Mkapa 'Atoroka' Sherehe za muungano.

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,649
Katika hali ya utatanishi, kwenye sherehe kubwa ya muungano ambayo ilihudhuliwa na viongozi mbalimbali na wale wastaafu lakini Rais wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa hakuonekana uwanja wa Taifa ambapo sherehe hizi zilifanyika. Je Mkapa kaogopa Kuzomewa na wananchi? au alijua waandishi wa habari wangemuhoji kama alivyohojiwa mzee Mwinyi?
 
Ni Haki Yake Ya Msingi Kama Raia Wowote Wa Tanzania Kuondoka Katika Sherehe Wakati Wowote Anaotaka Yeye
 
Ujumbe unaonyesha hakufika kabisaaa. Sijui atajificha mpaka lini.
 
Ni Haki Yake Ya Msingi Kama Raia Wowote Wa Tanzania Kuondoka Katika Sherehe Wakati Wowote Anaotaka Yeye

Shy mambo naona yanaenda yanakuwa magumu sijui utatetea mpaka lini, ni haki yake lakini kama kiongozi wa kitaifa alitakiwa kuwepo.
 
Shy huyu jamaa aliondo kakabla ya sherehe kwisha au hakuja kabisa??

Maro sio kama hajasoma na kuelewa kilichoandikwa ila anataka tusisome tuanzie kutoa hoja pale alipo andika yeye na tuamini kuwa mkapa alihudhuria ilhali hakuhudhuria Sherehe za "Mnyongano"

Hawa ndio watu wanaona nyekundu wakaiita kijani tena kijani kibichi ( deep green )
 
Wakuu huyu mzee hawezi kukaa karibu ya wananchi bila kujificha maana anaona aibu jinsi alivyowaibia hakujua kama kuna siku kila kitu kitakuwa wazi kama ilivyosasa. hawezi kuudhuria sherehe yeyote maana anajua waandishi wa habari watamuuliza na ndo maana hata kuonekana haonekani kama wenzake, au ndo kashakimbia nchi?
 
mkapa ana observe policy ya WAIT AND SEE..anasoma upepo unaendaji ....ukweli ni kuwa public critisism baada ya mafaili X yake kufunguliwa ni kubwa....lakini pia fact kuwa serikali ya kikwete perfomance yake ipo chini kabisa..pamoja na nia njema anayoweza kuwa nayo kikwete inamuharibia na inaweza kusababisha hata tuhuma za kifisadi zinazoibuliwa na awamu hii siku moja kugonga sikio la uziwi kwa watanzania ambao watakuwa hawaoni maendeleo aliyoleta kikwete anyway pamoja na nia yake...

juhudi za kupiga vita ufisadi za kikwete ziende sambamba na maendeleo katika sekta zote za kiuchumi.....ili asije onekana siku moja kuwa hizi kashfa zilikuwa zinaibuliwa ili ku divert attention ya wananchi kutoka critism kwa serikali yake!
 
Ina maana Bongo imekuwa ndogo mara hii,ana bahati mbaya Zimbabwe wamekataa kupigana,labda angeenda huko kusuluhisha ugomvi,lakini yaani ameamua kuuchuna pale sea view sio, poa ipo siku ambayo haiko mbali sana.Hawakawii kupandisha BP ili wasiende kwa pilato.BWM ni mmakonde hana kwa kwenda, ni lazima atajibu hoja.
 
Ina maana Bongo imekuwa ndogo mara hii,ana bahati mbaya Zimbabwe wamekataa kupigana,labda angeenda huko kusuluhisha ugomvi,lakini yaani ameamua kuuchuna pale sea view sio, poa ipo siku ambayo haiko mbali sana.Hawakawii kupandisha BP ili wasiende kwa pilato.BWM ni mmakonde hana kwa kwenda, ni lazima atajibu hoja.

..siku hizi amehama sea view...anaishi masaki na mostly lushoto....

tunaye rais mstaafu aliyefanya kazi kubwa kujenga uchumi...lakini yupo kati kati ya kashfa....

na tunaye rais anayetusaidia kujua upande wa pili wa shilingi wa mkapa tuliyemsifu sana ...lakini yeye akiwa hana analofanya kukuza uchumi zaidi ya kuudidimiza ...

historia itakuja kuwapa nafasi gani hawa wawili??
 
Serikali yenyewe buzi hii hata ningekuwa mimi ningejitenga nayo!Brother Ben anakula good time saa hivi kasema kurupushani za siasa hataki wewe mtoa hoja unakuwa kama mbea yaani hujaona hoja ya maana ya kuanzisha unaongelea kutokuja kwa mtu kwenye sherehe.Angekuja ingeongeza nini au kutokuja kwake hasara gani tumepata?
Unajua wewe pia unalikosema taifa lako na vizazi vyako vijazo !Unatakiwa u play your part kama mwanainchi kuhakikisha unazuia maovu na kutoa masuhurisho ya matatizo na kufanya kazi kwa bidii bila kusahau kuchagua viongazi bora ili uwe na imani na kodi yako inatumika vema.
Ila acha kupoteza muda kujadili non sense,kama una data za kutosha mwaga hapa ila zilizopo za brother Ben hazitoshi kumuona muovu mpaka zitazotoka zilizo jificha kama zipo.Mtufunulie hizo if any!.
 
Wewe ndio unapoteza muda kweli
yaani unaweza kusema hakuna data za kutosha kueleza kuwa Mkapa ni mwizi na muhujumu wa Nchi yetu?? Unataka ushahidi gani na data gani wewe??
Huu upole na amani ya kulazimisha ndio zinatufanya tuendelee kuwa wazembe na wapumbavu uku mali za taifa zikiliwa na wakoloni wa kitanzania
Hawa inabidi tuwafunge jiwe shingoni na kuwatupa baharini ukiwa pamoja nawe unaye mtetea

Kaa pembeni wenye uchungu wapiganie haki yao

Unaongea nini wewe ?ongea kwa vituo sio kuwa na gadhabu ndio kutatua tatizo ,unauchungu zaa! Good Approach ndugu is what matters siku zote ,sio kulalamika kama mtoto wa kambo mvivu ,dont play uchungu card here do the man things.
Hapa inaongelewa kutohudhuria sherehe inahusu nini ?Dont fly your big mouth just because your free to do so!
Ati mtu analeta habari za viroja unaonga mkono kisa uchungu.Inafikia kipindi mtu anaambiwa kuwa kwa umbea huu ulioleta tutaonekana hakuna point badala yake ongea guniune issue kuhusu vitu si viroja.
Serikali inafatilia sasa shut up ,play your part kwa nchi yako kuzua maovu sio usubiri kuraumu,chagua viongozi bora ukiangalia sura au tshirt mnazopewa taimba uchungu mpaka uchifungue mapacha ,kazi kwa bidii ,dont just blow up as if you talk using ya ass , lame!.
 
Ni Haki Yake Ya Msingi Kama Raia Wowote Wa Tanzania Kuondoka Katika Sherehe Wakati Wowote Anaotaka Yeye

Mkuu Shy,

Heshima mbele mkuu, unajua kuna wakati wengine tunataka kuamini unaporushiwa maneno mazito hapa huwa unaonewa, then unakuja na maneno ya pumba kama haya na kuthibitisha kuwa wanaokutukana huwa wako karibu na right,

Hivi kweli unaamini kuwa hapa JF hakuna anayejua kuwa makapa ana hizo haki ulizozisema? Hivi hizo haki zinahusiana nini na makapa kukwepa kwenda kwenye sherehe za muungano, ambazo huko nyuma kabla ya tuhuma zake kutoka kwenye public alikuwa hazikosi na ni itifaki ya taifa yeye kuwepo? Mbona alikuwa wa kwanza Nairobi bila hata ya kuitwa?

Mambo mengine unashusha hadhi yako wewe mwenyewe na unaishia kuwalaumu wengine, jaribu kujiheshimu ili uheshimiwe mkuu!
 
Haraka haraka sijaona kama alitoroka au hakuhudhuria kabisa... Title ya thread hii nayo ina mashaka au ndio kivutio? Ene wey. Hivi kutoroka kiongozi-ex/kiongozi-sasa nongwa?
 
Unaongea nini wewe ?ongea kwa vituo sio kuwa na gadhabu ndio kutatua tatizo ,unauchungu zaa! Good Approach ndugu is what matters siku zote ,sio kulalamika kama mtoto wa kambo mvivu ,dont play uchungu card here do the man things.
Hapa inaongelewa kutohudhuria sherehe inahusu nini ?Dont fly your big mouth just because your free to do so!
Ati mtu analeta habari za viroja unaonga mkono kisa uchungu.Inafikia kipindi mtu anaambiwa kuwa kwa umbea huu ulioleta tutaonekana hakuna point badala yake ongea guniune issue kuhusu vitu si viroja.
Serikali inafatilia sasa shut up ,play your part kwa nchi yako kuzua maovu sio usubiri kuraumu,chagua viongozi bora ukiangalia sura au tshirt mnazopewa taimba uchungu mpaka uchifungue mapacha ,kazi kwa bidii ,dont just blow up as if you talk using ya ass , lame!.


huh!? :confused:
Unatumia na matusi katika ukumbi wetu mwanana!? Moderators hebu mfungieni huyu kijana aliyekosa adabu.
 
shy inabidi tukakupime kichwani kama kuko sawasawa. hivi kweli ni hujui alichofanya mkapa kiasi cha kuwa unamtetea?
kweli wajinga ndo waliwao
 
Ufanisi wa kiutendaji wa Mkapa hakuna anayeweza kuutiliashaka, kwa kiasi kikubwa ni Rais ambaye naweza kusema ni mzuri kuliko wote ambao Tanzania iliwahi kuwapata, (this is debatable). Alikoitoa nchi na alipoifikisha wakati anaondoka anapaswa kushukuruwa sana. Hata jumuiya ya kimataifa (ndani na nje ya Afrika na kwa watanzania wenye akili) wanatambua wazi kuwa Ben alikuwa ni mmoja kati ya viongozi wapya wa Afrika wenye kuletea matumaini. Aliweza kudhibiti mfumuko wa bei, aliweza kutoa leadership ambayo sasa haipo tena, alijaribu kuleta heshima kwenye Ikulu ya Tanzania ambayo iliezuliwa na Mwinyi, na kuondoa uswahiliswahili serikalini, at least Tanzania ikaonekana tena kuwa ni nchi, na sio kama genge la wajinga.
Lakini baada ya kusema haya inabidi tukubali ukweli kuwa yeye kama kiongozi mkuu wa nchi, alikalia kimya mambo mengi ambayo ninahakika yeye mwenyewe aliyajua kuwa ni uhalifu na wizi, ambayo ni kinyume na maadili ya Chama chake na conscience yake binafsi, na kinyume na kiapo alichotoa wakati anachukua urais mara mbili, kinyume na dini yake, na kinyume na aliyosema kuwa napaginaia, na baya zaidi alitumia vibaya cheo chake kujinufaisha (sio kuiba japo sina hakika). Haya yote na mengine mengi ambayo siwezi kuyasema na mengine ambayo siyafahamu yanamfanya asiwe kwenye kundi la watu waadilifu, he is equally liable kama mafisadi wengine.
NI kweli mimi ni-admirer wa Ben and i will keep on being so, lakini mazuri aliyotufanyia hayawezi kumfanya awe immune kwa ujinga aliousimamia, ambao angeweza kuusimamisha alipokuwa na uwezo kama Rais wa nchi na mwenyekiti wa Chama. Ni sawa na kusema mtu anakaa pembeni anaangalia jambazi linaua na anaweza kabisa kulishimamisha, halafu anasema mimi sikuhusika na uuaji huo, that is madness. Unless there is something we do not know! Ben is in for it and he must speak out, kwanini ametufanya hivyo.
The guy is more smart than many in the administration now, kwa hiyo kauli yake inaweza kuwa na mawili, kwanza inawezekana kabisa akisema tu watu wakakaa kimya na kuacha kupiga domo anajua sana kujenga hoja na kuzitetea hata kama ni za uongo, au anaweza kumwaga sumu ambayo ita-i palaralyze kabisa CCM na serikali. Inategemeana tumejiandaa kwa lipi!
 
Back
Top Bottom