Mkanganyiko wa kauli ya Mzee Mangula, Rais Samia, Waziri Mwambe na ya Hayati Magufuli inaonyesha Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni ‘White Elephant’

Sema hoja ya kipi kipo kwenye ilani au hakipo haina mashiko kabisa maana katika awamu iliyopita mengi yalifanyika na hayakuwa kwenye ilani na hakuna aliehoji ni wakati huu Tu sasa cjui.

Sent from my CPH2185 using JamiiForums mobile app
 
Bandari ya Bagamoyo ikikamilika haiwezi kuwa 'White elephant' tena itatupunguzia na foleni Mandela Rd.

'White elephant' ni ile Chato International Airport ya Magufuli.
 
Huu mkanganyiko wa kauli za hawa viongozi waandamizi wa chama na serikali kuhusu bandari ya Bagamoyo inaonyesha kuna madudu sana ndani ya terms of contract,na hii inatokana na baadhi ya viongozi wachache waliolenga kujinufaisha na mradi huo .

Rejea jinsi dharura iliyotumika kupitisha miswaada hiyo na idadi ya wabunge waliotumika kufanya ufedhuli huu,idadi walikuwa ni sitini tu kati ya wabunge mia tatu.

Mzee Mangula anasema bandari haimo kwenye ilani ,bali ilani inataja ujenzi wa gati tu. je nini tofauti ya gati na bandari?

Wanaopanga kujinufaisha na huu mradi kwa kuliingizia Taifa hasara kama ni kweli, wajue kwamba tutawadai wao pia tutakidai kizazi chao kwa gharama yoyote ile warudishe walichopora
Kadiri muda unavyo kwenda tutaona mengi.

Katikati ya 2023 pia hoja ya hii ni awamu ya ngapi itaibuka upya ilikuweka mambo sawa, sasaivi wakulungwa wamekausha kidogo kwanza mambo yaende sababu ni mapema mmno.
 
Waafrica sijui tumekosa nini kwa Mungu, hii bandari ya bagamoyo ikijengwa tutapoteza hata hichi kidogo tunachopata kwenye bandarizetu.

Yani Mungu ametupa kitegauchumi cha bure msingi maji piatunataka kuwapawatu wengine fursa ya kupiga pesa!!!.

Kwanini kuingia mkataba wa miaka mingi kiasihicho katika njia zetu kuu za uchumi, ivi tuna taka nini hasa.
 
Wa Oman hawana tatizo,ni ndugu zetu wale miaka mingi.tatizo hii Mi China ni tatizo haswa,
Yakiingilia mradi ni shida tu.
Na viongozi wetu walivyo na tamaa wanaingizwa king kilaini tu.
Then tunabaki maskini mpk kufa.
Na vizazi pia.
Kiongozi mmoja anasaini mkataba na hao watu miaka 90+ kivipi?
 
Bandari ya Bagamoyo ikikamilika haiwezi kuwa 'White elephant' tena itatupunguzia na foleni Mandela Rd.

'White elephant' ni ile Chato International Airport ya Magufuli.
Magufuli Airport International,nimali ya Watanganyika haidaiwi na chochote, Bandari ya Bagamoyo itakuwa mali ya Nani?kuwa mzalendo, inawezekana leo una nafasi,kumbuka uzao wako.
 
Huu mkanganyiko wa kauli za hawa viongozi waandamizi wa chama na serikali kuhusu bandari ya Bagamoyo inaonyesha kuna madudu sana ndani ya terms of contract,na hii inatokana na baadhi ya viongozi wachache waliolenga kujinufaisha na mradi huo .

Rejea jinsi dharura iliyotumika kupitisha miswaada hiyo na idadi ya wabunge waliotumika kufanya ufedhuli huu,idadi walikuwa ni sitini tu kati ya wabunge mia tatu.

Mzee Mangula anasema bandari haimo kwenye ilani ,bali ilani inataja ujenzi wa gati tu. je nini tofauti ya gati na bandari?

Wanaopanga kujinufaisha na huu mradi kwa kuliingizia Taifa hasara kama ni kweli, wajue kwamba tutawadai wao pia tutakidai kizazi chao kwa gharama yoyote ile warudishe walichopora
Hakuna lolote yatapiga pesa na yataenda kutubu na kutoa sadaka
 
Wanaopanga kujinufaisha na huu mradi kwa kuliingizia Taifa hasara kama ni kweli, wajue kwamba tutawadai wao pia tutakidai kizazi chao kwa gharama yoyote ile warudishe walichopora
Mkuu kama ni kuwadai inapaswa tuwadai sasa wakati tunayo hiyo nafasi, baaadae nafasi inaweza isiwepo!
 
Namsikitikia Sana Hangaya kaingizwa mkenge na Msoga gang,itamugharimu Sana.
Unamsikitikia kwa lipi wakati yeye hakusikitikii? Maana inawezekana hata hakujui na hatakaa akujue.

Wewe unajua kwenye kibubu chake ameshafungia kiasi gani mpaka hapo alipo? Pakichafuka hapa hutamuona, atakuacha uendelee kusikitika vizuri.
 
Mkumbusheni mzee Mangula kwamba:-
-ujenzi wa daraja la Busisi
- kuhamisha wanyama kwenda kuanzisha hifadhi ya Burigi
-ununuzi wa ndege
-ukusanyaji wa tozo
-n.k

Vyote hivi havikuwemo/havimo kwenye ilani ya ya uchaguzi ya ccm.
Mangula anajua kabisa Chama kilikosea kumpitisha Mrundi kushika hatamu!Toa mifano ya awamu nyingine ya uongozi wa nchi yetu!sio hii iliopita ya Mrundi!!!
 
Kwa jinsi ninavyokereka na bandari ya bagamoyo tusilaumiane baadaye halafu na huyu naye anataka avute na bomba la gesi liende bagamoyo tutamwaga mboga
 
Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2015 UK. 66 iliahidi ujenzi wa Bandari hii.
 
Back
Top Bottom