Mkapa, Mwinyi, Karume, kung’olewa Kamati Kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa, Mwinyi, Karume, kung’olewa Kamati Kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145


  • Ni kutokana na mabadiliko ya Katiba ya CCM

  • Waundiwa Baraza la Ushauri, wanachama watoswa
  • Utekelezaji waanza kabla ya Mkutano Mkuu kupitisha
  Na Mwandishi Wetu

  [​IMG]

  Chini ya marekebisho hayo, marais hao ambao kwa mujibu wa Katiba ya CCM ni wajumbe wa Kamati Kuu, wataundiwa chombo kipya kiitwacho Baraza la Ushauri, litakalokuwa na jukumu la kukishauri chama na Serikali inayoongozwa na CCM kwa namna litakavyoona inafaa.

  Pamoja na marais hao kuondolewa katika kikao hicho, wajumbe wa baraza hilo wanaweza kualikwa kuhudhuria vikao vya chama ngazi ya taifa, ama wote kwa pamoja au mwakilishi wao pindi busara zao zitakapohitajika, hasahasa katika masuala magumu na nyeti.

  Katika baraza hilo, marais hao watakaokuwa wametokana na CCM, watakuwa na wajumbe wengine wa heshima wasiozidi watano watakaopendekezwa na CCM kutokana na uongozi wao unaotukuka. Katika baraza hilo, watakuwamo Marais Wastaafu wa Zanzibar wanaotokana na CCM na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Wastaafu. Baraza hilo litafanya vikao vyake kulingana na mahitaji kama itakavyoamuliwa na baraza lenyewe.

  Kwa mujibu wa waraka huo kutoka Idara ya Oganaizesheni ya CCM ambao MTANZANIA ina nakala yake, endapo NEC itaridhia mapendekezo hayo, inashauriwa itumie madaraka yake iliyopewa na ibara ya 107 (18) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2010 kuidhinisha marekebisho hayo ili yaanze kazi.

  Hata hivyo, taarifa zinasema utekelezaji wa mapendekezo hayo umeshaanza kabla ya kupitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM na kwamba hata katika kikao cha watendaji wa chama kilichomalizika juzi Mjini Dodoma, washiriki walijadili suala hilo na kupewa maelekezo ya utekelezaji wa maagizo mengine ya chama.

  Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipopigiwa simu, alisema utekelezaji wa marekebisho hayo ya Katiba haujapitishwa na vikao na kusema kuwa bado utaratibu unafuatwa.

  "Hayo marekebisho unayosema bado ni mapendekezo tu na ndiyo maana hata katika vikao vya Kamati Kuu vilivyomalizika Mjini Dodoma hivi karibuni marais wastaafu unaowasema walishiriki.

  "Kilichopo sasa ni mchakato ambao bado unafanyiwa kazi kwa sababu tutakapoyapitisha kuna mambo mengi ya kuangalia ili kusiwepo na mgongano kati ya Katiba, kanuni na taratibu za chama.

  "Kuhusu kikao cha makatibu na watendaji wengine wa chama waliokutana mjini Dodoma, walikuwa wakipewa maelekezo ya utekelezaji wa mageuzi ya chama," alisema Nape.

  Mjumbe mmoja wa NEC ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kilichofanywa na CCM ni ukiukwaji wa Katiba ya chama kwa kuwa mkutano mkuu wa chama haujakaa kwa ajili ya kupitisha mabadiliko hayo, ingawa kuna taarifa kwamba yameshaanza kutekelezwa.

  "Huu ni ukiukwaji wa chama na kutokana na mazoea ya watu kukiuka Katiba, ndiyo maana tulipokuwa Dodoma wiki iliyopita, ilifika mahali tukashindwa kuwachukuliwa hatua hao watu wanaoitwa mafisadi.

  "Hatukuweza kuwachukulia hatua kwa sababu utaratibu ulikuwa haukufuatwa, yaani watu walikuwa wanazunguka mikoani na kusema tumetoa siku tisini kwa mafisadi, sasa angalia, siku tisini zimepita hakuna kilichofanyika.

  "Utaratibu wetu sisi mtuhumiwa unampa nafasi ya kujieleza, halafu wewe unayemtuhumu unatoa ushahidi na hilo lilikuwa halijafanyika, ndiyo maana nasema hata utaratibu ulikuwa umekiukwa na hata haya mabadiliko ya Katiba, mambo ni yale yale, hakuna utaratibu uliofuatwa," alisema Mjumbe huyo wa NEC.

  Pamoja na mambo mengine, mabadiliko hayo ya Katiba yalipendekezwa na Sekretarieti ya chama katika Kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, kilichokaa Mjini Dodoma Aprili 10 na 11 mwaka huu na kuwasilishwa tena katika kikao cha NEC kilichomazilika wiki iliyopita na sehemu ya taarifa hiyo inasema:

  "Halmashauri Kuu ya Taifa katika mkutano wake wa kawaida uliofanyika Dodoma Aprili 10 na 11 mwaka 2011, pamoja na mambo mengine, ilifanya maamuzi ya kubadilisha muundo wa Chama Cha Mapinduzi katika maeneo kadhaa yafuatayo.

  "Uwakilishi wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nafasi ya Mkoa kuwa na nafasi za Wilaya, kundi la Wajumbe 85 wa Halmashauri Kuu ya Taifa wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu lipungue kwa namna itakavyoonekana inafaa, kuandaa chombo kipya cha Baraza la Ushauri ngazi ya Taifa ambacho wajumbe wake watakuwa ni Marais Wastaafu na wajumbe wengine wa Heshima wasiozidi watano.

  "Utaratibu wa kura za maoni kufanyika Mwezi Mei wa mwaka wa Uchaguzi unaohusika ili kupata muda muafaka wa kushughulikia malalamiko yanayotokana na kura za maoni na kuundwa kwa chombo kipya cha Tume ya Udhibiti na Nidhamu.

  "Maamuzi haya ya Halmashauri Kuu ya Taifa yaliyotajwa hapo juu, yatahitaji marekebisho kadhaa kufanyika katika Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2010, Kanuni za Uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola, toleo la Februari, 2010, Kanuni za Uchaguzi wa CCM, toleo la Februari, 2010 na Kanuni za Uongozi na Maadili, toleo la 2010.

  "Mapendekezo ya kupunguza wajumbe hao yamewekwa katika sehemu ya waraka huu unaohusu marekebisho katika Kanuni za uchaguzi wa CCM.

  "Sehemu ya mwisho ya uamuzi huo inataka idadi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa isiwe kubwa mno, kwa ajili hiyo, yametolewa mapendekezo mengine ya kupunguza idadi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wanaotokana na makundi mengine, zaidi ya kundi hilo moja la Wajumbe 85.

  "Hii ni kwa sababu punguzo la Wajumbe katika kundi hilo moja tu halitatosha kufanya idadi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa isiwe kubwa mno na uwakilishi katika Halmashauri Kuu ya Taifa uteremshwe kutoka ngazi ya Mkoa uende katika ngazi ya wilaya," ilisema sehemu ya waraka huo.

  Pamoja na hayo, waraka huo unalenga kuanzisha Baraza la Wazee wanaotokana na CCM katika kila ngazi ya uongozi, isipokuwa ngazi ya Taifa ambamo watakuwamo wazee wote wanaokubali imani, malengo na madhumuni ya CCM na kwamba sababu ya kutumia maneno wazee wanaotokana na CCM ni kuwatofautisha na wazee wengine nchini.

  Mabadiliko hayo pia yanalenga kufanya marekebisho yanayotokana na mabadiliko ya Katiba ya Serikali ya Zanzibar ambayo sasa haina maneno Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi.

  Katika mabadiliko hayo, maneno Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yatafutwa katika ibara ndogo (e) ya Ibara ya 104 (1) na Ibara ndogo ya (e) ya Ibara ya 108 (1) na badala yake yatawekwa maneno, Makamu wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar anayetokana na CCM.

  Waraka huo unapendekeza pia chama kirejeshe Mkutano Mkuu wa Jimbo kwa upande wa Tanzania Bara, ingawa mkutano huo ulifutwa katika marekebisho ya Katiba ya mwaka 2010 na katika marekebisho hayo kikao hicho kiitwe Mkutano Mkuu wa Jimbo linalohusika.

  UCHAGUZI WA WAJUMBE WA NEC

  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa watakaochaguliwa katika ngazi ya Wilaya watachaguliwa kwa lengo la kupanua nafasi za uwakilishi wa wilaya katika vikao vya kitaifa ili uwafikie wanachama wengi zaidi, nafasi ya mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka Wilayani haitagombewa na mwanachama yeyote ambaye tayari ni mwakilishi wa wilaya hiyo katika vikao vingine vya kitaifa, hususani Bunge na Baraza la Wawakilishi.

  "Isipokuwa kwamba, kwa sababu maalum Kamati Kuu yaweza kutengua kanuni hii ili kuruhusu mwanachama wa aina hiyo aweze kugombea nafasi hii na pia mgombea Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka wilayani sharti awe ni mkazi ambaye kwa kawaida anaishi katika wilaya hiyo.

  "Lengo la kufanya hivyo ni kumfanya mwanachama huyo awe karibu zaidi na wanachama anaowawakilisha, kwa madhumuni hayo, ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa kutoka katika Wilaya utahesabiwa kuwa ni kazi ya muda wote.

  "Majina yote ya Wagombea Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Wilaya yaliyoteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa, yatapigiwa kura na Mkutano Mkuu wa Wilaya," ilisema sehemu ya waraka huo.


   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tufike mahala tuwe na japo na kundi fulani la watu katika taifa letu WASIOZUNGUMZA ITIKADI ZA KICHAMA ila kubakia tu wazee wa taifa ili kunapotokea mihitilafiano fulani basi waweze kuwa ni kimbilio la KUAMINIKA NA KUTEGEMEKA kupata suluhu usioacha uchachu mdomoni wala maswali ya kutokuonekana haki kutendeka.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwahiyo bado watakuwa wanalipwa na CCM? au Serikali?
   
 4. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Uzalendo hamna ndo maana hatupigi hatua za kimaendeleo yaani mkuu wa nchi bado ana chukua upande wa chama hata kama anaona kunamakosa kumbuka yaliyotokea Igunga.
   
 5. L

  LAT JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  thanks brother
   
 6. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani siasa za makundi bado kikwete anaziendeleza!
   
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "Nadhani siasa za makundi bado kikwete anaziendeleza!"
  Hapana mi naona anafanya maboresho kwenye chama chake.
   
 8. t

  thatha JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  ni uamuzi mzuri
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Lakini ni kwanini bado wanatukuzwa kote kwa kulipwa ndani ya chama na serikalini?
   
 10. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  SSSSSSSSSSSSSSSAAAAAAAAAAAFI SANA,manake hawa wameshatumika taifa kuendelea kuwa ni mali ya CCM nimakosa makubwa.
   
 11. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,590
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  Wameamua kufuata ushauri wa TB Joshua nahisi; ingawa yeye alishauri viongozi wastaafu wawe washauri wa kitaifa sio kichama!
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Bwana "mjumbe mmoja wa nec" kaniacha hoi sana,haya bwana mjumbe mmoja tumekusikia,lakini punguza uoga wa mabadiliko!!!!
   
 13. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe huna namna ya kutengeneza stori zako zaidi ya ku-reproduce mambo ambayo tayari magazeti yameshayatoa? Unatuchosha na urefu usio na tija wa nyuzi zako.
   
 14. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii yote imejengwa katika dhana kwamba sisiemu will rule this country milele!!!!!!!!!!!!!! Pole!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...