Mkapa ni mtu wa Msumbiji??

Nwaigwe

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
1,053
913
Mimi hili linanitatiza, labda wenzangu mnalo jibu.Wapo wanaosema kuwa Rais mstaafu ni raia wa Msumbiji na wala si mtanzania, eti aliingia kule Kusini akiwa na umri wa miaka mitano wakati huo na baba yake.

Wapo wanaoangalia matendo yake na kuona ni ya ajabu ajabu.Kama tunakumbuka Mtikila kipindi kile alishawahi kusema kuwa bwana huyu si raia.

Tafadhali wale wenye kumbukumbu na ushahidi mzuri mtupatie.
 
Jamani iwapo tutaanza kujadili hili watakaobakia ni wachache kwa maana wangoni wote ni wa Afrika kusini, wapo wanyamwezi, waha, wahaya, wachanga hasa makabila yote ya mipakani ambao siyo watanzania asilia. Naona tuliache hili kama lilivyo ila cha msingi ni kujihadha asipewe madaraka mtu ambaye siyo mzawa basi.
 
Mkisema muanze kuangalia hayo mwisho mtasema Obama sio mmarekani kwa sababu historia yake inaanzia Kenya...Licha ya hayo yote Utaifa unapatikana sio tu kwa kuzaliwa katika hiyo nchi,unaweza pia ukaomba........!Huyo bwana ni "ntu wa masasi" kwa hiyo ni myao pure!
 
Mimi ninachojua ni kwamba mkapa alikua rais wa tz basi labda sifa yake nyingine ni kwamba alikua mtemi katika uongozi wake! afu pia ni fisadi ktk viongozi tulokua nao mafisadi yeye na mke wake wameifanya chi hii kuwa mbaya siku zote na kwa kosa lake hilo limefanya rais huyu wa sasa kua kama gurudumu maana nchi isha uzwa kila kitu cha thamani - atafanyaje JK?
 
Habari hizi kwamba Mkapa alitokea Msumbiji zipo na inawezekana ni za kweli.Lakini kama wewe umefanikiwa kufuta umanade kidogo sidhani kwamba swala hili linapashwa kukusumbua sana.Historia inatuambia kwamba watu wote asili yao ni maeneo ya Iraq.Usaambaaji ulianza baada ya kutoelewana kwa lugha wakati wanajenga mnara wa Babeli wakati huo.Waliokuwa wanaelewana wakaungana wakatengeneza kabila moja na huo ukawa hata mwanzo wa lugha na waka immigrate pamoja to various parts of the world.Kwa hiyo hata wewe na mimi tu wahamiaji Tanzania.

Kwa hiyo swala hapa sio Mkapa ni Mtanzania au sio, swala ni committment yake to developing the people of this country ambao wote ni wahamiaji anyway!

mimi hili linanitatiza, labda wenzangu mnalo jibu..wapo wanaosema kuwa rais mstaafu ni raia wa msumbiji na wala si mtanzania, eti aliingia kule kusini akiwa na umri wa miaka mitano wakati huo na baba yake.wapo wanaoangalia matendo yake na kuona ni ya ajabu ajabu.Kama tunakumbuka Mtikila kipindi kile alishawahi kusema kuwa bwana huyu si raia..tafadhali wale wenye kumbukumbu na ushaidi mzuri mtupatie.
 
mimi hili linanitatiza, labda wenzangu mnalo jibu..wapo wanaosema kuwa rais mstaafu ni raia wa msumbiji na wala si mtanzania, eti aliingia kule kusini akiwa na umri wa miaka mitano wakati huo na baba yake.wapo wanaoangalia matendo yake na kuona ni ya ajabu ajabu.Kama tunakumbuka Mtikila kipindi kile alishawahi kusema kuwa bwana huyu si raia..tafadhali wale wenye kumbukumbu na ushaidi mzuri mtupatie.

Mkapa ni M-Tanzania Halisi kama tulivyo wewe na Mimi.
 
Last edited:
Haya masuala ya watu wa makabila ya mipakani kuitwa sio watanzania halisi si jambo jipya hata kidogo na halipo kwa tanzania tu kwa sababu hata hao wamakonde unaosema sio watanzania wana wenzao kule msumbiji ambao wanashare language,na mambo mengine mengi tu ya kijamii but still makabila mengine ya msumbiji wanadai waliivamia msumbiji wakitokea tanzania hali kadhalika kenya,burundi,malawi,uganda kwa mfano kabila la msevenini watusi wa uganda na si wa rwanda na mifano mingi tu.

Cha msingi ni kuwa na ufahamu wa kutosha tu wa katiba ya nchi juu ya urai wa mtu na pia ujue kuwa raia wa nchi zote waishio mipakani mwa nchi moja na nyingine bsi huwa wanakua na mengi sana yanayofanana.

Ni hayo tu!
 
Laana ya kutaka kunyang'anya Ulimwengu uraia wake utamtafuna Mkapa daima,yeye pia ndio chanzo cha kuvurugika maadili nchini.
 
We NNaigwe we haya ya Che Nkappa kwamba ni raia wa nchumbiji umeyatoa wapi tena? mwache baba wa watu ajipumzikie,umechikiya? ukiendelea kufatilia uraia wake ntakuchoma nchale ukikwepa nakupiga achumani,umechikiya? kwanja weye uraia wako wa wapi,mbona njina yako kama ya.......................?
 
We NNaigwe we haya ya Che Nkappa kwamba ni raia wa nchumbiji umeyatoa wapi tena? mwache baba wa watu ajipumzikie,umechikiya? ukiendelea kufatilia uraia wake ntakuchoma nchale ukikwepa nakupiga achumani,umechikiya? kwanja weye uraia wako wa wapi,mbona njina yako kama ya.......................?

We Bishanga nini tena ,mambo gani hayo ya kutaka kupigana mishale tena,eeh?!!
 
So what? So are Schwzzeneger and Murdoch Ruppert are Austrians, so as Mtikila is South African, So is Abeid Karume is an Arab. Lazima tuache upuuzi ili tuwe watanzania.
 
Mbona Nyerere hujamquestion wakati anakili kabisa kwamba yeye ni mtutsi, kwa maana kiasili hakuna kabila la kizanaki, wazanaki ni neno tu walilokuwa wanaulizwa hao wahamiaji wa kutoka Rwanda kwamba wamekuja na nini hapo walipo sasa (Mara),
ukipekua sana hata wewe mtoa hoja ni Mganda
 
Doesn't make any difference nao. Mtu alisha kua raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Does it really make any difference now?
 
So what? So are Schwzzeneger and Murdoch Ruppert are Austrians, so as Mtikila is South African, So is Abeid Karume is an Arab. Lazima tuache upuuzi ili tuwe watanzania.

Point of correction. Arnold Shwazaneger is originally from Austria but Rupert Murdoch is originally from Australia. Just thought I would correct you for the sake of anyone who reads this forum to get knowledge.
 
Kuanza kutafuta asili ya watu ni jambo lililopitwa na wakati.Either Mkapa alizaliwa Tanzania au Msumbiji yeye ni mtanzania na vile vile sisi ndiyo tuliompa dhamana ya kuongoza nchii hii kama rais kwa miaka 10. Mbona sasa hivi Jaluo (Obama) anaongoza marekani.
 
Mi nadhani hoja ya jamaa si kumpokonya uraia. nia yake ni kuona kuna ukweli wowote kwenye madai haya.thats why kataka mwenye kumbukumbu ya tuhuma hizi amkumbushe. mbona watu mmeanza kuihusisha na urais? sijaona aliyejibu chochote,ukweli ni kwamba jamaa anataka akumbushwe. hukumbuki au hutaki kukumbushwa ok.lkn mwache jamaa akumbushwe.
 
Back
Top Bottom