Mkapa kukataa uteuzi wa Kikwete kurudi Igunga?

Martoism

Member
May 31, 2012
36
21
Nianze kwa kutoa shukrani kwa mhimili wa utoaji haki nchini "The Judiciary" kwa kuwahuisha watanzani wanyonge jana kama chombo hiki kitajikita kwenye misingi yake kama "Intergrity, Impartiality and Independent of the court".

Rais Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi mkuu na mwenyekiti wa CCM kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi , alionekana kwa mara mbili mfulilizo wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga na Arumeru Mashariki akimbebesha Mzigo mkubwa Mkt mstaafu (CCM) na Rais mstaafu Benjamini Mkapa pamoja na shutma mbalimbali zinazomkabili, kufungua na hata kuongoza mapambano ya hoja alimradi wanaibuka na ushindi ukinzingatia mzee huyu ana falsafa yake ya " ushindi ni lazma na ili hayati Baba wa Taifa aendelee kuenziwa lazma CCM iendelee kutawala" hata kama haki za msingi zitakiukwa.

Leo hii mahakama inatuambia nini sisi watanzania? Nilibahatika kuwa na viongozi wa chadema pale Arumeru mashariki wakati wa uchaguzi mdogo kwa takribani wiki mbili.

Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni na mkt wa Chadema Taifa mh, Freeman Mbowe kwa macho yangu nilimshudia usiku na mchana na wakati mwingine sauti yake ilikuwa imekauka kwa sababu ya vumbi jingi wakati wa mikutano, alipanga na kupangua mara kwa mara Wabunge na viongozi wa chama chake huku akijua machungu, mateso, maumivu, uonevu wa vyombo vya dola na hata kutengana na familia zao kwa muda wote huo katika chaguzi ndogo za Biharamulo, Kiteto, Busanda, Igunga na hatimaye Arumeru Mashariki ambako kama si uzoefu ambao chadema waliupata kama asemavyo John Legend kwamba "Experience is a great teacher" hakika na ni ukweli ulio wazi kuwa Chadema wangeporwa ushindi wao kama ilivyokuwa maeneo mengine.

Narudia tena kuipongeza mahakama kwa kuutengua ubunge wa huyo DALALI na ni kwa Mkapa na safu yake ya kina Nchemba, Januari, Lusinde, Magufuli, Nape n.k kukataa au kuukubali utume wa pili kurudi Igunga kazi kwenu !
 
Kazi ipo wakirudi Igunga safari hii watakuwa wapole sana sijui watakuja na sera gani maana zote zimeisha na ni zilipendwa na zimeshindwa!! Poleni sana wana Magamba
 
hivi hiki chama kwa nini wasiende likizo tu maana vitu vinawaelemea hawaelewi what to do first and what to do last
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom