Mkapa Aliiogopa Katiba Mpya...Je! Kikwete Anaandaa Upinzani Kushika Dola? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa Aliiogopa Katiba Mpya...Je! Kikwete Anaandaa Upinzani Kushika Dola?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by eedoh05, Oct 30, 2012.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Wakati wa Utawala wa Mkapa suala la kuandika katiba mpya lilikuwa ni chungu kuliko hata uchungu wa mwarobaini. Nilimsikiliza Mkapa akijibu matokeo ya Tume yake Mwenyewe juu ya katiba. Ali-fume kweli kweli kuona dokezo la kuandika katiba mpya katika ripoti ya tume ile. Akikejeli hata tume yenyewe.

  Mkapa aliogopa katiba mpya na anaiogopa hadi sasa kwani hajui mustakabali wake na wa CCM baada ya katiba mpya. Kinachomtisha ni kuwa na katiba itakayotoa mwanya kwa vyama pinzani kuchukua dola.

  Kwa upande mwingine, inaonesha Kikwete haioni hofu walionayo wenzie ndani ya chama. Yeye anaonekana kuandaa mazingira sawa kwa chama cho chote kushika dola. Kwa katiba mpya yamkini kukawa na tume huru ya uchaguzi isiyochini ya rais. Takukuru isiyo chini ya rais, mahakama huru, bunge kutenganishwa na serikali (wabunge wasiwe mawaziri) nk.

  Katika haya, Kikwete anawaandalia wapinzani kucheza kwenye uwanja sawa na chama kilicho madarakani. Kwa hili, Kikwete ataingia kwenye historia ya Tanzania, Africa na Duniani kwamba alithubutu.
   
Loading...