Mkapa aliandaa shamba akalima akapanda akatunza adi kukomaa akampa kikwete avune sasa anakula mavuno | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa aliandaa shamba akalima akapanda akatunza adi kukomaa akampa kikwete avune sasa anakula mavuno

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by popobawa2012, Jul 19, 2012.

 1. p

  popobawa2012 Senior Member

  #1
  Jul 19, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wanajf wenzangu naomba tukumbushane kidogo tu kuhusu hili tatizo sugu la ufisadi! G
  kwa kweli kabisa kama sisi ni watu fair (unbiased) basi mtu anaitwa MKAPA ndo hasa alietuacha hapa leo katikati ya hili jangwa kubwa la UFISADI bila ata dira ya kutuonesha wapi tutokee ili tujiepushe na balaa hili. SABABU

  1.Huyu ndie hasa alieanzisha ufisadi uliotukuka kuliko rais yeyote kuwahi kutokea apa TZ, ktk kipind cha miaka 10 alipiga bei fastafasta mali za umma kama kichaa uku yeye na rafik zake wa karibu na mkewe wakiwa ni beneficiaries in one way or another kwa mfano NBC licha ya kukatazwa na baba wa Taifa aliempa nchi yeye aliuza kwa bei ya kutupa, TTCL, ATC, TANESCO Management, nyumba za serikali, viwanda n.k n.k
  hizo ni mali ziliztafutwa na umma sasa kuna mali za umma alitupa Mwenyez Mungu kwa mapenz yake kwa watz, migodi ya dhahabu, tanzanite,almas, makaa ya mawe, nia yake nchi hii kila kwenye mgodi yabaki mashimo na nyumba biscuti za wenyej ndo furaha yake! vitalu ktk mbuga za wanyama ndo usiseme: kabla ya hapo hapakuwai kutokea haya
  2.huyu ndie aliwatetea kwa nguvu zote wawekezaji wasio na tija waje wafanye adhalimu huu hapa nchini mfano mzur NETGROUP SOLUTION waliingia kwa mtutu wa bunduki coz wananch waligoma, ata hivo hao net group walionekana hawana jipya. hivo basi kipind chake ilikua ngumu ata kuhoj mambo ndo mana nchi ikatafunwa vilivo. tofauti na leo au kabla yake.

  3.huyu ndie alietetea sana mafisad wenzake kua ni watu waadirifu; lilikua linasema tatizo watz ni WAVIVU,WAZUSHI, WANA WIVU NA WASIOPENDA KUFANYA KAZI matokeo yake akazalisha mafisadi wa nguvu adi hawashikiki! mathalani leo hii mtu anaitwa CHENGE humuwezi ata ufanyaje mana ana nguvu ya pesa karibu ama sawa na ya serikali na wengine wengi kama rostam, white hair, n.k yaani hawa hata wakosee dola dhaifu hii haina cha kuwafanya. Kwa mfano rostam aligoma alipotwa na kamati ya BUNGE! Hadi leo ndo kwanza anaheshimika zaidi;wote hawa walizalishwa na mtu anaitwa MKAPA.

  mengine mnaweza yaongeza hapo lakini kwa ujumla wake MKAPA aliiweka nchi mahali fulan pabaya kabisa kwa anaemfuata lazima angekutana na mziki mnene ndo huu JK anacheza adi anashangaa!
  Kumbe huyu JK ambae naungana na Mnyika kua ni dhaifu anajitahid sana kurectify weather hii mbovu aliopewa na lile jamaa kwa kweli pamoja na UDHAIFU wake JK, amejitahid sana kwani mkapa alimwachia BOMU LILILOIVA.
  Pamoja na hayo MKAPA aliweza kustabilize shiling, hazina kua na pesa, uwanja wa taifa na daraja la mkapa: tatizo mabaya yalikua mengi sana kias kwamba kwa sisi wanahisabati tuna assume kama yale mazuri ni sawa na hayapo KABISA kama tukicompare na mabaya yalio kua mengi kupitiliza.

  sasa basi uyu MKAPA ndo haswaa wa kulaumiwa na kama me ningekua naweza ningemuondolea kinga ashtakiwe na akikutwa na hatia ANYONGWE ADI AFE mana yote haya ya leo kuanzia migomo ya vyuoni, Ulimboka adi meli kuzama kila mwaka, chimbuko lake ni MKAPA japo na waliojihusisha na hayo mambo nao wangeambulia jela za maisha tue kama CHINA nchi hii itasonga mbele.
  huo ni mtazamo wangu tu
   
 2. Zagazaga

  Zagazaga JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 519
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  hujui unalonena wewe..piga kimya
   
 3. M

  Mkuki JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 363
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Fanya kazi acha kumlaum mzee wetu mkapa muache apumzike kazi aliyoifanya ni kubwa huioni?
   
 4. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  "jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza"
  Hajui analoliongea. Mzee mwinyi ndiye aliye asisi ufisadi kwa lile Azimio la Zanzibar. Kuwaruhusu vuongozi kufanya Biashara.Na pia ndie aliyeanza kubinafsisha viwanda, ikiwemo TBL, sigara n.k.Kipindi cha Mkapa watu tayari walikua wameishaelevuka namna ya kupiga Dili ndio maana inavuma kwamba ni yeye.

  Zigo lote la lawama huwa namtupia Mzee Ruksa.Ukitaka kujua fuatilia Hotuba ya Nyerere Mby siku ya Mei mosi.Nyerere alilalamika walipokua wanataka kubinafisha kiwanda cha sigara.Yule mzee kumbe alikua anaona jamaa walikokua wanatupeleka.
   
 5. p

  popobawa2012 Senior Member

  #5
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jibu hoja acha porojo!
   
 6. p

  popobawa2012 Senior Member

  #6
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwa mana io wewe adi leo unaamini kweli watz hatuwez kumanage tanesco, nyumba za serikali hazina maana, ni sahihi kuuza vitalu kwa wagen, kuuza madini kwa mrahaba wa 3% kwako ni poa tu, ni sahih kua na nchi ambayo haina benk ya Taifa ya biashara NBC, bei ya NBC ya kutupa kwako c tatizo, na pia madhara yote ya watu kupoteza ajira kutoka NBC kwako inakupendeza, acha unazi na siasa za chuki kama ni udhaifu wa jk me cjabisha namkubali mnyika kwa kauli yake lakin kuna mengi tu JK kafanya ata Mayala Pasco alishawawekea apa JF acheni chuki! jibu hoja
   
 7. p

  popobawa2012 Senior Member

  #7
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  jibu hoja acha porojo!
   
 8. p

  popobawa2012 Senior Member

  #8
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sawa cheichei lakini unapaswa kuzingatia kua yeye alikua na dola na kwa wakat ule hukukua na UNTOUCHABLES wa nguvu kama ilivo sasa alishindwa nini kufutilia mbali kabisa janga ilo katka wakati ambao hulijaota mizizi tena minene kama wakati huu!??? acha jazba na unazi usio na maana coz ata elimu tu Mzee wetu RUKSA na lili JAMBAZI MKAPA hawafanani so tulipompata mkapa tulidhan yeye angerekebisha but for sure alikoleza chumvi kwenye kidonda au wewe hulion hili tafadhari!
   
 9. fisadigamba

  fisadigamba Member

  #9
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaumiza kichwa chako bureee popobawa hapa tayari ushaingia udini, kila mmoja kwa wenye ufinyu huo wa mawazo atavutia kwake. huyu Ruksa yule mzee wa Uwazi. Nchi hii!
   
 10. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wewe umetaja weakness za Mkapa ungetaja na mafanikio yake ili tuone kama kweli unachosema kina uzito wowote vinginevyo hizo zitabaki kama porojo za mitaani. Hayo mashirika uliyotaja ilikuwa lazima yauzwe maana mengi yalikuwa dhoofu kabisa yalipouzwa ndio angalau yakapata uhai.
   
 11. p

  popobawa2012 Senior Member

  #11
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ushaanza udini! kweli ww huna maana, mimi ni mkristo tena safi lakin siwez kuacha kusema ukweli eti kisa nisimseme mkapa mkristo mwenzangu zigo lote apewe JK coz ni muislam au RUKSA ambae pia ni muslam, mtazamo pofu kama huo haufai apa mjomba hio ni dosari kubwa sana ktk ubongo wako, KUA KIFIKRA MJOMBA! ni ushauri tu
   
 12. p

  popobawa2012 Senior Member

  #12
  Jul 20, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kama kawaida yako hujasoma vzuri hoja nmetaja vzuri tu mema yake lakin hujaweza kusoma mjomba!! kuhusu uuzaji huo je ndo ulipasa kufanyika ivo!!???
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Bora aliyeuza kwa bei rahisi kuliko aliyetoa bure.Kwani yeye ndie alifanya auction?Kama unathubutu sema makosa ya JK ni ya watendaji wake kwanini na mkapa yasiwe ya watendaji wake?Kwa taarifa yako Mkapa publicly na vitu alivyovifanya directly alifanya vizuri na wajinga wajinga wa type ya JK hawakuweza m beat kwa hoja ndio maana wanamwita dictator kwa vile alikuwa jasiri.Mkapa aliunda PCB, tume ya kurekebisha sheria, TRA, na taasisi nyingine nyingi, kilichoharibika ni kuwa Usalama wa taifa ulikuw aukifanya kazi kwa huu utawala na kuweka mamluki kila mahali, na sasa hawana option nyingine zaidi ya kumchafua ili kumlinda JK.

  Sasas kama vimeo kama akina werema na chenge walishindwa soma mikataba na kuitekea haki kitaaluma na si kisanii, kama polisi na wengine wangefanya kazi vizuri, kama wachumi wetu na negotiators na deal breaker wetu wangekuwa competent enough wange tupa bei njema, sasa hawa takataka wa UDSM ambao hata wanafunzi wao wamewazidi uelewa baada ya kuenda jifunza mapya uraian huku wakitaka kuwa wamiliki wa elimu ya bongo ndio matatizo zaidi.Kazi kupika data kwa manufaa ya CCM.
   
 14. B

  BMT JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  popobawa,nenda kajipange hatudanganyiki kamwe,hivi kweli wananchi maisha walioishi kpndi cha mkapa na kikwete huoni kuna tofauti?mkapa alilipa madeni yote sugu na alitmia pesa za ndan kwa maendeleo,leo hii jk wetu kaongeza deni kufikia trilion 20,kashusha mfumko wa bei toka asilimia 30 mpaka 4,mafanikio ya mkapa ni mengi mno,
   
 15. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2012
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,867
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Turejee quotation hizi, si maneno yangu:

  "Problems cannot be solved by the same level of thinking that created them" - Albert Einstein

  "Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Rais Jakaya Kikwete, kwa uzembe wa Bunge na kwa sababu ya upuuzi wa CCM." - Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), John Mnyika
   
 16. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,629
  Likes Received: 9,847
  Trophy Points: 280
  mtoa mada unaongea vitu vya msingi sana japo baadhi vina mapungufu...

  Unapozungumzia mafanikio ya kiongozi wa wananchi kwa anaowaongoza lazima yawe "people centered" ... kama utaweza kushusha mfumuko wa bei, ajira zikapatikana, ardhi ikalindwa isiuzwe hovyo hovyo, haina shida kuwa utakua umegusa maendeleo ya wananchi moja kwa moja japo pia nchi inawezekana ikawa ina hali mbaya..tatizo jk vyote kavurunda.
   
Loading...