Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,435
- 4,151
Mie nadhani kasema jambo la maana....hebu tumpe heshima mzee wetu......pamoja na mapungufu bado kaijengea misingi nchi hii.......tumuheshimu kwa mazuri aliyotuachia....
Tatizo ni kwamba kuna maovu ukitenda, basi mema yako yanakuwa na maana ndogo sana kama si kupotea kabisa. Ndio maana inakuwa taabu sana kukumbuka mema ya Idd Amin, Hitler, Mobutu, n.k. Maskandali makubwa ya ufisadi, mauaji ya kisiasa, kuzalisha wakimbizi wa kwanza wa Kitanzania, kauli za jeuri na kibri kwa wananchi ndiyo kumbukumbu nzito alizowaachia Watanzania. Labda aanze kwa kuomba radhi, kuacha kauli mbovu na kutojihusisha na siasa za vyama ndipo chati ipande. Hakuna sababu ya kumfanya kuonekana chini ya mzee rukhsa kihadhi zaidi ya kwamba haonyeshi kuheshimu wananchi; bado anafikiri jeuri itamrejeshea heshima aliyokuwa akiipata akiwa magogoni.