Mkapa ni Sawa na Ungo Kwa Majirani, Kibeku Kwa Watanzania

MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,383
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,383 280

Rais wa awamu ya tatu Tanzania, Benjamin William Mkapa.

February 11, 2010

SIAMINI kama huyu anayezungumziwa hapa ni Rais wangu wa awamu ya tatu nchini Tanzania Benjamin William Mkapa. Wakati huo nilikuwa najiandaa kuvuka mpaka wa Zambia na Tanzania katika mji wenye vurugu wa Tunduma mkoani Mbeya ili niweze kuingia nchi jirani ya Zambia.

Mbele yangu naona mchanganyiko wa raia wa Tanzania na Zambia wakihangaika huku na huko kujitafutia riziki, wengi wao wakiwa wafanyakazi wa magari ya mizigo.

Mji huu una pilikapilika kama zile za Manzese Jijini Dar es Salaam, lakini hauna tishio la vibaka zaidi ya watu kujitafutia maisha kutokana na shughuli wanazozifanya.

Si rahisi kupata mtu wa kuzungumza naye labda wafanyabiashara wa vyakula waliojitenga kandoni mwa kituo kikuu cha magari yatokayo kila upande.

Uzuri wa sehemu hii ya biashara hakuna anayeilaumu Serikali, wengi wanalaumiana wenyewe kwa wenyewe kwa kuzembea jambo fulani lililowakosesha kipato.

Ukivuka salama kutoka Tunduma utakaribishwa na kitongoji cha Nakonde hapa tayari utakuwa umekanyaga ardhi ya Zambia.

Hapa hakuna pilika pilika nyingi kama zile zilizokuwa Tunduma, watu wanaonekana wakihangaika na shuguli za kawaida, hata wakulima wanaweza kuonekana hapa.

"Murishani anwe" unaweza kuulizwa ikiwa ni salamu ya moja ya kabila moja la nchini Zambia.

Utakapojibu vizuri na kuulizwa nchi uliyotokea na kwa bahati nzuri ukiitaja nchi ya Tanzania hasa Jiji la Dar es Salaam utaongeza heshima kidogo.

Wataanza kudadisi kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na mengine kadhaa kuhusu Tanzania.

Humuulizia zaidi Benjamin Mkapa ambaye alipata kuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania.

"Murishani Mwapungule Mkapa?" wakiwa na maana anaendeleaje Mheshimiwa Mkapa"

Utakapojibu kwamba hajambo na sasa amejipumzisha ila bado amekuwa akishiriki na ujenzi wa taifa la Tanzania, hawatasita kumpa sifa zake alizojipatia kutokana na uongozi wake shupavu na hapo utaweza kusikia jibu hili.

Wanasema kwamba Mkapa ndiye Rais shupavu wa Tanzania ambaye anapaswa kuwekwa kwenye kumbukumbu za utendaji uliotukuka.

Wanakubali kwamba Tanzania ni moja ya nchi iliyobarikiwa na Mungu kupata viongozi bora tangu aliyekuwa muasisi wa taifa la Tanzania hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hadi Rais Kikwete ila kwa Rais mstaafu Mkapa wanazidisha sifa.

Wanamsifu Mkapa kwa namna ambayo hata raia wa Tanzania asingeweza kujua au kueleza sifa ambazo kiongozi huyo anazo.

Ukiachilia kitongoji hicho cha Nakonde utaweza kuvipitia vingine kama vile Mwenzo, Kapwila, Chozi, Chandananeyaya, na Lusiwasi, mji ambao ni makao makuu ya Jimbo la Kaskazini.

Katika vitongoji vya Mfumu, Mpika, Nkulushi River na Chambeshi wanatamani kumuona mkuu huyo wa nchi wa zamani wa Tanzania angalau aende akawatembelee.

Ukitokea Zambia unaweza ukashangazwa na kauli zinazoshabihiana katika miji mbalimbali nchini humo kuhusu sifa za Rais mstafu Mkapa, zinazotokana na uongozi shupavu uliojikita katika kukusanya kodi na kuimarisha miundombinu hasa ile ya barabara.

Wakati unapovuka mpaka wa Tanzania na Malawi ukiwa mjini Kaporo na kuelekea Kalonga maswali ya kuhusu Tanzania na uongozi wake yatazidi kuwa kero kwako.

Unaweza ukatamani usijitambulishe kuwa wewe ni Mtanzania hasa kama hutokuwa na elimu ya kutosha juu ya uraia na hatma ya nchi pamoja na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini.

Watakapomtaja Rais Mkapa wataongeza maneno haya nanukuu: 'Sieni Mkapa akale pa pepo'

Maana yake 'mwacheni Mkapa apumzike'.

Wanalaani sana pale wanaposikia kiongozi huyo wa nchi akihusishwa na ubadhirifu.

Ukiweza kukaa katika baadhi ya hoteli zilizopo kwenye miji mikuu kama vile Blantyre au Lilongwe utapata sababu kuu za wananchi hao kumlilia Mkapa.

Kama ilivyo kwa Wazambia huorodhesha kero alizopambana nazo Mkapa katika utawala wake wa awamu ya tatu ya uongozi wa Tanzania.

"Kwanza alipata changamoto ya kwanza kabla ya kugombea Urais kwa vile hakuwa akifahamika sawa kwa Watanzania," anasema mkufunzi wa chuo cha Ualimu Usisya.

"Lakini pia alizuia mfumuko wa bei hadi anaondoka madarakani tulikuwa tumewazidi kwa bei ya vyakula kama vile mchele, unga na hata mafuta huyu aliwawezesha watu wenye kipato cha chini kufurahia maisha," anasema Mwalimu huyo.

Lakini Rais Mkapa anasifiwa kwamba licha ya kumudu kudhibiti mfumuko wa bei lakini ndiye aliyewawezesha Watanzania kupata elimu kuhusiana na uanzishaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) na Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES).

"Mpango huu umeifanya Tanzania itukimbilie kwa kiwango cha elimu, hapo zamani tuliwazidi kabisa," anaongea msomi Alex Chingalaba kutoka mji wa Lumph.

Uthamani wa Rais mstafau Mkapa kwa wananchi wa nchi jirani ni sawa na ungo ingawa hapa nchini thamani yake kwa baadhi ya watu ni sawa na uongo uliochakaa ambao katika baadhi ya maeneo hapa nchini hujulikana kama Kibeku.

Na pindi utakapoaga kutoka kwenye vijiwe hivyo wananchi hao wan chi jirani watakusisitiza kwamba "Nyie Wabongo...Sieni Mkapa".

Chanzo: nifahamishe.com
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
82,102
Likes
121,590
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
82,102 121,590 280

Rais wa awamu ya tatu Tanzania, Benjamin William Mkapa. Thursday, February Humuulizia zaidi Benjamin Mkapa ambaye alipata kuwa Rais wa awamu ya tatu wa Tanzania.

Utakapojibu kwamba hajambo na sasa amejipumzisha ila bado amekuwa akishiriki na ujenzi wa taifa la Tanzania, hawatasita kumpa sifa zake alizojipatia kutokana na uongozi wake shupavu na hapo utaweza kusikia jibu hili.

Wanasema kwamba Mkapa ndiye Rais shupavu wa Tanzania ambaye anapaswa kuwekwa kwenye kumbukumbu za utendaji uliotukuka.

Wanakubali kwamba Tanzania ni moja ya nchi iliyobarikiwa na Mungu kupata viongozi bora tangu aliyekuwa muasisi wa taifa la Tanzania hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hadi Rais Kikwete ila kwa Rais mstaafu Mkapa wanazidisha sifa.

Wanamsifu Mkapa kwa namna ambayo hata raia wa Tanzania asingeweza kujua au kueleza sifa ambazo kiongozi huyo anazo.
Mhhh! Kiongozi shupavu aliyeiba mgodi wa Kiwira kwa kutumia wadhifa wake, aliyeliingiza Taifa hasara kubwa kwa kusaini mikataba ya kuchimba madini ambayo haina maslahi kwa Watanzania, aliyewaleta Wazungu wa Netgroup kwa mtutu wa bunduki na kuwapa nafasi zote za juu za TANESCO pamoja na kuwa walikuwa hawajui lolote lile kuhusu umeme. Rais ambaye aliamua kufanya biashara akiwa Ikulu tena kwa kificho. Rais ambaye aliamua kuuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupa ambayo imeliingizia hasara Taifa ya karibu shilingi bilioni 200! Rais ambaye alilazimisha kununua Rada uamuzi ambao ulipingwa na Watanzania wengi na kuliingizia Taifa hasara ya $12 million.

Rais ambaye alilazimisha kununua ndege ya Rais akiwa amebakisha miezi mitatu katika awamu yake na ndege hiyo sasa hivi iko juu ya mawe pale JKN Airport, Rais ambaye alihusika na maamuzi ya kununua magari ya jeshi na helicopters ambao ulikuwa umegubikwa na ufisadi wa hali ya juu. Rais ambaye siku chache kabla ya kumaliza awamu yake mabilioni ya pesa yalichotwa kupitia EPA, Meremeta na Mwananchi Gold. Kweli Mkapa alikuwa ni Rais shupavu!
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Ni kiongozi hodari, shupavu na mkakamavu katika kuiba na kufisidi! tena kwa jeuri ha ha!
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,680
Likes
5,094
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,680 5,094 280
As any leader his strength and weakness lies on what good and what bad he did. The balance will always be there. Let people blame him on all those wrongdoings and let people kudos him on the things that was good. However, for serious leader and country, there must be no room for someone to make mistake as Mkapa did.
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
As any leader his strength and weakness lies on what good and what bad he did. The balance will always be there. Let people blame him on all those wrongdoings and let people kudos him on the things that was good. However, for serious leader and country, there must be no room for someone to make mistake as Mkapa did.
I haven't seen something extra ordinary Mkapa did in his 10th years of leadership, anyperson (ordinary human being) can do what mkapa did, just entirely agreed with WB, IMF and wazungus ...

I expect nothing extra ordinary from JK, however JK will have less mistakes kwasababu siyo Jeuri na kiburi kama mkapa sioni kama anapenda mshiko (pesa) kama huyo chinga!!! hana ambitions

We have only one serious leader in our time JKN who did extra ordinary things
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,556
Likes
2,369
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,556 2,369 280
Mwacheni mzee apumzike, hawa jamaa tulonao madarakani kwa miaka minne tu washamzidi mkapa mabaya alotenda kwa miaka kumi sasa wakitimiza kumi, mkapa tutamwona mtakatifu. Ila huyu mzee pamoja na mapungufu yake alitusaidia mengi manake me na umri wangu huu barabara ya lami nimeiona katika kipindi chake wala usiniulize kwanini nilikuwa sitembei. Ngoja tumsubiri Kiwete wetu kwa miaka kumi tutasemaje.!
 
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
5,575
Likes
3,354
Points
280
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
5,575 3,354 280
Proverb Champions PSA.mp4
[ame]http://www.youtube.com/watch?v=YrY_j6S1BQ4[/ame]
 
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2007
Messages
20,563
Likes
1,591
Points
280
Kigogo

Kigogo

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2007
20,563 1,591 280
I haven't seen something extra ordinary Mkapa did in his 10th years of leadership, anyperson (ordinary human being) can do what mkapa did, just entirely agreed with WB, IMF and wazungus ...

I expect nothing extra ordinary from JK, however JK will have less mistakes kwasababu siyo Jeuri na kiburi kama mkapa sioni kama anapenda mshiko (pesa) kama huyo chinga!!! hana ambitions

We have only one serious leader in our time JKN who did extra ordinary things
kweli he did extra ordinary things including kutuingiza katika vita na Uganda ambavyo vimeitia umasikini hii nchi mpaka leo kwa sababu zisizo na msingi...kweli JKN he did extra ordinary things
 
annamaria

annamaria

Senior Member
Joined
Apr 1, 2009
Messages
135
Likes
2
Points
33
annamaria

annamaria

Senior Member
Joined Apr 1, 2009
135 2 33
I haven't seen something extra ordinary Mkapa did in his 10th years of leadership, anyperson (ordinary human being) can do what mkapa did, just entirely agreed with WB, IMF and wazungus ...

I expect nothing extra ordinary from JK, however JK will have less mistakes kwasababu siyo Jeuri na kiburi kama mkapa sioni kama anapenda mshiko (pesa) kama huyo chinga!!! hana ambitions

We have only one serious leader in our time JKN who did extra ordinary things
wewe huwa unasema Mkapa na Mwinyi ndiyo wame deliver,leo umepiga u turn unamsifia Nyerere??
 
Mlalahoi

Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2006
Messages
2,124
Likes
485
Points
180
Mlalahoi

Mlalahoi

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2006
2,124 485 180
Mwacheni mzee apumzike, hawa jamaa tulonao madarakani kwa miaka minne tu washamzidi mkapa mabaya alotenda kwa miaka kumi sasa wakitimiza kumi, mkapa tutamwona mtakatifu. Ila huyu mzee pamoja na mapungufu yake alitusaidia mengi manake me na umri wangu huu barabara ya lami nimeiona katika kipindi chake wala usiniulize kwanini nilikuwa sitembei. Ngoja tumsubiri Kiwete wetu kwa miaka kumi tutasemaje.!
Busara nyingine bwana,ni zaidi ya kichekesho.Hivi mtu akimbaka mkeo,then akatokea mbakaji mwingine aliyebaka wanawake watani,ina maana yule mbakaji wa mkeo anakuwa hana kosa?

Hujawahi kusikia usemi wa Kiingereza kuwa TWO WRONGS DO NOT MAKE A RIGHT?
 
M

Mwakaleli

Member
Joined
Sep 23, 2008
Messages
46
Likes
0
Points
0
M

Mwakaleli

Member
Joined Sep 23, 2008
46 0 0
Tumlaumu Mkapa kwa mambo mabaya aliyoyafanya. Lakini pia tunastahili kumpongeza kwa mazuri aliyoyafanya. mabaya ya mkapa hayatakiwi kuyafundika mazuri yote aliyoyafanya.
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Tumlaumu Mkapa kwa mambo mabaya aliyoyafanya. Lakini pia tunastahili kumpongeza kwa mazuri aliyoyafanya. mabaya ya mkapa hayatakiwi kuyafundika mazuri yote aliyoyafanya.
Ni wajibu wake kufanya alichofanya bila shukrani yeyote ile kutoka kwetu kwanza alituomba kura akiahidi kutufanyia hayo, pili tumemlipa in full (mshahara na marupurupu bila kumkopa) tatu anaendelea kula pension kutoka kwa kodi bila asante damn

Mabaya aliyofanya kwa kiburi, jeuri na dharau hakuna atakayemsamhehe na ataulizwa pia akiwa kaburini kama uwizi lakini makosa aliyofanya bila kudhamiria tumeshamsamehe kwakuwa tunafahamu kwamba siyo kamili period!
 
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined
Aug 3, 2008
Messages
12,680
Likes
5,094
Points
280
Waberoya

Waberoya

Platinum Member
Joined Aug 3, 2008
12,680 5,094 280
Ni wajibu wake kufanya alichofanya bila shukrani yeyote ile kutoka kwetu kwanza alituomba kura akiahidi kutufanyia hayo, pili tumemlipa in full (mshahara na marupurupu bila kumkopa) tatu anaendelea kula pension kutoka kwa kodi bila asante damn

Mabaya aliyofanya kwa kiburi, jeuri na dharau hakuna atakayemsamhehe na ataulizwa pia akiwa kaburini kama uwizi lakini makosa aliyofanya bila kudhamiria tumeshamsamehe kwakuwa tunafahamu kwamba siyo kamili period!
hivi ni tendo au neno gani aliloliongea au kufaya huyu mtu kinachoelezea kuwa anakiburi na dharau?
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
hivi ni tendo au neno gani aliloliongea au kufaya huyu mtu kinachoelezea kuwa anakiburi na dharau?
Alishauriwa net group solution ni bomu kwa kiburi hakusikiliza mtu akawaiingiza kwa nguvu makaburi wakachukua mali zetu kwa malipo makubwa -kiburi

Alishauriwa asiuze nyumba za serikali na asivunje NBC eti kwakuwa ni kubwa sana nakumbuka nyerere alimwambi hivi NBC ni kubwa kuliko barclays? hakujibu alivunja kwa jeuri na kiburi

Alitumia nguvu za ziada akaua wapemba 2001 kwa kiburi na jeuri badala ya kujutia mauaji aliwapandisha vyeo askari waliofanya unyama huo mpaka leo kuna vilema na wakimbizi wa kitanzania..kiburi dharau na power egoism

Aliiba na kujiuzia kiwira na kuanzisha kampuni akiwa ikulu uvunjaji wa katiba ..hii ni dalili ya dharau na kiburi..

list goes on...
 
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2009
Messages
4,057
Likes
1,823
Points
280
Abunwasi

Abunwasi

JF-Expert Member
Joined Jun 25, 2009
4,057 1,823 280
Sio siri weye ndugu una talanta ya kuandika - una kipaji cha kutumia maneno - ila maneno hayo matamu hayaondoi ukweli kuwa Mkapa mwenyewe amekiri kuwa alichemka!

Rejea: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/41545-the-confession-of-benjamin-william-mkapa-6.html
Alichemka kwenye nini?????? Wakati mkapa anaingia madarakani inflation ilikuwa 'double digit' akaishusha hadi 5 or 6%, Nchi hii ilikuwa haikopesheki kutokana na madeni ya nyuma lakini kwa ujasiri mkubwa alifanya maamuzi magumu ya kulipa madeni hayo ingawa tulikuwa na matatizo makubwa ya kifedha lakini mwishowe tulisamehewa madeni mengi kutokana na azma yake ya kulipa madeni ili kulinda heshima ya nchi.
Wakati mkapa anaingia madaraka mzee ruksa alikuwa ameachia kila kitu [hapo ninahisi ndiyo mwanzo wa ufisadi] lakini rais mpya alibadili na kurejesha kanuni na sheria .
Mkapa alichukua uamuzi mgumu wa kuuza/kubinasisha mashirika ambayo mengine yalikuwa magofu na mengine yalikuwa yanachungulia kaburini kutokana na uchakavu, uzembe, umangimeza na ufisadi . Leo hii TBL, TCC na mengi mengineyo ni mfano mzuri ingawa kuna mengine hayajasimama vizuri [lakini hii inatokana na udhaifu wetu wa kuhakikisha mashirika haya yaliyobinafsishwa yanaendelea kama makubaliano kati yake na serikali]
Mkapa aliridhi nchi ambayo haikuwa na fedha ya kigeni lakini alipoondoka aliacha akiba ya kutosha sana [akiba hiyo iliwezesha serikali ya awamu ya nne kuwa na jeuri ya kuhakikisha wakati wa njaa hakuna mtanzania aliyekufa njaa na wakati wa matatizo ya umeme serikali kuweza kununua[siyo kukopa] mitambo mbadala.
Raisi huyo alifanya hivyo hivyo kwenye elimu ustawi wa jamii na kadhalika . Lakini leo kuna watu kama nyinyi mnakaa kwenye meza na kumbeza yote aliyoyafanya kutokana na machache aliyofanya vibaya. Mbona hamsemi yale ambayo baba wa taifa mwenye alikiri kufanya vibaya, au mzee ruksa ambayo kwa upande fulani matokeo ya sera zake ndiyo zimeleta matatizo makubwa hadi sasa??????
Nadhani wana JF tuchangie maendeleo ya nchi yetu kwa kufanya analysis ya mambo na kuacha hisia zetu zitawale hata kuficha ukweli halisi.
UKWELI ZIKU ZOTE HUBAKI KAMA ULIVYO HATA UKIUPAKA RANGI NYEUSI LAKINI IKICHUJA UTAONEKANA
 
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2007
Messages
4,699
Likes
101
Points
145
Kasheshe

Kasheshe

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2007
4,699 101 145
Compare with other african leaders Mkapa was/is far better than many!

Back to Tanzania
Ben was a good administrator with some fairly leadership skills.
Ali was good reconciliator
Kambarage was a leader of course with vision and focus
Jakaya is ....
 
B

Bumela

Senior Member
Joined
Sep 23, 2009
Messages
148
Likes
6
Points
35
B

Bumela

Senior Member
Joined Sep 23, 2009
148 6 35
Compare with other african leaders Mkapa was/is far better than many!

Back to Tanzania
Ben was a good administrator with some fairly leadership skills.
Ali was good reconciliator
Kambarage was a leader of course with vision and focus
Jakaya is ....

Jakaya is the most bogus of all
 
The Quonquerer

The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
781
Likes
2
Points
0
The Quonquerer

The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
781 2 0
Alishauriwa net group solution ni bomu kwa kiburi hakusikiliza mtu akawaiingiza kwa nguvu makaburi wakachukua mali zetu kwa malipo makubwa -kiburi

Alishauriwa asiuze nyumba za serikali na asivunje NBC eti kwakuwa ni kubwa sana nakumbuka nyerere alimwambi hivi NBC ni kubwa kuliko barclays? hakujibu alivunja kwa jeuri na kiburi

Alitumia nguvu za ziada akaua wapemba 2001 kwa kiburi na jeuri badala ya kujutia mauaji aliwapandisha vyeo askari waliofanya unyama huo mpaka leo kuna vilema na wakimbizi wa kitanzania..kiburi dharau na power egoism

Aliiba na kujiuzia kiwira na kuanzisha kampuni akiwa ikulu uvunjaji wa katiba ..hii ni dalili ya dharau na kiburi..

list goes on...

Hiyo ni sahihi. Ni dikteta, nduli tena joka kuu alistahili kuhukumiwa kifungo cha maisha, ailitakiwa awe gerezani sasa hivi. Ni vile analindwa na mwizi mwenzake, huyu hajui chochote, ni kwenda kubembea tuu na kuharibu fedha za wananchi maskini. They are all devils! Tuache kuchagua voingozi bomu kama hawa, tunaongozwa na wahuni, ni magaidi. We have to change jamani!
 
Forum statistics

Threads 1,251,756
Members 481,857
Posts 29,784,014