Mkapa ni mnajimu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa ni mnajimu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mvaa Tai, May 12, 2011.

 1. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #1
  May 12, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,909
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Mwanzoni kabisa mwa utawala wa Kikwete (nasita kuweka neno Rais), vyombo vya habari vilimuandama sana Mkapa na kuandika kila kukicha maovu aliyoyafanya ikiwemo kashfa ya Kiwila, kila kukicha utasikia hili na lile kuhusiana na udhaifu wa utawala wa wake, ninaamini mengi yaliyokuwa yakisemwa dhidi yake yalikuwa ya kweli kwasababu hakuwahi kushtaki kwamba anasingiziwa na kushushiwa heshma yake bure, sana sana nakumbuka alisema "Watanzania mtanikumbuka" mmoja wa watu waliokasirishwa na kauli yake hiyo nilikuwa ni mimi maana sikuona tutamkumbuka kwa lipi? kumbe huyu mtu anaona mbali sana yeye binafsi utawala wake ulikuwa una madhaifu mengi tuu lakini aliweza kutabiri kwamba kipindi cha Kikwete hali itakuwa mbaya zaidi yatajitokeza mambo ambayo lazima tutamkumbuka hata kwa udhaifu wake, hebu fikiria yafuatayo katika utawala wa Mkapa.

  1. Kasi ya Mfumuko wa bei ilikuwaje? Na spidi ya kuanguka kwa shiringi dhidi ya fedha za kigeni ilikuwaje?
  2. Kasi ya ukuaji wa uchumi ilikuwaje?
  3. Ni mara ngapi uongozi wake ulikwenda kukopa katika mabenki ya biashara ili kughalamia shughuli za kawaida za serikali kutokana na serikali kutokuwa na pesa?
  4. Wakati gani serikali yake iliagiza kila wizara au mkoa ikate bajeti ya matumizi yake kwa zaidi ya 30% kutokana na kukosa uwezo?
  5. Deni la Taifa lilikuwaje?
  6. Kasi ya ongezeko la mapato ya serikali ilikuwaje? (hivi karibuni TRA wameshindwa kufikia lengo kwa zaidi ya 10?)
  7. Ni mara ngapi wananchi walijitokeza hadharani kupinga ugumu wa maisha?
  8. Ni miradi mingapi mikubwa ya maendeleo ilianzishwa katika kipindi chake?
  9. Kiwango cha ubabaishaji katika uteuzi kilikuwaje rejea "turnover" ya mawaziri.
  10. Katika sector ya michezo mkapa hakuwa karibu sana kama kikwete, lakini mkapa alijenga uwanja wa soka na baadaye Kikwete akamleta maximo na kula chakula cha jioni na timu ya taifa mara kadhaa.
  11. Ni kiasi ganii neno udini lilitamkwa hadharani aidha na yeye mwenyewe kama kiongozi wa nchi au wananchi.
  12. Mara ngapi alijitokeza hadharani kulumbana kisiasa kwa minajiri ya kujisafisha?

  Haya ni machache yanayonifanya nimkumbuke Mkapa nikilinganisha na yanayojitokeza ktka utawala Kikwete na yamenifanya niamini kwamba huyu mtu ni mnajimu alijuaje kwamba nitamkumbuka?
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  May 12, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,134
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Mnajimu? au elimu ya anga?
   
 3. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #3
  May 12, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 4,033
  Likes Received: 11,839
  Trophy Points: 280
  Kikwete katika awamu yake ya kwanza aliinjinia kutolewa kwa kashfa dhidi ya BWM na hapo kwenye red, ni kweli jamaa hakushitaki bali aliamua kukaa pembeni na hata wakati wa kampeni zilizomfanya JMK kurudi madarakani jamaa alikaa pembeni kabisa na ilibidi watumwe wazee kwenda kumwomba ashiriki kampeni (mmoja wa wazee ni kingunge) kwani upepo haukuwa upande wao.

  Nakuhakikishia kabisa kuwa aliposimama BWM pale jangwani wananchi waliisikia sauti yake na kukumbuka mazuri aliyowafanyia yanayojumuisha hayo uliyoyaainisha.

  Mkapa sio msafi lakini anabaki kuwa kiongozi makini aliyekuwa anaijua Tz na umaskini wake na hivyo akajitoa kuiba huku akirahisisha maisha kwa mtz wa hali ya chini
   
 4. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #4
  May 12, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,273
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Mh Rais Mkapa ninakukumbuka sana!Hii awamu ya nne inaongozwa na marais watatu(RA, EL na JK) na kila mtu ana mawaziri wake sasa ndio matatizo tulionayo!
   
 5. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 1,810
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Ilikua rahisi kwa Rais wa tatu kutabiri kinachokuja kwani alimfahamu ajaye nyuma yake (rais wa nne) ana uwezo gani kiutendaji kwani aliufahamu utendaji wake kwa miaka kumi aliyofanya kazi chini yake kama waziri wa mambo ya nchi za nje. Kama asingelazimishwa na nguvu ya 'Mtandao' iliyokuwepo kuna kila dalili ya kuamini kwamba 'kijiti' kingekwenda kwa mtu mwingine kabisa.
   
 6. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa mkuu Hilo halina ubishi, BWM alikuwa mtaalamu na kukaa kimya kwake ilkuwa nibusara. Si unajua wahenga walisema "don't argue with a fool people might not distinguish who is a fool between you". Kwa vile BWM alijua aliyowafanyia watanzania ni makubwa, lakini akaona hizo cheap media mudslinging campain zilizoanzishwa na wanasiasa wasio makini akaona akae kimya. Nakuhakikishia ktk miaka 4 ya awamu ya JK iliyobakia mengi mutayaona yatakayo waumiza kiuchumi
   
 7. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 160
  Mi ntamkumbuka zaidi ndugu yangu,****** mwenzagu alhaj alfan jmk, kwa kuniletea machungu ya maisha na kuufanya ubongo wangu ufikirie kama kesho itafika! Namshukuru mkapa kwa kunipa mazingira tulivu na ktk kipind chake nliweza kupiga miayo kijanja na si kama siku izi ambapo tumbo na mgongo viko zero distance kwa kukosa kitenganishi(mkate/chakula ). Jk ntakukumbuka daima kwa kuifanya akili yangu iwaze itaishije leo na si kuwaza ntafanyeje ili taifa letu listawi!
   
 8. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Kwanini Mkapa hakusimama ahesabiwe akiwa na msimamo wake? nashindwa amini unajimu wake mbali na kuwa alikuwa anatuambia kuwa tunamwona yeye ni mchafu ila ajaye tutakoma! je hapo alitutakia mazuri?
   
 9. Mwana CCM.

  Mwana CCM. Member

  #9
  May 12, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nitamkumbuka Mkapa kwa kujenga Uwanja wa mpira wa kisasa, na pia nitamkumbuka Kikwete kwa kujenga chuo kikuu cha Dodoma(UDOM)
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,134
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Mi ntamkumbuka shehe yahaya
   
 11. Binti Magufuli

  Binti Magufuli JF-Expert Member

  #11
  May 12, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 7,372
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Jamani "Mkweeeri" toka lini??? Babu wa taifa alishaliona mapeeema, mtu ana experience ya kucheza ngoma na utawala wapi na wapi......c makosa yake. Makosa ni ya wadanganyika waliomchagua kwa kuuza kura (maendeleo yao) kwa ku-exchange na kanga na kofia.
   
 12. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #12
  May 12, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,641
  Likes Received: 2,549
  Trophy Points: 280
  Mganga/kigagula wa ccm aliwatapeli kuwa Mkweree ndio chaguo la watz! Inawezekana na nao walimdhurumu akageuza ungo!!!
   
 13. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #13
  May 12, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mwaka 1995 Kikwete aliposhinda raundi ya kwanza Nyerere alisema 'bado mdogo' wakati umri wa kikwete wakati huo ni mkubwa kuliko umri wa Nyerere wakati anaukwaa urais 1961. Watu hawakumwelewa Nyerere kuwa alimaanisha Kikwete hawezi urais kistaarabu. Leo ndo tunajua ukweli kile alichokimaanisha Nyerere kuwa ni Kikwete hawezi kuwa Rais tatizo halikuwa umri.
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  May 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Udogo wa ubongo,kufikiri na kufanya maamuzi....si umri
   
 15. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #15
  May 12, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,140
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  silence is the best noise one can make...........mkapa ni kiongozi shupavu sana.......sio kama huyu mwizi, mtoto mwizi na sasa amemfundisha mkewe wizi ( rejea ile hundi feki)
   
 16. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #16
  May 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkapa kichwa bwana
   
 17. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #17
  May 12, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wote yale yale tu...

  si ni mkapa huyuhuyu juzi aliita wapinzani wa tanzania ni kokoto?
   
 18. Kirode

  Kirode JF-Expert Member

  #18
  May 12, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 3,575
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kihwa akajiuzia mali ya uma kwa bei poa ref,kiwira nbc nk.
   
 19. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #19
  May 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sasa si hiyo ni siasa, kila mwanasiasa anavutia kwenye chama chake. Wewe unatarajia Dr. Slaa awasifie CCM?
   
 20. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #20
  May 12, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Umeambiwa anamapungufu yake lakini hayawezi kulinganishwa na yuleeeeeeeeeee
   
Loading...