Haya ni maoni yangu ambayo ni vigumu kuthibitisha empirically. Hata hivyo, tafuta vigezo vyovyote vya kiongozi bora uwapime hawa ndugu zetu wawili. Tatizo la Mkapa alikuwa hapendi mtu mwingine am-outshine, na nafikiri ni sababu moja ya kutuachia JK maana alijua siku ya siku tutamkumbuka sana. In fact ni aibu kulinganisha hawa viongozi wawili-moja ni monitor wa darasa la I na mwingine ni kiranja mkuu, haiji. Kwa maneno ya Mzee Mwinyi ni makosa kulinganisha mlima na kichuguu!
Labda kukusaidieni wale ambao wanasema matatizo ya leo yaliachwa na Mkapa. Yes, ni kweli kabisa. Sasa cha kujiuliza ni kwa nini tuyaone au tuyabebee bango leo? Kwa nini walimu na kila mtu anagoma leo na sio jana? Moja ya maelezo hapa ni kwamba mosi, Mkapa alikuwa na uwezo wa kushawishi kuhusu mipango na sera zake. Kama ni madai ya walimu yalikuwepo na walimu walielezwa sababu za kuchelewa kulipwa na wakaelewa, wakasubiri na wakalipwa. Kama ni wazee wa EAC walielezwa kwa nini wanalipwa wanavyolipwa na kwa nini wale ambao hawakulipwa hawakulipwa, walielewa, japokuwa waliendelea kunung'unika lakini walikubaliana. Uwezo wa kushawishi ni sifa muhimu ya kiongozi wa kisiasa ambayo hawa ndugu zetu wa leo wanapwaya mno. Wao wanafikiri wanaweza kutawala kwa amri, hawataweza. Bahati mbaya hii tabia chafu ya kutawala kwa amri inaelekea imesambaa kwenye taasisi zote hadi chini, ni hatari na haitawasaidia!
Pili, wakati wa Mkapa kila idara ilikuwa inafanya kazi. Kila waziri aliwajibika ipasavyo. Wanafunzi wa vyuo vikuu walipogoma watu walimnyooshea kidole waziri husika, na wala sio rais. Katika awamu zote tatu zilizopita kulikuwa na mawaziri vinara: Akina Sokoine wakati wa Nyerere, akina Mrema wakati wa Mwinyi na akina Magufuli wakati wa Mkapa. Leo hii mawaziri wote wanaonekana kama vile hawapo, na kila kitu kinamtegemea rais-hiyo ndiyo failure ya uongozi. Kwa nini mawaziri kipindi hiki hawafanyi kazi na kwa nini hakuna mawaziri vinara? Hakuna hatari kwa kiongozi kama kukumbatia majukumu yote na kutokuwaamini wale uliowateua, na hasa pale ambapo uwezo wa kiongozi mwenyewe ni mdogo!
Endeleeni kumshambulia Mkapa, lakini ukweli ni kwamba yeye alishafanya sehemu yake, tunataka hawa waliopo nao wafanye. Sasa kama barabara ya KM 5 ya Sam Nujoma inachukua zaidi ya miaka mitatu kukamilika-bado unatafuta uthibitisho kwamba hawa wenzetu wamekwama na akina Magufuli walikuwa bora mara 600 zaidi ya hawa akina...(hivi by the way waziri wa ujenzi siku hizi ni nani vile? Tazama hata majina ya mawaziri hatuyajui halafu utasema hawa wanafanya kazi?).
Ugomvi hapa ni nini hasa?! Kwamba Mkapa alikuwa bora kuliko hawa jamaa zetu wa sasa hivi nalo ni jambo la kujadili? Of course, hata kwa Africa, kwa aina ya viongozi tulio nao, huwezi kumkwepa Mkapa katika list ya viongozi bora! Inaweza ikauma lakini ndio ukweli huo. Hii inakuonyesha jinsi tulivyo na uhaba wa viongozi bora katika bara letu.
Kitila,
Mkuu usiseme nalaumu tuu bila kupima..
For real mkuu, nambie Mkapa kafanya kitu gani huo Uwanja wa Taifa, bridge to nowhere na barabara za mikopo au? mimi sioni zaidi ya kuona kilimo kilishuka, maji yakawa taabu (City water), Umeme wa mgao tukakaangwa na Richmond, Afya - Muhimbili imekufa wakati wake na Kibaya zaidi let the record show kuwa ktk historia ya Tanzania, kwa mara ya kwanza watu walikufa njaa wakati wa Mkapa.. Cholera, ndui na maradhi kibao yakarudi nchini baada ya kuendelea kutumia madawa mabaya..U name it yaani inachefua roho kumsikia Mkapa...ALL THESE ARE FACTS!
I mean guys what good mnaweza kunambia hata kama tukiacha Ufisadi nje!..
Wewe vipi, hujui kuwa miafrika hii ya JF ndiyo iliyogundua JF machine ambayo na wewe unajidai leo kupiga soga? Nikutajie lingine?
Ndio. ........ .....hivi ndivyo itakavyokuwa 2010,
Acha ndoto Pasco
This is just a suppositioh incase opposition wins 2010. Please dont say its imposible!. The Bible says 'Nothing is impossible under the sun'.Ndio. ........ .....hivi ndivyo itakavyokuwa 2010,
Acha ndoto Pasco
Hata Obama alianza tuu kama ndoto. Kenya, Zambia, Malawi na sasa Zimbabwe kote ni ndoto tu.
But I have to admit I am a dreamer just like Martin Luther King Jnr 'I have A Dream...'.
Rais Mstaafu ana kinga ya kutoshitakiwa kwa maaamuzii yoyote aliyoyafanya akiwa madarakani,
hata hivyo kinga hiyo haizuii rais kushtakiwa yeye binafsi katika kesi za madai.
Kinga hiyo inaweza kuondolewa
na iwapo mbunge yoyoote atatoa hoja... ya rais kutumia madaraka yake vibaya kwa lengo la kujinufaisha isivyo halali, bunge likaridhia hiyo hoja, likatoa Azimio la Bunge kumuomba rais aondoe kinga kwa rais mstaafu ili ashitakiwe.
Mwamuzi wa mwisho ni rais anaweza kulisaini hilo azimio ama kuliacha.
Hata hivyo kama raisi hata lisaini, Bunge linaweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais. Ikipitishwa na robo 3 ya wabunge wa kuchaguliwa, raisi anafukuzwa kazi na serikali yake yote
mafao wanapata) Bunge linavujwa.
Kinga ya Rais mstaafu, chini ya Ibara ya 46 (3), ni dhidi ya "jambo lolote alilofanya yeye kama Rais" na sio "kwa maaamuzii yoyote aliyoyafanya akiwa madarakani." Rais akifanya uamuzi wa, kwa mfano, kubaka mfanyakazi jikoni Ikulu, au kufungua kampuni Ikulu kinyume na maadili ya uongozi, au kushirikiana na Waziri wa Madini kununua mgodi kwa idhini ya Waziri wa Madini, hapo hatakuwa hana kinga akistaafu.
Provision ya kinga dhidi ya madai, chini ya Ibara ya 46 (2), haihusiani na Rais Mstaafu bali wa madarakani.
Haiwezi.
Kinga dhidi ya Rais mstaafu kwa mambo aliyoyafanya kama Rais ni absolute, categorical and unqualified. Haiwezi kuondolewa na chombo au kiumbe chochote kile.
Rais wa Tanzania hana nguvu ya kutangua kinga ya Ibara ya 46 ( 3 ). Na Bunge haliwezi kupinda Katiba.
Hicho kitu umetunga!
Rais afukuzwe kazi kwa kukataa kutia saini ? Sasa kama hana choice ya kutia ama kutotia kwa nini kuwe na hiyo step ya kupitia thru idhini ya Rais? Na mbona mwanzoni umesema "mwamuzi wa mwisho ni Rais"? Uko wima hapo ulipo wewe ? Hebu levuka, unajua jinsi ya ku speed up kulevuka ? Kanywe maji mengi, au shtua kakikombe ka kahawa, halafu pata nap fupi.
Tundiko zima ni punch lines za kipindi cha mahoka.
DPP adaiwa kumkingia kifua Nazir Karamagi
2008-11-27 12:07:13
Na Abdallah Bawazir
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP), amezuia kupelekwa mahakamani aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.
Karamagi anatuhumiwa kutumia madaraka vibaya katika kusaini mkataba wa mgodi wa madini wa Buzwagi.
Imedaiwa kuwa, DPP alichukua hatua ya kuzuia kufikishwa mahakamani kwa Karamagi kutokana na ushahidi dhidi ya tuhuma zinazomkabili kutojitosheleza.
Kesi dhidi ya Karamagi, ilikuwa iwasilishwe katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kukamilisha kazi yake.
Habari kutoka ndani ya kikao watendaji wa serikali na wafadhili wanaochangia bajeti ya serikali kilichofanyika Dar es Salaam jana, zilisema kuwa Takukuru walikwisha baini matumizi mabaya ya madaraka katika sakata zima la Buzwagi, lakini DPP akakataa kesi dhidi ya Karamagi isifunguliwe.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mabalozi wote ambao nchi zao zinachangia bajeti kuu ya serikali na Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali.
Chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya kikao hicho, kilieleza kuwa, wafadhili walielezwa kuwa, Takukuru ilipeleka majalada ya kesi mbili kwa DPP, ikiwemo inayowahusu mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona ambayo ilitajwa juzi katika Mahakama ya Kisutu pamoja na la Buzwagi.
Ilielezwa kuwa, liliporudi jalada la mawaziri hao wawili wa zamani, lilipitishwa kwa ajili ya kupelekwa mahakamani, lakini la Buzwagi DPP alisema hakuna ushahidi wa kutosha kuifikisha kesi hiyo mahakamani, hivyo kulifunga.
Inadaiwa kuwa, uamuzi huo wa DPP, umeikasirisha Takukuru, ambayo ndiyo iliyokuwa ikikusanya ushahidi ili kesi hiyo iweze kufikishwa mahakamani kwa kuanza kusikilizwa.
Chanzo hicho cha habari cha kuaminika, wafadhili walielezwa kwamba, majalada ya kesi nyingine nne kubwa, zikiwemo zinazoihusu kampuni ya uchimbaji madini ya Meremeta na Deep Green, bado yapo kwa DPP yakisubiri uamuzi wake.
Pia Mabalozi hao waliwaomba kushawishi nchi za Ufaransa, Uswisi, Afrika Kusini, Mauritius, Hong Kong kutoa ushirikiano ili kesi hizo tatu ziweze kukamilika.
Ilidaiwa kuwa, nchi hizo zimekuwa hazionyeshi ushirikiano mara maaofisa wa Takukuru wakihitaji taarifa.
Jitihada za Nipashe za kumpata DPP, Elieza Feleshi jana ziligonga mwamba, kwani baada ya kuwasiliana naye alieleza kuwa, yupo kwenye kikao na kutaka apigiwe baada ya nusu saa.
Lakini baada ya muda huo kupita na kupigiwa, alipokea msaidizi wake ambaye alieleza kuwa, bado yupo kwenye kikao na hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kikao hicho kilikuwa bado kikiendelea.
Nipashe ilipowasiliana na msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Omega Ngolle kuhusiana na suala hilo, alisema angeeleza kwa undani suala la jalada la Buzwagi, lakini hakufanya hivyo alipopigiwa simu baadaye.
Sakata la mkataba wa Buzwagi kusainiwa nje ya nchi kwa mara ya kwanza liliibuliwa Bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini.
Zitto alidai kuwa, waziri huyo wa zamani alikwenda kusaini mkataba huo, London nchini Uingereza, kwa kutumia mfumo wa mikataba wa zamani wakati serikali ikiwa inajadiliana na wawekezaji kurekebisha mikataba ya madini nchini.
Suala hilo alilieleza katika mkutano wa nane wa Bunge mjini Dodoma, ambapo alihoji hatua ya Nazir Karamagi kusaini mkataba huo nje ya nchi.
Baadaye, Zitto aliwasilisha hoja binafsi bungeni, akiomba kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge, kuchunguza hali hiyo.
Zitto alieleza kushangazwa na uamuzi wa Karamagi kusaini mkataba wa madini kati ya serikali na kampuni maarufu ya madini hapa nchini ya Barrick Gold Mine kwa ajili ya mgodi ya Buzwagi nchini Uingereza badala ya Dar es Salaam.
Mbali ya kuhoji uhalali wa Karamagi kusaini mkataba huo, kinyume cha maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete ambaye aliagiza kupitiwa upya kwa mikataba yote mipya ya madini, Zitto alikielezea kitendo hicho kuwa kinaongeza wasiwasi wa kuwepo kwa ushawishi wa rushwa.
Hata hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali na Bunge na hatimaye Zitto aliishia kusimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa kile kilichoelezwa amelidanganya Bunge kuhusiana na madai yake hayo.
Alipewa adhabu hiyo kwa madai ya kutoa kauli ya uongo Bungeni dhidi ya Karamagi, inayohusu kusaini mkataba na kampuni ya Barrick, juu ya mradi wa Buzwagi, jijini London nchini Uingereza.
SOURCE: Nipashe
Pamoja na maelezo yote hapo juu wote ni mahoka ibara 46 (3) ya mawe? au maji? au mbuzi? au mchicha? au riwaya ya shigongo?
Tangu kesi za mafisadi zianze siku chache zilizopita, watanzania wengi walifurahi kuona kuwa sasa kweli serikali yao inafanya kazi kama walivyotegemea. Ni watanzania wachache tu ambao walikuwa wamefaidika na ufisadi ndio waliokarahika na kuanza kwa kesi hizo.
Nimekuwa najiuliza hii nguvu na kasi ya uendeshaji wa kesi hizi imetoka wapi. Mwanzoni nilidhani kuwa JK alitishiwa maslahi yake na hao mafisadi, baadaye nikadhani kuwa huenda ameamua kuonyesha rangi yake kweli kweli kuitumikia Tanzania kwa maslahi ya umma. Lakaini leo nilivyosoma gazeti la Nipashe, nimegundua kuwa kuwa kuendeshwa kwa kesi hizi kunatokana na shinikizo kutoka kwa wafadhili (soma hapa chini).
Hapo ndipo nilipochoka kabisa,
Yaani kweli Tanzania tuna haja ya kuwa na serikali kubwa kama hii ya JK iawapo maamuzi makubwa ya nachi yanaendelea kutolewa na wafadhili?
BTY: Kwa Vile DPP ametumia madaraka yake vibaya kuzuia kuendeshwa kwa kesi dhidi ya Karamagi ambayo ina ushahidi wa kutosha kutoka TAKUKURU, kwa nini naye asiwajibishwe?