kivipi umeweza kumiliki TBL unatamjibu nini na wewe humiliki hiyo TBL? Nadhani hata wewe jibu lako litakuwa huo uongo hakuna details zote ambazo unaweza kuzitoa.
 
Yaani huyu fisadi Mkapa anafanya biashara akiwa Ikulu, anafanya ufisadi ikiwemo ununuzi wa rada, ununuzi wa ndege ya Rais, helicopters na magari ya jeshi. Katika mazingira ya kifisadi anajimilikisha Kiwira Coal Mining, ananunua majumba chungu nzima Tanzania zikiwemo hosteli na majumba mengine nchi za nje. Halafu wewe unashangaa kuona Watanzania wanazifanya hizi tuhuma nzito dhidi ya Mkapa kuwa national debate!!!! Kijana mtazamo wako wa mambo na uchambuzi wako ni finyu mno!!! Sasa kama hizi tuhuma dhidi ya fisadi Mkapa haziwi national debate twambie ni issue gani ambayo wewe unaiona inastahili kuwa national debate!!!? Simba na Yanga???? :confused::confused::confused::confused::confused:
 
We can debate on this. Mimi sifanyi uchambuzi wa upashkuna na base kwenye facts. Hayo mambo uliyosema sikatai kama hayawezi kuwa nationa debate but you must have facts that support. Kama kuna sheria inayomkataza rais au ndugu zake au watu ambao ana uhusiano wake wa karibu kununua majumba hapo kutakuwa na tatizo na inaweza kuwa nationa debate au kama kama wananchi wanadhani sheria/utaratibu wa sasa hivi hazifai basi hapo inaweza kuwa natinal debate. Mkapa hawezi kuwa debate hapa kama ni kweli amefanya ame take advantage of the system ambalo silo kosa. Unaposema amejimilikisha Kiwira inamaanisha amejimilikisha kwa jina lake hata kama amejimilikisha kwa jina lake je anaruhusiwa kufanya hivyo? Je, taratibu zilifuatwa? Those are the issues we can debate. Kama haruhusiwi hilo ni kosa na anatakiwa kupelekwa mahakamani hakuna debate hapo labda tunakosa chombo au sheria ya kufanya hivyo na tunazihitaji. Kumtaka Mkapa ajibu I do not see how that is going to help us na hata kama alifanya kweli we all know what is going to answer ni kupotezeana muda tu.

Kwa kuongeza kidogo. Kwenye orodha ya Dr. Slaa ya mafisadi sikuwa na tatizo nayo kwa sababu moja kubwa ali define vigezo alivyotumia kumuita mtu fisadi.. sijui wewe unautafsiri vipi ufisadi au ni vigezo gani unatumia kumuita Mkapa fisadi kama ni tofauti na Dr. Slaa.
 
Tufahamishe tafadhali ni "facts" gani hizo zinazokufanya uamini kwamba tuhuma zote za ufisadi dhidi ya Mkapa (kuanzia kuanzisha kampuni ya biashara ANBEN Ikulu, hisa kwenye Bank M hadi kutaifisha mgodi wa Kiwira) zote ni uwongo (na zinatokana na chuki binafsi ya baadhi ya watu aliowanyima vyeo wakati wa urais wake?)
 
Kwa kuongeza kidogo. Kwenye orodha ya Dr. Slaa ya mafisadi sikuwa na tatizo nayo kwa sababu moja kubwa ali define vigezo alivyotumia kumuita mtu fisadi.. sijui wewe unautafsiri vipi ufisadi au ni vigezo gani unatumia kumuita Mkapa fisadi kama ni tofauti na Dr. Slaa.

Hivyo hivyo alivyotumia Dk Slaa. Facts zipi tena unazozitaka zaidi ya zilizokwishawekwa hadharani!? Si unakumbuka wale wote ambao majina yao yalitajwa na Dk Slaa walitishia kumfungulia mashtaka Dk Slaa kwa kuwaharibia reputation yao kwenye jamii ya Watanzania? Jina la fisadi Mkapa pia lilikuwemo. Hadi hii leo pamoja na miezi chungu nzima kukatika hatujaona hata mmoja aliyefungua kesi dhidi ya Dk Slaa. Sasa wewe ni mtetezi wa hao mafisadi kuliko ambavyo wanavyoweza kujitetea wenyewe!!!!???? Kwanini hadi hii leo hawajamshtaki Dk Slaa?

Upashkuna unaingiaje tena katika haya majadiliano? Kumbuka matusi hapa JF hayaruhusiwi, kama huwezi kujadiliana bila kutumia lugha ya matusi basi ni bora ukae pembeni.
 
Aibu kubwa kwa Dr. Mlima kuendelea kuzunguka na fisadi Mkapa.

Sisi wasomi tena tuliosoma nje na kufanya kazi nje ndio tunaongoza kwa uzezeta wa
kujali maslahi yetu binafsi na ksahau wananchi.

Huyu Dr. Mlima kweli ameishia kujidhalilisha hivyo na kuendelea kuwa mbeba mkoba wa fisadi Mkapa?
 
Mkapa hawezi kuwa debate hapa kama ni kweli amefanya ame take advantage of the system ambalo silo kosa. Unaposema amejimilikisha Kiwira inamaanisha amejimilikisha kwa jina lake hata kama amejimilikisha kwa jina lake je anaruhusiwa kufanya hivyo? Je, taratibu zilifuatwa? Those are the issues we can debate. Kama haruhusiwi hilo ni kosa na anatakiwa kupelekwa mahakamani hakuna debate hapo labda tunakosa chombo au sheria ya kufanya hivyo na tunazihitaji. Kumtaka Mkapa ajibu I do not see how that is going to help us na hata kama alifanya kweli we all know what is going to answer ni kupotezeana muda tu.

Kiini cha shutuma dhidi ya Mkapa ni kwamba alitumia visivyo cheo na wadhifa wake akiwa Rais kuendesha biashara na kujitajirisha yeye binafsi, familia yake na maswahiba wake. Hii ni kinyume na maadili, kanuni na taratibu za Uongozi serikalini na ni kosa kubwa sana. Ile kwamba amediriki kufanya yote hivi kwa kutumia nguvu kubwa (na isiyo na kipingamizi cha aina yoyote ile Jamhuri nzima ya Tanzania) ya cheo chake kama Rais wa nchi ni ukiukaji wa taratibu tayari na haisaidii kama procedure nyinginezo (maombi ya mkopo, usajili wa kampuni, nk) zilifuatwa. Jee, unabisha hata hili?
 
Tuhuma ameshajibu tatizo lenu mnataka ajibu manavyotaka ninyi. Na kama hamjalizika nadhani hayo mabango yenu myapeleke kwa hao wanaotakiwa kumchukulia hatua. By the way, mtanzania yeyote anaweza kufungua kesi unaweza kujinyoshea bango mwenyewe kwa kutomchukulia hatua.

yaani hapa yamewaendea ndivyo sivyo ! maana mzee mkapa hajibu wanavyotaka wao bali anajibu yaliyojiri lakini watu hawataki, hapa mbona patamu !
 
Hata mkapa asipokwenda arusha. Nadhani kwa kuwa anajua siri anafahamu hakuna la maana kule. Na nahisi anafikiri watakwenda kumsumbua tu kwa maswali ya Tanpower yake na Yona
 
Back
Top Bottom