Mkapa aliweka ripoti ya Jaji Warioba Kabatini, Tuseme ukweli

Amani iwekwenu.
Jana tumemlaza mzee wetu kaburini. Ni bwana BWM.

Huyu ni raisi wa awamu ya tatu wa Tanzania. mengi yalisemwa ya kweli na ya uongo. ni hulka ya mtu mweusi.mfanowe ni musiba, huyu alimwita marehemu mwizi lakini juzi aliibukia msibani hata kupiga magoti mbele ya mjane. mnafiki mkubwa.

Nakuja kwenye hoja. mwaka 1996 baada ya BWM Kuingia madarakani aliunda tume "TUME YA JAJI WARIOBA" tume ilichunguza vitendo vya rushwa na mianya yake ncini Tanzania.

Kwa weledi mkubwa kabisa, Mzee Warioba alifanya kazi yake vizuri na kumkabidhi bwana mkubwa ripoti ya tume yake.

Tume ilisheheni mambo mengi na ilibainisha maeneo mengi yaliyokubuhu kwa rushw awakati ule. ikiwemo polisi, mahakama na serikalini kwa ujumla achilia mbali siasani.

Warioba alimkabidhi BWM ripoti ile ni MKAPA huyu anaysifiwa leo akaitupa KAPUNI kama vile sio yeye aliyeiunda. hapakuwa na hatua yeyote ya maana iliyochukuliwa kuziba mianya zaidi ya kuipanua na kuwa KORONGO.

BWM hakuishia hapo aliunda Tume ya jaji Simkumbuki vizuri kama ni Kisanga au nani. Hii Tume ilichunguza mambo ya muungano baada ya kuletewa taarifa za tume bwana MKAPA alimtukana na kumnanga yule jaji pale Dimondi jubleel kwamba aliandika asiyomtuma.

BWM aliwananga na kuwadharau wanahabari wetu akiwaita hawajui kufanya tafiti na wenye wivu wa kike wakiwemo watanzania wote waliohoji ufisadi wake. marehemu alikuwa mwenye kiburi na mjivuni haswa

Ni BWM ambaye katika awamu yake rushwa ilibadilishwa jina na kuitwa TAKRIMA. kwamba mwanasiasa kutoa rushwa halikuwa kosa bali ilikuwa ni takrima siyo kweli kwamba alipambana na rushwa semeni ukweli

Huyu BWM mnayemuita shujaa leo ndiye aliyeuza banka ya NBC kwa makaburu tena siku isiyo ya kazi kwa bei ya kutupwa. ni yeye huyu aliyetumia anuani ya Ikulu kukopa mkopo binafsi kwa ajili ya kununulia jumba la kifahari.

Huyu BWM alijimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa KIWIRA. Yeye na mkewe walianzisha bank wakiwa bado ikulu

Alitangaza mali zake kwenye tume ya Maadili wakati anaingia madarakani ila hakufanya hivyo wakati anatoka ikulu

Aliuza nyumba za Serikali kwa bei ya kutupwa. hadi baadhi ya mawaziri kama bwana JPM akwawapa mahara na vimada wake.

Mkapa alihongwa mnara wa dhahabu huko Geita. alinunua mashamba ya miwawa na kuibinafsha TANESCO kwa NETGROUP SOLUTION ya SA. akisema haangalii rangi ya paka anaangalia uwezo wa paka kukamata panya

KAGODA, MEREMETA, EPA na kila aina ya ufisadi mkubwa ulitokea enzi za BWM anakuwaje shujaa huyu?

Pumzika unapostahili mzee wangu hakika awamu yako rushwa ilitamalaki.
Ripoti yake ndiyo iliyopelekea uundwaji wa Idara mbalimbali za Serikali Mfano Takukuru
 
Back
Top Bottom