Mkapa na Kikwete Walidanganywa na Wakadanganyika!, Magufuli Anadanganywa!, Jee Atadanganyika?

Bora umerudi Mkuu....kwa hiyo yale mapendekezo yalipokewa jana pale getini badala ya ndani ya bunge Serikali haibanwi kwa lolote kwenye utekelezaji wake?

Kwa hiyo Magufuli atakachokifanya ni kuchagua vifungu atakavyovutiwa navyo kufanyia kazi.

Hata ile ripoti yote akiamua kuitekeleza kabatini ni yeye, hakuna kifungu kinachombana.

Hivi kamati za bunge hufanya kazi za kibunge au serikali.?

Lini Rais amewahi kuunda tume, mapendekezo yake yakapelekwa bungeni.....?

Kwa nini tunafika hatua ya kumwamini mtu binafsi badala ya mfumo.?
Kuna mtu alikuwa anatibiwa India huku akilala 5 star hotel, hana ubavu wa kutunishiana msuli na jiwe hana usafi huo.

Tatizo la Tanzania ni ccm, kwingine kote tunazunguka, nadhani umemsikia msomi Bashiru ameweka wazi yeye sasa hivi hawezi kuongelea katiba mpya. Utaratibu ni uleule si vizuri kuongea ukiwa mezani unakula.

Ndugai anaijuwa vyema kazi yake ila ukumbuke yupo mezani kwa bwana kwenye kalamu.
 
Umeandika As If Mheshimiwa huyu tumemkodisha toka Ujerumani kumbe Na yeye Ni Mtanzania kama hawa wote unaowatukana kuwa Ni wezi.

Mwenye kuelewa Na aelewe.
Na wewe ni mmoja wa hao wezi. Mnakodisha watu kwenye mitandao. Mh. Ni mzalendo kindakinda ndio maana mnaweweseka
 
tulitajiwa matarakimu ya futi za ujazo ya gesi asilia niambie leo km kuna mahali utasikia gesi ikitajwa tena. kimyaaaaaa hadi milele.
 
Wanabodi,
Tunachosikia na ndicho kitakachotokea ni mazungumzo ya kitu kinachoitwa amicable settlement ya a win win situation, kwa sisi kulambishwa asali kidogo, Acacia wapewe Mchanga wao, tuendelee kuibiwa!. Time will tell!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
[/SIZE]
Wanabodi, mimi mwenzenu mtanisamehe bure, nahisi kama hiki ndicho kinakwenda kutokea...
Tusubiri taarifa rasmi ya makubaliano ya mwisho ya mazungumzo na Barrick, ila mazungumzo yamemalizika wamefikia makubaliano ya mwisho zile fedha za goodwill, sasa ndio kifuta machozi!.

Kuna kitu nilikisema hapa kuhusu kudanganywa na kudanganyika,
Tunapigwa!.

Kwa vile details za makubaliano hayo bado hayatangazwa rasmi, there is still room kuzuia Tusidanganyike na tusipigwe tena.

P
 
Dalili kuwa kuna watu walidanganya na kuna watu walidanganyika, zimeisha anza kujionyesha, kwa sababu tayari tumeisha samehe lile deni lote la dola bilioni 190 za Acacia, hivyo tutakapoelezwa the basis ya kusamehe zote, nitarejea kuwaeleza nani muongo, nani kadanganya, kadanganya wapi kwenye nini, nani kadanganyika, kadanganyika wapi na kivipi, hivyo next time tutauheshimu ukweli.
P
 
Wanabodi,
Angalizo!.
Wanabodi, naomba kuanza na angalizo hili kuwa hii ni thread ya swali, maana watu humu, tunatofautiana sana uelewa, mtu unaweka alama ya kuuliza, msomaji haioni, , akaona thread imeandikwa fulani amedanganywa!. Hapa nimewataja waliodanganywa na kudanganyika, na kwa vile wadanganyaji bado wapo na wanaendelea kudanganya, swali ni kwa wanaodanganywa, jee nao wataendelea kudanganywa na kudanganyika ili hali wameelezwa bayana kuwa wanadanganywa?.

Ni Kwa Kutokujua, Tulidanganywa, Tukadangayika, Jee Sasa Tunajua Ili Tusidanganywe?.
Katika suala zima za kuibiwa kwa rasilimali zetu, kupitia mikataba mibovu ya kinyonyaji ambayo ni wizi mtupu wa mchana kweupe, vita vya kupambana na rushwa kubwa "the grand corruption na vita dhidi ya ufisadi na uhujumu uchumi, marais wamekuwa wakidanganywa na kudanganyika, hivyo tunapigwa. Kwenye hili sakata la mchanga wa makinikia wa Acacia, rais Magufuli tayari kadanganywa, swali linabaki jee atadanganyika?.

Naomba nisizungumze kuhusu awamu ya Nyerere na Mwinyi, mimi bado nilikuwa mdogo, lakini awamu ya Mkapa, Kikwete na hii ya Magufuli, mimi ni mtu mzima ninayejielewa, hivyo nazungumza vitu nilivyovishuhudia vikitokea na sio vitu vya kuambiwa.

Kwenye mikataba ya madini, na manunuzi makubwa, Mkapa alidanganywa sana tuu na akadanganyika, tukaibiwa sana kwa kupigwa kwenye madini yetu na tunaendelea kuibiwa mpaka kesho, kupitia sheria mbovu, Kikwete nae pia kwenye mikataba ya Umeme, gesi asili, na manunuzi makubwa, alidanganywa na akadanganyika, hivyo pia tukapigwa na tukaibiwa sana na tunaendelea kuibiwa kupitia mikataba hii mibovu ya kinyonyaji, huku rushwa kubwa kubwa, the grand corruption na ufisadi mkubwa vikishamiri. Yote haya yaliweza kufanyika na kufanikiwa kutokana na kutokujua kwetu!. Sasa ili haya yasiendelee kufanyika, lazima kwanza mambo matatu makubwa yafanyike.
1. Kwanza tuwe na uwezo wa kujua kuwa tunadanganywa.
2. Tuwe na uwezo wa kutokubali Kudanganywa, na
3. Tukidanganywa, Tuwe na Uwezo wa Kuzuia Tusidanganyike!.

Rais Magufuli tangu alipoingia, akatangaza kupambana na rushwa na ufisadi, na alipoanza, alianza kwa kasi kubwa, zile tumbua tumbua za mwanzo na ziara za kushtukiza za mwanzo, ziliamsha amsha, ilikuwa ni hakuna kulala!, kumbe ilikuwa ni nguvu ya soda tuu, lakini kadri siku zinavyokwenda, spidi inazidi kupungua kidogo kidogo, zile shtukiza na amsha amsha za mwanzo, sasa zimetulia au hazipo tena!, kilichobaki sasa sio tena ziara za kushtukiza kweli kama mwanzo, bali sasa naona kama yanafanyika maigizo ya ziara za kushtukiza!, au labda ni mimi tuu ndio naona kama ni maigizo, lakini in reality ya ukweli wenyewe bado ni
ziara za kushtukiza.

Walidanganywa, Wakadanganyika!. Sasa Anadanganywa, Jee Atadanganyika?.
Kwa vile watangulizi wake walidanganywa na wakadanganyika na kuzidi kulizamisha taifa letu kwenye lindi la umasikini huu unaondelea hadi sasa, huku tukibebeshwa mzigo mkubwa wa madeni, sasa kuna kila dalili kuwa hata rais Magufuli naye naona kama vile ameanza kudanyanywa na mifano nitatoa!, Ila pia sio naona kama ameanza Kudanganywa tuu, bali naona kama ameanza kudanganyika!.

Kipimo kuwa rais Magufuli anadanganywa hakina mjadala, kwa sababu ya documentary evidence ya data's , wataalamu wanasema numbers don't lie, rais kadanganywa in numbers na kadanyika, kipimo cha taifa letu kujua kuwa rais wetu kadanganywa na kudanganyika, tutakipima kwa matokeo, results oriented outcomes za baadhi ya mipango mkakati yetu ya mendeleo ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu katika sekta muhimu za uchumi wetu, ikiwemo sekta nyeti ya madini, mimi nikijikita kwenye specific hili la makinikia ya Acacia, ununuzi wa ndege na ujenzi wa miundo mbinu mikubwa Kama SGR kwa mtindo wa zimamoto huku tukiambiwa ni fedha za ndani lakini muda sii mrefu tutashuhudia hata yeye atatuingiza Tanzania kama taifa kwenye mzigo mkubwa madeni kwa taifa letu kutokana na makosa fulani fulani ya kiutendaji, kama ilivyotokea kwa watangulizi wake na zaidi!, ila hili la taifa kubebeshwa mzigo wa madeni, linaweza lisizungumzwe sana sasa kutokana na kutokuwepo transparency ya ni lini serikali yetu huwa inakopa fedha, inakopa wapi, kiasi gani, kwa riba gani, na fedha hizo zinazokopwa ni fedha zinakopwa kufanyia nini?. Haya yote hatutayajua kwa sababu huwa serikali zetu hazina utamaduni wa transparency kwenye deni la taifa lakini kitakacho kuja kuonekana na kujulikana baadaye ni kutuna tuu kwa deni la taifa kwenye Ripoti ya CAG, watu watashangaa tuu deni la taifa linazidi kukua na kutuna, lakini tunakopa fedha za kufanyia nini, huwa hatuambiwi, Bunge letu sio tuu haliambiwi!, bali hata kuombwa kuidhinisha hayo matumizi, haliombwi!, itakuja tuu taarifa ya kuongezeka kwa deni la taifa ndani ya taarifa ya GAC. Bunge ambalo moja ya majukumu yake ni kuisimamia Serikali ikiwemo kuhakikisha matumizi yote ya fedha za umma, lazima yafuate sheria, taratibu na kanuni, ikiwemo kuidhinishwa na Bunge, lakini katika ripoti ya CAG, kila mwaka tunashuhudia Serikali yetu ikifanya matumizi makubwa yasiyo ya dharura bila kuidhinishwa na Bunge,
sasa unajiuliza, huu usimamizi wa Bunge kuisimamia serikali ndio usimamizi gani?, ukisema Bunge ni dhaifu katika kuisimamia serikali, utakuwa umelikosea, au tukisema Bunge halitimizi wajibu wake kikamilifu tutakuwa tunalionea au kulidhalilisha?.

Mfano Hai ni Suala la Makinikia ya Acacia Mining
Swali ni jee baada ya rais Magufuli kushtukia kuwa tunadanganywa kwenye makinikia, jee naye yeye ataendelea kudanganyika kama watangulizi wake?, au yeye atabadilisha sheria ili tusiendelee kudanganywa?. Na jee Watanzania wazalendo wa taifa hili, wenye insight, mnapoona rais wetu anadanganywa, wazi wazi mchana kweupe tena mbele ya kadamnasi ya watu na mnajua kabisa kuwa hapa rais wetu anapigwa kamba, anadanganywa, jee mtanyamaza tuu na kumuachia rais wetu aendelee tuu kudanganywa na watu waliomzunguka, kwa sababu yeye ndiye mkuu wa nchi anayepaswa kujua kila kitu kama malaika?, au tutapaza sauti zetu kumgutusha rais wetu kuwa kwenye hili, hapa Mhe. rais wetu unadanganywa?. Hiki ndicho ninachokifanya kwenye bandiko hili.

Mwanzo nilikuwa sina uhakika kwanza kama Magufuli anadanganyika, au kama atakubali kudanganywa kwenye mikataba, kama Mkapa na Kikwete. Ila kama nilivyosema mwanzo na yeye ni binadamu na sio malaika, hivyo anaweza akadanganywa na akadanganyika, lakini Watanzania wazalendo wenye uoni mkubwa, wenye uwezo wa kuona kuwa hapa rais wetu anadanganywa!, tusikubali rais wetu adanganywe, na akidanganywa, tusikubali adanganyike, kwa kumweleza wazi kuwa hapa mhe. rais unadanganywa!, ili ikitokea, akadanganywa na akadanganyika iwe ni yeye tuu kwa ubinaadamu wake, amekubali kudanganywa na kudanganyika, lakini sisi Watanzania wengine wazalendo, kamwe tusikubali rais wetu kudanganywa na kudanganyika!.

Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, wajameni kiukweli kabisa, rais wetu amedanganywa mchana kweupe, na masikini rais wetu tayari ameishadanganyika kupitia ripoti ya makinikia, imemdanganya rais wetu kuwa Tanzania ndio inchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi nyingine yoyote lakini dhahabu hiyo imekuwa ikiibiwa kupitia mchanga wa dhahabu!, uongo huu ni kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu vilivyokokotolewa na tume yake kwenye makinikia yaliyomo ndani ya makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia, nashauri tusilinyamazie hili, tuungane na rais wetu katika kutafuta ukweli hakika na bayana kwa maslahi mapana zaidi ya taifa letu.

Hapa nimesema rais amedanywa na akadanganyika kwa sababu sii kweli kuwa Tanzania ndie mzalishaji mkubwa kabisa wa dhahabu duniani, hata tungekuwa tunaibiwa vipi, tungeibiwa viwango vya ndani lakini hiyo dhahabu inayoingia kwenye soko la dunia, ingeonyesha wazi kabisa kuwa inatoka Tanzania!. Ni kama ilivyo kwa Tanzanite, japo Tanzania ndio mzalishaji pekee wa Tanzanite duniani, anayeongoza kuuza Tanzanite ni India, Afrika Kusini halafu ndio Tanzania. Unless wathibitishe kwa ushahidi usiotia Shaka kuwa kuwa Tanzania ndio inaongoza kuzalisha dhahabu duniani, lakini dhahabu hiyo hairekodiwi kuonyesha inatoka Tanzania, hivyo dhahabu hiyo inaibiwa kupitia makinikia, na kuingizwa kwenye soko la dunia ikiandamana na certificates of origin za kutokea nchi nyingine!, hivyo hairekodiwa na WB na haionyeshi kuwa inatoka Tanzania, hivyo kwenye records Tanzania ndio ilipaswa kuwa ndio inaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani kitu ambacho sii kweli. Kitu cha kwanza kwenye international business ya bidhaa ni certificates of origin, unless wathibishe kuwa ni kweli Tanzania ndio ya kwanza ila tumekuwa tukiigwa na kuwa biwa dhahabu yetu!.

Hii maana yake ni kuwa kwenye ripoti za tume ya makinikia, rais wetu amedanganywa kiasi cha dhahabu kilichomo, na kupitia uongo huo, TRA ikatoa deni la ajabu la dola bilioni 191 kwa Acacia ambalo kiukweli kabisa, halilipiki!, ukweli wa uongo huu utajulikana pale tuu, tutakapouchenjua wenyewe Mchanga unaoshikiliwa katika makontena 277 tunayoyashikilia na kuuthibitisha sio ukweli wa tunachoibiwa bali uongo wa tume ya rais ya makinikia!.

Ukweli huu kuwa rais wetu amedanganywa kiwango cha dhahabu kilichopo ndani ya makinikia, utabainika only if kama sisi wenyewe kama nchi na ndio wenye mchanga, tutauchenjua wenyewe mchanga huo na kuthibitisha kilichomo kwa kuzianika mbichi na mbivu!, lakini kwa vile waliomdanganya rais, pia wanajua kuwa wamemdanganya, ili kumpa rais ripoti ya kile anachopenda kusikia kuwa tunaibiwa, watahakikisha, hakuna juhudi zozote za kuuchenjua mchanga huo, ili kilichomo kisijulikane!, na kwa mahesabu ya Acacia, hana the capacity kulipia kiasi hicho tunachowadai ambacho hadi sasa sio cha kweli na sio cha uongo hadi verification ifanyike na kiukweli sijasikia juhudi zozote kuutafuta ukweli kupitia verification!,

Tunachosikia na ndicho kitakachotokea ni mazungumzo ya kitu kinachoitwa amicable settlement ya a win win situation, kwa sisi kulambishwa asali kidogo, Acacia wapewe Mchanga wao, tuendelee kuibiwa!. Time will tell!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Paskali kwenye mchanga bila shaka tulikuwa tunapigwa boss wangu.

Mwaka 2001 nikiwa nilifanikiwa kufika Buly kutafuta fursa ya kupata japo kibarua wakati nasubiri matokeo ya kidato cha 6.
Niligadi kwa miezi 4 na kila siku nilikuwa nikisogea getini walau kuona fursa ya kuwa underground miner inaweza kupatikana.
My observation wakati huo; mara 2 week gari za mchanga zilikuwa zinatoka mgodini Buly na full escort kwenda Tanga.
Mbele gari ya KK seurity na wana askari wa bunduki hali kadhali nyuma kuna askari wenye bunduki.

Swali; nani ni mjinga kila week atoe mchanga toka Kahama to Japan via Tanga port?
Kwanini kupeleka Japan na sio kufanyia ndani?
Toka miaka hiyo ya late '90 mpaka JPM anaingia 2015 hawakuwa wameona cost benefit analysis ni bora kuchakata ndani; wao waliona Japan tu??
Kama si kitu cha thamani kwanini askari wa bunduki?
Kwanini walikubali mazungumzo na kulipa kishika uchumba cha $ mil 300 kama hawakuwa wamekosea kabisa?

By the way ni wazungu hawa hawa wanasemaga Tanzania ni maskini wakati tunanunua ndege mpya kwa cash.
Ni wazungu hawa hawa wakitudai wanatupeleka mahakamani. Unawezaje kumpeleka mahakamani masikini ambae hana uwezo wa kulipa??

Mzungu bana si wa kumwamini sana. Kwa wale ambao tumefanikiwa kufanya kazi nao; they always very smart in hiding what is of beneficial especially in creating wealth.

Anyway.
I hope JPM hatadanganywa kama waliomzunguka sio wapigaji. Kama kuna walaji, basi ipo siku somewhere watatafuta fursa ya kupiga. Kumbuka hadithi ya ndege ya rais waliyopewa ATC kupakwa rangi, bei waliyotoa watathmini na kama ingepelekwa "bondeni" hapo napo mzee asingeshtuka wangepiga mpunga mchana peupe

These are my
 
Wanabodi,
Tunachosikia na ndicho kitakachotokea ni mazungumzo ya kitu kinachoitwa amicable settlement ya a win win situation, kwa sisi kulambishwa asali kidogo, Acacia wapewe Mchanga wao, tuendelee kuibiwa!. Time will tell!.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Wakati tukisubiri kupata details za kilichosainiwa, pia tuanze kufanya rejea za tulisema nini, tulishauri nini, na nini kilichotokea. Kama tuliuzuia mchanga kwasababu tunaibiwa kwa kutojua kilichomo, tukatunga sheria mchanga hauondoki, tutauchenjua tujue kilichopo, kama sasa mchanga unaendelea kuondoka kwenda kuchenjuliwa kule kule bila sisi kujua kilichomo, mwanzo tuliuzuia huo mchanga ili iweje?
P
 
Hadanganyiki.

Na hizo za kushtukiza usiseme spidi imepungua bali sema hajamua, ana uwezo wa kuzifanya dakika yoyote anapoamua. Ila zimesaidia sana kwa asilimia kubwa. Mabadiliko ya watendaji wa kazi yanaonekana, na bado watazidi kunyooshwa.

Hapa kazi tu

Magudfuli 2020
Unajifariji tuu sababu ya umaskini wako.hakuna nafuu yoyote kwa mlalahoi.unga 1800/=sukari 3000/=hospital dawa hakuna,elimu bure hakuna walimu wa sayansi.huduma gani iliyoboreshwa??mahakamani kabendera ndani,lugola anachunguzwa.wapi na wapi???
 
Katika uongozi, kuna kanuni moja ya kumlinda mkubwa inaitwa "plausible deniability".

Plausible deniability ni watu walio karibu na mkubwa, kufanya mambo na mkubwa katika namna ambayo, wakishtukiwa baadaye, mkubwa anaweza kujitetea kwamba hakujua, alidanganywa etc.

Kwa mfano, mkubwa anaweza kukubali mambo kwa maneno tu, bila kuweka saini kokote wala kuwa na nyaraka zinazoonesha kukubali huko.

Sasa kama Mkapa na Kikwete walishiriki haya mambo, ila kwa kutumia "plausible deniability", na sasa wanakataa kwa kusema walidanganywa na hawakujua, sisi tutajuaje?

Nimetoka kusoma kitabu kipya cha Mkapa, alivyoelezea kuhusu EPA, ameelezea kitoto sana, kama kadanganywa kijinga.

That is not the Mkapa I know.
 
Acha kujitoa iufaham hio ngoma ingekuwa nyepesi kama unavyofikiri wala isingekesha kwa 2 years kwenye deadlock.

We si ni mwandishi makini?

Mbona hutaki kuhoji au kuandika chochote kwanini Barrick walikubali kusign deal siku moja iliyofuatia baada ya kampuni 3 za wawekezaji wa madini zilipo declare kwenda mahakama ya kimataifa kupinga sheria mpya ya madini?.

Kwanini Barrick wasingepotezea GoT tuu ili na wao pia wakajiunge na wenzao huko mahakamani?

Huoni kuwa mahakama zote zitatumika makubaliano ya Barrick na GoT kama ndio mfano bora wa kuendesha shughuli za uwekezaji wa madini si kwa TZ tu bali ktk nchi zozote za third world zenye migogoro na multinationals Mining companies like Barick?

Umeshsambiwa badili mindset, kila kinachouzwa sasa ni chetu sote kupitia Twiga Mining Co. mskinikia yakiwemo pamoja na vingine vyote tutakavyouza huko mbeleni..

Hii ni hatua kubwa sana na historia ktk Afrika, ni Botswana pekee kwa diamond pamoja na jamii ya watu wa jimbo la North West kule SA kwa platinum ndio waliofanikiwa kuwa na mikataba yenye ufanano kidogo na huu wa Barrick na GoT.

Ni suala la mda tu makubaliano hayo yatakuwa ndio mwanzo wa makubaliano mapya na na makampuni yote ya wawekezaji ktk sekta ya madini nchini.

Neema ya kweli ya marndeleo itaanza kuonekana kwa jamii zinazo zunguka maeneo yenye madini kama vile kanda ya ziwa, Chunya, Kaskazini, Morogoro, Kusini etc...
Wakati tukisubiri kupata details za kilichosainiwa, pia tuanze kufanya rejea za tulisema nini, tulishauri nini, na nini kilichotokea. Kama tuliuzuia mchanga kwasababu tunaibiwa kwa kutojua kilichomo, tukatunga sheria mchanga hauondoki, tutauchenjua tujue kilichopo, kama sasa mchanga unaendelea kuondoka kwenda kuchenjuliwa kule kule bila sisi kujua kilichomo, mwanzo tuliuzuia huo mchanga ili iweje?
P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kujitoa iufaham hio ngoma ingekuwa nyepesi kama unavyofikiri wala isingekesha kwa 2 years kwenye deadlock.

We si ni mwandishi makini?

Mbona hutaki kuhoji au kuandika chochote kwanini Barrick walikubali kusign deal siku moja iliyofuatia baada ya kampuni 3 za wawekezaji wa madini zilipo declare kwenda mahakama ya kimataifa kupinga sheria mpya ya madini?.

Kwanini Barrick wasingepotezea GoT tuu ili na wao pia wakajiunge na wenzao huko mahakamani?

Huoni kuwa mahakama zote zitatumika makubaliano ya Barrick na GoT kama ndio mfano bora wa kuendesha shughuli za uwekezaji wa madini si kwa TZ tu bali ktk nchi zozote za third world zenye migogoro na multinationals Mining companies like Barick?
Mkuu Bantogbro, majadiliano yoyote yenye afya ni majadiliano yenye hoja, jee wajua sheria mpya ya madini inasema nini kuhusu utatuzi wa migogoro?.
Soma hapa
1580450266483.png

Jee kilichosainiwa katika mikaba hiyo ni hiki?. Hiki ndicho sheria yetu inachosema, kusaini mkataba wowote wa madini bila kipengele hiki mkataba huo ni illegal, jee wewe mwenzetu unakijua kilichosainiwa?.
Mimi nasubiri kukiona kilicho sainiwa ndipo tuje tujadili.

Hoja za bandiko hili ni rais wetu kudanganywa na kudanganyika. Toka sakata hili limeanza wewe bado hujajua rais kadanganywa wapi?.
P
 
msambaa1, Nadharia yako ni nzuri sana lakini kiuhalisia hutafanikiwa kama unavyofikiria.

Serikali ya Indonesia walijenga concentrate smelter kwa $700m. Imefungwa na haikuwahi kutengeneza faida yoyote. Concentrates zimerudi kusafirishwa nje.

Kwanza hii smelter siyo kama zile smelter za single mineral commodity. Hii ni smelter aghali. Lakini ujue kuwa anayesafirisha concentrates siyo Barrick bali ni mnunuzi. Concentrates zinajulikana zina kiasi gani cha madini yenye thamani ya kibiashara. Mnunuzi analipa kisha anaamua yeye akachenjulie wapi. Mnunuzi hawezi kupeleka tu kwa mchenjuaji yeyote bali kwa yule ambaye anamwamini na ana mkataba naye. Utajenga plant yako Tanzania lakini concentrates toka Zambia na DRC zitaendelea kwenda Japan.

Pamoja na teknolojia waliyo nayo US na Canada, bado wanapeleka concentrates Japan.

Kuamini kuwa tunaibiwa kupitia concentrates ni ujinga na mawazo ya kimaskini kutoka kwa watu waliotopea kwenye ujinga wa taaluma.

Concentrates zinapimwa na certified laboratories zilizosajiliwa na taasisi za kimataifa na masoko ya hisa Duniani. Reports zao ni legal documents ambapo kama wamedanganya, upande wowote ule yaani Serikali, mnunuzi na muuzaji anaweza kuishtaki maabara, na hilo litakuwa janga kubwa kwa hiyo maabara maana itazuiwa kufanya kazi hiyo mahali popote Duniani, na kulipishwa gharama kubwa ya kifedha kuanzia mteja aliyeathirika mpaka na wanahisa waliouza au kununua hisia kwa kutegemea taarifa za maabara hiyo.

Maabara hizi zinafanya kazi hii Dunia nzima. Kule hakuna watu wapu.mbavu eti watoe report za uwongo, halafu waondolewe kwenye biashara Duniani nzima. Hizi maabara siyo zile za akina Mruma za pale Dodoma ambazo instrument inasoma 200g per ton, wanasema andika kilo 200 per ton.

Watanzania amkeni. Jielimishe msipende kulishwa ujinga nanyi mkauchukua ujinga mzobemzobe, kwa vile tu mmelishwa ujinga na watawala.

Kwa uhakika wa 100% hakuna chochote tulichokuwa tunaibiwa kupitia makinikia. Ujinga wa Watanzania wengi unawafanya watawala kuwalisha uwongo mwingi kwa kujua kuwa watanzania watameza taarifa wanazopewa kama zilivyo.

Taarifa zile za kijinga za akina Mruma, leo kwa aibu zimetupwa kwenye mashimo ya takataka kiasi cha kushindwa kuamini kuwa kazi ile eti ilifanywa na maprofesa! Report ile hata mwanafunzi wa Geology wa mwaka wa 2 angeweza kujua bila shaka kuwa ulikuwa ujinga mtupu. Maana viliandikwa vitu ambavyo havijawahi kuwepo tangu Ulimwengu uwepo.
Mkuu Bams, watu kama nyinyi ndio mnatakiwa pale Ikulu kumsaidia rais Magufuli na kuisaidia serikali yetu. Nimekileta hapa kwasababu kuna kitu umekisema katika posti yako hiyo na mimi nilikisema katika bandiko hili.

Rais Magufuli amedanganywa kiwango cha dhahabu kwenye makinikia kwa lengo la kumfurahisha rais kuwa he did the right thing kuuzuia mchanga usitoke.

kufuatia uongo huo, TRA nao wakatoa tax bill ya ajabu!.

Matokeo ya mwisho, mchanga haujapembuliwa, bill ya uongo imetupwa kule, sasa mchanga unaondoka tena bila kuchenjuliwa wala Watanzania kujua kilichomo.

Tumesamehe tax bill yetu ya $ 190n kimya kimya bila Watanzania kuelezwa why?, maana itajulikana rais amedanganywa!.

Nasubiria kuona kilichosaniniwa ndipo niibuke na kusema for sure kuwa rais wetu Magufuli alidanganywa na akadangayika, waliomdanganya ni nani, wamemdanganya nini na matokeo ya udanganyifu huo, bandiko hili linaendelea...

Paskali umeongea suala la maana sana.
Hatuna tatizo na professorial research za wasomi wetu kama akina Mruma. Ila kuna wakati ambapo iko haja ya kuchukua tafiti zao na kuziweka kwenye mizania ya business model.
Mathalani, kama tunaibiwa/tulikuwa tunaibiwa, what can be the best practised business model ambayo kama tukiweka into practice tutauza final product.

Naomba kuweka wazi, mwaka jana katika hotuba za PM, kwenye agro-sector kuna mahali PM Majaliwa alikuwa mislead. Model ya alichotoa kwenye hotuba yake model ile haipo applicable kwenye ulimwemngu wa sasa.

Suala ni namna gani wadau wengine nje ya circle ya #1 au #3 wanaweza kumpa mbadala ili kuwa na comparative analysis which strategy can make us arrive to the promise land earlier and with more outcome in term of earnings.

I am saying with boldness, kuna watu yet hawajapewa platform ya kufanya mashauriano na wakubwa. Bahati nzuri, it always begin with leadership.
Toka mbingu na nchi zinaumbwa, ili mambo yakae sawa, install right leadership, ambayo kwa sasa tunayo. Ila kwenye strategy, oohh ee Mola tusaidie
 
Wanabodi,
Rais Magufuli Amedanganywa Kiwango cha Dhahabu Kwenye Makinikia
Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, wajameni kiukweli kabisa, rais wetu amedanganywa mchana kweupe, na masikini rais wetu tayari ameishadanganyika kupitia ripoti ya makinikia, imemdanganya rais wetu kuwa Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi nyingine yoyote lakini dhahabu hiyo imekuwa ikiibiwa kupitia mchanga wa dhahabu!, uongo huu ni kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu vilivyokokotolewa na tume yake kwenye makinikia yaliyomo ndani ya makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia, nashauri tusilinyamazie hili, tuungane na rais wetu katika kutafuta ukweli hakika na bayana kwa maslahi mapana zaidi ya taifa letu.

Hapa nimesema rais amedanywa na akadanganyika kwa sababu sii kweli kuwa Tanzania ndie mzalishaji mkubwa kabisa wa dhahabu duniani, hata tungekuwa tunaibiwa vipi, tungeibiwa viwango vya ndani lakini hiyo dhahabu inayoingia kwenye soko la dunia, ingeonyesha wazi kabisa kuwa inatoka Tanzania!. Ni kama ilivyo kwa Tanzanite, japo Tanzania ndio mzalishaji pekee wa Tanzanite duniani, anayeongoza kuuza Tanzanite ni India, Afrika Kusini halafu ndio Tanzania. Unless wathibitishe kwa ushahidi usiotia Shaka kuwa kuwa Tanzania ndio inaongoza kuzalisha dhahabu duniani, lakini dhahabu hiyo hairekodiwi kuonyesha inatoka Tanzania, hivyo dhahabu hiyo inaibiwa kupitia makinikia, na kuingizwa kwenye soko la dunia ikiandamana na certificates of origin za kutokea nchi nyingine!, hivyo hairekodiwa na WB na haionyeshi kuwa inatoka Tanzania, hivyo kwenye records Tanzania ndio ilipaswa kuwa ndio inaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani kitu ambacho sii kweli. Kitu cha kwanza kwenye international business ya bidhaa ni certificates of origin, unless wathibishe kuwa ni kweli Tanzania ndio ya kwanza ila tumekuwa tukiigwa na kuwa biwa dhahabu yetu!.

Hii maana yake ni kuwa kwenye ripoti za tume ya makinikia, rais wetu amedanganywa kiasi cha dhahabu kilichomo, na kupitia uongo huo, TRA ikatoa deni la ajabu la dola bilioni 191 kwa Acacia ambalo kiukweli kabisa, halilipiki!, ukweli wa uongo huu utajulikana pale tuu, tutakapouchenjua wenyewe Mchanga unaoshikiliwa katika makontena 277 tunayoyashikilia na kuuthibitisha sio ukweli wa tunachoibiwa bali uongo wa tume ya rais ya makinikia!.
Paskali
Nb: Rais hadanganywi, mpaka atake mwenyewe. Anavyo vyanzo vyake vya taarifa ambavyo ni vya kuaminika.

Ukiona kadanganywa jua ni mchongo anaoujua.
Hapa pia Magufuli alidanganywa akapigwa changa la Macho!. Sasa ni zamu ya Samia, naye kuna vitu kadanganywa akaingizwa kingi na kujaa top!.

Hivyo sii kweli kuwa rais hadanganywi, rais anadanganywa kama binadamu mwingine yeyote.
P
 
Wanabodi,
Rais Magufuli Amedanganywa Kiwango cha Dhahabu Kwenye Makinikia
Kwenye hili la mchanga wa makinikia ya dhahabu, wajameni kiukweli kabisa, rais wetu amedanganywa mchana kweupe, na masikini rais wetu tayari ameishadanganyika kupitia ripoti ya makinikia, imemdanganya rais wetu kuwa Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha dhahabu nyingi duniani kuliko nchi nyingine yoyote lakini dhahabu hiyo imekuwa ikiibiwa kupitia mchanga wa dhahabu!, uongo huu ni kupitia taarifa ya viwango vya dhahabu vilivyokokotolewa na tume yake kwenye makinikia yaliyomo ndani ya makontena 277 ya mchanga wa dhahabu wa migodi miwili tuu ya ya Acacia, nashauri tusilinyamazie hili, tuungane na rais wetu katika kutafuta ukweli hakika na bayana kwa maslahi mapana zaidi ya taifa letu.

Hapa nimesema rais amedanywa na akadanganyika kwa sababu sii kweli kuwa Tanzania ndie mzalishaji mkubwa kabisa wa dhahabu duniani, hata tungekuwa tunaibiwa vipi, tungeibiwa viwango vya ndani lakini hiyo dhahabu inayoingia kwenye soko la dunia, ingeonyesha wazi kabisa kuwa inatoka Tanzania!. Ni kama ilivyo kwa Tanzanite, japo Tanzania ndio mzalishaji pekee wa Tanzanite duniani, anayeongoza kuuza Tanzanite ni India, Afrika Kusini halafu ndio Tanzania. Unless wathibitishe kwa ushahidi usiotia Shaka kuwa kuwa Tanzania ndio inaongoza kuzalisha dhahabu duniani, lakini dhahabu hiyo hairekodiwi kuonyesha inatoka Tanzania, hivyo dhahabu hiyo inaibiwa kupitia makinikia, na kuingizwa kwenye soko la dunia ikiandamana na certificates of origin za kutokea nchi nyingine!, hivyo hairekodiwa na WB na haionyeshi kuwa inatoka Tanzania, hivyo kwenye records Tanzania ndio ilipaswa kuwa ndio inaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani kitu ambacho sii kweli. Kitu cha kwanza kwenye international business ya bidhaa ni certificates of origin, unless wathibishe kuwa ni kweli Tanzania ndio ya kwanza ila tumekuwa tukiigwa na kuwa biwa dhahabu yetu!.

Hii maana yake ni kuwa kwenye ripoti za tume ya makinikia, rais wetu amedanganywa kiasi cha dhahabu kilichomo, na kupitia uongo huo, TRA ikatoa deni la ajabu la dola bilioni 191 kwa Acacia ambalo kiukweli kabisa, halilipiki!, ukweli wa uongo huu utajulikana pale tuu, tutakapouchenjua wenyewe Mchanga unaoshikiliwa katika makontena 277 tunayoyashikilia na kuuthibitisha sio ukweli wa tunachoibiwa bali uongo wa tume ya rais ya makinikia!.

Paskali
niliishiwa nguvu, na kuamini kuwa kumbe Mwendazake alikuwa anatudanganya mambo mengi sio hili tu.

Niwatakie Jumamosi nono.

Tril.360 ni "KANYABOYA".
Nashauri tupunguze kumsema kwa ubaya na kumtuhumu mtu asiyeweza jitetea!. Hizo triioni 360, JPM hakutudanganya bali ni yeye ndiye alidanganywa, watu wakusaidia asidangayike tukamwambia anadanganywa, very unfortunately akadanganyika,
ila baadaye akaambiwa ukweli, hivyo tukalifuta hilo deni kimya kimya. Maendeleo ya kweli Tanzania yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!
 p
 
Back
Top Bottom