Mkanganyiko wa kiumbaji; kwanini mganga wa kienyeji haagizi kuku wa kisasa?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,530
Wanajulikana pia kama kuku wa kizungu ama kuku wa kufugwa. Ni tofauti na hawa kuku wetu wa 'kienyeji' kukipambazuka unawafungulia wanaenda wenyewe kuzurura hawa wa kufugwa masaa 24 wako bandani

Mayai ya kuku wa kufugwa ni tofauti kabisa na mayai ya kuku wa kienyeji. Haya ya kuku wa kienyeji yana uhai kwakuwa yanapatikana baada ya kufanya ngono na jogoo (dume) lakini haya ya kisasa hayana uhai yanapatikana baada ya kuku kulishwa vyakula vyenye protini ya kutengeneza pamoja na madawa

Roho ni nishati hai huria. Ipo tu kama nishati nyingine zozote. Nishati haitengenezwi inategwa (taping), kuanzia nishati gesi, nishati mafuta, nishati moto, nishati nyuklia mpaka nishati maji... hizi zote zipo tu... Hatuziundwi wala kuzitengeneza bali tunazitega, kuzikusanya, kuzihifadhi na kuzisambaza... Na kila nishati moja ina mchakato wake tofauti kabisa na nishati nyingine japo mwisho wa siku kazi ni moja...

Nishati hai kwenye uumbaji hupata nguvu ya kuwepo kwake kutokana na mkutaniko wa nishati hai mbili pinzani.. KE na ME... Hata wale watoto wa maabara ama watoto wa chupa ni matokeo ya mkutaniko wa mayai ya KE na manii za ME... nje ya hapo hakuna uumbaji wa kinachoitwa Binadamu labda awe ni robot (kinyago) na hata wanyama pia?
Sasa vyovyote iwavyo hao kuku wa kufugwa wana asili na huu uumbaji lakini baada ya hapo huchakachuliwa mno mpaka nguvu ya uumbaji ule wa asili kupungua kabisa na kuwa kama roho zisizotimia

Mganga wa kienyeji anapoagiza kuku, hitaji kubwa sio nyama... Ni damu... Damu ndio imebeba uhai wa roho iwapo mwilini... Kama hii damu sio matokeo ya uumbaji wa jinsia mbili tofauti basi hata nguvu yake kiroho ni asilimia 25/75.. Hivyo haina uwezo wa kwenda kupambana na damu yenye asili mbili....

Swali la mkanganyiko wa kiumbaji ni hili.... Kwanini yai lililotokana na muunganiko wa jinsia mbili tofauti... Baada ya vizazi kadha bila uwepo wa jinsia ya pili, roho yake hupoteza nguvu na uwezo wa kutengeneza uumbaji tena?
 
Mkuu nnaomba unitafunie kidogo hili swali.

Swali la mkanganyiko wa kiumbaji ni hili.... Kwanini yai lililotokana na muunganiko wa jinsia mbili tofauti... Baada ya vizazi kadha bila uwepo wa jinsia ya pili, roho yake hupoteza nguvu na uwezo wa kutengeneza uumbaji tena?
 
Hivi mwisho wa siku baada ya mganga wa jadi kuchukua damu aliyo itaka ni nani anaye kula nyama?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom