Mkapa na Kikwete: Ole wenu..Tuepushieni balaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa na Kikwete: Ole wenu..Tuepushieni balaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Jun 9, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Waheshimiwa Mkapa na Kikwete,

  Mmekuwa mashuja wa kupuuza vilio vya wananchi na kushughulikia kwa nguvu kubwa matakwa ya Wanyonyaji.

  Mmeachia nchi yetu itekwe na majambazi wa kimataifa wa uchumi, mmekula nao mvinyo na hata jibini, lakini kushughulikia na kuweka kipaumbele matatizo ya Tanzania kwa manufaa ya Watanzania mmekuwa ni wagumu kufanya kazi hiyo.

  Haya ya Uhujumu Uchumi yaliyotokea katika miaka 12 ya Uongozi wenu ambayo yamelitia aibu na kuongeza umasikini Taifa letu, si mambo ya kupuuzwa na kushughulikiwe Kesho au Keshokutwa. Yangeshughulikiwa Jana na Juzi.

  Wote nyie wawili mnatuhumiwa kujihusisha na kuwa karibu sana na Watu ambao wanaonekana ni Wahujumu wa Uchumi wetu na mafisadi.

  Kikwete unawekwa kundi moja na wale wanaotuhujumu madini, na urafiki wako na Sinclair, unatatiza Watanzania wengi. Umeingia madarakani kwa kusadikika pesa za hujuma zilitumika na ndio maana unakuwa mzito kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na Uhujumu wa BOT.

  Tangu uingie madarakani, miaka miwili na nusu iliyopita, tumekumbwa na Kashfa ya EPA uliyorithi kutoka kwa Mkapa, Richmond, TRC, ATCL na sasa Rada ambayo nayo uliirithi kutoka kwa Mkapa.

  Umeshindwa kuchukua hatua kali za kinidhamu hata kama ingekuwa ni geresha toto kwa Lowassa, Karamagi na Chenge, ambao wana tuhuma kubwa za uhujumu, lakini wanapeta kama wafalme kila kona ya nchi na kujisifu.

  Mkapa wakati wa himaya yako, BOT ilifanywa kuwa kisima cha wahujumu, Tangold, Meremeta, EPA, Mwananchi Green na kashfa kibao ambazo jumla ya fedha zilizohujumiwa ukiwa Rais wa Taifa si chini ya Dola za Marekani Millioni Miatano ($500,000,000.00)

  Wakati wa utawala wako, Tumenunua Rada kwa ulaghai na Rushwa, Tumeingia mkataba na IPTL kwa rushwa, tumenunua ndege ya Rais kwa rushwa, inasemekana umenunua Mgodi wa makaa ya mawe, kuanzisha kampuni, kuhodhi nyumba za Serikali, Msajili, Shirika la Nyumba na ardhi nyingi kwa kutumia rungu la Urais.

  Katika utawala wako tumeuza kiholela mashirika mengi ambayo yalikuwa ni manufaa ya wananchi, na kwa Taifa, lakini yakauzwa kwa Idhini yako kiholela na kwa bei ya kutupunja.

  Nawaombeni sana muwe wazi na Watanzania. Kama mlifanya uzembe, kubalini kufanya Uzembe. Kuendelea kutudharau na kutudhalilisha si haki, si sawa na si Uungwana.

  Hasira ya Raia na Wananchi wa Tanzania inachemka. Nyinyi wawili mnauwezo mkubwa kusawazisha yote yaliochafua sifa ya nchi yetu na kutudumaza katika umasikini.

  Naomba niwakumbushe yaliyotokea kwa yule aliyekuwa Rafiki yetu mkubwa Bwana Nicolae Ceausescu. Jiulizeni, je siku ikifika ngome ya ulinzi ikapasuka na hasira za Wananchi zikazidi kikomo, je yaliyomfika Ceausescu yatawafikia? kama yatawafikia, itakuwa ni aibu gani kwenu binafsi na familia zenu na kwa Mwalimu wenu Julius Kambarage Nyerere , Chama cha Mapinduzi na Watanzania?

  Najua wengi watauliza Mchungaji kulikoni, na wengine watadai ni mchochezi. Mimi sichochei kibaya kitokee kwenu, nataka muondoke na mema na mtuepushie balaa. Haya mtakayoyasoma hapa chini na kuona huo mkanda, ni kujikumbusha, je itakuwaje ikiwa nchi yetu itafikia hapo?

  Kama kero za Umasikini na Dhuluma zitaendelea na nyinyi mkaendelea kuwa watalii na kutupuuzia au kushindwa kufanya kazi zenu na kuwajibika kwa Taifa, je mnategemea mpaka lini Mtanzania ataendelea kusema hewala?

  Pamoja na kuwa Mkapa ameshastaafu, na tunambiwa tumuache, lakini kuna maswali mengi ya kumhoji na uongozi wake ambao ulilea uharamia na uanaharamu wa wahujumu.

  Kitendo cha Benki Kuu kuhujumiwa pesa nyingi kiasi hicho bila kudhibitiwa kwa kipindi cha miaka takriban 7 ya Utawala wa Mkapa ni jambo la kusikitisha na kutisha.

  Swali ni hili, wakati uanatalii kutuombea misamaha ya madeni, ulikuwa wapi kuhakiki vitabu vya mahesabu?
  http://www.youtube.com/watch?v=5D5Gnq0xzKM&feature=related

   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kikwete hajali. Hana sababu:

  1) Sisi emu ina sheria moja ambayo haiko vitabuni: Ukishinda tiketi ya ugombea, hiyo ni tiketi ya vipindi viwili.

  2) Sisi emu inajua kwamba hata kama wangesimamisha mgomba - mti wa ndizi, that is - bado itashinda iwapo itawaambia wananchi huu mgomba uta maintain amani ya nchi. That is their trump card, and nothing else.

  Kwa hiyo hata Kikwete na Sisi emu wangeharibu vipi, hawana wasiwasi.

  Katika kupita katika vilima na mabonde ya maisha yangu, nimegundua kwamba binadamu ambae hana sababu ya kujali matokeo, ambae hana bosi wa kumkoromea, hana mkosoaji wa kumkalia kooni, binadamu katika mazingira hayo ni wachache wachache mno ambao wanaweza kuji ajibisha wenyewe. Nadhani hii ni asili ya binadamu. Kikwete hayuko katika kundi la viumbe wachache wanaoweza kujali kama hawana sababu ya kujali!
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2008
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,590
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kama nimekuelewa unamaanisha iwapo tunataka marais wetu, in this case kikwete, wawe makini basi kuna haja ya kubadilisha katiba ili rais awe answerabla kwa chombo fulani.

  kama nimeelewa sahihi, nakuunga mkono.
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  picha ya youtube na maelezo yake hapo wakioana mbona mishipa ita washituka!

  Ila kweli nchi yetu inahitaji mabadiliko ya haraka,sasa ni juu yetu !
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  I have seriuose pbroblem with My President.

  Moyoni na kwenye fikra zake ANA AMINI NINI?

  Anaamini na kusimamia nini?

  Ameshikilia nini?

  Na hatimaye ANATEGEMEA NINI?

  AU?

  Anategemea kupata majibu ya maswali yangu kwa safari mbalimbali?

  Anaamini kwenye kukaa kimya na kimya kiendeshe Taifa...

  Anaamini na kutegemea ..wapige kelele finaly watanyamaza...

  sijui ameona kilichomponza Rafiki yake..BENJAMINI Mkapa?

  Ameona kosa na shimo alilitumbukia..Ben?...Au yuko mbioni..kufuata nyayo?

  Au:

  Anategemea Kipindi kijacho kukabili mambo kwa kina na mapana?
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Azimio,

  Maandiko yalisema, nitaifanya mioyo yao iwe migumu...

  Hawa jamaa wamekuwa si mioyo migumu tuu, bali pia kichwa ngumu!
   
 7. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Waache waendelee kupuuzia. Waulize kina Marcos, Bokassa, Mobutu, Shah, Fujimori na wengine waliojineemesha na kuwafanya wananchi wao masikini wa kutupa.
   
 8. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Sasa imefika wakati Taifa linatekwa nyara kwa mambo ya Ushirikina na kupeana sumu ili kuficha madhambi, when will these two heads come out of molehill and clear the mess they created?
   
 9. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2008
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna mengi yamesemwa/andikwa kuhusu Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh. Benjamin William Mkapa: "Oh, mkapa ni fisadi," "Mkapa alitumia madaraka ya Urais vibaya," "Mkapa ajitete mbele ya umma," "Blah... blah... blah..."

  Lakini ukweli ni kwamba: ni Mzee Ben, na sio Mzee ruksa, wala this Kikwete guy, ambaye ameifanyia nchi hii mema na mazuri. Ikumbukwe kuwa baada ya uchaguzi mkuu wa 1995, Mkapa alipokea nchi iliyokuwa katika hali mbaya kupindukia.

  Rushwa ilikuwa imekithiri. Pato la taifa lilikuwa chini. Ukwepaji kodi ulikuwa katika kiwango cha kuogofya. Na miundo mbinu ilikuwa imechoka kupindukia.

  Ni chini ya utawala wa mzee Ben ndipo watanzania kwa mara ya kwanza tulipoanza kuona sera ya taifa kuhusu uchumi ikipewa kipaumbele. Miundo mbinu ikiboreshwa. Pato la taifa likikua. Na kamba dhidi ya vita ya rushwa ikikazwa.

  Lakini pia katika viongozi tuliowahi kuwapata, ukimuacha Mwalimu, ni Mkapa peke yake aliyekuwa na ubavu wa kupinga kuendeshwa na nchi za Magharibi. Mwinyi alikuwa anajikojolea wahisani wakikohoa, Kikwete (sote tumeshuhudia) anacheza samba kila mara nchi za magharibi zikimuamuru afanye hivyo.

  Yes, kuna mabaya amabayo Mkapa ameyafanya ktk kipindi cha miaka 10 akiwa ikulu: (1) mikataba mibaya hususani madini (ambayo hata hivyo ni mwanasheria mkuu ndiye anapaswa kulaumiwa);(2) kumuachia mke wake a—dictate badhi ya shughuli za kiserikali ( one of his weakness). (3) kujihusisha na bishara akiwa ikulu (which is a minor thing)...

  Cha msingi hapa ni kujua kuwa Mkapa sio Malaika bali mwandamu. na kama mwadamu, naye pia anahadawa na tamaa ya kuwa na maisha yaliyotulia. You know, financial security and all those things, kwa ki-inglish.

  Hitimisho: Hapa suala ni kwamba, Kikwete and his inner circle wameshaona kuwa wamechemsha big time, hivyo wanachokifanya ni kumchafulia mzee Ben jina ili watu wasipate fursa ya ku-compare utawala wake (mtalii Kikwete) na ule wa mzee Ben (mtu safi).
   
 10. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mbona kila mtu anadai kapokea nchi ikiwa mbovu au imeharibika! Mwinyi alidai alipopewa nchi hata haikuwa na pesa, Mkapa hivyo hivyo, Kikwete naye kadai matatizo aliyoyakuta ni ya Mkapa. Point ni kwamba kwani kama umekuta mabaya utayaendeleza au utayarekebisha? Mkapa has to get his share of the blame too!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jul 12, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Hebu changanua kwa kina ulinganishe mabaya na mema ya Mkapa halafu utuambie uzito umelalia wapi. Utakapofanya mchanganuo wako jitahidi uwe kiona mbali, usiwe myopic wa kuangalia mambo mdogo madogo yenye upeo wa miaka miwili au mitatu huku ukiacha mambo yenye athari za miaka 30 na zaidi ijayo.
   
 12. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kichuguu,

  Hapa umenena sio watu wanakurupuka usingizini wanakimbilia hapa JF eti Mkapa!
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  BongoTZ,

  Lo salaaale!! Umeniacha hoi na kichwa kinanizunguka... ngoja nikapate aspirin kwanza. Nitakujibu baadaye maanake kwa sasa hivi sina la kusema. My God, I cant believe the audacity and impunity surrounding this post. Let me sleep over it....For now it could only be dream
   
 14. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2008
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nashangaa watu wanavyomsifia Mkapa,Don’t praise Mkapa that much, When you look at the Tanzanian economy timeline you will realise Mwinyi had a country at hard time .it was a time when Tanzania was going under structural adjustment programme, which helped the country on prevailing economic, social and political structures from socialism . all of the structural adjustment programmes experienced in the 1980-1990s e.g multy party democracy .In general, adjustment measures included exchange rate devaluation, fiscal policy restructuring, monetary discipline and interest rate rationalization, as well as an array of institutional reforms that involved redefining the role of the state and public enterprises engaged in a range of activities that why during mwinyi time the exchange rate was very good. Let’s say TSH 400 was equal to 1 USD.
  When Mkapa came in power the world Bank, Initiated new polices at time and that was Market Economy, that was the time when all the public company was sold. and it did open up the economy by more FDI inflows , which stabilised the economy but at same time people used that chance to benefit themselves mafisadi hao.
  In conclution it doesn’t matter who is a president, what worries me is all the polices from world bank, because they are ones can determine the state of the county therefore Mkapa has nothing to credit himself because hata Mr Nice angekuwa raisi it would happened.
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Could we have tailored the SAP to our own models and not completely adopt to IMF ways? If we would have taken a different approach during conception of Structrural Reforms, by making it slide parallel to our social economic pillars such as Azimio la Arusha, Madaraka Mikoani, Kilimo cha kufa na Kupona and Vijiji vya Ujamaa, could we have been at better place today than what we are facing?

  Maana so far naona hizo SAP hazijafanya kazi kumuinua Mtanzani kutoka Umasikini, sanasana zime-polish umasikini na sasa unang'aa zaidi huku wachache na hasa wageni wakituvuna!

  Ndio maana nawataka Mkapa na Kikwete, waje na kukiri kuwa wamefanya mambo kutumia madaraka yao ambayo hayamsaidii Mtanzania iwe ni short term au long term!
   
 16. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ben Mkapa is the biggest hypocrite Tanzania has ever seen.Usimpe sifa kwa kufanya kazi yake, na wala usitake kutufanya tuamini kuwa Mkapa kile kidogo alichoweza kafanya single handedly.

  Ana integrity gani ya kujifanya anakataa zawadi za Kitwana Kondo (baada tu ya kuukwaa urais) na kumwambia KK "aende kumpongeza kwenye magazeti" wakati huo huo m-Range Rover ule aliopewa na Andy Chande kautia kibindoni vizuri sana. Ndiyo Mr. Clean huyo? Alishaanza vituko tangu mwanzo!
   
 17. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mkapa alifanya mazuri kidogo lakini yamefunikwa na mbaya aliyofanya na ni mengi.
  KIBURI na UFISADI.
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Apr 2, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Je tunaseleleka kwenye balaa? mauna nilipoadhini kuwa watu wafanye toba, mwenzao kanaswa kibao cha Kelb na Jambawazi mmoja limeuwa vidosho wawili!
   
 19. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #19
  Apr 2, 2009
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  Rev.
  Nadhani hali inazidi kuwa mbaya, nimesoma hotuba ya JK nikabaki kujiuliza kwamba kweli huyu ni raisi au ni mwenyekiti wa mashindano ya UMITASHUMITA tarafa? The guy is a scum, he can't talk about economics (Nadhani umeona ile video ya IMF summit Concluding Plenary » Africa is changing...)

  Nadhani Rev kuna umuhimu wa kufanya Summit ambayo tutajadili kwa nini JK amekuwa rais? What are long term implications of the choice? Will Tanzania survived at the end of day? and Many other questions are need a strong debate.... Kwa wale wa USA nadhani badala ya kwenye Easter Dallas basi tutafute mahala tufanye summit ambayo itaongelea wapi Tanzania inakwenda. May be tunaweza kupata strong solutions.
   
 20. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #20
  Apr 2, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kiufupi Nyanja ya uongozi wa juu wa taifa imepwaya mpaka inakera!
   
Loading...