tramadol
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 5,383
- 4,317
Tunaelewa sana usifikiri hatuelewi kilichoandikiwa.Umemuelewa?! The problem nyie watu ama huwa hamuelewi watu wanaongea nini au mnajifanya hamuelewi!! Rudia kusoma hapa:Hoja ya wale mnaowaona wanatetea wezi ipo hapa!!!
Kwa mfano, mkataba wa Acacia unawapa haki ya kusafirisha makinikia.
Taasisi za serikali ndizo zilibariki viwango vya madini mbalimbali yaliyomo kwenye makinikia!
Aidha, ni taasisi hizo hizo za serikali ndizo hukagua na kusema "everything is fine."
Hapo ndipo ina-cover Ulimwengu aliposema "....to accept as its own obligations commitments made by its predecessors."
Kama ndivyo, ili kuwabana hawa jamaa JPM alitakiwa ku-play by the rules ili wasiwe na pa kutokea!!!
Kwa mfano, Acacia wanadai hawakushirikishwa kwenye kupima zile mineral compositions. Sasa kama ni kweli hawakushirikishwa, unafikiri ni mahakama gani inaweza kukubali utafiti uliofanywa na upande mmoja?!
Hivi kulikuwa na taabu gani kuwashirikisha Acacia kwenye kila hatua hususani zile za kuchukua samples na kuzipima?! Hivi unadhani kama Acacia wangeshirikishwa kwenye uchukuaji wa samples na kwenda kuzipima hadi kutoka kwa results leo hii wangekuwa na pa kutokea?!
Kama ingefanyika hivyo ingeonekana ni Acacia ndio waliovunja makubaliano kwa kudai makanikia yana kiwango X cha madini wakati kumbe kuna X+n!!! Kinyume chake, leo hii Acacia ana kila sababu na haki ya kuikataa ripoti kama kweli hawwakushirikishwa!
PLAYING BY THE RULES!!!!
Tunachosema kwanini kuwe na taarifa potofu kuhusu kilichopo ndani aidha kimeidhinishwa na Serikali au la hiyo siyo issue kwasababu tunajua kilichokuwa kinaendelea kupitia Mgongo wa Serikali.
Hata kama acacia wana haki kisheria kusafirisha makinikia hilo linajulikana wala halina shida.
Hapa tunataka kujua kwanini taarifa zilizokuwa zinaandikwa hazikuwa na ukweli kuhusu kilichokuwa ndani ya makontena mpaka Tume imeyaona yote hayo.