Mkandarasi wa Usafi Kata ya Mbuyuni - Morogoro haonekani, hali ya uchafu ni mbaya mtaani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Hali ya usafi wa mazingira ilivyo Mkoani Morogoro katika Kata ya Mbuyuni, Mtaa wa Msikiti wa Masai karibu na Muslim University of Morogoro.

Mkandarasi wa usafi anaitwa Kajenjere lakini inadaiwa zaidi ya mwezi hajafika eneo husika kukusanya taka, hivyo kusababisha hali kuwa mbaya hadi taka zimeanza kutengeneza funza.

Serikali ya mtaa wanalijua na kila siku linajadiliwa kwenye vikao lakini halijafanyiwa kazi.

photo_2023-06-08_09-10-00 (3).jpg

photo_2023-06-08_09-10-00 (2).jpg


photo_2023-06-08_09-09-57.jpg

photo_2023-06-08_09-09-57 (2).jpg

photo_2023-06-08_09-09-59 (2).jpg

photo_2023-06-08_09-10-00.jpg

UPDATES...
Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa Mbuyuni, Jerald Mawanja amesema "Mkandarasi aliyepewa hii tenda anaitwa Kajenjere, kazi imemshinda na hakuna chochote anachokifanya au hatua zinazochukuliwa dhidi yake.

"Alianza vizuri akawa anapita kila wiki kukusanya taka, akawa anapita baad aya wiki mbili ikaja tatu na sasa ni zaidi ya mwezi. Kwa mazingira ya mitaa yetu kutozoa taka zaidi ya mwezi unataegemea nini kitokee.

"Kunapokuwa na changamoto kama hivi huwa tunaenda kuripoti kwa Afisa Afya ambaye ndiye anatakiwa kulifanyia kazi jambo hilo, lakini hakuna taarifa yoyote, hali ni mbaya na kuna uwezekano wa kutokea kwa milipuko ya magonjwa.

"Hali hii si mtaani kwetu tu bali Kata nzima kuna changamoto hii ya takataka kutozolewa."
 
Yule jamaa kazi haiwezi ila anabebwa na viongozi huko juu. Umeviona vile vibajaji vyake vya taka kwanza, kwa picha hizo tuu vinajaa anaweza somba taka siku nzima na asimalize mtaa mmoja.
 
Back
Top Bottom