Mkapa alitumia 2.65bln Kusuluhisha Kenya!

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Kwa Mujibu Wa Mbunge Aliyechangia Bungeni Leo Imetolewa Taarifa Na Waziri Hawa Ghasia Kuwa Eti Mkapa Alitumia Bilioni 2.65 Yaani Kwenda Kusuluhisha Kenya Hii Ni Kashfa Nyingine .

Na Tena Katibu Mkuu Wa Wizara Alimwambia Mbunge Huyo Kuwa Eti Ni Kutokana Na Delegation Ya Mkapa Kuwa Kubwa , Sasa Kumbe Hakuna Maana Ya Kujifanya Wasuluhishi Kwani Kama Gharama Ni Hizo Tunaliumiza Taifa .

Kesho Watatoa Tamko La Serikali Bungeni Asubuhi, Sasa Hii Ni Kazi Kweli Kweli.
 
what? labda hujasikia vizuri Mkuu, inawezekana ni 2.65M. Kama jina lako lilivyo hapa mapaka kieleweke.
 
Hizo pesa za usuluhishi wa KENYA HIVI MAJUZI?
Tena baada ya kashfa zote hizi?
Ama kweli Kikwete alitaka amsafishe jamaa yake.
Kwani jamaa aliitumia nafasi ya mgogoro ule wa Kenya kukimbia kelele za UFISADI!
Sasa wako nyumbani na ukweli wote uwekwe wazi.
Itakuwa vipi serikali itumie fedha zote hizo na wakati si haki kuendelea kumlisha fisadi ambaye sasa anamiliki TAIFA NA WATU WAKE?
 
Amejibu Hawa Ghasia Akitaka Kupotosha Na Aliposimama Zitto Kutaka Kanuni Zitumike ,mwenyekiti Wa Mjadala Aliitaka Serikali Kwenda Kuleta Majibu Ya Kina Kesho Na Kuufunga Mjadala .

Wanaofuatilia Bunge Wanaweza Kutoa Ushahidi Hapa .
 
Sasa Mkapa alitumia feza ya serikali kama nani ? Na nani alieizinisha donge lote hilo ,yaani hapa nashangaa ,hawa wezi wanaposikia Clinton ameenda kusuluhisha wanazani feza inatoa serikali na si kwamba hawajui ila wanatufanya WaTanzania ni mambumbumbu.
Kama Mkapa alikwenda huko kusuluhisha basi angelitumia fedha yake mwenyewe sasa ikiwa Mkapa ambae si raisi tena wala hayuko katika asasi yeyote ya kidiplomasia katika serikali hii alichotewa kiasi hicho je Mkuu wa Misafara ambae ni Raisi wa Tananzia na Mwenyekiti wa AU alimegewa kiasi gani ? Naona na huyo mmegaji kisu chake hakikukosa gundi.
Ila haya mambo yana mwisho.
 
nadhani kunapokuwa na mediation, kanselieshen o eni adha pis proses ni jukumu la eidha UN,AU au EAC kugharimu.....!
bado nafikiri ni pesa toka UN au AU...!
 
what? labda hujasikia vizuri Mkuu, inawezekana ni 2.65M. Kama jina lako lilivyo hapa mapaka kieleweke.
Jamani mbunge kasema bilion sio m kama unamashaka na limeleta mzozo bungeni kama kawaida kuna baadhi ya mibunge kule ndani ni kama watoto mi sijui mana walianza kupiga kelele wenzao akina zitto wanaomba mwongozo wa spika wanakataliwa wakaamua kuongea na makelele yao.
 
Amejibu Hawa Ghasia Akitaka Kupotosha Na Aliposimama Zitto Kutaka Kanuni Zitumike ,mwenyekiti Wa Mjadala Aliitaka Serikali Kwenda Kuleta Majibu Ya Kina Kesho Na Kuufunga Mjadala .

Wanaofuatilia Bunge Wanaweza Kutoa Ushahidi Hapa .
Ni kwamba huyu mbunge alipokuwa anachangia akasema alitaka kujua kiwango cha hela wakati wa usuluhishi wa kenya kwa nini kiliongezeka kama sijakoseana majaibu aliyopwa ni hayo ya delegation lakini na mHawa ghasia na akaongeza ziliongezeka kwa ajili ya matibabu ya viongozi wengine wastafu. kama nimekosea mnaofutilia bunge rekebisheni
 
Kwa Mujibu Wa Mbunge Aliyechangia Bungeni Leo Imetolewa Taarifa Na Waziri Hawa Ghasia Kuwa Eti Mkapa Alitumia Bilioni 2.65 Yaani Kwenda Kusuluhisha Kenya Hii Ni Kashfa Nyingine .

Na Tena Katibu Mkuu Wa Wizara Alimwambia Mbunge Huyo Kuwa Eti Ni Kutokana Na Delegation Ya Mkapa Kuwa Kubwa , Sasa Kumbe Hakuna Maana Ya Kujifanya Wasuluhishi Kwani Kama Gharama Ni Hizo Tunaliumiza Taifa .

Kesho Watatoa Tamko La Serikali Bungeni Asubuhi, Sasa Hii Ni Kazi Kweli Kweli.

Alikuwa anakaa hoteli ya peponi? Watupe break down alikaa Nairobi siku ngapi? Bei ya chumba au nyumba ilikuwa ni kiasi gani? Breakfast, lunch na dinner zilikuwa mi kiasi gani kwa siku na huo usafiri wa kutoka Nairobi ambapo alitumia ndege expensive kuliko zote duniani 'Concorde' walikuwa wanamlipia kiasi gani. Huu ni wizi wa mchana kweupeee! Duh! Mafisadi wanafyoanza tu hawana hata huruma na nchi yetu!!!
 
Sikio la kufa halisikii dawa; njia nzuri ya kumponyesha mama Tanzania ni kulikata kabisa sikio hilo na kulitupilia mbali.
 
kama yaliyoletwa hapa ni kweli,basi ni bora kila mtanzania agawiwe chakwake,ili kila mmoja wetu atafute pa kwenda baada ya kupata urithi wake.
 
kwa mtaji huu naelewa kwa nini tanzania hakuna huduma bora za jamii na miundombinu ni duni kabisa. Kwani ilikuwa lazima kwenda kupatanisha? hawakufanya cost analysis before kabla hawajatuma delegate? au ndo kukurupuka kwa kwenda mbele.
 
kama yaliyoletwa hapa ni kweli,basi ni bora kila mtanzania agawiwe chakwake,ili kila mmoja wetu atafute pa kwenda baada ya kupata urithi wake.

Inamaanisha unataka tupige nchi bei halafu yaishe nini?

Hila huyu baba kazidi kweli hivi inamaana alikuwa anajimwagia pesa au nini?

Hawa naona hawajui kabisa vipato vya watawaliwa.
 
Kwa jinsi nilivyofuatilia, inaonekana yule Mhe. ni mjumbe wa kamati ya Utawala Bora, walivyokuwa wako kwenye kamati kujadili bajeti ya Ofisi ya Rais ilionekana kuwa kuna ongezeko la matumizi kutoka Bil 6 hadi 12, ikabidi amuulize katibu mkuu Bw. Yambesi, na akajibiwa kuwa Sh. 2.6bilioni zilitumiwa na Mkapa wakati wa mgogoro wa Kenya. Wakati mabishano yanaendelea leo bungeni, Bw. Yambesi akatuma ki note kwa Ghasia kuwa si kweli, fedha hizo ziliongezeka kwa sababu ya gharama za matibabu na kuongezeka kwa idadi ya viongozi wastaafu. Ingawa ukweli inaonekana awali Bw. Yambesi aliiambia kamati kuwa zimetumika kusuluhisha Kenya, lakini kama kawaida, tutapigwa changa la macho, kesho watasafisha. Jamani serikali imeshikwa pabaya, mlio mstari wa mbele aluta continua
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom