Mkapa atawanusuru Mramba, Yona, Mgonja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa atawanusuru Mramba, Yona, Mgonja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 21, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,810
  Trophy Points: 280
  Mkapa atawanusuru Mramba, Yona, Mgonja?

  • Ni siri ya waendesha mashtaka, ni jambo la kuvuta subira

  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  RAIS wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, anatajwa kuwa huenda akawa miongoni mwa watu watakaopanda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa ushahidi dhidi ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka yanayowakabili waliokuwa mawaziri wake, Daniel Yona (Nishati na Madini), Basil Mramba na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja, wanaoshitakiwa kwa kulisababishia taifa hasara ya sh bilioni 11.7.

  Mramba, Yona na Mgonja wanakabiliwa na kosa la kutumia madaraka yao vibaya kwa kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya M/S Stewart kinyume na ushauri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutoa matangazo ya misamaha hiyo kwenye gazeti la serikali.

  Mkapa anaweza kuwa shahidi wa upande wa mashitaka au wa washtakiwa kwa kuwa amefanya kazi kwa karibu na watuhumiwa hao na anajua mambo mengi yaliyofanyika katika utawala wake ambao katika siku za hivi karibuni umekumbwa na shutuma nyingi za matumizi mabaya ya madaraka pamoja na vitendo vya rushwa.

  Baadhi ya watu kwa muda mrefu wamekuwa na shauku ya kutaka Mkapa ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya madaraka ambapo baadhi yao wanamhusisha na kumiliki miradi mbalimbali kinyume na sheria ya maadili ya watumishi na viongozi wa umma lakini hivi sasa hali hiyo inaanza kuangaliwa kwa mtazamo tofauti.

  Mtazamo huo wa kumuona Mkapa kama mtu muhimu katika ushahidi wa watuhumiwa wa matumizi mabaya ya madaraka unatokana na ukweli kuwa Mkapa hawezi kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya mpaka Bunge lipige kura ya kumuondolea kinga ambapo theluthi tatu za kura zinahitajika.

  Baadhi ya wanasheria waliozungumza na Tanzania Daima Jumapili wamesema Mkapa anaweza kutoa ushahidi kwa upande wowote ila hatoweza kuwa mtuhumiwa kwani analindwa na Katiba ambayo inaweka wazi kuwa rais hatoweza kushtakiwa kwa kosa alilolifanya ama kwa bahati mbali au kwa kutotimiza wajibu wake akiwa madarakani.

  “Mkapa anaweza kuwa shahidi katika kesi yoyote ile si hizi wanazozitaja taja watu, lakini hatoweza kushtakiwa kwa kuwa Katiba inamlinda labda kufanyike mabadiliko katika katiba,” alisema mwanasheria mmoja ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini.

  Alisema suala la nani atoe ushahidi kwa upande wa mashitaka ni jukumu la waendesha mashitaka hivyo si rahisi kujua kama hali hiyo ikitokea Mkapa naweza kuwa upande wa mshitaka au kwa washitakiwa ambao walipandishwa mahakamani kwa nyakati tofauti.

  Mwanasheria mwingine alisema sheria ya nchi ya mwaka 1962 inaainisha wazi kuwa rais aliyepo madarakani hawezi kuitwa mahakamani kutoa ushahidi ila yule aliyestaafu anaruhusiwa kufanya hivyo ili mradi asiwe mshtakiwa katika kesi husika.

  “Rais aliyestaafu naweza kupandishwa kizimbani kwa kutoa ushahidi kwa mujibu wa sheria yetu ya mwaka 1962 ambayo inaweka wazi masuala haya, hivyo kama Mkapa ataonekana ni mtu muhimu katika kesi yoyote ile,” alisema mwanasheria huyo.

  Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wamedai kuwa endapo Mkapa atapanda mahakamani kutoa ushahidi wake, itakuwa kesi ya kihistoria kwa rais mstaafu kutoa ushahidi kwa waliokuwa viongozi wake waandamizi.

  “Kesi hii itakuwa na mvuto zaidi, kwani haijawahi kutokea rais mstaafu akapanda kizimbani kutoa ushahidi,” alisema mmoja wa wachambuzi.

  Hadi sasa viongozi watatu wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu Mkapa, wameshafikishwa mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi ya umma na kuisababishia serikali hasara inayofikia zaidi ya sh bilioni 11.

  Viongozi hao ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, Basil Mramba (Fedha) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Stay tuned mengi zaidi kuja na kutokeaa....yetu macho.....
   
 3. H

  Herbert Member

  #3
  Dec 22, 2008
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  This is realy very interesting comedy.
  Ila mimi natamani wabunge wakubaliane kumtolea raisi mstaafu protection la sivyo maraisi watakua wanatumia vibaya madaraka wakijua wako protected.

  Swala la ushahidi ni zuri ila what if alitoaga kimemo kuyapa baraka haya mambo ya kifisadi na jamaa wakawa wanacopy ya kimemo??
  Kesi itaendeleaje na mheshimiwa ana protection???

  Wataalam wa sheria jamani tusaidieni ili tupate mwongozo
   
 4. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2008
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bunge linaweza kutoa kinga kwa former president when there are some evidence of individual wrong doing, and this do not have to mean will apply to all future president..is this right? if yes why not bunge lipige kura?
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Dec 23, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  mpoki, masanja mkandamizaji, vengu, joti. Mac-regan, wakuvanga.
   
Loading...