Mkapa agoma kuzungumza na waandishi wa habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkapa agoma kuzungumza na waandishi wa habari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ALEX PETER, Jun 1, 2012.

 1. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #1
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]
  RAIS mstaafu, Benjamin Mkapa, jana alisema kwa sasa hataki kusumbuliwa kwa namna yoyote, badala yake ameomba aachwe huru ili ashughulikie matatizo aliyonayo.

  Bila kutaja aina ya matatizo hayo, Mkapa alikataa kuzungumza na waandishi wa habari akidai kuwa hataki kuongeza matatizo mengine, kwa vile aliyonayo kwa sasa yanamtosha.

  Mkapa alitoa kauli hiyo baada ya kuombwa na kundi la waandishi wa habari mara baada ya kutoka kwenye mjadala maalumu kuhusu uboreshaji wa mazingira ya uwekezaji barani Afrika, ulioandaliwa na Taasisi ya Uwezeshaji na Uwekezaji (ICF).

  Waandishi walitaka kufanya mahojiano na Rais huyo mstaafu kuhusiana na mambo kadhaa yakiwemo aliyozungumza katika mkutano huo, ambayo yalikuwa mazito na ‘mwiba' kwa watawala wengi wa serikali barani Afrika.

  "Niacheni, nina matatizo yangu ya kunitosha, sitaki kuongea kwa sasa," alisema na kisha akaondoka.

  Rais Mkapa amekuwa akishambuliwa na viongozi mbalimbali wa siasa kwa madai ya kuuza mashirika ya umma, kutumia wadhifa wake na kujimilikisha kampuni ya uchimbaji madini, akishirikiana na baadhi ya waliokuwa mawaziri katika serikali yake.

  Baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakipendekeza Rais huyo wa zamani akamatwe kwa kuhusika na tuhuma za ufisadi, kama ilivyofanywa kwa baadhi ya mawaziri wake wa zamani kwa tuhuma za ubadhirifu.

  Mkapa aliingia hivi karibuni katika mzozo mzito na familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, baada ya kukaririwa akisema Mbunge wa Musoma, Vicent Nyerere (CHADEMA), hakuwa mtoto wa Mwalimu, kauli aliyoitoa wakati wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru Mashariki, wakati akimnadi mgombea wa CCM, Sioi Sumari.

  Mapema akizungumza katika mjadala uliohudhuriwa na washiriki toka makampuni na taasisi mbalimbali za bara la Afrika, Mkapa alisema alifanikiwa wakati wa utawala wake kutokana na sera yake ya uwazi na ukweli, na pia kujikita katika utekelezaji wa mipango.

  Alisema sio vema kwa viongozi wa nchi za Afrika kuzungumzia mipango na mikakati ya maendeleo kila kukicha, badala yake waingie kwenye utekelezaji.

  Alisema kuwa sera yake ya uwazi na ukweli ilisaidia kuwapa wananchi taarifa sahihi kuhusu hali ya uchumi, fedha na changamoto zote zilizoikabili serikali na wao kupata fursa ya kushiriki kuzitafutia ufumbuzi.

  Mkapa alisisitiza umuhimu wa serikali za Afrika kuwawezesha kiuchumi wanawake na vijana waweze kujiajiri kwa kuwa hayo ndio makundi makubwa kuliko makundi mengine katika jamii hivyo itaziwezesha nchi hizo kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka na kukabiliana na tatizo la umaskini wa kipato.

  Alisema kuwa tatizo la ajira limesababisha vijana wengi kughiribiwa na wanasiasa ambao huwapa matumani hewa ya mafanikio, na wengi kuamini kuwa njia sahihi ya kujinanusa ni kujiingiza katika siasa.

  Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa ICF, Omary Issa, alisema taasisi hiyo imefanikiwa kuboresha mifumo mbalimbali inayopunguza usumbufu kwa wafanyabiashara na wawekezaji huku akitolea mfano wa mpango wa kuboresha mfumo wa usafirishaji mizigo toka bandarini mpaka nchi jirani wanaoutekeleza kwa pamoja na mamlaka ya mapato nchini TRA na Jeshi la Polisi ambao utawezesha kuondoa vizuizi vyote vya kodi barabarani.

  Alisema kuwa ICF imesaidia kuboresha mfumo wa usajili wa makampuni nchini Rwanda ambapo kwa sasa huchukua siku 2 kusajili biashara tofauti na awali ambapo ilikuwa mpaka siku 16 huku gharama zikipungua kutoka dola za Marekani 433 mpaka 25.

  Issa alisema kuwa taasisi yake katika kuhakikisha shughuli za biashara zinafanyika kwa urahisi na ufanisi zaidi imesaidia kuboresha mfumo wa mahakama nchini Zambia kwenye mahakama tatu na kutoa mafunzo kwa majaji wapya 14 huku nchini Sierra Leone wakifanikiwa kuboresha mfumo wa mahakama ambapo kwa sasa huchukua miezi miwili tokea kufungua kesi za biashara na kupata uamuzi ambapo awali ilikuwa inatumia mpaka miaka sita.
   

  Attached Files:

 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Bora amewafanyia hivyo manake shida ya Waasndishi wa habari wengi hapa Bongo ni makanjanja tu!!!!! Wanataka wammis quote halafu wamzushie kwa umma!!
   
 3. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #3
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Namwunga mkono Ben. Asilimia kubwa sana ya waandishi wetu hakuna kitu kichwani. Kazi yao kubwa ni kuandika mambo ya kimbea mbea, kutafuta mabaya baadala ya kuandika issues za maendeleo ya nchi yetu.
   
 4. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Teh,teh,teh...anamaumivu ya makombora ya Mhe Lema,ameumia sana mpaka anahisi kuchanganyikiwa,maana kashikwa pabaya...teh,teh
   
 5. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani hakuwa na cha kuongea hivyo aliona itakuwa majungu tu, ndiyo maana kagoma. Mwacheni apumzike, tafuteni habari za kujenga nchi sasa.
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,450
  Likes Received: 5,841
  Trophy Points: 280
  Asingemsikiliza Bakili Muluzi saa hizi angekuwa bonge la legend
   
 7. m

  mjibu hoja New Member

  #7
  Jun 1, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bila yeye tusingekuwa popote, mwacheni apimzike. Maswali welengeni viongozi wa sasa kwani ndio wanawajibika kwetu. Atakalosema yeye ni opinion tuu.
   
 8. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #8
  Jun 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  eti mkapa anasema ana matatizo ya kutosha...huyu jamaa ni bilionea...sasa wananchi wa kawaida wasemeje kama mkapa ana matatizo mengi
   
 9. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #9
  Jun 1, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,775
  Trophy Points: 280
  Matatizo yana tabia ya kukaribishana.
  Asubiri tu ataona.
   
 10. Ndekirhepva

  Ndekirhepva JF-Expert Member

  #10
  Jun 1, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  ahahhah....
  jamaa naona anaugulia makondo ya makamanda manake walimtonesha na vindonda vya tokea arumeru
   
 11. B

  BMT JF-Expert Member

  #11
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  tutamkumbuka sana,tatizo humu jf ushabiki mwingi sana,akiogelewa kiongoz wa chadema wanakuwa wakali,akiongelewa mkapa litaongelewa kila jambo,,pumzika mzee wetu
   
 12. m

  mlandali honoli Member

  #12
  Jun 1, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  unajua waandishi wakibongo me nawashangaaa baada yakuchunguza kesi za mafisad ambazo zipo mahakaman na kwa dpp wanang'ang'ania mtu mmoja
   
 13. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #13
  Jun 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nadhani a dialogue na waandishi ingekoleza utamu wa mada yake zaidi badala ya on way communication
   
 14. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #14
  Jun 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Pumzika mzee, achana na Makanjanja hayo
   
 15. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #15
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwani walimuuliza kwanini alimuua Mwalimu Julias Kambage Nyerere?
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Jun 1, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Unaposema apumzike wakati kampeni zikianza yeye ndiyo wa kwanza kuzindua anapumzika nini, ngoja vijana wa mvue nguo mpaka atajuata..
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Jun 1, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ninachompendea Mh. Rais Mtaafu Mkapa anajua kudeal na waandishi wa habari. He is smart in this!! Good
   
Loading...