MKANGAFU (airbus) WA ATCL-hatimaye kuwasili

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,050
baada ya muda mrefu serikali kuheshimu matakwa ya wana JF Na kujua kumbe mengi tyasemwayo huku ni ya kweli tofauti na walivyojua mwanzoni,,serikali imeamua kutoa gov gurantee kwa masharti mengi tu ambayo kwetu sie tunaona kama kumwambia bwana DAVI na wenzake wajitayarishe kufunga virago,,na hapo ndipo tulipogundua kwa nini hawa ndugu zetu wanakula kwa fujo hivi,,,hebu angalia gurantee aijatoka wamepeleka RUBANI anajiita mazulwa na kakaa wiki mbili majuzi kapiga simu anawaambia nakaa ten wiki mbili nitumieni hela,,embu angalieni wasivyo na uchungu analipwa doller 400 kwa siku anakaa siku 31,,doller 12,000..
jamani kampuni ikifa mungu ataweza hata kuwanyanyua kwa ulaji huu.....mi sisemi niko nje kwa raha zangu kazi kwenu watanzania....sisi tumeamua kubeba mabox imani imetushinda kwa watanzania,,,mwisho nashauri wawepo wanaandishi wengi na watanzania siku ya kupokea mkangafu wetu ambao ni laana kwa wajukuu zetu wajayo....tatizo si watu bali ni roho zao hazina uwepo wa mungu kabisa wala kumwogopa mungu,,,swali je hii ndege itaimaliza atcl???????????????????au itaimarisha atcl?????????
kwenu wadau hii ni kampuni yenu na wala si watu binafsi tunaitaji hoja zenu,,,
wenu
mtanzania-mzamiaji
 
Dear All,



Please find herewith attached the Scanned Guarantee given on behalf of the
Government of the United Republic of Tanzania.



The Guarantee has got ten (10) pages in total. Kindly acknowledge receipt.



Regards,







1. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ni David Mataka. Yeye aliteuliwa na Rais JK baada ya rais aliyemtangulia kumtimua kwa ufisadi. JK alimuonea huruma DM baada ya kukaa ubaoni kwa muda na pia kushindwa kinyang'anyiro cha ubunge kwa tiketi ya chama tawala. Wananchi wa jimbo lake na wa chama chake hawakumpa kura kwa kuwa alikwisha onekana mbele ya rais BM kuwa ni fisadi wa hali ya juu japo yeye rais BM alikuwa anawakumbatia mafisadi kama Balali.


Mkuu huyu wa kampuni ameanzisha uongozi wa dharura(Management by crisis) ambapo kila asubuhi wakurugenzi na mameneja wateule katika ufisadi hukaa vikao vya kuangamiza kampuni. Amepata Benz ya kisasa katika mgao wa magari yaliyotolewa na wauzaji baada ya kununua magari ya kampuni huko Dubai kwa bei ya juu. Magari hayo ni ya mwaka 1998 japo bei yake ni karibu na mara mbili ya yale yanayouzwa na makampuni mengine ya Dubai. Yeye huwa anasuka jambo halafu anamwachia George, Eliasaph au William walichochee katika kikao cha hao viongozi.

2. Mark Manji yeye ni mtu wa Musoma japo jina lake la kihindi. Huyu ni mshauri wa mkurugenzi mkuu. Alikuwa mkurugenzi wa idara ya operations wakati wa makaburu japo idara hii huwa inaongozwa na marubani. Alipewa cheo hiki na makaburu ili kuwaweka marubani katika himaya ya makundi. Makaburu walipoondoka aliomba kuacha kazi kwa hiari na akastaafu akaomba kuendelea na kazi tena kama mshauri wa mkurugenzi mkuu. Kwa kuwa alikuwa na mapenzi na makaburu na kwa kuwa ameshapata mafao yake, hana huruma na kampuni kwa sasa badala yake yeye ni kichocheo na hujifanya analijua shirika. Anatumia utoto wa mjini kufanya kazi kwani hana shahada hata moja japo amepewa nafasi nyeti.



3. Eliasaph Mathew aliajiriwa na makaburu kama meneja wa fedha kwa maana hiyo ni mtu wa makaburu. Baada ya mkurugenzi wa fedha aliyekuwa kaburu kuondoka amekaimu nafasi hiyo hadi leo. Huyu ndie kinara wa kupindisha taratibu za matumizi ya fedha na ununuzi. Ni mfuasi namba moja wa DM kwani kwa sasa pesa za kampuni hutolewa kiholela kulipia gharama kwa ufisadi. Mfano kabla ya kufunga mwaka 2007 shillingi millioni mia mbili hamsini zilichotwa kulipa gharama za kutoa magari nane yaliyokuwa katika yadi ya kuweka mgari iliyo ya watu binafsi. Haishi hapo huchota dola elfu tatu taslimu toka kwa mtunza fedha kila mwezi na kumpa huyu mwenye yadi ya kuhifadhi magari. Huidhinisha malipo kwa ankara tu bila kujali taratibu nyingine. Ndiye aliyejumuika katika jopo lililokwenda Dubai kuchagua magari ya kampuni na kuyanunua kwa bei mbaya bila kufuata taratibu za ununuzi. Magari haya ni ya 1998 japo ATCL ni mali ya serikali,hilo halikutiliwa maanani. Yeye amepata zawadi ya VX Landcruiser ya kisasa kama mgao katika hayo manunuzi na sasa ameweka pembeni Vitara yake. Hutumiwa katika mikakati ya kuwaondoa watu wa zamani na wenye sifa kwa kuwazulia kesi na shutuma za matumizi mabaya ya pesa kitu ambacho si kweli.
Waliyoonja joto hilo ni pamoja na Hassani ambaye aliamua kuacha kazi, Hamisi na Mndeme ambao wamesimamishwa kwa suala la bwana Mohamed Makaratasi ambaye ni rafiki wa George Mazula.

4. George Mazula yeye eti ndiye rubani kiongozi na mshauri wa DM. Huyu aliwahi kuachishwa kazi wakati mwenyekiti wa bodi alikuwa ni Abasi Sykes. George aliwahi kuunguza injini mbili za Fokker kwa mpigo pale Tanga. Amewahi kuangusha ndege aina ya Fokker hapa Dar es salaam. Amewahi kuua mtu pale uwanja mpya wa JK Nyerere kwa kukatwa na pangaboi baada ya yeye kuzembea kuzima injini. George ni kiungo wa mikakati yote ya ufisadi na kuondolewa watu katika nafasi zao. Alikuwa mfadhili wa DM wakati akiwa ubaoni. Ni rubani mwenye makeke na mikosi mingi. Katika dili ya Dubai yeye amepata Volvo na kujidai amekopa.

5. Amin Mziray huyu ni katibu wa kampuni. Yeye ni chapombe. Alipewa gari ya kampuni na makaburu na kulipindua kwa ulevi. Anayo shahada ya sheria lakini haitumii kwa maslahi ya kampuni. Kampuni imeshindwa kesi nyingi kwa kutokuwa makini huyu mwanasheria. Yumo katika hili jopo la ufisadi wa kampuni. Katika mgao wa magari ya Dubai yeye amepata VX Landcruiser la nguvu. Hayupo tayari kutetea hoja mbovu zinazotolewa ndani ya vikao vya hili jopo la ufisadi.

6. William Haji, anakaimu nafasi ya mkaguzi mahesabu wa ndani. Aliajiriwa wakati wa makaburu kama mkaguzi wa mahesabu wa ndani chini ya bwana Yakubu. Baada ya muda bwana YAkubu aliwekwa pembeni na huyu bwana kukaimu nafasi yake. Kwa sasa yeye ndiye anayekagua malipo (Pre-audit) hivyo yumo ndani ya mtandao wa ulaji. Ndiye anayetumiwa kutengeneza taarifa za kuzua kesi na uonevu kwa wafanyakazi wa chini. Huchukua nafasi ya afisa usalama wa kampuni ili kupindisha ukweli na hatimaye kuwadhalilisha ama kuwatimua wafanyakazi wasiyo na hatia. Ni hatari sana kwani yupo karibu na DM na Eliasaph katika kila mpango.

7. Sadiki Muze, Yeye ni mkurugenzi wa idara ya operations kwa sasa. Amepewa nafasi hiyo yeye kwani ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa DM wakati akiwa ubaoni. Pia ni mshirika wa DM katika vinywaji na mwanachama wa kijiwe kimoja na George. Ni Sadiki na George pekee waliyopewa vyeo na kuenguliwa wengine baada ya DM kuchukuwa uongozi ATCL na ni chapombe. Sadiki na George wamelipwa fadhila.

8. Heho Mbiru ni Mkenya, aliajiriwa kwa nguvu enzi za makaburu kama mkurugenzi wa masoko. Aliajiriwa kwa nguvu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya ATCL wakati huo Ali Mufuruki kwa kisingizio kuwa hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kushika nafasi hiyo. Ni mzalendo wa Kenya kweli kweli kwani kazi zinazoweza kufanyika hapa (kama Graphics) huzipeleka kwenye kampuni yake. Anayo mapenzi na makaburu hivyo kuleta mabadiliko tunayotaka yeye ni kikwazo na ndiyo maana ni rahisi kutumiwa katika hujuma. Kumbuka tunaushindani na Kenya Airways huyu atatumaliza.

9. Ajay Gopinath raia wa India. Aliajiriwa kwa nguvu wakati wa makaburu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi Ali Mufuruki. Ajay aliwahi kufukuzwa nchini lakini kwa sababu zake Ali alifanya juu chini na kumrudisha kama mkurugenzi wa mauzo. Anatumiwa katika upatikanaji wa fedha na kutumika vibaya. Hana sauti ndani ya utawala huu kwani ni mgeni.

10. Alphonse Mkinga ni meneja utumishi. Alistaafu na kuchukua mafao yake baada ya makaburu kutimka. Anafanya kazi kwa mkataba na kuzuia ajira kwa waliomaliza vyuo.
Ameidumaza idara ya utumishi kwa kutoweka muundo wa utumishi na taratibu mbalimbali za ajira. Matokeo yake mkurugenzi mkuu huleta watu wake japo wapo waliofanya usaili. Mfano ni ajira ya mhudumu katika ofisi ya mkurugenzi mkuu,ajira ya afisa majengo na mali ambaye ni jamaa yake. Huyu bwana Peter Gosh anachukua nafasi ya bwana Hassan Kikoko alieandamwa na huu mtandao wa ufisadi na hatimaye kuamua kustaafu mapema. Yupo dereva aliajiriwa kwa hila japo wapo waliofanya usaili na hadi sasa hawajapata ajira. Bwana Mkinga hana sauti kwani yupo kulinda maslahi yake baada ya kupata ajira ya pili.

11. Fidelis Tarimo ni mkurugenzi wa uhandisi. Historia yake ni ufisadi mtupu. Aliwahi kusimamishwa kazi na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi wakati huo Mzee Abasi Sykes. Tarimo alikwenda kusimamia matengenezo makubwa ya Boeing ya ATC wakati huo (major check) nchini Ireland. Hakuwa anafuatilia gharama halisi za matengenezo na kujali maslahi yake hivyo kusababisha gharama kupanda kwa shilingi bilioni moja na nusu toka ghrama halisi na kulitia shirika hasara na kusimamishwa kazi. Alipata nafasi wakati wa makaburu kwani hakuwa mtetezi wa wazalendo. Kwa sasa wafanyakazi wa idara yake hawamtaki na wameandika barua ya kumkataa na wizara inajua hilo. Ni bingwa wa kuuza ndege za kampuni kwa bei ya kutupwa badala ya ile ya makubaliano ya awali. Ana ukabila na hadi sasa ana jamaa yake anasimamia ujaji wa ndege ya kukodi kwa muda mrefu yuko nje ya nchi. Ni fisadi wa kutupwa kwa ajili ya kutaka pesa za kuendeleza biashara zake.

12. Rajabu Itambo ni meneja Galileo Tanzania kampuni tanzu ya ATCL. Rajabu alipewa kazi ya ushauri katika kitengo cha Galileo na aliyekuwa meneja wakati huo Maalim Ali. Kaburu mmoja aliyekuwa mkurugenzi wa biashara Mike Bond aliamua kumuondoa Maalim Ali katika nafasi hiyo na kumuweka Rajabu kwa maslahi yake kwani walitaka kuuza Galileo kabla ya kuondoka jambo ambalo hawakufanikiwa. Mpaka sasa Rajabu ana uhasidi na wafanyakazi wa zamani kwani anataka awe mkuu wa kitengo cha ITC (Information and Technology Communication) Ni mmoja wa vibaraka wa DM.


Hadi tunakwenda mitamboni ATCL haina bajeti na hili linatokana na Eliasaph kutayarisha bajeti hiyo kwa usiri mkubwa akiweka vipengele hewa ambavyo bodi ina wasiwasi navyo hivyo kuikataa kila wakati. Bajeti huwa inatengenezwa na kitengo maalum katika idara ya fedha lakini safari hii imekuwa na usiri mkubwa. Ilibidi iwekwe hadharani kwa wafanyakazi kupitia workers council ndiyo iifikie bodi jambo ambalo halikufanyika.


Kama tulivyoeleza awali matumizi mabaya ya pesa yanapeleka kampuni kusikoeleweka. Pesa huchotwa kama za mtu binafsi bila kujali taratibu za kihasibu. Viongozi hawa kwa vikundi huenda safari kila wakati kuliko viongozi wote waliopita. Posho wanayolipana ni kubwa mno kwa kila siku hivyo hata safari za watendaji wa chini huenda wao.


Mwenyekiti wa bodi Mustapha Nyang'anyi aliliambia Sunday Citizen tarehe 12 januari 2008 kuwa uzembe wa menejimenti ya ATCL kutoingia mkataba na kampuni iliyokuwa ikodishe ndege kwa ajili ya mahujaji ndiyo chanzo cha sakata zima la hasara katika usafirishaji wa mahujaji. Ukweli ni kuwa menejimenti haikutaka kushirikisha wafanyakazi wa kawaida kuratibu safari hii kama ilvyokuwa miaka iliyopita. Hii ni kwasababu walitaka iwe siri yao kwa kutafuta ndege ya bei poa kuliko hiyo iliyopatikana kitu ambacho hakikuzaa matunda na hatimaye kusema ATCL haiwezi kusafirisha mahujaji.



Mbona kabla ya makaburu iliwezekana. Hapa pana ufisadi sio uzembe tuu. Wapo wazoefu wa kazi ndani ya kampuni lakini wamekodi mtu wa nje Mtambalike rafiki yake DM kwenda kusimamia kurejea mahujaji. Tunasema hii ni hujuma na kuwadharau watendaji wa ndani.
Magari ya kampuni yamenunuliwa kwa bei kubwa bila kufuata taratibu na viongozi wanne kupata magari kutokana na gharama hiyo kubwa na bila kufuata utaratibu wa ununuzi. Hivi sasa kampuni ina madeni mengi kutokana na ufisadi.
Wafanyakazi wasiotakiwa hasa wale wa zamani hutafutiwa sababu za kuwaondoa ili ajira wapewe watu wa DM. Mifano hai tumetaja hapo juu na mingine mingi tunayo kama ule wa Said Ibrahimu kufanyiwa visa na Mark Manji hadi kuamua kustaafu ili yeye Manji aongeze muda alipoamua kustaafu kwa kisingizio kuwa hakuna wa kuchukua nafasi yake.
 
Either you send us today more evidence that Attorney General and other
authorities ex finance ministry approve dthe guarantee and copy wording
guarantee,

Or tomorrow Mr. will be requested to leave aeroman -

Regards'

Nemr Diab
 
KESI YA MATTAKA: Korti ya Kisutu, Dar leo yaahirisha kesi ya mkurugenzi wa zamani ATCL David Mattaka hadi Oktoba 28. Anadaiwa kusababisha hasara ya USD 143,443.

Mytake: ni kwanini kesi za ufisadi zinachukua muda mrefu sana?

"nakumbuka kesi hii upelelezi wake ulikamilika mwaka 2011, lakini cha kushangaza kila ikitajwa inasogezwa mbele! sijui tatizo ni nini? au wanasubiri jamaa afe?
 
KESI YA MATTAKA: Korti ya Kisutu, Dar leo yaahirisha kesi ya mkurugenzi wa zamani ATCL David Mattaka hadi Oktoba 28. Anadaiwa kusababisha hasara ya USD 143,443.

Mytake: ni kwanini kesi za ufisadi zinachukua muda mrefu sana?

"nakumbuka kesi hii upelelezi wake ulikamilika mwaka 2011, lakini cha kushangaza kila ikitajwa inasogezwa mbele! sijui tatizo ni nini? au wanasubiri jamaa afe?


"KUMBUKUMBU KUTOKA MAKTABA ...."

UPELELEZI KESI YA
MATTAKA TAYARI
Na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya
matumizi mabaya ya madaraka na
kununua magari ya mitumba
kinyume na Sheria ya manunuzi ya
umma ya mwaka 2004 inayomkabili
aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la
Ndege(ATCL), David Mattaka na
wenzake umeileza Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,
kuwa upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika.
Wakili Mwandamizi wa Serikali
Oswalid Tibabyemokya alieleza hayo
mbele ya Hakimu Mkazi Ritha Tarimo
wakati kesi hiyo jana ilipokuja
kwaajili ya kutajwa ambapo alieleza
kuwa upelelezi huo umekamilika na
kwamba wanaiomba mahakama hiyo
ipange tarehe kwaajili ya kuja
kuwasomea washtakiwa maelezo ya
awali.
Kwa upande wake Hakimu Tarimo
alisema anaiarisha kesi hiyo hadi
Januari 5 kesi hiyo itakapokuja
kwaajili ya kutajwa na kwamba
usikilizwaji wa awali utafanyika
Januari 23 mwakani.
Novemba 22 mwaka huu, Mattaka
anayetetewa na wakili Peter Swai na
Kaimu Ofisa Mkuu wa Kitengo cha
Fedha Elisaph Mathew Ikomba na
Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya
Ndani, William Haji anayetetewa na
wakili Alex Mgongolwa walifikishwa
mahakamabi hapo kwa mara ya
kwanza wakikabiliwa na makosa
kushindwa kutunza kumbukumbu za
mawasiliano ya manunuzi
waliyokuwa wakifanya na mtoa
huduma kinyume na kifungu cha
55(3),87(1)(f) cha Sheria ya
Manunuzi ya Umma Na. 21 ya mwaka
2004 na kanuni ya 17(1) ya Sheria ya
Manunuzi (Goods,Works,Non-
Consultant Services and Disposal of
Public Asets by Tender)
Regulation,G.N. No.97 of 2005.
Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupamba na Rushwa(TAKUKURU)
alidai shtaka la pili ambalo
linawakabili ni la kushindwa
kutimiza matakwa ya vifungu vya
Sheria ya Manunuzi ya Umma na
Kanuni zake kinyume na kifungu cha
87(1)(f) cha Sheria ya Manunuzi ya
umma ya mwaka 2004.
Shtaka la tatu lina mkabili Mattaka
peke yake ni matumuzi mabaya ya
madaraka kinyume na kifungu cha 31
cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na
Rushwa ya mwaka 2007 ambapo
Mattaka alitoa idhini ya kununuliwa
kwa magari hayo bila ya kuwepo kwa
mkataba wa pande zote mbili na bila
idhini ya Bodi ya ATCL.





Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la
Jumanne, Desemba 6 mwaka 2011.
 
Wana muonea tu DM, Sita amekula kiasi gani kwenye kukodisha vipaza sauti kwenye BMK? Membe amechikichia kiasi gani ktk lile fungu la Ghadaffi? Pinda amekunja kiasi gani kwa kuidhinisha matumizi ya BMK bila kufuata taratibu?... EUWRA iko kwaajili ya walaji ama kwa ajili ya Mafisadi? Mbonna bei zina chumpa kwa kwenda mbele?... ESCROW a/c iliyochotwa 400 Billions wahusika wamechukuliwa hatua gani? Si tetei majanga ila nachukia sana double standard approach ya kumshughulikia DM na kumuacha Prof Tibaijuka beneficiary wa fedha zetu via IPTL...
KESI YA MATTAKA: Korti ya Kisutu, Dar leo yaahirisha kesi ya mkurugenzi wa zamani ATCL David Mattaka hadi Oktoba 28. Anadaiwa kusababisha hasara ya USD 143,443.

Mytake: ni kwanini kesi za ufisadi zinachukua muda mrefu sana?

"nakumbuka kesi hii upelelezi wake ulikamilika mwaka 2011, lakini cha kushangaza kila ikitajwa inasogezwa mbele! sijui tatizo ni nini? au wanasubiri jamaa afe?
 
Hiyo nchi yenu hiyo tukisema sana mtatuambia tuna chuki binafsi. Ila ukweli ni kwamba teuzi za JK ni ngumu sana kuamini ikiwa zinazingatia maslahi na uzalendo wa kitanzania. Ngoja nipate lunch mie niwaachie nchi yenu ya mauzauza hiyo. Byeeeee
 
Hiyo nchi yenu hiyo tukisema sana mtatuambia tuna chuki binafsi. Ila ukweli ni kwamba teuzi za JK ni ngumu sana kuamini ikiwa zinazingatia maslahi na uzalendo wa kitanzania. Ngoja nipate lunch mie niwaachie nchi yenu ya mauzauza hiyo. Byeeeee

...mkuu nchi yetu imekuwa shamba la bibi kwa sababu ya viongozi wetu tunaowaweka madarakani ni DHAIFU, na karibia wote ni wachafu, hakuna aliyemsafi....!
 
Back
Top Bottom