Mkapa ana matatizo gani? Angalia na hili....

...Mkapa ana mapungufu yake, kama walivyo Watanzania wengine wote na Marais wote waliowahi kuitawala nji hii..

...lakini kama tukiwa-rank hawa wanne kwa waliyoyafanya katika nchi hii, hasa kwenye uchumi, Mkapa amewaacha akina Nyerere, Mwinyi na Jakaya kwa mbali mnoo..

...Hivyo mpaka pale atakapopatikana mzuri zaidi ya Mkapa na asiye na madhaifu ya Mkapa, bado ana haki yakutembea kifua mbele...

Una haki ya kumsifia, huenda ni kutimiza ule usemi wetu wa kisuahili ...asifuye mvua....

Mafanikio ya uchumi kwa kuuza bank, madini, mashirika ya umma, nyumba za serikali mbona ni rahisi kama kuteremka mlima? Hata mtoto wa darasa la nne ukimpa nafasi ya raisi wakati huo kisha ukamruhusu kuuza mashirika yaliyoanzishwa na Nyerere ataweza kukusanya pesa ya kutosha na kuonesha mafanikio ya muda. Subiri matokeo ya sera hiyo miaka michache ijayo ndiyo utajuuta kumfaham Mkapa mwenye kipara
 
naona ukizeeka ndio unaona mengi sana na ukiwa madarakani huwezi kuona mengi yeye alikuwa Rais kwa muda miaka10 lakini alilifikisha wapi tatizo na nishati dani ya nchi? hii nikama kutuhadaa tu. kweli kulia lia hakusaidii bali ni kuamua kila jambo nje ya hapo ni usanii
 
Sikiliza alichosema kwani aliyofanya mtu mwaka jana na leo yanalingana na hata hivyo ameshauri namna ya kuondokana na tatizo wewe badala ya kukubaliana nae na kumsapoti unapiga kelele njoo na njia yako ya kumaliza tatizo la nishati.

Maana unapokosoa mtu toa na wewe ufumbuzi wa tatizo. Hii ndio tabu yetu watanzania kukosoa bila kutoa ufumbuzi.

Tatizo ni kwamba huyo msemaji anakosa sifa za kusema hayo anayo yasema. Alikuwa na fursa ya miaka 10 kuongoza nchi hii kwa nini hakufanya hayo anayosema sasa? bali alifanya na bado tunaendelea kupata machungu ya hayo aliyoyataja BAK hapo juu. Hastahili kusamehewa na watanzania, ni msaliti.
 
Nyerere akilia asilie inasaidia nini?

NBC ilishakuwa hoi bin taabani inangoja serikali iiendeshe kama ilivyokuwa mashirika mengine yote ya umma, chali.

Tazama mabepari wameyachukuwa, mambo mazuri kabisa.
ni bora wakoloni warudi ili mambo yawe mazuri zaidi, hizi ni akili za kimagamba!@zombe
 
Mikataba mingi ambayo serikari yake ilisaini itaigharimi nchi hii kwa zaidi ya miaka 100 na ndiyo maana namchukia kweli kweli?
 
Mkapa.JPG


HABARI LEO

RAIS mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa, amesema matatizo ya nishati katika mataifa ya Afrika hayawezi kumalizika kwa kulia, bali kuwa na mikakati maalumu inayotekelezeka.

"Hata mkilia mpaka Mbinguni, lakini bila kuwa na mikakati bora na utawala bora kamwe hamtamaliza matatizo ya nishati katika nchi zenu," amesema Mkapa katika mkutano wa wakuu wastaafu wa mataifa ya Afrika uliokuwa ukifanyika jijini hapa.

Akiongoza mjadala kuhusu mustakabali wa kuwa na nishati ya uhakika juzi Mkapa alisema mataifa mengi yanayoendelea yamekuwa yakilalamika kukosekana nishati ya uhakika, lakini bila kufanya chochote cha kuondoa tatizo hilo.

Alisema pia dhana kuwa sekta binafsi ndiyo suluhisho la tatizo hilo ni potofu kwa kuwa Serikali zinapaswa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tatizo hilo linatoweka.

"Ni vema serikali zikawa na mipango mizuri kuanzia uzalishaji wa nishati mathalan umeme, usambazaji na upatikanaji wake wa watumiaji," alisema Mkapa.

STORI NZIMA HAPA


My Take:
Yeye kwa miaka 10 aliyokaa madarakani alifanya nini zaidi ya yeye naye kulialia? Hivi Mkapa wakati anauza makampuni yetu kama njugu alihakikisha vipi kuna nishati ya kutosha wakati makampuni yanafufuliwa au alifikiria watatumia nishati ya kuni?

Kumbe tunalia wenyewe tu, yeye sio mwenzetu tena? Doh!
 
Posts za Zomba zikinukuliwa zinaonesha kuwa ni nukuu ya Ribosome! Je, wataalam wa mitambo tuelezeni huu muujiza unatokana na nini? Mimi nilikuwa siku zote naamini kuwa Ribosome ni FF aliyekula ban ya maisha, je inawezekana kuwa Zomba = Ribosome= FF?

Mara nyingi huwa natatizwa na hoja za hao watautu katika utu mmoja wao kuwa, huwa wanasimamia masilahi ya nani? Taifa? au nin? Mara zote hoja zikimgusa Nyerere wanaanza kumshambulia, zikimgusa Dr Slaa wanaanza kushambulia kanisa na Pengo. Lakini hapa kwa Mkapa ambaye ni m-Kristo wanamsifu kwa kuwa aliuza mashirika na kuondowa mtizamo wa kijamaa wa Nyerere. Je, inawezekana hawa ni miongoni mwa mabepari waliodhibitiwa na Nyerere na sasa ndio mafisadi wanaotusumbua?
 
Kwenye kigoda cha mwalimu Mkapa alisema, hata kama kuna makosa ya kimaamuzi alifanya wakati wake, suluhisho ni kulalamika tu? akahoji, ''hata kama ni kweli naambiwa niliuza mashirika ya umma, mbona sijaona kiwanda hata kimoja kilichoanzishwa toka nimeondoka?'' - MM, hata kama hatutaki, hapa kuna hoja!

Ni kweli kuna makosa ya kimaamuzi na ufisadi wakati wa mkapa, lakini toka braza achukue nchi ni mwaka wa saba sasa, mkapa alipaswa awe amewajibishwa toka 2005 baada ya kutoka madarakani na sasa tungekua tunaongelea mambo mengine. Kama Mkapa ni Tatizo, Kikwete ni Tatizo kubwa zaidi

Mkapa ni mwizi kama mwizi mwingine yeyote. Hakuna hoja katika maneno yake, miaka saba baada ya yeye (Mkapa) kuchukua nchi alikuwa amejenga viwanda vingapi? Na wala asifananishwe hata kidogo na Nyerere kwani Nyerere alikuwa mwanaume wa shoka, alijenga viwanda na mashirika ya umma 360+ katika miaka 20+ ya utawala wake, yaani wastani wa takriban viwanda na mashirika 16 - 18 kwa mwaka. Watawala waliomfuatia wameshindwa kujenga hata kiwanda kimoja kwa miaka kumi kumi ya tawala zao.

My take:
Mkapa akae kimya hana cha kutuambia watanzania. Atuache tuendelee na mapambano ya kuinyoosha nchi yetu. Alituambia tu wavivu wa kufikiri sasa tunafikiri na siku moja atalipa mshahara wa maovu yake. Mchambuzi mmoja mahiri wa nchi hii alisema nami namuunga mkono, ili tuendelee tunahitaji mambo manne; uongozi bora, uongozi bora, uongozi bora na uongozi bora. Tutumie fursa ya kuandika katiba mpya kuweka misingi ya uongozi bora, tutakwenda mbele tu tena kwa kasi.
 
Kinachonisikitisha ni kuwa, Kikwete atakapomaliza ngwe yake ya pili ya "uongozi", atatuacha watanzania tukihesabu miaka 30 iliyopotea bure bileshi. Mwinyi +Mkapa+Kikwete. Kwa miaka 30 hakuna chochote kwa sababu ya kuchagua "viongozi" wasiokuwa na ajenda za msingi kwa manufaa ya wananchi.
 
Kwenye kigoda cha mwalimu Mkapa alisema, hata kama kuna makosa ya kimaamuzi alifanya wakati wake, suluhisho ni kulalamika tu? akahoji, ''hata kama ni kweli naambiwa niliuza mashirika ya umma, mbona sijaona kiwanda hata kimoja kilichoanzishwa toka nimeondoka?'' - MM, hata kama hatutaki, hapa kuna hoja!

Ni kweli kuna makosa ya kimaamuzi na ufisadi wakati wa mkapa, lakini toka braza achukue nchi ni mwaka wa saba sasa, mkapa alipaswa awe amewajibishwa toka 2005 baada ya kutoka madarakani na sasa tungekua tunaongelea mambo mengine.

My Take:
Kama Mkapa ni Tatizo, Kikwete ni Tatizo kubwa zaidi
Mimi namheshimu sana Mh.Mkapa kwa mambo aliyofanya hasa awamu yake ya kipindi cha miaka mitano ya kwanza.
Lakini ukweli lazima usemwe na akubali kuwa alifanya makosa ambayo inabidi yasahihishwe.
Hata Mwalimu alifanya makosa.

Katika kuuza mashirika na vitega uchumi vilivyokuwa vikiiendeshwa moja kwa moja na serikali, hapakuwepo mkakati tosha wa kizalendo ndani yake.Serikali ya Mkapa ilitegemea tu kuwa "the highest bidder secures" na si "the highest payer" for the going concern.
Sasa hivi kwa mazingira tuliyoweka,tulisema kuwa tunaweka ya kiuwezekaji lakini wanunuzi karibu woote waliendelea kuua kabisa viwanda/mashirika hayo, na wengine wakaenda mbali zaidi kukopea mali hizo walizopewa.

Wengi wa "wawekezaji" hao waliouziwa mpaka leo hawajalipia mali hizo.
Wapi Bora Shoes, wapi TANHIDES,wapi SUGURATEX,MWATEX.
Ni aibu kufanya maamuzi bila mchanganuo wa kina.

Sasa Mkapa anaposema, baada yake "ni viwanda vingapi vimeanzishwa", hivi alitegemea nini?
Ni ukweli usiopingika kuwa serikali kwa mazingira ya kuuza mashirika haingeweza kujenga viwanda vipya!
Vile vya binafsi na tulivyotegemea kuwa ni wawekezaji ni utapeli mtupu!

Hili ni fundisho kuwa tuwe makini katika kuendesha uchumi wetu tukitilia maanani kuwa na mikakati mikubwa iwe kuwaendeleza wananchi wetu na sio wa nje katika kuanzisha viwanda/miradi ya uzalishaji.
 
Wabe, kilichokufurahisha ni nini hapo? Kidhungu? Hoja? au Kuenziwa na wa-Sauzi kwa kuwapa uruwa katika nchi yetu takatifu? Nini unafurahia na Mkapa????

Kama ni hotuba za kufurahia ungetuwekea za kina Nyerere, Obama ..lakini siyo mashairi yaliyoimbwa zamani na magwiji wa ukweli. Mkapa mimi sitamsema sana, namjuwa, ni kiongozi feki hamjawahi kumjuwa...

Aisee Mkapa ananifurahisha kwa kila kitu, uongozi wakem misimamo, speech zake n.k. Unachosema is one of old songs, 'alikosea' kwa hilo niko na wewe...ila siwezi kumchukia kiasi hicho mtu ambaye at least alionyesha njia fulani, akina nyerere wote wana makosa yao tena terrible, obama unayemsema ana yake yanatisha..likiwamo la ndoa ya jinsia moja ambayo ni linaingia kwenye 'new world order'

mkuu when you hate someone so much others like him so much!! its normal, its natural
 
Kinachonisikitisha ni kuwa, Kikwete atakapomaliza ngwe yake ya pili ya "uongozi", atatuacha watanzania tukihesabu miaka 30 iliyopotea bure bileshi. Mwinyi +Mkapa+Kikwete. Kwa miaka 30 hakuna chochote kwa sababu ya kuchagua "viongozi" wasiokuwa na ajenda za msingi kwa manufaa ya wananchi.

+28 ya Nyerere!! acha uoga wewe , Nyerere may be alikuwa worse kuliko hao wote hapo juu!! usipime
 
Huyu ni MWIZI tu ambaye ameamua kubwabwaja kila anapopata nafasi lakini wizi alioufanya kupitia ununuzi wa rada, uuzwaji wa nyumba za Serikali, Kukwapua Kiwira, ununuzi wa ndege ya Rais akiwa kabakisha miezi mitatu tu kumaliza awamu yake, wizi kupitia netgroup solutions, ununuzi wa helicopters na magari ya jeshi na hadi hii leo hataki kuzungumzia kuhusu ni nani aliyekuwa anafanya naye biashara alipokuwa Ikulu.

Huyu jamaa anatunanga kwa maneno, akiona tuna dhamira ya kumfikisha mahakamani kwa uozo na wizi alioufanaya atafunga mdomo. Huyu ni wa kuvutia pumzi maana angeandaa mazingira mazuri haya yasingetupata. Yeye pia ni sababu kubwa ya kilio chetu
 
Alifanya hivyo kwa kutumia pesa za nani ?Jee ilikuwa ni hisani yake tu kuwafanyia hayo wa Tanzania au niwajibu wake?wacha wewe wa Tanzania wana hali ngumu tena ngumu sana usione wanacheka na kufurahi pamoja hali halisi familia nyingi za kitanzania zinateketea kimaisha

Mkapa alijitahidi bana, hali haikua mbaya kipindi chake kama ilivyo sasa!, tusimbebeshe makosa ya JK.

Kwa kweli hali kwa sasa hata mtoto mdogo anaijua kuwa ni mbaya sana! Hayo yanayotokea zanzibar yote ni njaa! Hata USA kungekua na njaa kama hii majimbo yangekua yameshajitenga.
 
Aisee Mkapa ananifurahisha kwa kila kitu, uongozi wakem misimamo, speech zake n.k. Unachosema is one of old songs, 'alikosea' kwa hilo niko na wewe...ila siwezi kumchukia kiasi hicho mtu ambaye at least alionyesha njia fulani, akina nyerere wote wana makosa yao tena terrible, obama unayemsema ana yake yanatisha..likiwamo la ndoa ya jinsia moja ambayo ni linaingia kwenye 'new world order'

mkuu when you hate someone so much others like him so much!! its normal, its natural

Nimekupata vizuri ...
Mimi simchukii kama Mkapa, huyu jamaa ni wa kwetu kabisaaa ... ha ha ha! Lakini uongozi wake naufananisha na triangular waves, unatowa unachukuwa, net inakuwa zero. Huyu jamaa namfahamu wewe humjuwi. Ni mwizi na ana dharau na kibri haina kiwango. Lakini ni mwoga sana ndio maana hupenda kuongea kwa jazba na vitisho.

Nakubali kuwa Nyerere ni old song, lakini hata yeye ni old song pia. Tuna kina Zito, Dr Slaa, Lema na wengine ambao ni more current na wanaleta matumaini kwa nchi. Acha kushabikia majizi utafanana nayo..

Nakubali Nyerere ana makosa, lakini makosa ya Nyerere hayakutokana a ubinafsi na ulafisi kama wa huyo home-mate wangu na rafiki yako. Makosa ya Nyerere ni sawa na makosa ambayo baba anaweza kufanya lakini akisukumwa na mapenzi ya familia yake. Naomba usilinganishe Nyerere wetu na Mkapa wangu, haviendani.

Waberoya, kuhusiana na Obama. New world order ni pamoja na huyo Mkapa ... hivi hujuwi? Pole ndugu yangu...yapo makubwa .... achana na Nkapa wa kwetu ni mwizi na mwuaji ...
 
Mkapa ni janga la kitaifa, pia ni boriti inayomtafuna Kikwete kiana.

1. Mandela katika hotuba yake iliyofanyika bandarini, alimwonya mkapa kutouza mashirika ya uma hasa yale ya msingi na faida kwa nchi. Alijiuzia Ticts kwa miaka 15, halafu akajiongezea mingine 10 kinyemela na Kina karamagi. Pamoja na speech anayodaiwa kusifiwa humu (SA), Mandela hakuhudhuria na hakutaka kuonana na Mkapa tena fuatia jitihada za Mkapa kutaka aonane naye.

2. Mkapa ameongelea utawala bora, kibaya zaidi ni kuwa yeye akiwa kama Rais alishindwa kufanya hilo. Alifungua kampuni binafsi na mkewe akiwa ikulu (AnnBen), kinyume na sheria za utawala bora. Alizuia wachina kupewa Kiwira kwa bei ya juu, matokeo yake akajiuzia kwa bei chee mgodi ule, huku akiingia mkataba na tanesco wakulipwa mamilioni kwa siku, ukiacha mabilioni aliyopewa kwa dhamana ya serikali kwa ishu hiyo tu.

3. Ndege aliyojinunulia, rada chakavu iliyowekwa cha juu ni vitu ambavyo watanzania hawakuwa na umuhimu navyo, ndiyo ilikuwa dira yake, hapa siongelei Net-Group Solution ambayo mwane Nc alikuwa mmoja wa wakurugenzi waliokuwa wanalipwa siyo chini ya 20m kwa mwezi, na hapakuwa na lolote. Achilia mbali kuwa makampuni mengi ya nishati yanayo tunyonya yalisainiwa wakati wake.

Kinachokera watu hapa ni kuwa, anachohubiri siyo alichokifanya na matokeo ya aliyoyafanya ndio maana leo Tanzania ina matatizo ya umeme, madini, gesi, maji n.k! Tuzo ya Rais bora ambayo hutolewa kila mwaka na MO-Ibrahm, haijawahi kuona kutukuka kwake na huwa anaiotga. Hiyo nchi ya bondeni wana haki ya kumpa tuzo watakayo kwani, Tanzanite yetu wao ndio yao, alishawapaga migodi na haki zote. NBC aliyokuwa anaipigia debe iuzwe huko bondeni, imechoka na tayari ishauzwa kwa benk ingne.

Kwa swala la nishati, madini, maji NKapa hatakiwi kunyanyua mdomo wake, kwa hata Transparency International, walimwambia Jakaya katika jitihada zake za kurudisha migodi kwa wananchi au kuwepo na uwiano wa mapato, kuwa hana cha kufanya bkoz mtangulizi wake Ben, alishafunga loki zote.

Kibanga Msese
 
+28 ya Nyerere!! acha uoga wewe , Nyerere may be alikuwa worse kuliko hao wote hapo juu!! usipime

Nyerere? Nyerere yupi aliyetawala kwa miaka 28? Achilia mbali haikuwa point yangu hiyo. What legacy will we attach to the trio? Honestly, what?
 
Katika hali ya kawaidi Mkapa amefanya mengi mazuri..ila aliharibu sana tena vibaya miaka 3 ya mwisho sijui alikuwa anawazia nini. Tena uharibufu wa mwisho umechangia sana hata kumharibia JK kutake-off vizuri. Pamoja na hilo ananiudhi zaidi pale anapojiona as if hakufanya makosa makubwa ie kujigawia nchi kama shamba/kampuni yake binafsi. Ukitaka uheshimiwe kubali makosa na uwashauri wenzio wasifanye kama ulivyofanya wewe. Hata Nyerere alisema tuige yale mazuri mabaya tuyaache maana alifanya mengi mabaya.
 
Kibanga, umeweka muhtasari wako vizuri na umemaliza yote... tuko pamoja sana mkuu
 
Back
Top Bottom