Mkapa akwepa maswali ya wasomi adai naye ni mwanafunzi

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
Na Burhani Yakub Lushoto

RAIS wa serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa jana alikuwa kivutio wakati alipopangua maswali ya wanafunzi kuhusu wimbi la migomo kwenye vyuo vya elimu ya juu, akisema na yeye "sasa ni mwanafunzi mwenzao".

Mkapa alikuwa Chuo Kikuu cha Sekuco kilicho wilayani hapa akiwa amealikwa kutoa mada katika mdahalo wa wazi wa wanafunzi wa chuo hicho kikuu kishiriki cha Tumaini. Mkapa alishangiliwa sana na wanachuo kutokana na umahiri wake wakati wa kuwasilisha mada yake.

Lakini hali iligeuka wakati wa kipindi cha maswali baada ya naibu mkuu wa chuo hicho, Dk. Fanuel Shechambo kuwapa wanafunzi nafasi ya kuuliza maswali.

Mwanachuo aliyejitambulisha kwa jina la Ogaka Lameck wa mwaka wa kwanza ambaye anasomea Ualimu, alimtaka Mkapa kueleza kwa nini serikali inakwepa kutekeleza jukumu lake la kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo kikuu na hivyo kusababisha migomo ya mara kwa mara.

Mwanachuo huyo alifafanua kuwa migogoro ya wanafunzi ilikuwepo katika awamu zilizopita, ikiwemo ya Mkapa, lakini akasema kwa sasa migogoro hiyo inaonekana kuzidi na hivyo kuhoji kwa nini zisitafuwe njia za kuitatua kutokana na ukweli kuwa wasomi wa vyuo vikuuu ndiyo rasilimali ya maendeleo ya nchi.

Lakini Mkapa hakutaka kutoa maelezo marefu kujibu swali hilo akijitetea kuwa ameshamaliza kipindi chake cha uongozi na kwamba hivi sasa anasoma, ingawa hakutaka kuelezea anasomea nini.

"Mimi si rais kwa sasa," alisema rais huyo aliyeiongoza nchi kutoka mwaka 1995 hadi 2005. "Mimi ni mwanafunzi kama nyinyi... hamuoni kama mnatumia muda wenu kumuuliza maswali mwanafunzi mwenzenu,"aliongeza na kusababisha wanafunzi ukumbi wote kucheka.

Mkapa aliwahi kuongoza Wizara ya Sayansi na Elimu ya Juu mwanzoni mwa miaka ya tisini baada ya kumalizika kwa mgomo mkubwa wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam mwaka 1990 uliosababisha wanafunzi kurudishwa nyumbani kwa takriban miezi nane.

Katika kipindi chake cha urais hakukumbana na migomo mikubwa ya wanafunzi.

Katika siku za karibuni serikali imelazimika kufunga vyuo vikuu saba baada ya wanafunzi kugoma kuingia madarasani wakishinikiza kupewa mkopo kwa asilimia 100 badala ya utaratibu wa sasa wa kuchambua uwezo wa kiuchumi wa mwanafunzi na baadaye kuamua alipie kwa asilimia ngapi. Hata hivyo, serikali imekataa katukatu na kueleza kuwa sera hiyo ya uchangiaji elimu itadumu.

Akiwasilisha mada ya "Wajibu wa Elimu ya Juu Katika Maendeleo," rais huyo mstaafu alisema ili kujenga maendeleo ya kweli ni lazima kuwe na uwiamo katika utoaji wa elimu kwa kuzingatia jinsia na makundi ya walemavu.

Alisema kufanya hivyo kutasaidia kutawanya ujuzi na hivyo kuiwezesha jamii kuwa na uwezo wa kujitegemea.

Katika mada yake Mkapa alisema kwa Tanzania na nchi zinazoendelea ni lazima wasomi wa elimu ya juu waondokane na kasumba ya kutegemea kuajiriwa baada ya kuhitimu masomo na badala yake wajikite katika kubuni njia za uzalishaji na ufundi.

Akitoa shukrani kwa Mkapa, askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, DK. Steven Munga alimsifu kwa umahiri alioonyesha wakati akiwasilisha mada hiyo.

Dk. Munga, ambaye Dayosisi yake ndiyo inayoendesha chuo hicho alisema uongozi uliamua kumwalika Mkapa kutoa mada hiyo ikiwa ni mipango yake ya kuwaalika wasomi mashuhuri na kwamba mpango huo utakuwa ukifanyika kila mwaka.

"Tumemwalika Mkapa kwa kuwa ni kiongozi wa kwanza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kutunukiwa sahada ya falsafa ya udaktari na Chuo Kikuu cha Cape Coast cha Ghana," alisema Askofu Munga na kuviomba vyuo vingine vikuu nchini kumtumia kwa kuwa ameonyesha uwezo mkubwa.

Chuo hicho kilianzishwa rasmi mwaka jana kikiwa na jumla ya wanachuo 138 sasa wameongezeka hadi kufikia 450.
 
Kwa nini migomo ya wanafunzi wa vyuo vikuu haikutokea wakati wa utawala wa Mkapa?
 
Migomo ya wanafunzi ilitokea hata wakati wa utawala wa Mkapa. Muhimbili waligoma chuo chao kikafungwa mwaka 2002. Mlimani pia waligoma 2001 na 2004 chuo kikafungwa kwa muda wa wiki mbili(2004) hadi ikafikia hatua mh. Ng'wandu kumtaja jamaa mmoja aitwaye Bahati Tweve wa Mlimani kuwa ni kinara wa Migomo. Tofauti iliyopo kati ya awamu ya tatu na nne ni kiwango cha migomo. Migomo haikuwa mingi awamu ya tatu na nitakupa sababu

Moja: Waziri anayyeshughulikia Elimu ndiye huyo huyo anashughulikia elimu ya juu. Huyo huyo ahangaikie migomo ya walimu na wanafunzi wa chuo kikuu. Inamshinda. Kwa kifupi Waziri mwenye dhamana hii ameshachemsha ila anaogopa kusema

Mbili: Wanafunzi wa vyuo vikuu sasa hivi wana mwamko sisemi hata wale waliopitia awamu ya tatu hawana mwamko, la hasha. Isipokuwa wao sasa hivi wameunda umoja wao wa TAHLISO kwa hiyo ni rahisi kuratibu migomo yao na pia kuwa na sauti moja.

Tatu: Sera ya bodi ya mikopo nchini haiwezi kumuingi mtu akilini eti mtoto wa mkulima wa pamba (na hata pamba yenyewe haina soko), wa Kolandoto Mwanza amlipie mwanawe asilimia 40 ya mkopo wa chuo kikuu pesa ambayo hata yeye akidunduliza hawezi kufikia kiwango hicho na hata akienda benki hapati na hakubaliwi kwa sababu atakuwa hajafikia vigezo vyao. Wakati wa awamu ya tatu hiki chombo cha kuratibu mikopo kilikuwa hakijaanza rasmi na ni kutokana na uongozi mbovu wa watu fulani wa DARUSO wa miaka hiyo ndiyo waliyowaingiza chumvini. Muulizeni Zitto Kabwe ni shahidi.

Nne: Hali ngumu ya maisha, ufisadi, ulanguzi na mambo mengine kama hayo yanawafanya watu wajiulize maswali mengi hasa wasomi kwa nini wafanyiwe mambo kama haya na watu ambao wamesomeshwa bure na serikali. Baada ya kulewa mvinyo wa madaraka wanawasahau watoto wa makabwela kwa kuwa wao wanawasomesha wa kwao nje ya nchi. Kwa kubuni sera za kuikandamiza nchi yetu na kutudumaza na hii Vicious Cycle of Poverty kiaina na kinamna. Huku akaunti zao zina mabilioni ambazo zinaweza kuwasomesha wanafunzi wa chuo kikuu kwa miongo mitano na zaidi pesa ambazo ni mali ya serikali zikihifadhiwa kwenye akaunti za vigogo hao nje ya nchi.

Tano: Sera ya Elimu ya juu haijampa uhuru mwanafunzi kutoa maoni yake juu ya kuboresha kwa kuwa hao waheshimiwa hujitengea bajeti zao pamoja na perdiems na kwenda Bagamoyo picknick na viburudisho vyao wakidai wanafanya strategic plan , pamoja na risk assessment ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini. Matokeo yake ndiyo hayo. Wawakilishi wa wanafunzi wanakuwa bribed na nafasi mbalimbali za ajira serikalini pamoja na shahada za uzamili ushahidi upo.

Kwa hiyo mkuu pamoja na yote katika yote wengi wetu tunatambua hali ngumu ya uchumi iliyokuwa ikitukabili miaka ya 1984 enzi za utawala wa Nyerere na chama kimoja . Kitu ambacho sitamsahau Nyerere ni kwenye upande wa elimu yeye hakulifanyia mzaha kwa sababu alijua ndio msingi na ufunguo wa maisha na ndio maana hakuna mtu aliyedaiwa mkopo . Na wewe waulize hao ambao wanajifanya kusema wanafunzi wanastahili kulipa mikopo kama wao walidaiwa senti tano na Taifa hili wameshalichangia nini na mabadiliko gani ambayo wameyafanya kama sio ufisadi na kuvimba matumbo tu. Wewe unaweza kwenda chooni ukajisaidia halafu hujaflash watu wakaja juu unajifanya unaona kinyaa wakati kinyesi ni cha kwako?

Hii nchi bwana we iache tu.
 
Heshima Mbele,

Mkapa kwenye suala la kupangua Hoja ni kiboko na kamwe hautakuja kumsikia akijibu hoja zozote za kisiasa tena zinazohusu msuala ya Serikali ya awamu ya nne.


Hivi kitila unarudi lini Tanzania?
 
Either Tanzanians are easily impressed or the reporter botched the story.

Of course there is no reason why both should not hold.
 
Back
Top Bottom