MKAPA: Kutovumiliana (intolerance) na kutoshirikishana (exclusion) umeletwa na demokrasia ya kimagharibi, si Uafrika

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,220
5,943
Katika makala yake Mkapa anaandika:-
Yet, when we embraced Western forms of democracy we fell into the trap of making political parties, not as mechanisms for tolerance and inclusion, but of intolerance and exclusion. The concept of “winner takes all” has no African roots. Traditional Africa is corporate, if not communal. It is inclusive (2008:67)
 
Attachments

  • Mkapa.pdf
    1.6 MB · Views: 12
Hata kabla ya vyama vingi hakukuwa na tolerance wala inclusion.

Nyerere aliwafunga watu kisiasa, kina Kassanga Tumbo na Kassella Bantu.
Mkuu niruhusu nikutaarifu kuwa vyama vingi vilikuwepo hata kabla na baada ya uhuru rejea uchaguzi wa kwanza 1958
 
Mkuu niruhusu nikutaarifu kuwa vyama vingi vilikuwepo hata kabla na baada ya uhuru rejea uchaguzi wa kwanza 1958
Sababu ya kufutwa mfumo wa vyama vingi kipindi hicho ilikuwa ni Nini mkuu? Na kwanini aliyeshiriki kufuta ndo akawa mbele pia kuhamasisha virudi 1992?
 
Sababu ya kufutwa mfumo wa vyama vingi kipindi hicho ilikuwa ni Nini mkuu? Na kwanini aliyeshiriki kufuta ndo akawa mbele pia kuhamasisha virudi 1992?
Soma hiyo makala ya Mkapa utaelewa vizuri zaidi- ila ilikuwa ni lazima ili kujenga utaifa- Nation building.
 
Kuna kitabu fulani alikuwa anajibu maswali ya mwandishi mmoja wa SA 1994/95 kinaitwa BUILDING A VISION kama sijakosea mule kaongea nondo sana ila alivyoingia madarakani alichokifanya. Mungu amrehemu tu kwakweli
Alafu unaweza shangaa hata huyu mama siku akistaafu atakuja kusema katiba ni muhimu kwa maendeleo ya nchi
 
Mkuu niruhusu nikutaarifu kuwa vyama vingi vilikuwepo hata kabla na baada ya uhuru rejea uchaguzi wa kwanza 1958
Unaweza kufikiri unanitaarifu, lakini taarifa hizo ninazo.

Kwa mfano.Nimesoma "Building A Peaceful Nation: Julius Nyerere and The Building of a Sovereign Tanzania 1961-1964"

Nimekiweka hapo chini kwa wanaotaka kusoma zaidi.

Kwa hivyo, hili si jambo ulilonitaarifu wewe.

Ninachokuambia mimi ni kwamba, hata kabla ya vyama vingi kuruhusiwa 1992, hakukuwa na inclusion wala tolerance. Na zaidi, hata kwenye vyama vingi kabla ya 1964, hakukuwa na tolerance wala inclusion.

Tangu mkoloni aondoke hatujawahi kuwa na tolerance wala inclusion. Kuna siasa tu zinazotumia dhana za tolerance na inclusion.
 
Attachments

  • Building_A_Peaceful_Nation-Julius_Nyerere_And_The_Establishment_Of_Sovereignty_In_Tanzania_196...pdf
    10 MB · Views: 11
Unaweza kufikiri unanitaarifu, lakini taarifa hizo ninazo.

Kwa mfano.Nimesoma "Building A Peaceful Nation: Julius Nyerere and The Building of a Sovereign Tanzania 1961-1964"

Nimekiweka hapo chini kwa wanaotaka kusoma zaidi.

Kwa hivyo, hili si jambo ulilonitaarifu wewe.

Ninachokuambia mimi ni kwamba, hata kabla ya vyama vingi kuruhusiwa 1992, hakukuwa na inclusion wala tolerance. Na zaidi, hata kwenye vyama vingi kabla ya 1964, hakukuwa na tolerance wala inclusion.

Tangu mkoloni aondoke hatujawahi kuwa na tolerance wala inclusion. Kuna siasa tu zinazotumia dhana za tolerance na inclusion.
Asante kwa PDF nitapata kitu cha kusoma.
Mkuu naona kama unamatatizo ya uelewa au umeamua kuwa mbishi tu bila sababu. Maneno mawaili hapa ni muhimu na yanaweza kutuongoza.- UAFRIKA na UMAGHARIBI.
Kwa maoni yangu Uafrika ni kabla ya muingiliano wetu na WAMAGHARIBI. Kama unakubaliana nami basi toka mwarabu aje hapa tukaanza kupoteza uafrika wetu.
 
Back
Top Bottom