Mkandarasi wa mradi wa umeme Kinyerezi One afilisika, mradi wakwama

mr yamoto

JF-Expert Member
Oct 2, 2016
923
1,393
Kampuni ya Jacobsen elektro ya nchini Norway iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme Kinyerezi One Extension imeshindwa kuendelea na ujenzi baada ya kufilisika jambo linalosababisha mradi huo wa Megawatt 185 kutokamilika kwa wakati.

Hayo yamebainika jijini Dar es salaam wakati Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la ugavi wa umeme (TANESCO) ilipokuwa ikitembelea mradi wa kufua umeme kwa gesi asilia uliopo Kinyerezi ambapo Mwenyekiti wa bodi Dk Alexander Kyaruzi amesema kutokana na hatua hiyo kwa sasa imeundwa tume maalum ambayo itamuhusisha mwanasheria mkuu wa serikali ili kushughulikia swala hilo pamoja na kumpata mkandarasi mpya.

Mkandarasi huyo ambaye alianza kazi mwezi wa nane mwaka 2016 na ilikuwa amalize mwezi wa sita 2018 ambapo serikali ya Tanzania imemlipa fedha zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 128 huku gharama ya mradi ikiwa ni dola milioni 188.

Hali mbaya!! Nadhani watakuwa wapiga dili hawa.
 
mr yamoto,
Yaani hata hizo Dola million 128 sawa na 68% ya gharama za mradi alilipwaje? Serikali kwa kawaida hulipa kwa awamu kulingana na kazi iliyokamilika unakaguliwa unapewa cheti unalipwa na unaenda hatua nyingine. Sasa kama hela yoote hiyo kalipwa bila kuendana na kazi aliyoifanya alilipwaje sasa hizo hela ndefu zaidi ya 68%. Uchunguzi ufanyike kazi iliyofanyika iendane na fedha zilizolipwa vinginevyo arudishe hela!
 
Mwandishi kila alipouliza maswali yanayohusu hasara tuliyoipata jamaa alikuwa anayakwepa.
 
Itakua kampuni ya mjinga fulani mbongo lkn kaifungulia ughaibuni. Wa TZ kwa vi dili vya kitoto tunawajua
 
Yaani hata hizo Dolla million 128 sawa na 68% ya gharama za mradi alilipwaje? Serikali kwa kawaida ulipa kwa awamu kulingana na kazi iliyokamilika unakaguliwa unapewa cheti unalipwa na unaenda hatua nyingine. Sasa kama hela yoote hiyo kalipwa bila kuendana na kazi aliyoifanya alilipwaje sasa hizo hela ndefu zaidi ya 68%. Uchunguzi ufanyike kazi iliyofanyika iendane na fedha zilizolipwa vinginevyo arudishe hela!
Nchi hii tunaongozwa kisanii Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
68% itakuwa imesababishwa na procurement ya electrical equipments.
 
Itakua kampuni ya mjinga fulani mbongo lkn kaifungulia ughaibuni. Wa TZ kwa vi dili vya kitoto tunawajua
Kampuni ni ya wa Norway kweli, na huo mradi wa Kinyerezi wamefanya phase one ambayo by 2012 tayari walikuwa wanaifanya.

Nmefanya fanya kazi na kampuni mtoto wa Jacobsen Electro, Jarlso Telecoms. So nawajua vizuri hawa jamaa, na sababu ya kulala mbele naweza ihisi pia.
 
Sababu ya kulala mbele ni ipi? Ukishindwa nieleza hapa njoo PM plz.
Kampuni ni ya wa Norway kweli, na huo mradi wa Kinyerezi wamefanya phase one ambayo by 2012 tayari walikuwa wanaifanya.

Nmefanya fanya kazi na kampuni mtoto wa Jacobsen Electro, Jarlso Telecoms. So nawajua vizuri hawa jamaa, na sababu ya kulala mbele naweza ihisi pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawalipwi madai yao ukiona hivyo. Muda sio mrefu utasikia wameishitaki serikali.
Hakuna mkandarasi atafanya kazi tu bila kulipwa.
 
"Mkandarasi huyo ambaye alianza kazi mwezi wa nane mwaka 2016 na ilikuwa amalize mwezi wa sita 2018 ambapo serikali ya Tanzania imemlipa fedha zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 128 huku gharama ya mradi ikiwa ni dola milioni 188."
 
Hizo zingine kwanini halipwi?! Kalipwa 128 gharama ya mradi ni 188.
Ni rahisi kuandika, lakini ukielewa kazi yake ilivyo unaweza kumuelewa.
 
Kampuni ya Jacobsen elektro ya nchini Norway iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa kufua umeme Kinyerezi One Extension imeshindwa kuendelea na ujenzi baada ya kufilisika jambo linalosababisha mradi huo wa Megawatt 185 kutokamilika kwa wakati.

Hayo yamebainika jijini Dar es salaam wakati Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la ugavi wa umeme (TANESCO) ilipokuwa ikitembelea mradi wa kufua umeme kwa gesi asilia uliopo Kinyerezi ambapo Mwenyekiti wa bodi Dk Alexander Kyaruzi amesema kutokana na hatua hiyo kwa sasa imeundwa tume maalum ambayo itamuhusisha mwanasheria mkuu wa serikali ili kushughulikia swala hilo pamoja na kumpata mkandarasi mpya.

Mkandarasi huyo ambaye alianza kazi mwezi wa nane mwaka 2016 na ilikuwa amalize mwezi wa sita 2018 ambapo serikali ya Tanzania imemlipa fedha zenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 128 huku gharama ya mradi ikiwa ni dola milioni 188.

Hali mbaya!! Nadhani watakuwa wapiga dili hawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwanini wasimlipe hizo dollar mil 60 zilizobakia amalizie kazi kuliko kutafuta mkandarasi mwingine ambapo gharama zitakuwa kubwa zaidi...
 
Back
Top Bottom