#COVID19 Mkanganyiko wa chanjo ya Corona

Liability

Member
Oct 20, 2019
75
100
Baada ya mheshimiwa Rais Samia kutoa mwelekeo wa taifa kuhusu mapambano ya Corona zimeibuka hoja nyingi sana hasa kuhusu hizi chanjo.

Jana nilipata nafasi ya kumtembelea rafiki yangu hapa Morogoro. Nilichokisikia sikuamini. Watumishi wengi wa kada moja iliyopewa kipaumbele cha kupata hawataki chanjo.

Magufuli alipanda mizizi Fulani kwa Watanzania kuhusu namna ya kujilinda na Corona na watu wakaamini hata kama siyo njia sahihi.

Nashauri mizizi hii ivunje kwanza ili watu wafuate kauli ya mheshimia rais Samia.

Juzi baada ya Gwajima kutoa Yale matamko ndio yameongeza hamasa na kuwa reference ya watu wanao kataa chanjo.

Mimi,wewe na yule tunawajibu wa kupambana na Corona
 
Unajidai una upendo sana na raia. Wee kale chanjo ambaye hataki achana nae. Yaani watu wale wale waliotuaminisha haifai sasa hivi mnatuambia inafaa halafu mnataka tuawaamini tuu hivyo.
 
Hivi kama chanjo ni hiari ya mtu, ni kwa nini nguvu kubwa inatumika kushawishi wasiotaka kuchanjwa wahamasike na kubadilisha misimamo yao?.

Hivi ni kwa nini asiyetaka kuchanjwa alazimishwe kuchanjwa eti kulinda wengine?

Hivi ni kwa nini chanjo imekuwa muhimu zaidi kuliko Corona yenyewe? Chanzo chake na tiba bado havifahamiki, iweje chanjo iaminiwe na wizara kutoa matokeo chanya?.

Maswali yako mengi tu dhidi ya majibu machache!.
 
Attachments

  • AUD-20210930-WA0000.aac
    255.5 KB · Views: 1
Baada ya mheshimiwa Rais Samia kutoa mwelekeo wa taifa kuhusu mapambano ya Corona zimeibuka hoja nyingi sana hasa kuhusu hizi chanjo.

Jana nilipata nafasi ya kumtembelea rafiki yangu hapa Morogoro. Nilichokisikia sikuamini. Watumishi wengi wa kada moja iliyopewa kipaumbele cha kupata hawataki chanjo.

Magufuli alipanda mizizi Fulani kwa Watanzania kuhusu namna ya kujilinda na Corona na watu wakaamini hata kama siyo njia sahihi.

Nashauri mizizi hii ivunje kwanza ili watu wafuate kauli ya mheshimia rais Samia.

Juzi baada ya Gwajima kutoa Yale matamko ndio yameongeza hamasa na kuwa reference ya watu wanao kataa chanjo.

Mimi,wewe na yule tunawajibu wa kupambana na Corona
  • Kinachohitajika na kilichotakiwa kufanywa tangu mwanzo ni wahusika kupewa elimu sahihi ili kuwaondoa kwenye mtazamo wa awali kuhusiana na chanjo hizi;
  • Ikumbukwe pia suala la chanjo hizi ni la HIYARI na hili limeshawekwa bayana. Hivyo kama mtu ameelimishwa na bado haoni umuhimu/ulazima wa kubadilisha mtazamo wake then hilo liheshimiwe na isiwe chanzo cha kuleta chuki ama uhasama kati ya wanaokubali kuchanjwa na wasiokubali kwani chanjo hizi zinasaidia kupunguza makali ya ugonjwa pale mtu anapopata maambukizi.
 
Back
Top Bottom