Mkanganyiko mkubwa wanasheria naomba ushauri wenu hapa tafadhali

Atclkwanza

JF-Expert Member
Dec 20, 2015
823
998
Wafanyakazi wa Fastjet wameipeleka Fastjet CMA wakiomba walipwe stahiki zao za tangia mwezi February.

Ili kufanikisha malipo hayo, wafanyakazi waliomba zuio mahakama kuu kitengo cha kazi ndege isiondoke hapa nchini mpaka walipwe Chao,x na ndege Hiyo ilikuwa leased kutoka Celestial Aviation na Fastjet lakini kwa muda mpaka sasa bado IPO mikononi mwa Fastjet.

Celestial aviation wakawafungulia case wafanyakazi na Fastjet mahakama kitengo cha kazi wakioomba mahakama itengue zuio kwani ndege si mali ya Fastjet, lakini mahakama ilikataa na kuwaaambia mpaka case ya msingi iliyopo CMA imalizike.

Cha ajabu hawa Celestial baada ya kushindwa mahakama ya kazi wamefungua madai yale yale mahakama ya biashara, je mahakama ya biashara ikiamua vinginevyo na Mahakama Kuu kitengo cha kazi ni hukumu ipi itatekelezwa, na iweje wafanyakazi waunganishwe kwenye mahakama ya biashara?

Ni kwa nini ile hukumu wasingeikatia rufaa kule walikoshindwa Mahakama Kuu kitengo cha kazi? Naomba watalaam wa mambo haya tujadili hapa.
 
Back
Top Bottom