Mkapa above the law?: Allegations

Hapa hatari sio kwa Mkapa tu, ni kwa taifa lote ambalo linapata kodi na pia wafanyakazi wa huo mgodi. Haya ndio mambo yanayonisikitisha mimi, kama quality mbovu, tunashindwa nini kurekebisha? Technology ipo, kweli mpaka mkaa wa mawe ukatolewe SA? Huyo CEO inatakiwa apoteze kazi, tumezidi ujinga.


Mgodi wa Mkapa, Yona wazua balaa



*Kiwanda chasusa makaa yake, ni kutokana na hofu ya ufisadi

Na, Rashid Mkwinda, Kyela

WIKI chache baada ya Mbunge wa Vunjo,Bw. Aloyce Kimaro (CCM) kupinga bungeni ununuzi na umiliki wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira uliowahusisha Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Bw. Benjamin Mkapa na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Bw. Daniel Yona, Kampuni ya Saruji ya Mbeya imesusa kununua nishati hiyo kwa hofu ya kuhusishwa na hujuma na ufisadi dhidi ya mali Watanzania.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili hivi karibuni ndani ya mgodi huo, umebaini zaidi ya tani 4,000 za makaa ya mawe zinazozalishwa kwa mwezi sasa zimedoda kutokana na hatua ya Kiwanda cha Saruji cha Tembo kilichopo Songwe, kuacha kununua makaa hayo.

"Tunaamini wananchi ndio wanaohitajika kunufaika na uwekezaji...lakini tunaposikia viongozi waliopata kuongoza serikali wakitajwa kuhusika na ununuzi wenye utata wa mgodi wa Kiwira, tunachelea kuonekana tunaendelea kuunga mkono ufisadi na hujuma dhidi ya mali za walipa kodi", alidai mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo.

Alisema baada ya kiwanda hicho kuacha kununua nishati hiyo Kiwira, sasa kimelazimika kuagiza makaa hayo kutoka Afrika Kusini ili kuendesha shughuli za uzalishaji kiwandani hapo.

Alidai awali Kiwanda cha Saruji ambacho kilikuwa mali ya serikali na baadaye kupewa mwekezaji, kililazimika kununua makaa ya mawe kutoka katika mgodi huo kwa kile kilichodaiwa, shinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi hali iliyochangia kuchangia kupanda mara kwa mara kwa bei ya saruji kutokana na malighafi hafifu za makaa ya mawe yanayozalishwa na mgodi wa Kiwira.

Katika hoja yake binafsi aliyoitoa hivi karibuni bungeni, Bw. Kimaro, alisema mgodi wa Kiwira ulijengwa na Serikali ya China kwa kwa dola bilioni 4 na kukabidhiwa kwa Serikali ya Tanzania mwaka 1988 na baadaye kuuziwa Bw. Mkapa na Bw. Yona kwa sh. milioni 700. Hadi sasa wamelipa sh. milioni 70.

Wamiliki wa mgodi huo ambao gazeti hili limepata orodha yake ni pamoja na Kampuni ya ANBEN Limited ambayo wamiliki wake wamebainishwa kuwa ni Rais mstaafu wa awamu ya tatu Bw. Mkapa na mkewe Mama Anna ,Kampuni ya DEVCONSULT Limited ambayo imeoneshwa kuwa ni ya Bw. Daniel Yona mwenye hisa ya asilimia 90 na mtoto wake Danny Yona mwenye hisa asilimia 10.

Wanahisa wengine ni Kampuni ya Universal Technologies Limited ambayo imeoneshwa mmiliki wake kuwa ni Bw. Evans Mapundi na Bw. Wilfred Malekia,Kampuni ya Choice Industries Limited iliyooneshwa kuwa ni ya Bw.Joseph Mbuna na Kampuni ya Fosnik Entreprise Limited ya Bw.Nicholas Mkapa na Bi. Foster Mkapa ambao wana hisa ya asilimia 50 kila moja.

Bodi ya Wakurugenzi wa awali wa mgodi huo ilivyooneshwa kwa gazeti hili mwaka 2004 iliongozwa na Mama Anna kama Mwenyekiti na mwaka 2005, Mwenyekiti alikuwa Bw. Evans Mapundi.

Majira limedokezwa kwamba mbali na uzalishaji wa mgodi huo kudorora, wafanyakazi wapatao 515 wamekuwa wakipunjwa mishahara yao tangu ulipobinafsishwa kutoka serikalini Julai 2005.

Vyanzo vyetu ndani ya mgodi huo vilisema hivi sasa mfanyakazi mmoja hulipwa kima cha chini cha sh. 60,000 bila kujali muda wa ziada na mazingira magumu na ya hatari ya kazi ambapo baada ya makato hujikuta akiambulia sh 49,000 tu.

Pia vilieleza kuwa mgodi huo unakabiliwa na tatizo la uchakavu wa mitambo ya uzalishaji umeme ambao ulikuwa umeunganishwa katika gridi ya Taifa kwa matumizi mengine ya wananchi, hivyo kusababisha kutoa megawati 1 hadi 2 kutoka megawati sita zilizokuwa zikizalishwa kabla ya kubinafsishwa.

Mgodi huo ambao hapo awali ulikuwa una maeneo ya uvunaji wa makaa ya mawe kwa sehemu tatu, hivi sasa maeneo hayo yamesimamishwa na kubakiwa na uvunaji na uchimbaji wa eneo moja ambalo linatarajiwa kumalizika Desemba mwaka huu jambo linaloashiri kufa kwa mgodi huo kutokana na kile kinachodaiwa kutokuwa na maandalizi ya kuwepo maeneo mengine ya uvunaji.

Majira limedokezwa kuwa tangu kubinafsishwa kwa mgodi huo hakuna vifaa vipya vilivyofungwa kiwandani hapo ilhali mashine zilizokuwepo awali kama zile za kubangulia makaa na viberenge vimeanza kuuzwa kama vyuma chakavu. Kulikuwa na viberenge 12 vya tani saba na tani mbili na nusu ambavyo vimeuzwa na kubaki vinne.

Vile vile mashine za kubangulia makaa ambazo awali zilikuwa sita nazo zimeuzwa kama vyuma chakavu na kubakiza moja ambayo utendaji wake umekuwa hafifu kutokana na uchakavu, pia mashine zinazotumika kuzolea makaa mgodini zilikuwa nane, sita kati yake zimeuzwa kama vyuma chakavu na kubakiwa mbili ambazo nazo ziko katika hali duni ya utendaji kutokana na uchakavu wake.

Kulingana na rekodi ambazo gazeti hili inazo ni kwamba mgodi huo kabla ya kubinafsishwa ulikuwa ukizalisha tani 300 kwa siku na sasa unazalisha tani 30 hadi 50 kwa siku kutokana na uchakavu wa mitambo.
 
There you go, ni kweli mkuu kulikuwa na mtu alikuwa na jina kama lako Zanaki, aliyesema kuwa Mungai ndiye next pm, anyways unajua fumbo huwa tunafumbia mjinga maana werevu hunga'mua,

Heshima mbele kwa elimu yako nzito, tuendelee kukata ishus mkuu, taifa liko njia panda!

Yamekuwa hayo?
 
mbaroni kwa kumzomea Mkapa
Na Mwandishi Wetu, Masaki

VIJANA watano wa jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na Polisi kwa madai kwamba walimzomea Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa kwa kumwita kuwa ni fisadi.

Tukio hilo la aina yake limetokea jana saa 11 jioni,katika maeneo ya Masaki karibu na kituo cha Daladala cha Masaki ambapo vijana hao kama kawaida yao walikuwa kijiweni wakipiga stori zao.

Imedaiwa kuwa kundi hilo la vijana wakiwa eneo hilo la stendi ya daladala walianza kupiga kelele baada ya kuona msafara wa Mkapa ukipita n kuanza kuzomea kwa mayowe wakisema fisadi huyo!!!, fisadi huyo!!!.

Tukio hilo lililoshtua watu waliokuwepo karibu na kituo hicho ambapo baada ya muda mfupi polisi walifanya msako mkali kituoni hapo na kufanikiwa kuwasomba vijana watano lakini wengine baada ya kuona hivyo walitimua mbio wakielekea kusikojulikana.

Rais huyo mstaafu amekumbwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi kwa siku za karibuni ingawa mara zote amekuwa mkimya huku wananchi vikiwamo vyama vya upinzani vikimtaka azijibu tuhuma hizo.

Katika mkutano wa Bunge lililopita mjini Dodoma alishambuliwa na Mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro akisema yeye na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona walinunua mgodi wa Mawe wa Kiwira kwa sh. milioni 70 wakati thamani yake ni sh. bilioni 4.

Katika madai hayo Kimaro alisema kwamba viongozi hao wawili walitumia nafasi zao za uongozi kuiingiza nchi katika matatizo makubwa ya kiuchumi. Akasema kwamba ilikuwa wanunue mgodi huo kwa sh. 700 lakini hadi sasa wamelipa sh. milioni 70 tu.

Mkapa pia anakabiliwa na tuhuma za kutumia nafasi yake alipokuwa Ikulu kufanya biashara ikiwa ni pamoja na kupata mkopo wa Sh milioni 500 benki ya NBC ili awekeze katika biashara zake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Kanda Maalum Dar es Salaam, Jamal Rwambow alipopigiwa simu kuelezea tukio hilo alisema kuwa yupo kwenye msafara na ataelezea kwa undani taarifa hizo pindi atakapozipata.

" Nipo kwenye msafara na taarifa hizo bado sijazipata nitakapozipata nitaelezea kwa undani,"amesema Rwambow alipopigiwa simu leo asubuhi.


source: http://www.darleo.co.tz/kurasa.php?soma=habari&habariNamba=795
 
Haya ndo matokeo ya kuiba na kujilimbikizia mali ya umma.

Bado viongozi hawajajua watanzania wa leo ni wanajua wameibiwa haki zao
 
kwa mwendo huu uelewa upo kwa sasa kwa jamii yetu,,,,hakuna kumsujudia mwizi,,, ni kumrushia mawe au kumzomea hadi wafe kwa pressure
 
Nyani Ngabu,

Kwanini Wamrushie Mawe,Kwa kosa gani??hakuna aliye juu ya sheria,kama watanzania tunaona ana kosa basi ttumpeleke Mahakamai ili asurubiwe na sio kumuita Mtu fisadi.

Wewe binafsi unaonaje, ana cha kujibu au kuzungumzia (address) au?
 
Nyani Ngabu,

Kwanini Wamrushie Mawe,Kwa kosa gani??hakuna aliye juu ya sheria,kama watanzania tunaona ana kosa basi ttumpeleke Mahakamai ili asurubiwe na sio kumuita Mtu fisadi.

kwa sababu wezi wote wanaokamatwa manzese na Kariakoo wanarushiwa mawe!
 
Mi mbona sijaelewa, sassa hapo hao vijana kosa lao nini,

kama yeye si fisadi kwanini apate shida???
kama yeye si fisadi kwanini asikanushe hizo tuhuma kwenye vyombo vya habari(kama haviamini aende pale MAELEZO)
na hii inaonyesha ni jinsi gani polisi iko kwa kwaajili ya WEZI
 
Hivi:

a. Kama walikuwa kwenye msafara wakaona watu wanapiga kelele "Fisadi" "Fisadi" wanapoteremka na kufanya msako, wanajuaje walioawakamata NDIYO waliosema "fisadi"?

b. Je kama vijana hawa wangesimama na kupiga kelele "Mtukufu" "Mtukufu" ni hatua gani wangechukuliwa au zawadi gani wangepewa?

c. Uhuru wa maoni ni pamoja na uhuru wa maoni ya kijinga. Katiba haisemi mahali popote kuwa maoni yatakayotolewa na wananchi lazima yawe mazuri au yanayopendeza ili yakubaliwe.

d. HIvi wanazojela za kutosha? Maana tukianza hii movement ya "Fisadi" "Fisadi" wataweza kweli kuwasweka watu ndani au watalazimika kutumia njia "kali" zaidi... ?
 
Polisi ingewatendea haki hao vijana kwa kuwaachia huru mara moja na bila masharti yoyote.
 
Mi mbona sijaelewa, sassa hapo hao vijana kosa lao nini,

kama yeye si fisadi kwanini apate shida???
kama yeye si fisadi kwanini asikanushe hizo tuhuma kwenye vyombo vya habari(kama haviamini aende pale MAELEZO)
na hii inaonyesha ni jinsi gani polisi iko kwa kwaajili ya WEZI

Hii ndio shida polisi wetu wanafanya kazi kwa hisia. Ukiwauliza hawa vijana wamevunja sheria gani utakuta wala hawajui. Sasa kwa mfano kama hao vijana wangeamua kumshangilia wakati akipita wangewakama?
 
Teana katika misafara yake magari huwa yanasimamishwa kwa muda hadi robo saa mkisubiri "bwana mkubwa" apite!

Siku moja ilinikera sana!

Bongo Hovyo kabisa.
 
Kazi kweli kweli sasa hapo ndipo aone ya kuwa anatakiwa kujibu tuhuma dhidi yake...akikaa kimya tunapata majibu tofauti kabisa...na kumuona hafai na labda...akikata kimya chake ili tuwe na cha ku define mustakabari wake
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom