Mkanganyiko wa kauli ya Mzee Mangula, Rais Samia, Waziri Mwambe na ya Hayati Magufuli inaonyesha Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni ‘White Elephant’

wakatanta

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
1,911
2,000
Huu mkanganyiko wa kauli za hawa viongozi waandamizi wa chama na serikali kuhusu bandari ya Bagamoyo inaonyesha kuna madudu sana ndani ya terms of contract,na hii inatokana na baadhi ya viongozi wachache waliolenga kujinufaisha na mradi huo .

Rejea jinsi dharura iliyotumika kupitisha miswaada hiyo na idadi ya wabunge waliotumika kufanya ufedhuli huu,idadi walikuwa ni sitini tu kati ya wabunge mia tatu.

Mzee Mangula anasema bandari haimo kwenye ilani ,bali ilani inataja ujenzi wa gati tu. je nini tofauti ya gati na bandari?

Wanaopanga kujinufaisha na huu mradi kwa kuliingizia Taifa hasara kama ni kweli, wajue kwamba tutawadai wao pia tutakidai kizazi chao kwa gharama yoyote ile warudishe walichopora
 
Tangawizi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
4,264
2,000
Mkumbusheni mzee Mangula kwamba:-
-ujenzi wa daraja la Busisi
- kuhamisha wanyama kwenda kuanzisha hifadhi ya Burigi
-ununuzi wa ndege
-ukusanyaji wa tozo
-n.k

Vyote hivi havikuwemo/havimo kwenye ilani ya ya uchaguzi ya ccm.
Two wrongs dont make another wrong thing becomes right. Kuna kitu hakiko sawa. Tunalazimisha sana huu mradi kwa sababu zipi?
 
Imalamawazo

JF-Expert Member
Jul 27, 2021
243
500
Mkumbusheni mzee Mangula kwamba:-
-ujenzi wa daraja la Busisi
- kuhamisha wanyama kwenda kuanzisha hifadhi ya Burigi
-ununuzi wa ndege
-ukusanyaji wa tozo
-n.k

Vyote hivi havikuwemo/havimo kwenye ilani ya ya uchaguzi ya ccm.
Waambieni ukweli wa Oman, hata kama hiyo bandari itajengwa na hata kama tukishindwa kulipa deni lao, huyo mtu wao Sultan wa Zanzibar hatarejea Zanzibar kamwe.
 
michosho

JF-Expert Member
Mar 17, 2012
576
500
Huu mkanganyiko wa kauli za hawa viongozi waandamizi wa chama na serikali kuhusu bandari ya Bagamoyo inaonyesha kuna madudu sana ndani ya terms of contract,na hii inatokana na baadhi ya viongozi wachache waliolenga kujinufaisha na mradi huo .

Rejea jinsi dhararura iliyotumika kupitisha miswaada hiyo na idadi ya wabunge waliotumika kufanya ufedhuli huu,idadi walikuwa ni sitini tu kati ya wabunge mia tatu.

Mzee Mangula anasema bandari haimo kwenye ilani ,bali ilani inataja ujenzi wa gati tu. je nini tofauti ya gati na bandari?

Wanaopanga kujinufaisha na huu mradi kwa kuliingizia Taifa hasara kama ni kweli, wajue kwamba tutawadai wao pia tutakidai kizazi chao kwa gharama yoyote ile warudishe walichopora
Uko sawa mkuu,ila anza na wenye gesi ya mtwara...ukiwamudu....basi hata huko kwenye bandari utawamudu,. otherwise acha wenye nchi yao waendelee kula matunda ya nchi yao wenyewe na familia zao
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,855
2,000
Huu mkanganyiko wa kauli za hawa viongozi waandamizi wa chama na serikali kuhusu bandari ya Bagamoyo inaonyesha kuna madudu sana ndani ya terms of contract,na hii inatokana na baadhi ya viongozi wachache waliolenga kujinufaisha na mradi huo .

Rejea jinsi dhararura iliyotumika kupitisha miswaada hiyo na idadi ya wabunge waliotumika kufanya ufedhuli huu,idadi walikuwa ni sitini tu kati ya wabunge mia tatu.

Mzee Mangula anasema bandari haimo kwenye ilani ,bali ilani inataja ujenzi wa gati tu. je nini tofauti ya gati na bandari?

Wanaopanga kujinufaisha na huu mradi kwa kuliingizia Taifa hasara kama ni kweli, wajue kwamba tutawadai wao pia tutakidai kizazi chao kwa gharama yoyote ile warudishe walichopora
Hakuna mkanganyiko hapa bali ukweli kuwa CCM na serikali yao wameishiwa, wanapingana, wanapigana vita na hawajui walitendalo. Rais anasema hili, waziri mkuu lile na wazir hili. Kuna harufu ya ufisadi na ujinga vya kutisha hapa.
 
Ligaba

JF-Expert Member
Oct 12, 2018
1,031
2,000
Hapa unatukosea wengine. Umetaja Maguli, Samia, Mwambe, sijui Mangula kwamba wametoa kauli.
Kuna sisi ambao hatujui wamesemaje tunashindwa kuelewa.

Nakuomba utuambie kauli za hao watu ili na sisi tufahamu na tuchangie.

Kauli ya Magufuli ni ipi?
Samia kasemaje?
Mwambe kazungumzaje?
Mangula anasemaje?
Ukipenda ongeza na Ndugai ana kauli gani?
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
31,826
2,000
200 (1).gif
 
ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,187
2,000
Mkumbusheni mzee Mangula kwamba:-
-ujenzi wa daraja la Busisi
- kuhamisha wanyama kwenda kuanzisha hifadhi ya Burigi
-ununuzi wa ndege
-ukusanyaji wa tozo
-n.k

Vyote hivi havikuwemo/havimo kwenye ilani ya ya uchaguzi ya ccm.
Kwenye kampeni 2015 ccm Kirumba, Ujenzi wa daraja la busisi kigongo ilikuwa hoja kwenye hitimisho la kampeni ya mgombea. Tena Jk alikuwepo.
Ujenzi wa viwanja vya ndege 11 vipya ilikuwa sehemu ya ilani.
 
Imalamawazo

JF-Expert Member
Jul 27, 2021
243
500
Nonsense!
Huu mradi una mahesabu makali ya kimkakati ambayo mtu mwenye uelewa wa kawaida hawezi kuelewa kabisa. Lakini ntajaribu kukuelewesha.

Mjenzi wa mradi ni mchina, msimamizi wa mradi mchina. Mtoa pesa za mradi, Oman. Mradi unatekelezwa Bagamoyo. Bagamoyo ni sehemu ya ile ardhi ya Oman kupitia Sultan wa Zanzibar.

Mpaka hapo nikikuambia Oman anajenga nchi yake ya Bagamoyo utaelewa au bado uko na nonsense kwa kichwa?
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
11,806
2,000
Huu mradi una mahesabu makali ya kimkakati ambayo mtu mwenye uelewa wa kawaida hawezi kuelewa kabisa. Lakini ntajaribu kukuelewesha.
Mjenzi wa mradi ni mchina, msimamizi wa mradi mchina. Mtoa pesa za mradi, Oman...
Watanzania tumejaa visumbufu kichwani. Bagamoyo ni ardhi ya Oman? Kwa mintarafu na mikataba ipi? Tusikariri zile porojo za jiwe.

UAE wanageliendela kuwa na mawazo mgando ya kuwanyima wazungu mkataba wa kujenga bandari mahala ilipo Dubai Port miaka ile ya 47 nadhani mpk Sasa wangelikuwa bado wamekala.

Bagamoyo port ijengwe
 
Imalamawazo

JF-Expert Member
Jul 27, 2021
243
500
Watanzania tumejaa visumbufu kichwani. Bagamoyo ni ardhi ya Oman? Kwa mintarafu na mikataba ipi? Tusikariri zile porojo za jiwe.

UAE wanageliendela kuwa na mawazo mgando ya kuwanyima wazungu mkataba wa kujenga bandari mahala ilipo Dubai Port miaka ile ya 47 nadhani mpk Sasa wangelikuwa bado wamekala.

Bagamoyo port ijengwe
Tafuta notisi zako za sekondari kuna mahali uliandika 'ten miles coastal strip'. Mengine ntakuwa nakufafanulia taratibu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom