Mkanganyiko katika Gharama za Vocha za Simu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mkanganyiko katika Gharama za Vocha za Simu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Mwalimu, Jul 3, 2009.

 1. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Leo asubuhi nilikuwa nataka kununua vocha ya vodacom na muuzaji akaniambia bado sh 100. Nikamuuliza kulikoni, akaniambia vodacom wamepandisha gharama kwa sh 100 na hiyo ni kwa vocha za aina zote. Naomba kama kuna mdau yoyote mwenye taarifa zaidi kuhusu hii ishu atusaide tafadhali.
   
 2. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hata mimi jana niliambiwa hivyo
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Du hii hali sasa inazingua, jana nilitaka kumpatia vitasa muuza duka pale vijana kinondoni aliponiuzia Tigo ya buku tano kwa buku tano mia tano.
   
 4. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Jamani hata mimi imenitokea leo asubuhi. Huu ni wizi unauziwa kitu cha buku kwa buku na mia,siyo sahihi. Waongeze gharama za kupiga lakini si gharama za vocha. Maana sisi hatununui vocha,tunanunua muda wa hewani. Kama unamuuzia mtu muda wa hewani wa 1000 kwa 1100 huo ni wizi.
   
 5. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Huu ni wizi, Haiwezekani muda wa maongezi wa sh 2000 kwa sh 2100. Nakumbuka kwenye budget ya mwaka 2009/2010 lilizungumzwa swala la kodi kwenye muda wa hewani.
   
 6. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  huu ni wizi kabisa wanasema gharama za simu zimepungua lakini wanaongeza cha juu. waache ibaki elfu 1 mtu ajue atajibana vipi.
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Tutazoea tu!
  Hata bei za mafuta ilikua hivyo hivyo.walipandisha kwa ghafla watu wakapiga kelele.wakashusha kisha wakaanza kupandisha kidogokidogo
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Umenikumbusha issue ya mafuta... yalipofikia Tshs 1,350/= (petrol) kila mtu alipiga kelele, serikali kwa usanii mkubwa ikaonekana kuwajali wananchi kupitia EWURA, wakapunguza yakarejea Tshs 1,200/= na watanzania (wadanganyika) wakapoa kabisa na kuchekelea kuwa 'walau yamepungua'... nyuma ya pazia kilichofanyika ni kupandisha 'daily' kwa sh. 10 hivi na mpaka sasa nimefahamishwa kuwa Petrol (ndani ya miezi kama miwili tu...!) imefikia Tshs 1,550/= kwa lita moja.

  Hili la muda wa maongezi wa simu watanzania watazoea... wataanza na kelele kisha watapandishiwa kimtindo na kuhakikisha wenye uwezo wa kuongea kwa simu wanabakia kuwa aidha wabunge na viongozi wachache wa serikali ama watanzania wachache 'walioneemeka'.

  Hii ndiyo Tanzania zaidi ya unavyoijua!
   
 9. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Mie asubuhi hii nimenunua vocha za aina mbali mbali, zile za sh 1000/- wameniuzia kwa 1100/- na za 5000/- wameniuzia kwa 5500/-. nilipong'aka nikaambiwa kuwa kuanzia Julai mosi bei za vocha zimepanda bei tangu Julai Mosi. Nikanyong'onyea na kuondoka.

  Ila ninacholaumu ni kwamba wenye mitandao ya simu hawajatoa taarifa kwamba bei za vocha zimepanda bei tangu Julai ianze. May be hii ndio sababu ya tatizo hili!
   
 10. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Kwanini ulipie hela zaidi kwa vocha ambayo tayari imeandikwa thamani yake? Sidhani hii inaweza kusimama hata mbele ya sheria....

  WIZI MTUPU!
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Na watanzania asilimia kubwa huishia hivi...

  Unanyong'onyea kisha unaondoka hahahahahaha!

  Tanzania inaweza kuongozeka kirahisi nimeamini...
   
 12. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Burn!

  Hapo umechomekea leo asubuhi nimenunua tigo ya Elfu tano kwa bei hiyo hiyo! ya buku tano muza kadi kakufua tu !!!

  Watumiaji wa Voda walishauriwa na Mzee Mwanakijiji waachane na mtandao ambao umeingizwa hapa TZ kwa rushwa ya CCM hamkusikia litakalowafika ni shauri yenu hampaswi kulalamika.

  Wewe Burn hata TIGO wangepandisha kwa rate inayotumika ya Tshs.60 kwa dakika Tigo kwa Tigo bado inalipa. Kama uko Zain au Voda ambao inabidi uchague watu kumi au watano kwa bei ya Tshs.60 kwa dakika always ianakula kwako! Hivi nyie watu wa KIJANI hamkujifunza hata Table mlipokuwa bush school now chekechea !!!!

  Coming back to the stupid TCRA hivi kukimbilia kusajili simu kwa vile tu watu wezi wachache wametumiwa ujumbe wa matusi inasaidia kitu gani kuleta nafuu ya bei kwa watumiaji wa mitandao ya simu. Huko ulaya wanasajili simu and people have proper ID's LAKINI wizi wa simu na matusi mbele kwa mbele!!! Prof. Mkoma You are really dead and buried!!! Magari yenye ukubwa kama VX yanaibwa na ktokomea hayaonekani kwani si yamesajiliwa na majina ya wabunge!! Unatarajia simu isiibwe simply kwa kusajili acheni upuuzi hata watu wenyewe hawajulikani shit!!!!

  Kwa kweli haihitajiki mtu kuwa Profesa kuliona hilo. The challenge brought by TIGO kwa kushusha bei mpaka kufika 60/= per minute ni fundisho tosha kwa wapumbavu wa CCM I mean the JMK aka Matonya GVT kwamba tumekuwa tukiibiwa kichizi na makampuni ya simu!! now to Mkoma kwa nini usitumie Tigo kama Guinea pig na kupanga bei kama anavyofanya Sekirasa kwenye usafiri wa mabasi?? That man is not a Professor lakini take trouble and ask the wananchi on the streets ! Definately he is popular than many of our ministers!!! Na anafuatilia

  The bottom line nawashauri mjiunge na TIGO you won't regret tigo can as well expand and take up the influx na kumonopolize the market kama walivyofanya Tanzania Breweries walipoiua Kibo Breweries kule Moshi!! To HELL WITH ZAIN AND VODA kwani wana kiburi cha CCM.
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280

  Kwi kwi kwi!
  Sasa ningefanyaje mkubwa? Options nilizokuwa nazo ni kwa wakati huo (asubuhi ya leo) ni hizi!-
  1. Kuacha vocha na kuondoka, kisha nikose mawasiliano
  2. Kumshikisha adabu muuzaji na kukutana na mkono wa dola
  3. Kupiga simu ya huduma ya wateja na kuomba ufafanuzi

  Kwa sababu nilikuwa nina haraka ya kuwahi kazini nikachukuwa uamuzi wa kuumia kwa kununua vocha kwa bei tajwa na kuugulia maumivu mbele ya safari.
   
 14. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ipo siku stempu iliyoandikwa sh. 400 itauzwa kwa jero !!
   
 15. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #15
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Muuzaji hana kosa, wala usithubutu kumtendea visivyo... lakini haya mekundu ndiyo concern yangu....!
   
 16. K

  Kelelee Senior Member

  #16
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 113
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nasema hivi...hii nchi tunakoelekea sio kwenyewe.......ok kampuni zimeamua for whatever reasons kupandisha gharama ya voucher zao...imewazuia nini kuwatangazia wateja kabla hizo rates hazijaanza kutumika? mbona wakiwa wanafanya promotions za kuwaibia maskini hela zao wanatangaza mpaka masikio yanauma?

  Bw Ngowi ndani ya power breakfast clouds mara nyingi anakuwepo kuwaambia wadanganyika oh vodacom wameleta product mpya blah blah blah...sasa hili la bei mpya ya vouchers personally sijasikia ikipewa "airtime" kwa radio......anyway bottom line...kama voucher imeandikwa 5000, 2000, 1000, 500, 10,000 i for one am not going to add a single cent in order to buy it...wanataka kuuza 5500, 1200 etc let them print hizo vouchers with those prices sio kufanya mambo ya kiubabaishaji........
   
 17. H1N1

  H1N1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 4,201
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Wadanganyika... Mnastahili mnachopata kwani ndivo mlivyo.Kama vocha inathamani na imeandikwa Elfu tano nawe toa Fedha halali kwa malipo ya Elfu tano...
   
 18. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kama tulisikiliza vizuri bajeti 2009/2010, VAT sasa inatozwa kwenye vocha na siyo Muda wa hewani. Nadhani ndio sababu. Hata hivyo, makampuni ya simu yanatakiwa kubeba lawama hizi kwa kutowafahamisha wateja wao, maana sio watu wote walisikiliza na kufuatilia vizuri marekebisho ya kodi hasa VAT kwenye masuala mbalimbali.
   
 19. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Pengine ni mikakati ya uchaguzi mkuu 2010. Unajua hizi pesa wanazojifanya kwamba wanatoa msaada ni zetu? Yaani bila hata kujijua. Hii ndio VICIOUS CYCLE OF PEVERTY Bana! Matajiri wataendelea kushiba.
   
 20. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2009
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Na vocha hizo ziandikwa kabisa kama ni 1000 iwe 1000 + 18%VAT!!!!

  Ngereja kama ni VAT ndo imeongeza kwenye vocha kwa nini iwe ni 10% na sio 18%????

  Huu ni wizi tu na hakuna haja ya kuwatetea hawa VODA, ZAIN (VIVENDI), na mitandao yote mingine inayofanya mambo kiholela!!?

  Mbona hata bia huwa tunaambiwa kwamba bei zitapanda na TBL wanatangaza kwenye magazeti mabadiliko ya bei ya vinywaji vyao kulingana na athari za bajeti???

  All in all this is bullshit....
   
Loading...