Mkapa, Salim waenda Botswana kumzika Masire

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Viongozi mbalimbali duniani wameanza kuwasili nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo, Sir Ketumile Masire.
Masire alifariki dunia wiki iliyopita akiwa na miaka 91. Ibada maalumu inafanyika leo ( Jumatano) wakati mazishi yake yakitarajiwa kufanyika kesho kijijini kwake Kanye.


Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC limesema tayari viongozi kadhaa wa Afrika wamewasili mjini Gaborone kwa ajili ya kushiriki mazishi hayo.
Viongozi hao ni pamoja na Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika(OAU) Dk Salim Ahmed Salim. Wengine ni rais wa zamani wa Msumbiji, Armando Guebuza na wageni wengine mashuhuri.


Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki nao ni miongoni mwa viongozi waliotarajiwa kuwasili nchini humo wakati wowote kuanzia sasa.

jpm_mkapa.jpg
images.jpeg

Masire alikuwa rais wa Botswana kati ya mwaka 1980-1998. Aliongoza juhudi mbalimbali za kidiplomasia barani Afrika ikiwamo kuongoza jopo la wataalamu waliochunguza mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.
 
Yamekuwa hayo?
Achana nao Simple minds ndo wapo hivyo. By the way hawafahamu historia ya huyu baba na jinsi alivyoifanya Botswana kuwa nchi ya heshima na tajiri. For your Information huyu mzee aliwachukua wasomi wa TZ waliokuiwa wamechoka na siasa za bongo na ndo wameifanya nchi ile iwe kama ilivyo wakati sisi tumebaki na siasa zetu.
 
Sizonje hata haelewii mambo ya diplomasia!! Kwanza umtajie hilo jina Masire atasema atasema kuna ri nchi huko kusini rimeendereaa rinaitwa masire......haelewi lolote!! Sadam wa Kuwait
 
Back
Top Bottom